MAPOKEZI
wa Mshambuliaji Mpya wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga aliyetokea timu
ya Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA),Yayo Lutimba kwenye uwanja wa
Ndege Mkoani Tanga jana yalikuwa ya aina yake kutokana na kulakiwa na
wingi wa mashabiki,viongozi na wanachama wa timu hiyo.
Mapokezi
hayo yalianza saa mbili asubuhi na mchezaji huyo kutua saa nne katika
uwanja wa ndege akiwa na Meneja wa timu hiyo Akida Machai ambaye alikuwa
ameambatana naye kutoka nchini Uganda.
(picha kwa hisani ya binzubeiry)
....SOMA NA ANGALIA PICHA ZAIDI.....