facebook likes

Friday, August 2, 2013

KENYAN ARTISTE TO FEATURE IN JAY Z'S NEW VIDEO




TBS YAZINYANG'ANYA KAMPUNI 48 LESENI ZA ALAMA ZA UBORA...

Maji ya kunywa ya chupa.






















Shirika la Viwango Tanzania(TBS), limesitisha leseni za alama za ubora ya TBS, katika bidhaa za kampuni 48, zikiwamo za maji ya kunywa, magodoro, taulo za wanawake, mvinyo na vifaa vya magari.


Tangazo lililotolewa jana na TBS, lilieleza kuwa kampuni hizo ni za Tanzania Bara, Zanzibar na nje ya nchi zikiwamo za India, Misri na China.
Bidhaa za maji ya kunywa ya chupa ambazo leseni ya ubora imesitishwa ni pamoja na maji ya Great Zone ya kampuni ya Great Zone Investment na Raha ya kampuni ya Raha Pure Drinking Water zote za Dar es Salaam.
Mengine ni maji ya Uzima ya Kampuni ya Uzima Beverages Co. Limited na AAMFA Beverage Limited ya Dar es Salaam, maji ya Uluguru ya kampuni ya Uluguru Fountain ya Morogoro na maji ya Siha, ya kampuni ya Siha Beverages Limited ya mkoani Kilimanjaro.
Pia TBS imesitisha leseni ya bidhaa za karatasi laini ya Soft Facial Tissue ya kampuni ya Alawy Supplies Limited ya Zanzibar, biskuti za Milki Marie, zinazotengenezwa na kampuni ya Britania Products na nyavu za samaki za Nylon Fishing Twine & Fishing za Imara Fishnet (T) Limited zote za Dar es Salaam.
Bidhaa zingine ni fulana zinazotengenezwa na kampuni ya Kibo Trade, matofali ya GM Gross Africa Limited na taulo za kike, zinazotengenezwa na kampuni ya Hengan Sanitary & Baby Products Limited.
Zipo pia bidhaa za rangi za kampuni ya Chui Paints, mifuko ya plastiki ya kampuni za Centaza Plastics,  Tropical Plastics za Dar es Salaam na Roto Flex Packaging ya Moshi.
Katika bidhaa za betri zimo betri za Dry Cell (Euro Cell) za kampuni ya Euro Solo Energy ya India na Dar es Salaam, na betri za kampuni ya 777 Battery Factory ya China.
Bidhaa za magodoro zilizonyang’anywa nembo hiyo ni ya Jumbo Foam ya kampuni ya Sabira Investment ya Arusha na Foam ya Olyform (T) ya Dar es Salaam.
Pia sabuni za Laundry’s na za Jamii za kampuni ya Mbasira Investment ya Shinyanga, mbegu za korosho za Frabho Enterprices ya Dar es Salaam na Munawar Cashewnut ya Mbeya.
TBS pia imenyang’anya nembo yake kwa mafuta ya alizeti ya Sun Shine ya kampuni ya Mardona Edible Oil Millers ya Moshi, na ya A to Z Oil Mills ya Dar es Salaam.
Zipo pia bidhaa za mtindi uliosindikwa wa ladha ya nanasi, vanilla na strawberry, unaotengenezwa na kampuni ya Morani Dairy ya Tanga, jibini na mtindi vya kampuni ya Kyaka Milk Processing ya Bukoba.
Nyingine ni bidhaa za mvinyo Pineapple Wine ya kampuni ya Kivumbui ya Arusha, Fruit Wine (Golland Banana wine) ya kampuni ya Victoria Food ya Mara na juisi inayotengenezwa na Unnat Fruits Processing ya Morogoro.
Akizungumza na mwandishi jana kuhusu uamuzi huo, Msemaji wa TBS, Roida Andusumile, alisema kanuni za TBS zinataka kampuni husika kuomba leseni ya kutumia nembo hiyo kila mwaka.
Alifafanua kwamba sababu za kuzuia leseni hizo ni pamoja na baadhi ya bidhaa kusitishwa kuzalishwa na kampuni husika au viwanda kufungwa.

UHURU KENYATTA'S DAUGHTER'S PALATIAL BEDROOM

MAMA ASIMULIA MACHUNGU YA KUISHI GEREZANI NA BINTI YAKE WA MIEZI MINANE...

Khadija Shah akiwa na binti yake, Malaika.
Mwanamke mmoja wa Uingereza anayetuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin amezungumzia maumivu yake makali katika malezi ya binti yake mdogo ndani ya selo katika gereza nchini Pakistan.

Khadija Shah anasema binti yake huyo mwenye miezi minane, Malaika, ndicho kitu pekee kinachoendelea kumfanya timamu wakati akisubiria kujua kama atakabiliwa na adhabu ya kifo kwa makosa anayotuhumiwa kutenda.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 25 anayetokea Birmingham bado hajapangiwa tarehe ya hukumu, miezi 14 baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kujaribu kusafirisha dawa hizo zenye thamani ya Pauni za Uingereza milioni 3.2 kwenda nchini Uingereza.
Alijifungua Malaika Oktoba, lakini baadaye akalazimishwa kurejea jela kwenye Gereza Kuu la Rawalpindi, ambako anahofia mtoto wake huyo atashambuliwa na moja ya maradhi ya kuambukiza kama kifua kikuu ambacho kimetapakaa katika gereza hilo.
"Kama Malaika asingekuwapo hapa, ningeweza kuwa mwendawazimu sababu mambo ni magumu mno," alisema Khadija. "Ananifanya nizidi kuwa imara."
Taasisi ya haki za binadamu ya Reprieve imekuwa ikiwasaidia raia wa Uingereza, lakini yeye na mtoto huyo wanaendelea kukabiliana na hatma isiyojulikana inayochangiwa na kasi ndogo ya mfumo wa sheria wa Pakistan.
"Ninaendelea kunyonyesha," alisema Khadija. "Kila miezi mitatu wafungwa nchi za nje hunipa fedha kidogo kwa ajili ya kununulia bidhaa za kawaida za chakula na nepi maalumu kwa ajili ya mwanangu, ambaye ninamweka safi.
"Anapendelea kucheza na makasha matupu ya chakula. Kwa kawaida najaribu kuweka safi mazingira yanayotuzunguka, pia."
Mwaka jana mfungwa huyo alilalamika kwamba binti yake huyo mdogo amekuwa aking'atwa mara kwa mara na mbu, amekuwa akiharisha mno na hakuwahi kupatiwa chanjo za uhai.
Watoto wake wakubwa Ibraham, miaka sita, na Aleesha, miaka mitano, walishawahi kuwa jela pamoja na mama yao, lakini wakasafirishwa kwenda West Midlands zaidi ya mwaka mmoja uliopita na hakuwahi tena kuwaona tangu wakati huo.
"Wanatamani kuniona, lakini hawawezi kuniuliza nilipo," alisema Khadija. "Ninapuuza vitu. Ninapuuza kinachonitokea."
Maya Foa wa Reprieve alisema: "Tunahofia mno kuhusu Khadija na afya ya mtoto wake.
"Kinachoendelea kusumbua mno ni kwamba Serikali ya Uingereza inakula njama katika ahadi yake - kwa kutoa msaada kwa mpango wa Pakistan wa kupiga vita mihadarati, Uingereza iko mstari wa mbele katika kusaidia kupeleka watu kwenye kusubiria kifo kwa makosa ya dawa za kulevya, wakiwamo raia wake yenyewe."
Mama huyo kijana amekana kuhusika kwake tangu wakati huo alipokamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Islamabad mnamo Mei mwaka jana.

Anadai alikubali kusafirisha mabegi madogo kadhaa kama msaada kwa mwanaume waliyekutana hivi karibuni, na hakuwa akifahamu chochote kwamba mzigo huo ulikuwa umehusisha heroin.

MREMBO SHINDANO LA MISS AFRICA AUAWA KWA KUCHOMWA VISU...

Lina Keza (kulia). Nyuma yake ni jengo yalikofanyika mauaji hayo.






















Mrembo chipukizi amekutwa amekufa kwa kuchomwa kwa visu huku binti yake wa miaka mitatu 'akilia pembeni yake kwenye dimbwi la damu', wamesema marafiki jana.

Mwili wa Linah Keza, mwenye miaka 29, ambaye inafahamika alishiriki kwenye Shindano la Miss Africa 2010, ulikutwa kwenye ghorofa moja huko King Edward Road, Leyton, juzi mapema asubuhi.
Tukio hilo liliripotiwa kwenye Tume Huru ya Polisi ya Malalamiko, ambayo itatazama mawasiliano yake waliyokuwanayo polisi na mwanaume mwenye miaka 38 ambaye amekamatwa kuhusiana na kifo chake.
Madaktari wa Huduma za Gari la Wagonjwa London waliongozana na polisi kwenda mahali hapo kabla ya Saa 10:30 alfajiri, lakini Linah, raia wa Rwanda anayeishi London, alikuwa ameshatangazwa kufariki eneo la tukio.
Inafahamika kwamba binti yake alikuwa mahali hapo wakati wa shambulio hilo, kwa mujibu wa fafiki mmoja wa familia hiyo.
Herbert Muhire alisema: "Binti (yake) amepelekwa kwenye uangalizi na kupatiwa tiba ya kisaikolojia na matukio mengine baada ya kukutwa akilia kando ya mama yake huyo aliyekuwa amelala kwenye dimbwi la damu.
"Familia na marafiki wameelezewa jinsi alivyokuwa ameuawa na kufa kifo cha kutisha.
Rambirambi kwa Linah kutoka kwa marafiki na jamaa ziliachwa kwenye ukurasa wa Facebook uliofunguliwa mara baada ya kifo chake.
Azun Jezan aliandika: "Huzuni mno, roho yake ilale mahali pema peponi na binti yake na familia wajazwe nguvu katika wakati huu mgumu wa huzuni."
Mwingine, Justine Twongyeirwe, aliandika: "Nitakumbuka tabasamu lako mpenzi Linah. Ulale Mahali Pema."
Jana asubuhi, ukurasa huo ulikuwa na wafuasi zaidi ya 500 na baadhi walituma picha za Linah, ambaye alifanya kazi kama mrembo na kusomea huduma za jamii kwenye Chuo Kikuu cha Wolverhampton.
Kwa mujibu wa polisi, mwanaume huyo mwenye miaka 38 alikamatwa baada ya kujisalimisha mwenyewe kwenye kituo cha polisi cha north London juzi.
Msemaji wa polisi alisema: "Uchunguzi wa mauaji umeanza baada ya mwanamke huyo kushambuliwa huko Leyton.
"Polisi waliitwa na Huduma za Gari la Wagonjwa London majira ya Saa 10:29 alfajiri ya Jumatano kwa ripoti za kuchomwa kwa visu.
"Maofisa na Huduma za Gari la Wagonjwa walifika na mwanamke huyo mwenye miaka 29 alikuwa ametangazwa kufariki kwenye eneo la tukio."

Uchunguzi wa mwili wake ulipangwa kufanyika majira ya Saa 5 jana asubuhi kwenye Mochari ya Walthamstow.

BERLUSCONI ACHEMKA BAADA YA KORTI KUDUMISHA KIFUNGO

Silvio Berlusconi
Bw Silvio Berlusconi. Pichani.
Waziri Mkuu wa zamani Silvio Berlusconi amepeperusha ujumbe wa hasira wa video baada ya mahakama ya juu zaidi ya Italia kuthibitisha kifungo alichopewa kwa makosa ya ulaghai wa ushuru.
WAZIRI Mkuu wa zamani Silvio Berlusconi amepeperusha ujumbe wa hasira wa video baada ya mahakama ya juu zaidi ya Italia kuthibitisha kifungo alichopewa kwa makosa ya ulaghai wa ushuru.
Berlusconi alisema ni mwathiriwa asiye na hatia wa “msururu wa shutuma na mashtaka ya ajabu yasiyo na uhalisi wowote.”
Mahakama hiyo pia iliagiza uchunguzi zaidi wa mahakama iwapo anafaa kupigwa marufuku kushikilia wadhifa wowote wa umma.
Berlusconi, 76, yawezekana hataenda jela kutokana na umri wake.
Huku akitarajiwa kutekeleza adhabu yake kwa kifungo cha nyumbani, ana chaguo la kutumikia jamii badala yake, huku makataa ya kuwasilisha ombi hilo yakitarajiwa kuwa Oktoba.
Uamuzi wa mahakama hiyo ya Rome’s Court of Cassation, ambayo hawezi kukata rufaa dhidi yake, ulikujia baada ya siku tatu za kusikilizwa kwa kesi hiyo. Berlusconi hakuwa kortini.
Katika ujumbe wa dakika tisa wa video, Berlusconi alikashifu uamuzi huo kama “usio na msingi wowote, na unaoninyima haki yangu ya uhuru na kisiasa.”
“Hakuna anayeweza kuelewa shambulio hili la kunivuruga kabisa kufuatia msururu wa shutuma na mashtaka ambayo hayana uhalisi wowote,” alisema.
Anaelezea kesi hizo zaidi ya 50 alizokabiliwa nazo kama “dhuluma halisi ya mahakama ambayo haijaonekana kwingine katika ulimwengu wa sasa.”
Mgawanyiko
Alishutumu utendakazi wa idara ya mahakama ya nchi hiyo, akisema: “Je, hii ndiyo Italia tunayotaka? Je, hii ndiyo Italia tunayopenda? La hasha!”
Kesi ya kifungo alichopewa inahusu dili ambazo shirika lake la Mediaset lilifanya ili kununua haki ya kupeperusha filamu za Amerika kwenye televisheni.
Adhabu hiyo iliyotolewa Alhamisi ndiyo ya kwanza hakika dhidi ya mfanyabiashara huyo bilionea baada ya miongo kadha ya kuandamwa na mashtaka ya uhalifu.
Aidha, ni hatua ambayo pia imeyumbisha siasa za mgawanyiko nchini Italia.
Waziri mkuu Enrico Letta aliomba kuwe na utulivu “kwa manufaa ya taifa” huku kukiwa na hofu kuwa uamuzi huo wa aina yake ungesababisha mivutano katika serikali ya muungano inayojumuisha chama cha Berlusconi cha People of Freedom.
Mawaziri wa Berlusconi walisema wanatafuta uwezekano wa kukata rufaa katika Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu.

VIDEO: Dogo wa Kitanzania aibuka Bingwa Kuruka Kamba Duniani



KIJANA wa Kitanzania Hamisi Kondo ameibuka mshindi wa dunia katika mashindano ya kuruka kamba yaliyofanyika nchini Marekani Julia 5 hadi Julai 13 mwaka huu. Mashindano hayo yalihusisha nchi 14 zikiwa na wachezaji 480, huku Bara la Afrika likiwakilishwa na Tanzania, Kenya na Afrika ya Kusini ambapo kijana Hamisi mwenye umri wa miaka 14 Mtanzania aliweza kujinyakulia ushindi huo.Kijana huyo ambaye ni yatima aliyelelewa na kituo cha kulelea watoto yatima cha Dogodogo Center kilichopo jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya mchezo wa kuruka kamba kituoni hapo na baadae kupata ufadhili kutoka kwa Bwana na Bibi Amy Canady nchini Marekani ambako aliweza kusoma na kuendeleza kipaji chake.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Hamisi amezungumzia mafanikio yake na kuwaasa vijana wenzake kutokata tamaa ya maisha kwa kuwa na juhudi ya kupambana ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
“Nawaomba watoto wa mtaani na yatima kutokata tamaa ya maisha kwani hata mimi nilikuwa kama wao na nimeweza kufanya juhudi na kufanikiwa,” alisema Hamisi.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda aliwaomba vijana kutong’ang’ania michezo mikubwa kama mpira wa miguu kwani kuna michezo midogo midogo ambayo wanaweza kucheza na kufanikiwa kama ilivyo kuwa kwa Hamisi.
Pia Mwenyekiti wa Kituo cha Kufundisha Michezo Tanzania (TSTC), Bw. Dennis Makoi ambaye alishirikiana na kituo cha dogodogo kumtafutia ufadhili Hamisi nchini Marekani, ametoa shukrani zake za dhati kwa familia ya Bw. na Bi. Amy Canady wa huko Marekana kwa ufadhili na kusaidia kufanikisha ushindi huo. Hivi sasa Hamisi anaendelea na masomo nchini Marekani. 

Via: thehabari

ALLY KIBA KUFANYA SHOW YA KIHISTORIA YA MWAKA



NDANI ya wiki moja ijayo, Sikukuu ya Idd Mosi itaadhimishwa ambapo sambamba na hilo, mkali wa wakali kwenye Bongo Fleva, Ali Kiba anatarajia kuiandika historia kubwa ya mwaka katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar.
Mkali huyo anayetamba na nyimbo kali kama Dushelele, Single Boy, Nakshi Nakshi, Mac Muga, Cinderella na Karim amesema ataitumia shoo hiyo kuweka heshima yake kwa levo za kimataifa hivyo mashabiki watarajie maajabu.
“Ni shoo ambayo nitaandika historia ya mwaka, mara ya mwisho Dar Live nilifanya shoo mwaka jana lakini mwaka huu itakuwa balaa zaidi,” alisema Kiba.
Mratibu wa Dar Live, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ amesema siku hiyo itakuwa ni shangwe mwanzo mwisho kwani asubuhi kutakuwa na shoo maalum ya watoto kabla Kiba, Wanaume Family (Chegge, Temba, Aslay na Bi. Cheka), Bendi ya Mapacha Watatu na H. Baba hawajalivamia jukwaa kuanzia nyakati za jioni.

“Tunawasihi wazazi wawalete watoto wao mapema, kutakuwepo na mtaalam wa kuchezesha mazingaombwe anayeitwa Profesa Calabash, bembea, bwawa la kuogelea, disko toto na michezo mbalimbali.
“Ikifika saa kumi na mbili jioni, watoto watakwenda kulala na jukwaa litahimili midundo mfululizo ya wakali kibao wenye heshima kubwa kwenye Bongo Fleva,” alisema Abby Cool.
Pazia la burudani halitaishia hapo, Rais wa Ngumi za Kimataifa (TPBO), Yasin Abdallah ‘Ustaadhi’ ameiambia Showbiz kuwa bondia kutoka Kusini mwa Afrika, Zambia, Darius Lupupa atavaana na Mbongo, Francis Miyeyusho katika ndondi za kimataifa huku Chupaki Chipindi ‘Double C’ akizipiga na Ramadhan Kido ndondi za uzito wa juu.
“Ndondi za kufa mtu zitapigwa ukumbini pale, mashabiki wa ngumi wanatakiwa kufika mapema kushuhudia uwezo wa Miyeyusho kama ataibakiza heshima nyumbani au kuuachia ushindi uende Zambia,” alisema Ustaadhi.

MKE WA DR. SLAA AZUA TIMBWILI MAHAKAMANI

JOSEPHINE Mushumbusi, mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa,jana alisababisha vicheko mahakamani baada ya kushindwa kumtambua mshtakiwa anayedaiwa kumpora maeneo ya SUMA JKT.

 

Josephine alimuacha mshtakiwam katika kesi yake na kumtambulisha 
mshitakiwa wa kesi nyingine kuwa ni miongoni wa watuhumiwa waliomvamia.

Hayo yalitokea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa alipokuwa akitoa ushahidi kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali Leonard Chalo.

Washitakiwa katika kesi hiyo ambao wanakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha ni Getisi Mturi, Gake Mwita, Salum Mpanda na Charles Chasens.

Mturi na wenzake wanadaiwa Julai 13, 2011, eneo la Suma JKT makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi, walimvamia Josephine na kumpora vitu mbalimbali na kabla ya kufanya uhalifu huo walimtishia kwa silaha.

Josephine alidai Julai 13 mwaka 2011, aliingia ofisini kwake katika jengo la Mawasiliano Tower saa 2.00 asubuhi na kutoka saa 11.00 jioni kwenda nyumbani kwake eneo la Boko akiendesha gari aina ya Toyota Harrier.

Alidai akiwa eneo la tukio katika foleni alimwona mtu akipita mkono wa kushoto huku akimuangalia kwa kutumia kioo cha pembezoni na ghafla alimuona akivunja kioo cha gari lake.

Josephine aliidai alipoanza kuvunja dirisha alitahamaki lakini alisikia risasi hivyo aliamua kutafuta jinsi ya kujiokoa kwa kutoa gari eneo hilo na kwenda katika geti lililopo karibu na Suma JKT.

“Nilifanikiwa kuona sura ya mtu aliyenivamia kwa kuwa tulisimama wote kwa takribani dakika nane,”alidai Josephine.

Josephine alidai katika tukio hilo anakumbuka kulikuwa na watu si chini ya sita na walimwibia vitu mbalimbali. Kesi hiyo imepangwa kuendelea kusikilizwa Agosti 7 mwaka huu

source:thechoice
http://www.thechoicetz.com/2013/08/mke-wa-dr-slaa-azua-timbwili-mahakamani.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+blogspot%2FGDSbw+%28TheCHOICE%29

NEW JOINT: NEY WA MITEGO- SALAM ZAO: ,SIKILIZA NA DOWNLOAD HAPA.

 

Mfalme wa kudiss Tanzania, Nay wa Mitego amerejea tena kuchafua hali ya hewa kwa kutengeneza mijadala kwenye radio na kwenye mtandao kwa ngoma yake mpya, Salam Zao.

Kwenye Salam Zao, Nay ameendeela kufanya kile akifanyacho kwa uzuri (do what he does best) kuponda.


Awamu hii list ya aliowadiss imeongezeka zaidi na kuingia pia kwenye siasa huku akiendelea kuwapa madongo wana hip hop wenzie.

Ameanza kwa kumdiss Madee kwa kusema kuwa yeye ndio rais wa Manzese na kwamba Madee amesanda. “Mi ndo rais wa Manzese yule tozi kasanda, Manzese mikono juu naiongoza kamanda,” anachana Nay.
 

Nay wa Mitego ameendelea kuwadiss wana hip hip huku akiijita kuwa yeye ndio gangster rapper na anatengeneza hela huku wengine wakinuka vikwapa. Hakusita pia kuwarushia bombshell Weusi. “Yo Mchomvu wape salam ‘Kubumkubum’ waimbie watakufa njaa muziki umebadilika,” anarap Nay.


Nay pia amemdiss Zitto Kabwe kwa kurap:


 “Word up Diamond, mwanangu wewe si mtoto wa Kigoma, mpe salama Zitto Kabwe mwambie afanye siasa aachane na Bongo Flava huku hatumtaki kabisa, maneno mengi, propaganda hajui kutekeleza, Kigoma Allstars tayari kawatelekeza.”

Rapper huyo pia amerap kuwa wapo watu waliojipatia utajiri kutokana na misiba ya Mangwea na Kanumba.


“Wanamiliki gari, wameota na vitambi kwa hela za rambirambi, mkizingua nawataja,”anasisitiza. Anasema tangu kifo cha Kanumba Bongo Movies imekufa na haiuzi tena.

Pia hajamuacha mwanzilishi wa shindano la Bongo Star Search Rita Paulsen kwa kudai kuwa licha ya kuwapa zawadi kubwa washindi, wameendelea kupigika mtaani.


“Hizi Salam ziende kwa madam Rita na Bongo Star Search. Mshindi analipwa nini mbona kama magumashi?! Namuona Walter Chilambo kapigika kama zamani, Haji Ramadhani kachoka yupo kitaani. Nauliza milioni hamsini zao anazila nani, acheni ubabaishaji wekeni mambo hadharani.”
 

ZANU-PF WAJITANGAZIA USHINDI

 


 

 

 



 


























Duru za ngazi za juu katika chama cha ZANU-PF nchini Zimbabwe zimedai kuwa Rais Robert Mugabe amemshinda Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai wa chama cha MDC katika uchaguzi wa rais na bunge uliofanyka jana nchini humo.
Afisa mwandamizi wa ZANU-PF ambaye hakutaka kutajwa amenukuliwa na Reuters akisema: ‘Tumeshinda uchaguzi huu. Tumekizika chama cha MDC. Hatukuwa na shaka yoyote kuhusu ushindi wetu.’
Kutangaza matokeo ya mapema nchini Zimbabwe ni kinyume cha sheria na polisi wamesema watamkamata yeyote atakaye tangaza matokeo yasiyo rasmi.
Punde baada ya ZANU-PF kutoa tangazo hilo, chama cha MDC cha Tsvangirai kimesema kumekuwepo na ‘wizi mkubwa wa kura’ katika uchaguzi. Afisa mwandamizi wa MDC ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema hawatakubali matokeo ya uchaguzi na kwamba chama hicho kitaitisha kikao cha dharura baadaye leo.
Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe Rita Makarau amesema anaamini uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kwamba idadi kubwa ya wapiga kura milioni 6.5 walijitokeza. Aidha waangalizi wa Umoja wa Afrika katika ripoti ya awali wamesema uchaguzi wa Zimbabwe ulikuwa wa ‘amani, wenye nidhamu, huru na wa haki.’

KUMBE BARNABA ALIMTEMA SHILOLE BAADA YA KUMTWISHA ZIGO ZA KUMLELEA WATOTO WAKE, ...!



Baada ya siku nyingi kupita tangu Shilole na Barnaba  watemane,imebainika  kuwepo  kwa siri  kubwa  zilisababisha  wawili  hao  watemane ....

Chanzo cha karibu na Barnaba kimedai kuwa  sababu  zilizosababisha  wawili  hao  kutemana   ni  pale  shilole  alipodanganya  umri  wake  na  kumwachia  Barnaba  jukumu  la  kumlelea  watoto  wake...

"Suala  la  kulea  watoto  wasio  wa  kwake  lilikuwa  ni  gumu  sana  kwa  Barnaba  kwani  wakati  huo  ndo  kwanza  alikuwa anaanza  maisha na hakuwa na uwezo wa kumhudumia  mtu  na  wanae"..Kilisema  chanzo  hicho.

Chanzo hicho kiliendelea  kufunguka kuwa  Shilole  ndiye  aliye  mtongoza  Barnaba  kwa  staili  ya  kumdanganya  umri  huku  akimweleza  kuwa  swala  la  watoto  wake  lilikuwa  linasimamiwa  na  baba  yao.

Habari  zinadai  kwamba, baada  ya  Barnaba  kuingizwa  mkenge, penzi  lao  lilikuwa  kwa  kasi  sana  huku  Shilole  akijitahidi  kuuficha  ukweli  kwa  muda  mrefu.

"Cha  ajabu  ni  kwamba, kadri  siku  zilivyozidi  kusonga  mbele, Shilole  alijisahau  na  kuanza  kumwachia  mzigo wa  kuilea  familia  yote..

"Aidha, Shilole  aliusahau  uongo  wake  na  akajichanganya  kutoa  historia  ya  maisha  yake  katika  gazeti  moja  la  udaku ambako  alitaja  umri  wake  halisi huku  akisimulia  jinsi  alivyobakwa  hadi  kupata  mimba.Jambo  hilo  lilimstua  sana  Barnaba"..Kilisema  chanzo  hicho  na  kuongeza:

"Kipengele  cha  kubakwa  kilimchanganya sana  Barnaba  akawa  anajiuliza, kama  alibakwa  na  kupata  mtoto,matunzo  ya  mtoto  anayapataje  kwa  mtu  aliyembaka

"Tukio  hilo  lilo  lilimfanya  Barnaba  apoteze  imani  na  ndipo  alipoanza  alipoanza  kutafuta  visa  vya  kumtema  Shilole"

Shilole  alipotafutwa  kuzungumzia  suala  hilo  hakuweza  kutoa  ushirikiano  wa  kutosha.

chanzo:mpekuzi

MBUNGE WA CCM MTWARA AFUTIWA SHITAKA LA UCHOCHEZI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mtwara imemfutia shtaka la kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM)Hasnein Murji . 
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa upande wa utetezi, Peter Kibatala kuiomba mahakama kuifuta kesi hiyo iliposomwa Julai 3, mwaka huu kwa madai ya kuwa hati ya mashtaka ni dhaifu kisheria na haionyeshi ni makosa yapi mtuhumiwa aliyotenda.
Wakili Kibatala alieleza mahakama kuwa kifungu cha 129 na 132 cha sheria ya mwenendo wa makosa jinai ni lazima mshtakiwa aelezwe mashtaka yake wazi wazi yanayomkabili.
 
Murji alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo akikabiliwa na kesi ya uchochezi anayodaiwa kuifanya Januari 19,mwaka huu katika eneo la Ligula mkoani hapa.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Dynes Lyimo alifuta shtaka hilo na kumwachia mshtakiwa huru baada ya kesi hiyo kuahirishwa tangu Julai 3,mwaka huu. 

Wakati huo huo viongozi wa upinzani Katani Ahmed Katani (33) na Saidi Kulaga (45) wa CUF wanaokabiliwa na mashtaka matatu ya kula njama, kufanya uchochezi na kuamsha hisia mbaya kwa wakazi wa Jamhuri wamefikishwa mahakamani.

KOCHA WA TAIFA STARS KIM AMPONGEZA JUMA KASEJA

Dar es Salaam.Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Kim Poulsen amesema kitendo cha kipa Juma Kaseja kujiunga na klabu ya FC Lupopo, DR Congo kitafungua milango ya mafanikio ya soka la Tanzania.

FC Lupopo kupitia kwa meneja wake Balanga Ismail juzi ilitangaza kuridhia kumsajili Kaseja kwa mkataba wa miaka mitatu ukiwa na thamani ya Dola za Kimarekani elfu 30.

Akizungumza na Mwananchi jana, Kim alisema ni faraja kwake kuona idadi ya wachezaji wanaokwenda kucheza soka nje ya nchi inaongezea siku baada ya siku, kitu ambacho ni ishara ya mafanikio kwa soka la Tanzania.

“Nimepata taarifa ya Kaseja kutakiwa FC Lupopo, hakika ni jambo la kuleta matumaini katika soka la Tanzania,”alisema Kim na kuongeza:

“Mimi siifahamu vizuri, lakini nimeambiwa ni moja kati ya klabu kubwa kule, ni matumaini yangu uzoefu atakaoupata utaisaidia pia nchi yake,”alisema Kim.

Alisema, anatarajia baada ya miaka michache ijayo Tanzania itakuwa na idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, hivyo kumpa wigo mpana wa kuteua wachezaji kwa ajili ya kikosi cha Timu ya Taifa.

“Kama hivi sasa kuna Kapombe (Shomari) amekwenda Uholanzi kufanya majaribio kama akifanikiwa ni jambo zuri, ni matumaini yangu miaka michache ijayo watakuwa wengi zaidi na hivyo kufanya kazi ya kuteua wachezaji wa kuunda timu ya taifa kuwa rahisi,”alisema Kim.

Kaseja ataungana na nyota wengine wawili wa Tanzania wanaokipiga Ligi Kuu ya DR Congo ambao ni Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaoichezea klabu ya TP Mazembe.

MADUDU UWANJA WA NDEGE DAR ES SALAAM

TUKIO la wasichana wawili wa Tanzania waliokamatwa na dawa za kulevya Afrika Kusini, limechukua sura mpya baada ya kujulikana kwamba, siku ambayo watuhumiwa hao walisafiri kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam, mbwa wanaohakiki usalama wa mizigo hawakuwapo. Chanzo chetu cha habari kiliiambia MTAZANIA, kwamba pamoja na uwepo wa kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya uwanjani hapo, kitengo hicho kina kasoro kadhaa zinazotakiwa kurekebishwa.


“Mimi niko hapa, najua kila kinachoendelea, nakwambia siku hiyo ambayo wale wasichana walipitisha dawa hizo, hapakuwa na mbwa wa kunusa, naamini kama mbwa wangekuwapo, lazima siri ingefichuka,” kilisema chanzo hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, katika viwanja vya ndege kuna vitengo vingi vikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Idara ya Uhamiaji na askari polisi ambapo kila kitengo kina majukumu yake.

“Kwa hiyo, ninachotaka kukwambia ni kwamba, jukumu la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ambayo baadhi ya watu wanasema inachangia kupitisha dawa za kulevya, haihusiki kwa sababu jukumu lake kuu ni kuzuia vitu vinavyohatarisha usalama wa ndege na abiria.

“Kuhusu uzito wa mizigo na malipo, hilo linafanywa na shirika la ndege husika na baada ya shughuli zote kufanyika, mizigo hukaguliwa kwa mashine na kunuswa na mbwa kabla ya safari kuanza,” kilisema chanzo hicho.

Pamoja na hayo, utata mwingine juu ya hali ya usalama na uwajibikaji wa watumishi wa uwanja huo wa ndege umejionyesha kupitia nyaraka zilizopatikana.

Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA kwa siku kadhaa sasa, umebaini dawa hizo kilo 150 aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya Sh bilioni 6.8 zilizokamatwa na wasichana hao, zilimhusisha pia mshirika wao kibiashara aliyefahamika kwa jina la Mangunga ambaye majina yake matatu tunayo.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, wasichana hao, Agness Gerald (25) na Melisa Edward (24) walisafiri ndege moja na Mangunga wakitoka Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini.

Nyaraka hizo zinaonyesha kwamba, wakati Manguga na wasichana hao wakisafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA), namba SA 189, Julai 5 mwaka huu, walikuwa na mabegi tisa.

Nyaraka hizo zinaonyesha jina la Agness Gerald, kwamba ndiye aliyelipia mabegi hayo, lakini katika sehemu inayotakiwa kuandikwa barua pepe, imeandikwa barua pepe ya Mangunga inayosomeka, Nmangunga@Gmail.com.

Mabegi hayo, yalikuwa na kilo 150 za dawa za kulevya lakini kila mmoja alitakiwa kusafiri na kifurushi cha kilo 20 na hivyo kutakiwa kuwa na kilo 60 wote kwa pamoja.

Baada ya kila mmoja kuwa na kilo 20, zilibaki kilo 90 ambazo walizilipia Dola za Marekani 94 badala ya Dola 450.

Nyaraka zinaendelea kuonyesha kuwa, Mangunga, Agness na Merisa wakati wa safari yao walikaa kiti kimoja kilichokuwa na namba tofauti.

Agness alikaa kiti namba 23B, Mangunga alikaa kiti namba 23D na Melisa alikaa namba 23A.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Suleiman Suleiman, alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu taarifa hizo, alikataa kulizungumzia kwa undani na kusema hana majibu kwa kuwa suala hilo liko katika uchunguzi.

Agness na Melisa, walikamatwa Julai 5 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Thambo nchini Afrika Kusini wakiwa na dawa za kulevya.

Wakati wanakamatwa, walikuwa na mabegi sita kati ya tisa waliyokuwa nayo wakati wanapanda ndege jijini Dar es Salaam.

Inasemekana mabegi matatu yaliondoka na Mangunga ambaye hadi sasa hajulikani alipo.

"We Shot Our Leader" - Boko Haram Members Reveal


Sheikh Abubakar Shekau, leader of the violent Islamic sect, Boko Haram, has reportedly been shot and deposed by members of his own sect, Boko Haram.

Abu Zamira Mohammed, who is the sect’s leader  negotiating with the federal government has been appointed as the new leader by the group’s Shura Council.
The group also said that its ceasefire declaration is working, pointing  out that there has not been any suicide bombing since the declaration. It noted its condemnation of the Yobe massacre where 40 students were killed, adding that some politicians now commit murder and ascribe it to Boko Haram
On the Kano blasts last Monday, which led to the death of about 45 people, the group blamed it on  federal government’s tardiness in responding to the ceasefire agreement.
A joint report published yesterday, by Dr. Stephen Davis, a conflict resolution expert and an adviser to the last three Nigerian Presidents and  Phillip van Niekerk, President of Calabar Africa, a strategic advisory company focusing on Africa, and former Editor of South Africa’s Mail & Guardian newspaper, in the US based online newspaper, huffingtonpost.com, quoted one Imam Liman Ibrahim, spiritual leader of Boko Haram, as saying that "the change in leadership was prelude to peace negotiations with the federal government."

DPP ..."KESI DHIDI YA WAZIRI MKUU SIJAONA SEHEMU ALIYOVUNJA SHERIA"..


MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, amesema haoni mantiki yoyote au uhalali wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), kumshitaki Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Alisema hayo janai wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari, baada ya kufungwa kwa mkutano wa siku tatu wa mawakili wa Serikali wafawidhi, wakuu wa upelelezi wa mikoa na vikosi
vingine vya Polisi Alisema kauli aliyotoa Pinda bungeni, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu kuhusu Polisi kutumia nguvu kwa wananchi, ililenga wanaokaidi kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria na si kupiga na kuua kama ilivyotafsiriwa na wengi.

“Sijapata taarifa kwa maandishi juu ya azma ya kumshitaki Waziri Mkuu, lakini Pinda hajavunja sheria kwa kauli yake aliyotoa,” alisema.

Alisema kwa jinsi alivyosikia maelezo ya Waziri Mkuu bungeni, kama LHRC wanamshitaki kwa jinai Waziri Mkuu, haoni uhalali wa mashitaka hayo.

Usahihi wa Pinda Alisema Waziri Mkuu alieleza hatua zinazochukuliwa dhidi ya mvunja sheria, na kufafanua kuwa Mtanzania yeyote ana haki kwa mujibu wa sheria, lakini pia ana wajibu, ndiyo maana vipo vyombo na kila chombo kimepewa mamlaka na wajibu wa kutekeleza.

Alifafanua, kwamba kilichoongelewa ni dhana ya mkusanyiko ambayo ni haki kwa mujibu wa Katiba, ikiwemo uhuru wa kukutana, kutoa mawazo na kufanya mawasiliano.

Hata hivyo, alikumbusha kuwa Sheria ya Jeshi la Polisi, inasema ili mkusanyiko ufanyike, lazima taarifa itolewe kwa kiongozi wa Polisi wa eneo husika.

Sheria hiyo inasema, kama mkusanyiko una nia ya kutenda kosa na ikafanyika hivyo, kuna chombo kilichopewa dhamana ya kuhakikisha mkusanyiko haramu unatawanyika na sheria hiyo inaruhusu Polisi kutawanya mkusanyiko haramu.

“Unatarajia nini kama kuna watu wanafanya fujo na polisi wana mamlaka ya kuwakamata waliofanya fujo?” Alihoji Feleshi na kuongeza kuwa dhana ya matumizi ya nguvu ni ya kisheria pia.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, akizungumza kwa simu na gazeti hili, alisema utaratibu wa Polisi kulazimika kutumia nguvu upo. Aliutaja utaratibu huo kwamba unatumika hasa katika mikusanyiko isiyotakiwa, ambapo Polisi hulazimika kutoa tangazo la angalizo mara kadhaa kutaka watu watawanyike.

“Tangazo linapotolewa, Polisi kwa kutumia kipaza sauti husema, tawanyikeni, tawanyikeni na kusisitiza hivyo mara kadhaa, hapo wanaopaswa kutawanyika wakikaidi, nguvu hutumika ingawa inaweza isiwe ya kupiga risasi, pengine virungu, yote hiyo si kupiga?

“Risasi ni kitu cha mwisho, labda uwe unashambuliwa wewe (polisi), hata ikiwa hivyo, ukipiga risasi kuna maeneo ya kupiga, si kichwani, polisi wana mafunzo ya kupiga maeneo ya miguuni, hivyo kutumia nguvu kwa polisi kupo,” alisema Jaji Werema.

Soma maswali na majibu aliyoyatoa Nando kwenye interview yake ya kwanza toka atoke BBA.



2
Ile interview ya mshiriki wa Big brother the Chase Ammynando akiwa kwenye XXL  ya Clouds fm ndio hii, kwa kuelewa kwamba kuna walioshindwa kusikiliza Radio na kuona video za interview, hii time nimeitumia kuandika maswali na majibu ya yote aliyoyazungumza Nando.
Miongoni mwa aliyozungumzia Nando ni pamoja na kuingia na kisu kwenye party, maisha yake halisi na mambo mengine mengi ambapo aliambatana na Barbara Kambogi meneja uhusiano wa MultiChoice Tanzania.
ADAM MCHOMVU: Nando do you speak Swahili ?
NANDO: Mimi ni mtoto wa kitaa mzee kwetu ni Mikocheni napiga kiswahili kamakawa.
B12: Mimi nilijua unaongea sana kiswahili siku ambayo kulikuwa kuna party ndani ya jumba la big brother na ukawa unaongea na Feza ukamwambia, “Feza eh, mtoto Selly nishamalizana naye nipe Pokello” Feza ikabidi amvute Diamond house huku umalizane naye.
NANDO: Unajua tulishaonywa kama mara mbili tatu hivi tusiongee kiswahili sema mswahili si utamjua tu.
B12: Sema mlikuwa mnaelewana sana na mwanadada Annabel kutoka Kenya ukiachana na mshkaji wako Bimp, kwanini yani?
NANDO: Annabel yule mwanamke ana akili sana, anakimbilia Master sasa hivi, mchangamfu, anacheza, chakula ananipikia yeye, yani kila kitu tulikuwa tunafanya mimi na yeye…. kwanini nisimpinde mtu kama yeye ambaye ananirahisishia maisha mwanangu. ADAM MCHOMVU: Wakati upo Big brother ulikuwa unamiss kitu gani huku nje?
NANDO: Nilikuwa namiss sana internet aisee, yani nilitaka hadi nitengeneze kibox cha sabuni niandike namba nicheze nacho aisee.
ADAM MCHOMVU: Oky, sasa hivi umetoka kwenye lile jumba, ni nini unamiss?
NANDO: Kusema ukweli mi nilikua nishachoka mle ndani aisee sikutanii mwanangu, sema imetokea bahati mbaya sio kama nimekusudia, kila binadamu ana sehemu mbili, nzuri na mbaya… siku ikiwa mbaya basi ukiharibu tu ndiyo hivyo kama ilivyotokea.
2
DJ FETTY : Nando ulikuwa ni mshiriki ambaye unakubalika na karibia Afrika nzima kutokana na life style yako mle ndani, Japokuwa ulitolewa lakini tulikuwa tunasoma sms za watu wakiku-support, sasa maisha yale ndani ya jumba ndiyo yako halisi au ilikuwa mipango yako tu katika game?
NANDO: Unajua mimi mwanangu nimeingia kwenye jumba lile na kiatu pea moja tu, hichohicho nimechezea mpira yani nimeenda kama mimi, sijaenda eti sijui ninyoe nywele sijui nifanye hivi… mimi nimeenda nikawambia sikilizeni, sivai hizi bukta zenu wala nini….. walininunulia moja ya njano lakini sijaivaa hadi leo sema wanakuchukua wanaku-take care lakini nilibaki kuwa mimi.
ADAM MCHOMVU: Game ilikuwa ni kitu gani pale kwenye nyumba?
NANDO: Mimi sikucheza game pale kwa sababu hata niliwaambia mimi sitacheza game, mambo ya kusengenyana, kuchukiana mimi hapana, niliwaambia nitaishi maisha nyangu, ukiniambia ukweli nakwambia ukweli usiponiambia na mimi sikwambii.
B12: So umetoka kwenye Big brother Africa lakini kuna Watanzania kibao hawajui nini kili happen hadi ukatoka?
NANDO: Unajua yule jamaa tangu tumeingia siku ya kwanza alikuwa anatoa maswala ya kizushi kizushi halafu mimi nabaki namuangalia tu.
DJ FETTY: Jamaa mwenyewe unayemzungumzia ni Elikeem kutoka Ghana?
NANDO: Eh huyohuyo naskia siku hizi wanaandamana lakini fresh watanzania wako hapa bwana na mimi ni mtanzania,  kosa nililofanya lilikuwa ni pale mtu unapokuwa na dukuduku unatakiwa ulitoe lakini ukilijaza na kulijaza ukitoa linakuwa bomu, huyu jamaa bwana alichukua barafu alafu anarusha kwenye dance floor, sasa mtu utarushaje ice cubes kwenye dance floor then ndiyo huyohuyo jamaa Wanawake wanamuongelea kila kitu.
‘Sasa unamtetea kwamba huyu mwanangu kisa mvulana lakini basi hajaskia halafu kwenye topic ya kijinga sana pombe tu, ikabidi nimwambie yote, kila mtu anastaili yake… kuna ile ukiweka dukuduku likijaa tu haliishi vizuri’ – Nando
9
ADAM MCHOMVU: Oky labda ni bahati mbaya hiyo, mfano ungeshinda ule mkwanja ulikuwa na mpango gani?
NANDO: Tangu nimefika Big brother imepigwa video moja tu ya kitanzania ambayo ilikuwa ni ya Feza, Tanzania ndiyo tunakuwa kila siku sasa kuna ile kitu ya Wanigeria, West africa sana…  hata tukiwa mle ndani hakukupigwa hata wimbo mmoja wa Tanzania kwenye zile playback, sana sana ngoma za Kenya kama Wyre na ile ngoma ya nchi ya kitu kidogo…. So mimi nitaka tutoboe kiubishibishi sana hadi level zile, sikutanii kama ningeshinda ningekuja ku-invest kwenye Entertainment.
DJ FETTY: Katika historia yako umetoka US umekuja hapa kwa kuomba washkaji pesa ya ticket, tumeona kwa asilimia 90 umeweza baada ya kuingia mle ndani, what is the feeling baada ya ndoto zako kuishia njiani wakati umetoka Marekani hadi Dar kwa ajili ya hiki kitu.
NANDO: Bonge la swali, yani mimi ni mtu ambaye naishi maisha yangu with no regret, kila kilichotokea wacha kipite na maisha yanaendelea mbele, mangapi yametokea huko tangu niko mdogo hakuna anayejua labda Barbara ambaye aliniona kwenye audition wengine wote wamenisikia tu, mimi ni mtu wa vyovyote vile ninachoshukuru nimepokelewa vizuri kuanzia airport japokuwa wengine wanaongea tofauti lakini ndiyo hivyo tena, nimeingia mle nimepata platform ya kutengeneza jina kwa hiyo mambo mengine yanaendelea.
ADAM MCHOMVU: Hadi hivi sasa karibia Africa nzima inakujua, ni kitu gani unataka kukifanya kama Nando.
NANDO: Mimi ni mtu wa suprise sana kama ulivyoona kwenye Big brother nimeingia kwa suprise hakuna aliyejua, unatakiwa uumize kichwa juu ya kipi cha kufanya na mimi nahitaji huo muda wa kuchil na kuumiza kichwa nifanye nini.
ADAM MCHOMVU: Music labda,movie au soka?
NANDO: Kila kitu mwanangu lakini soka siwezi tena kama unavyoona nilivyoumia.
1
B12: Ilikuaje hiyo miguu?
NANDO: Hapa unajua nilitoroka shule tukawa tunapiga game pale shule ya ushindi, kipa akanirukia miguu yote miwili bwana, nikaenda nikafanyiwa upasuaji naamka asubihi miguu yote haifanyi kazi nikaenda kufanya majaribio ya mashule makubwa sana nikaumia tena, so ni kama haikupangwa mimi kwenye soka hivi.
B12: Bado tupo na Nando kwenye XXL tunataka atuambie nani anahisi atakuwa mshindi wa big brother the chase lakini hivi sasa itabidi atuambie ngoma gani anapenda kuisikiliza tuigonge hapa.
NANDO: Weka ngoma ya dada yangu Feza aisee, tumpigieni kura ashinde angalau aje anipe kama dola elfu kumi hivi tushaongea naye.
B12 : Tupo na meneja uhusiano wa Dstv Barbara, embu tuambie jinsi utaratibu wa kumpigia kura Feza.
BARBARA: Hii wiki ni kali sana kwetu tunasikitika kuona Nando amerudi lakini ndio hivyo kama binadamu unajirudi unaendelea na maisha lakini mshiriki mmoja ambaye ni Feza bado yupo BBA na yupo kwenye enviction wiki hii, dola laki tatu za kimarekani ni nyingi jamani tupige kura kumsave Feza ikiwa zimebaki wiki tatu tu.
Chakufanya ni kupiga kura kwa njia mbili moja ni kutuma neno Vote Feza kwenda 15456 kwenye mitandao yote pia kwa kupitia www.bigbrotherafrica.com ambapo ukipiga kura hapa unaweza kushinda zawadi mbalimbali.
11
B12: Kwa watu ambao wanataka kushiriki mwakani kwenye Big brother Africa, sifa ya kwanza ni ipi?
BARBARA: Kwanza pale tunavyotaka washiriki kwenda Big brother huwa tunatangaza rasmi kama tunataka washiriki, kigezo cha kwanza ni umri, mshiriki lazima awe na miaka 21 kwasababu mtu mwenye umri huu anaweza kufanya maamuzi mwenyewe, pili lazima awe na passport kwa ajili ya kusafiria, tatu lazima awe anajua lugha ya kiingereza kwa ajili ya kuwasiliana ndani ya jumba la Big brother.
DJ FETTY: Kuna watu wengi walifika kwenye audition wenye hizo sifa, lakini kipi kilikua special kwa Nando na sio wengine?
BARBARA: Kwanza kabisa wakati wa audition tunakuwa na Endemol ambao ndio main producers wa show ya Big brother, wao ndio wahusika wakuu kwenye audition sisi ni kama wenyeji tu.
DJ FETTY: Nando siku ya kwanza kabisa ulivyoingia Big brother ulimwambia Big we need more girls, dizain haukuwaona wa mle ndani nini?
NANDO: Mle ndani kuna hasara tupu yani hakuna kumwamini mtu kwasababu wengi wanaongea lakini action ndogo, Wanawake wenyewe walikuwa wanalalamika hasa kwenye diamond house ambako kulikuwa na young star sana sana yani kama yule Dillish ndiyo hakuna kitu kabisa.
B12: Lakini dezayn kama ulikoma naye sana mtoto Dillish yule wa Namibia.
NANDO: Si unajua yeye mbishi kama mimi, siku nyingine ananinunia lakini kesho yake kama kawaida.
Dillish
B12: So unafikiri nani atashinda kwenye Big brother.
NANDO: Kama sio brother wangu Bimp kuna Beverly na Cleo, Angelo na Elikeem sina uhakika ila wanaweza
B12: Mahusiano yako na Bimp yali-click vibaya mno zaidi ya mtu yoyote mle ndani unafikiri ni kwasababu gani?
NANDO: Bimp kwanza anafanana sana na kaka yangu, amenisaidia sana hadi siku ya mwisho alikuja kuniuliza kuhusu ule mkasi.
DJ FETTY: Kwanini uliingia na kisu kwenye party?
NANDO: Tangu niko mdogo nimekuwa naomba toys za mpira, kisu, bunduki lakini sio kwamba nimetumia hapana, napenda tu hata nikizeeka nitakuwa na visu.
DJFETTY: Au ndiyo ile kwamba kama hauna nguvu hata uwe na mkwara?
NANDO:Hapana mimi natembea na watu kama 20 niogope nini.
10
DJ FETTY:Wakati Big brother anakuondoa alishakupa warning tatu moja ni kuwa na kisu kwenye party nyingine kushika mkasi ukiwa unagombana na Elikem na kitu kingine sijui ilikuwa ni hasira pale ambapo uliposema alistahili kufa.
NANDO: Yah, that day wote tulikuwa na warning mbili mbili ila baada ya ku-provoke na ndio mimi akaniita ya tatu ndani mle na kunambia kuhusu kumtishia amani.
DJ FETTY: Lakini point yangu ni kwamba Bimp aliendelea kuwa mashkaji wako na alimnominate Elikem na kusema hayuko real na kusema Cleo ndio alichochea ule ugomvi
NANDO:Cleo ni mfuata mkumbo na Elikem anatabia za kitoto sana, mtu wa kuongea ongea sana… tabia aliyokuwa nayo sasa hivi yale mambo mimi nimeyafanya zamani sana nikiwa na miaka 16 au 17 huko, utakuta watu wote wapo kimya lakini yeye anaongea, sasa Cleo kuna siku alifanya hivyo Bimp akakasirika kwasababu walimshtumu kitu flani.
ADAM MCHOMVU: Kitu gani cha mwisho cha kuwambia mafans wako?
NANDO: Nawashukuru sana, mimi mwanenu mtoto wenu na ni mtanzania halisi nimekulia kule Mikocheni ndanindani kule, nimeumwa malaria sana kule, cheza sana kwemye vumbi.
8


source:millardayo

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...