WACHEZAJI wa Ligi Kuu na
ligi zote nchini Uingereza wanatarajiwa kupewa semina kutoka Chama cha
Wachezaji wa Kulipwa-PFA kuhusu mbinu za kupambana na kauli za
kibaguzi. ...SOMA ZAIDI....
Semina hiyo ya PFA italenga haswa kuangalia njia sahihi kwa mchezaji anazopaswa kuchukua pindi atakapokutana na tukio kama hilo. Mameneja wa vilabu 92 vinavyoshiriki ligi mbalimbali nchini Uingereza tayari wameshapewa taarifa na PFA kuhakikisha wachezaji wao wanahudhuria semina hiyo. Katika misimu miwili iliyopita kumekuwa na matukio ya kibaguzi ambapo beki wa Chelsea John Terry na mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez wote walipokea kibano cha kufungiwa baada ya kukutwa na hatia ya kutoa lugha za kibaguzi.
No comments:
Post a Comment