facebook likes

Friday, July 5, 2013

DANGURO LA "BANGI" NA "UKAHABA" LAGUNDULIKA TABATA-SHULE


  
NYUMBA iliyogeuzwa danguro la vijana kuvutia bangi na kufanyia ufuska imenaswa maeneo ya Tabata-Shule jijini Dar.
Kwa mujibu wa wananchi waishio maeneo hayo, wamekuwa wakikerwa na vitendo vya kifuska vinavyofanyika katika nyumba hiyo inayodaiwa kumilikiwa na mwanamke aliyefahamika kwa jina la Deograsia Nchimbi.
Baada ya wananchi hao kutoa malalamiko kwa mama huyo mara kwa mara bila mafanikio, waliamua kukitaarifu kikosi kazi cha waandishi  ili waweze kufanya kazi yao.

“Kwa kweli tumesema hadi tumechoka huyu mama amekuwa chanzo cha kuharibu tabia vijana wetu, nyumba yake imekuwa kero, tunaomba mfanye kazi yenu ya kufichua maovu.
“Ngono zembe zinafanyika waziwazi bila hata ya kificho, hata sijui tunakipeleka wapi hiki kizazi cha sasa!” alisema mkazi wa eneo hilo aliyeomba hifadhi ya jina.
OFM KAZINI
Baada ya kupokea taarifa hizo, kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) inayoendeshwa , kiliingia mzigoni na kufanya uchunguzi, kilipobaini ukweli ndipo kilipolitaarifu Jeshi la Polisi, Buguruni kisha kuvamia.
Kikosi kazi cha OFM na polisi walivamia katika nyumba hiyo hivi karibuni majira ya saa kumi na mbili jioni na kuwakuta vijana hao wakiwa na bangi lakini mama mwenye nyumba hakukutwa na kidhibiti.

Ndani ya nyumba hiyo walikutana na vijana wasiopungua kumi lakini waliposikia mlango unafunguliwa walitimka na kuiacha misokoto ya bangi sebuleni ambapo polisi walifanikiwa kumkamata Amosi Nchimbi aliyedaiwa kuwa ni mtoto wa mama mwenye nyumba pamoja na wasichana wawili. WAFIKISHWA POLISI
Baada ya purukushani ya hali ya juu kati ya polisi na vijana hao waliodaiwa kugeuza nyumba hiyo kuwa danguro, walifanikiwa kuwatia mbaroni wasichana wawili na mtoto huyo wa mwenye nyumba ambapo hadi OFM inaondoka eneo hilo, iliwaacha polisi wakiwa katika harakati za kuwapeleka watuhumiwa Kituo cha Polisi cha Buguruni.
WANANCHI WACHEKELEA
Wananchi pamoja na diwani wa mtaa huo, Mtumwa Mohamed walifurahi kuona vijana hao wakipelekwa polisi kwani hali hiyo ilikuwa ikiharibu tabia za vijana wao kwa muda mrefu hivyo kuishukuru OFM kwa jitihada zake za kufichua maovu katika jamii.
“Nawashukuru kwa kweli hapa palikuwa ni kama chaka la maovu nadhani sasa hali hii itatulia. Hili eneo lilikuwa linaleta picha mbaya kabisa katika jamii,” alisema Mtumwa.

DIAMOND AMTOLEA MAHALI PENNY....NA ANATAKA KUINGIZA PESA SIKU YA NDOA YAO....!


SIYO siri kwamba wapenzi wasio na kificho, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Penny Mungilwa wana malengo ya kuja kuishi kama mke na mume lakini maajabu ni namna mwanamuziki huyo alivyopanga sherehe ya ndoa yao iwe siku ikifika.Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akizungumza hivi karibuni, Diamond alisema kuwa yamekuwepo maneno ya chinichini kuwa ameshatoa mahari na siku si nyingi ataingia kwenye maisha ya ndoa ila ukweli ni kwamba kila kitu kinafanyika kwa umakini na mashabiki watajulishwa hatua kwa hatua.
 
Diamond.
Suala la ndoa yangu nalifanya kwa umakini sana, watu wawe na subira tu ila wanachotakiwa kujua ni kwamba nina plani za kuifanya sherehe ya ndoa yangu kwenye Uwanja wa Leaders Club, pale Kinondoni na watu wataingia kwa kiingilio kisichopungua shilingi elfu kumi. Itakuwa ni ndoa ya Wasafi bana,” alisema Diamond.

PATRICK WA KANUMBA ALIVYOFANYIWA NA RIYAMA KWENYE MOVIE YA MWEZI WA RAMADHAN

Kwenye moja ya scene ya movie mpya inayoandaliwa na Batuli kuhusu mwezi wa Ramadhan, utakuja kuipenda sana scene hii jinsi Riyama alivyomtenda vibaya patrick kwa kumwagia unga usoni akiwa anatoka kununua vitu kwa ajili ya kupeleka nyumbani kuandaa futali. Movie hiyo ambayo imemshirikisha na Swebe Santana ambaye kwa muda mrefu amekuwa nje ya bongomovie,kuna Barafu ndani humo na bila kumsahau batuli mwenyewe. 945026_270936609714497_2125063359_n 968978_270937123047779_9366600_n 992908_270937193047772_2120815497_n
More photos
1011037_270937059714452_684484688_n

JAJI MKUU WA MAHAKAMA YA KIKATIBA KUIONGOZA MISRI

Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani, Mohammed Morsi.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Kikatiba nchini Misri, Adli Mansour anatarajiwa kuapishwa kama rais wa mpito wa nchi hiyo baada ya jeshi kumng'oa madarakani rais Mohammed Morsi, ambaye ni kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini humo.
Mkuu wa Jeshi, Generali Abdul Fattah al-Sisi alitoa tangazo hilo kupitia televisheni Jumatano jioni.

Baadhi ya waandamanaji waliokuwa wakimpinga rais Morsi.
Generali Sisi alisema kuwa Morsi, ambaye ni rais wa kwanza kuchaguliwa amekosa kutimiza mahitaji ya watu.
Hatua hiyo inakuja baada ya siku nyingi za maandamano dhidi ya rais Morsi wa chama cha Muslim Brotherhood.
Waandamanaji walimtuhumu yeye na chama chake kwa kusukuma ajenda ya Kiislamu kwa taifa hilo na kukosa kusuluhisha matatizo ya kiuchumi yanayolikumba taifa hilo.

Chama cha Muslim Brotherhood kimesema kuwa bwana Morsi pamoja na washauri wake wako chini ya kifungo cha ndani na hawana mawasiliano ya nje.
Hapo awali, Mkuu wa Majeshi alisema kuwa jaji mkuu wa taifa hilo atachukuwa mamlaka ya rais.
Maelfu ya waandamanaji wanaompinga bwana Morsi mjini Cairo walisherehekea kwa shangwe na vifijo kufuatia taarifa hiyo ya jeshi lakini wale wanaomuunga mkono bwana wanasemekana kubaki kimya huku wakisubiri matukio yatakayofuata.

Rais Obama amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na matukio yaliyopo nchini Misri huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Banki Moon akitaka kuwe na utulivu.
(Habari: BBC Swahili)

New Video: Mr. Flavour - Ada Ada

Hivi ndivyo Jay Z alivyosherekea uzinduzi wa Albam yake - Magna Carta Holy Grail










Adrienne Bailon


Timbarland


Timbarland, Jay Z


Hov na J Cole

Muigizaji wa filamu Lulu (Elizabeth Michael ) Wiki hii Kwenye Take One Aliongelea Kuhusiana Kanumba na kitu ambacho kinamfanya amkumbuke .


Pia aongelea sababu za ukimya wake taingia ametoka jela

KABULA AKERWA NA ‘WANAUME SURUALI’

Na Imelda Mtema
MSANII wa filamu za Bongo, Miriam Jolwa ‘Kabula’ ameonesha kukerwa na wanaume ambao hawana hela ‘wanaume suruali’ lakini wamekuwa wakijifanya wanajua kupenda sana huku wakiwa na wivu kupitiliza.


Miriam Jolwa ‘Kabula'
Akipiga stori na paparazi wetu juzikati, Kabula alisema anajua kupenda ni suala la msingi lakini anawashangaa wale wanaokuwa na wivu wa kupindukia na wakati mwingine kutoa vipigo kwa wapenzi wao wakati wao ni wanaume ‘suruali’.
“Unajua nawashangaa sana wanaume wa aina hiyo, wanakuwa na wivu kupitiliza lakini hawawasaidii chochote wapenzi wao zaidi ya kuonesha wana wivu kweli na wakipishana kidogo tu kipigo kinatembea, mimi wananikera sana,” alisema Kabula.

SOURCE; Globalpublishers

Ethiopian Lawyers To Sue BBA Housemate Betty For Having Sex.

Betty_Ethiopia_BBA8















Don’t know why the lawyers in Ethiopia are referring to the Big Brother Africa house as been PUBLIC, actually the sex scene happened under a roof in a secured room so, what is it with threatening the lady with six years jail term… oh because of the Cameras.
5458-thumb
Some lawyers in Ethiopia are gearing up to sue BBA The Chase Housemate, Betty Aberra, for having sex in public. Betty had sex with fellow Housemate, Bolt from Sierre Leon, just three days after entering the BBA House. According to a local radio show in Ethiopia called Ethiopikalink, if Betty is convicted, she could face up to six years in prison as it is an offense to have sex in public in the country. (Well, she had sex on a bed, in a room…Hehe) The lawsuit is not the only thing Betty is facing since leaving the BBA House, she’s also facing nationwide condemnation from groups who have asked the media and companies to boycott her. Source

TOGO NAO WAKATWA POINT.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeikuta Togo na hatia ya kumchezesha mchezaji asiyeruhusiwa katika mechi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Cameroon hivyo kuwanyang’anya ushindi na wa kuwapa Cameroon. Uamuzi huo unamaanisha Cameroon ambao walipoteza mchezo huo kwa mabao 2-0 sasa wamepewa ushindi wa mabao 3-0 na wamekwea kileleni mwa msimamo wa kundi I, kwa tofauti ya alama moja na Libya wanaoshika nafasi ya pili huku wakiwa na mchezo mmoja wa kumalizia. FIFA ilitoa adhabu hiyo kwa Togo baada ya kumchezesha Jacques Alexys Romao wakati alikuwa na adhabu ya kutocheza mechi moja baada ya kupata kadi mbili za njano katika mechi mbili walizocheza. Cameroon sasa wamefikisha alama 10 katika mechi tano walizocheza huku wakitarajia kumaliza mechi yao ya mwisho nyumbani dhidi ya Libya September 6 mwaka huu.

MADEREVA WA LANGALANGA WATISHIA KUGOMA.

MADEREVA wa mashindano ya magari yaendayo kasi ya langalanga wametishia kususia michuano ya Grand Prix ya ujerumani itakayofanyika Jumapili ijayo kama kutatokea matatizo ya kupasuka magurudumu kama ilivyotokea katika mashindano ya British Grand Prix wiki iliyopita. Chama cha Madereva wa Langalanga-GPDA kimedai kuwa wanachama wake wameonyesha wasiwasi kuhusiana na matukio yaliyopita na kama yakijirudia tena watalazimika kujitoa kwa ajili ya usalama wao. Katika michuano ya wiki iliyopita madereva sita walipasukiwa na magurudumu wakati wakiwa katika mwendo kasi wakiwemo Lewis Hamilton wa timu ya Marcedes, Felipe Massa na Frnando Alonso wa Ferrari, Jean-Eric Vergne wa Toro Rosso, Esteban Gutierrez wa Sauber na Sergio Perez wa MacLaren. Tayari kampuni inayosambaza magurudumu ya Pirelli imeshabadilisha aina ya magurudumu yatakayotumika katika mashindano ya Grand Prix ya Ujerumani ili kuepusha matatizo yaliyojitokeza wiki iliyopita.

BALOTELLI USO KWA USO NA MESSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi anatarajiwa kukutana uso kwa uso na mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli katika mchezo wa kirafiki maalumu kwa ajli ya kumuenzi Pope Francis. Baada ya miezi kadhaa ya majadiliano, Shirikisho la Soka la Italia hatimaye limetangaza kuwa mechi ya kirafiki baina ya nchi hizo mbili itapigwa Agosti 14 mwaka huu katika Uwanja wa Olimpiki uliopo jijini Rome. Shirikisho hilo limedai kuwa wanatarajia Papa Francis ambaye anajulikana kuwa mshabiki mkubwa wa soka, atakuwepo kushuhudia nchi aliyotoka ya Argentina ikipepetana na Italia kwenye mtanange huo. Mara ya mwisho Italia kukwaana na Argentina ilikuwa ni mwaka 2001 jijini Rome katika mchezo wa kirafiki ambapo Argentina walishinda kwa mabao 2-1.

MIAKA 100 YA KOMBE LA DUNIA KUADHIMISHWA ARGENTINA NA URUGUAY.

 

RAIS wa Chama cha Soka nchini Argentina-AFA, Julio Grondona amedai kuwa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA linataka michuano ya Kombe la Dunia 2030 kuandaliwa kwa pamoja na Uruguay na Argentina. Mwaka 1930, Uruguay ambao walikuwa mabingwa wa olimpiki, waliifunga Argentina kwa mabao 4-2 katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia iliyochezwa katika Uwanja wa Centenario jijini Montevideo na kuhudhuriwa na mashabiki wapatao 80,000. Grondona ambaye pia ni mjumbe katika kamati ya utendaji ya FIFA amedai kuwa FIFA ingependa kucherekea miaka 100 ya Kombe la Dunia nchini Argentina na Uruguay ikiwa kama sehemu ya kumbukumbu ya mahali ilipofanyika michuano hiyo kwa mara ya kwanza. Grodona amedai kuwa tayari makubaliano baina ya mashirikisho ya nchi hizo yameshafikiwa na sasa wanasubiri muda ili kutuma maombi ya kuandaa michuano ya kipindi hicho. Nchi za Japan na Korea Kusini ndio pekee zilizoweza kuandaa michuano hiyo kwa pamoja mwaka 2002 toka kuanzishwa kwake mwaka 1930.

TANZANIA YAIPITA KENYA NA RWANDA KWENYE FIFA RANKING


Kwenye upangaji wa timu bora duniani unaofanywa na FIFA, Tanzania imeshika nafasi ya 121 na kupelekea kuipita Rwanda ambayo imeshika nafasi ya 134 wakati Kenya wameshika nafasi 123.
East Africa anyeongoza ni Uganda ambaye ameshika nafasi ya 80. Kutoka na takwimu zilizotolewa na FIFA mwezi wa tano, Tanzania ilishika nafasi ya 109. Tanzania imeshuka kwa jumla ya nafasi 12.

TIMU YA WASICHANA KINONDONI YATINGA FAINALI ZA AIRTEL RISING STAR






Mashindano ya Airtel rising star yanayofanyika Tanzania kwa kutafuta vipaji vya kuendelezwa zaidi katika mpira wa miguu ulimwenguni.
Leo timu ya wasichana ya Kinondoni imewavumilishia mvua ya magoli timu ya Mkoa wa Kigoma kwa mabao 7-0 mechi iliyochezwa muda wa saa 4 asubuhi katika Uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.
Timu ya Wasichana ya Mkoa wa Kinondoni ilionesha kandanda safi kwa vipindi vyote viwili vya dakika 40.
Hadi sasa timu ya wasichana ya Kinondoni inamsubiria mshindi kati ya mechi ya Mkoa wa Temeke na Ilala inachezwa mchana katika Uwanja wa Karume.
Fainali ya Mashindano ya Airtel rising star kwa wavulana na wasichana itachezwa kesho siku ya J,mosi kuanzia saa 7 mchana katika Uwanja wa Karume na kurushwa live na Super Sport.

KERRY WASHINGTON KAFUNGA NDOA NA NNAMDI ASOMUGHA



Kerry Washington is married!, Actress bora wa BET Awards 2013 na muigizaji wa Tv show ya scandal sasa amefunga ndoa na mchezaji wa kutoka huko San Francisco anayejulikana kama Nnambi Asomugha.
Ndoa ilifinyika kimya kimya tarehe 24/jun kwenye jiji la Hailey. Inavyosemekana Couples hao walianza mahusiano yao mwaka jana lakini mwanadada huyo alikuwa akificha mahusiano yake na mchezaji huyo.
Kerry Washington aliwahi kuongea na people.com mwaka 2007 na kusema “I am totally the girl who gets introduced to someone through a mutual friend at a dinner party, falls in love and then is with them for like two years.”

NEW SONG : GODZILLAH FT WALTER ~ THANKS GOD


PHOTOS AND VIDEO : UZINDUZI WA MSASANI SHOPPING MALL









Msasani shopping mall ilifunguliwa jana huku wasanii wakali kama Diamond, Dull, Shetta wakitoa show kali kwa wakazi walioweza kufika kwenye jengo hilo.
Baadhi ya maduka ambayo yapo kwenye hiyo shopping mall ni Slash,lifestyle,shoemart,babyshop,max na mengineo mengi. Jengo lipo karibu na ubalozi wa Marekani.

KUELEKEA KWENYE USIKU WA MATUMAINI 2013







Usiku wa matumaini 2013 inakuletea michezo mbalimbali kama mpira, ubondia, na live show kutoka kwa Prezzo, Diamond na wengineo wengi. Wasanii pamoja na wabunge watakaoshiriki walikusanyika na kueleza jinsi siku hiyo itakavyokuwa ya kipekee.
Kutakuwa na boxing kati ya Ray na Mbunge kutoka Kigoma Zitto Kabwe, Jacquline Wolper na Halima Mdee, Jb na Mh Idd Azzan.
Kwa upande wa mpira itakuwa ni kati ya Wabunge wa simba na wale wabunge wa yanga, Mechi nyingine kali ni kati ya Bongo movie na Bongo Fleva, pia bendi mbalimbali kama Msondo ngoma, Mlimani Park watatoa burudani kali, bila kuwasahau wanaume family.

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...