Raia wa kigeni kutoka katika nchi ya Uingereza ambao wanafanya kazi ya
kujitolea katika upande wa Ualim wamemwagiwa tindi kali mjini Zanzibar
jana mida ya saa moja usiku katika mitaa ya shangani mji mkongwe
Zanzibar habari kutoka katika chanzo chetu cha habari kinasema jeshi la
polisi zanzibar limeanza msako na kuwatafuta watu waliofanya kitendo
hicho walimu hao ambao wamefika mjini Zanzibar kwa kujitolea kufundisha
walitambulika kwa majina ya Kate Gee miaka 18 na kirsiwer Trup pia
miaka 18 walimu hao wa kujitolea wanatoka katika nchi ya Uingereza (UK)
raia hao wameingia kisiwani hapo takribani wiki mbili tu na kukutwa na
majanga hayo ambao walikuwa wanafanya kazi katika shule moja ya msingi
inayojulikana kama Mtakatifu Monika iliyopo chini ya kanisa la Aglicana.
habari tulizozipata hivi punde Raia hao hivi sasa wamehamishiwa katika
Hospitali ya Aghakani jijini Dar es salaam kwa matibabu zaid.
Tutazidi
kuwaleta habari zaidi
No comments:
Post a Comment