...SOMA NA ANGALIA PICHA ZAIDI......
Hili ni zao la ‘experiment’ ya Katibu Mkuu wa Yanga wakati ule
George Mpondela, baadhi ya wachezaji hawa walitokea timu ya vijana
wadogo ya Yanga, wengine kama Salvatory Edward alitokea moja mwa moja
shule ya sekondari ya Kibasila.Waliosimama kutoka kushoto ni: Anwar Awath, Mzee Abdallah, Sylvantus Ibrahim, Mahmoud Nyalusi, Salvatory Edward na Peter Louis.Waliochuchumaa kutoka kushoto ni: James Tungaraza, Mohammed Hussein, Reuben Mgaza, Vincent Peter na Ally Yusuph ‘Tigana’. |
Hii tena ni Yanga, mechi ilikuwa kati ya Yanga na Cadet Club ya
Mauritius katika kombe lililokuwa linaitwa ‘Africa Cup of Winner Cup’,
mwaka sikumbuki. Yanga tulishinda 3-1, magoli yaliyofungwa na Mohammed
Hussein (goli 1,3) na James Tungaraza (goli la 2). Unaweza kuamini
nimekumbana na tiketi ya mechi hii katika takataka zangu?Waliosimama
kutoka kushoto ni: Team Manager Nurdin Ally, Mahmoud Nyalusi, Keneth Mkapa, Reuben Mgaza, Sylvatus Ibrahim, Ismail Issa, Mathias Mulumba, Vincent Peter, Sadiq Kalokola, Kocha Mkuu Mkongo Tambwe Leya (kwa wasiomfahamu inabidi mtafute historia yake na soka la Tanzania), na kocha msaidizi Mrundi Nzoyisaba Tauzany.Waliochuchumaa kutoka kushoto ni: Maalim Saleh, James Tungaraza, Ally Yusuph Tigana’, Anwar Awath, Mzee Abdallah, Mohammed Hussein na Bakari Malima. |
Yanga ya msimu wa 1994.Kutoka kushoto ni: Joshua Kilale, Ally Yusuph ‘Tigana’, Willy Mtendawema, Fomu Felician, Keneth Mkapa, James Tungaraza, Suleiman Mkati, Said Mwamba ‘Kizota’ na Steven Nemes.Waliochuchumaa kutoka kushoto ni: Willy Martin, Mohammed Hussein, Nico Bambaga, Jose Ayoub, Sanifu Lazaro, Edibily Lunyamila na Sekilojo Chambua. |
Yanga tena, hii ni uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wakati wa
mashindano ya club za afrika mashariki na kati, mwaka 1995.Waliosimama
kutoka kushoto ni: Mahmoud Nyalusi, Reuben Mgaza, Nonda Shaaban, Sylvatus Ibrahim, Ally Yusuph ‘Tigana’, Mcongo Sammy Bitumba Iyela, James Tungaraza na Sadiq Kalokola.Waliochuchumaa kutoka kushoto ni: Mzee Abdallah, Bakari Malima, Steven Nyenge, David Mjanja, Mohammed Hussein, Salvatory Edward na Benny Luoga. |
Najua nitawakuna wengi sana kwa hii picha. Hii ndiyo Yanga
iliyobatizwa jina la ‘Umoja wa Mataifa’. Wazee hawa wangekuwa na
marupurupu wanayopata wachezaji wa siku hizi wangefanya maajabu.Kuanzia
kulia kwenda kushoto ni: Aboubakar Salum ‘Sure Boy’, John Alex, Thomas Kipese, Justine Mtekere, Said Sued ‘Scud’, nadhani ni mtoto wa Marehemu Abbas Gulamali, Said Zimbwe, Sanifu Lazaro, Salum Kabunda, Joseph Machela, Godwin Aswile, Athuman China, Issa Athumani, kipa msaidizi Sahau Kambi, kipa Steven Nemes na captain Keneth Mkapa. |
Mtu kapigwa bao hapo. Yanga vs Simba mwaka 1993, uwanja wa taifa.
Yanga walishinda 2-1. Magoli ya Yanga yalifungwa na Said Mwamba ‘Kizota’
na la Simba lilifungwa na Edward Chumila.Katika picha ni: Issa Athumani (10), Mtwa Kihwelu (15), Suleiman Mkati, Said Mwamba (14), Edibily Lunyamila (7), Method Mogella (anayeonekana sura tu), Keneth Mkapa (3) na kulia kabisa ndiyo Zamoyoni Mogella (nadhani Zamoyoni ndiyo alikuwa ametokea Simba, enzi hizo ni big deal ku-cross over katika timu mbili hizo). |
No comments:
Post a Comment