facebook likes

Thursday, July 18, 2013

CCM YAPINGA KODI YA LINE ZA SIMU



CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekuja juu na kuitaka Serikali kuangalia njia nyingine mbadala ya kukusanya kodi na kuachana na mpango wa kuanza kuwatoza wananchi tozo ya Sh 1,000 kila mwezi kwa kila laini ya simu ya kiganjani.

Hatua hiyo, inatokana na kilio cha wananchi ambao tangu Bunge la Bajeti kwa mwaka 2013/14 kupitisha sheria hiyo, kumekuwa na manung’uniko mengi.

Uamuzi huo, ulipitishwa na Bunge baada ya mjadala mkali pindi bajeti ilipotangazwa kitendo kilichomfanya Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. William Mgimwa kuomba Serikali ipewe muda wa kutosha wa kujadili suala hilo.

Baada ya majadiliano na Kamati ya Bajeti ambayo inaongozwa na Mbunge wa Bariadi, Chenge Chenge (CCM), Waziri Mgimwa pamoja na Bunge waliridhia wananchi waanze kutozwa fedha hizo, kuanzia Julai mosi mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye mjini Dar es Salaam jana, ilisema CCM inapinga tozo hiyo kwa sababu itaongeza mzigo kwa mwananchi wa kawaida na kusababisha usumbufu usiokuwa na sababu kwa walalahoi.

Tozo hiyo, ilipitishwa na Bunge la Bajeti ikielezwa kuwa ni utaratibu wa kawaida wa kuibua vyanzo vipya vya kodi pale vinapoondoshwa vilivyopo kwa sababu mbalimbali.

Katika taarifa hiyo, Nape alisema licha ya umuhimu huo, vigezo vilivyotumika kupanga viwango sawia vya kodi hiyo kwa kila mtu mwenye laini ya simu, havijazingatia hali ya utofauti wa kipato kwa Watanzania.

Alisema wengi wao, matumizi yao ya simu ni ya kiwango cha chini mno tofauti na Serikali inavyofikiria.

"Kama chama tawala, tunaona hatuwezi kukaa kimya kwenye jambo ambalo tunaliona linawabebesha mzigo wananchi na huenda likarudisha nyuma maendeleo na kuchelewesha jitihada za kuboresha maisha ya Watanzania kwa ujumla," ilisema taarifa hiyo.

STAMINA KUACHIA NGOMA MPYA SOON.


Msanii wa Hip hop Stamina anatarajia ku- release new single mwezi huu tarehe 24. The song is titled “Mwambie mwenzio” akishirikishana na mkali Hip hop “Darasa” pamoja na mwanadada Wada ambae ni mgeni katika ulimwengu wa muziki.
Stamina amepanga kuachia ngoma hiyo tarehe 24 siku ya kumbukumbu kwa Mama yake mzazi ambaye alifariki tarehe kama hiyo.

    JUSTIN TIMBERLAKE ANAONGOZA KWA KUPATA NOMINATIONS NYINGI KWENYE MTV VIDEO MUSIC AWARD

    Pop star mwenye miaka 32 “Justin Timberlake” mapema mwaka huu aliachia album mpya inayokwenda kwa jina la 20/20 experience.
    Mirror ni moja ya nyimbo ambayo imetamba sana na kufanya vizuri katika chart mbalimbali za music. Wimbo wa mirror umeweza kupata 4 nominations za MTV video music award (VMA).
    Mirror imekuwa nominated kwenye Video of the Year, Best Male Video, Best Pop Video and Best Editing while his “Suit & Tie” team-up with Jay-Z is in the running for Best Collaboration and Best Direction
    Mpaka sasa Justin Timberlake ameshinda jumla ya tuzo saba za MTV video music award.

      MZEE MAGARI KWENYE BONGO FLEVA,SIKILIZA WIMBO WAKE WA KWANZA



      ANGALIA PICHA ZA WEMA SEPETU NA MARTIN KADINDA WAKILA BATA HOTELINI







      MUSWADA WA NDOA KUWANUFAISHA WANAWAKE KENYA








      Mswaada unaolenga kuoanisha sheria za ndoa nchini Kenya umewasilishwa bungeni.Baadhi ya mabadiliko yaliopendekezwa katika mswada huo ni pamoja na kuhalalisha ndoa za wake wengi mbali na kuziimarisha sheria zote saba za ndoa.

      Mapendekezo mengine ambayo huenda yakazua hisia kali ni yale ya kugawa mali iliochumwa katika ndoa pamoja na adhabu ya wanaume ambao huvunja ahadi zao za kuwaoa akina dada.

      Licha ya kuwa ndoa za WAKE wengi hutekelezwa na jamii nyingi nchini kenya, bado hazijahalalishwa.lakini katika mswada huu mpya ,ndoa hizo zimependekezwa.Hatahivyo mwanamume ambaye angependa kuingia katika ndoa hizi ni sharti aweke wazi majina yote ya wake zake mbele ya msajili wa ndoa pamoja na rukhsa aliyopata kutoka kwa wake hao.Hatahivyo akina dada wana kibarua cha kuthibitisha mahakamani iwapo ahadi hiyo ilitolewa na kuvunjwa.

      Vilevile wake hao pia watalazimika kutia sahihi makubaliano kwamba wako tayari kumruhusu mume wao kuongeza mke mwengine.Makubaliano hayo yatalazimika kumfikia msajili wa ndoa siku 21 kabla ya harusi hiyo.hatua hiyo inalenga kupunguza migogoro ya ndoa inayotokana na kifo cha mwanamume aliyeoa.

      Hatahivyo mswada huo unashinikiza kwamba ni sharti mtu aingie katika ndoa hiyo kupitia dini ya kiislamu au sheria za ki-mila.Wale ambao wanataka kuoa au ambao wameoa kupitia sheria za ki-kristo,ki-hindu ama sheria za kawaida hawatakubaliwa kuongeza wake zaidi ya mmoja.

      Mabadiliko mengine ni yale ya walio katika ndoa kugawanya mali waliochuma kwa usawa bila kujali ni nani aliyechangia pakubwa kupata mali hiyo.

      licha ya mswada wa hapo awali kupendekeza kufutiliwa mbali kwa mahari ,mswada huu mpya uko wazi kuhusu hilo na kwamba mtu anaweza kulipa Mahari au la akizingatia desturi za jamii yake.Mswada huo pia unawalinda wahusika dhidi ya kulazimishwa kuoa.

      Hii ina maana kwamba wapenzi walioachana wana uwezo wa kwenda mahakamani kutokana na ahadi za uwongo zilizotolewa na wapenzi wao.

      Aidha wanaume au wanawake walio-ahidiwa kuolewa na ahadi hiyo kuvunjwa watahitaji kulipwa fidia.hatahivyo mwanamke atalazimika kudhihirisha mahakamani iwapo hatua hiyo ilimuathiri. Harakati za kuwasilisha mswada kama huo hapo awali zimegonga mwamba bungeni, huku wabunge wengi wa kiume wakisema kuwa unawapa wanawake uwezo mkubwa katika ndoa.
      source:pro24

      MAPYA YAIBUKA KUHUSU AGNESS MASOGANGE ALIYE KAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA


      BAADA ya kukamatwa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini, msanii anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, ukweli umeibainika kwamba dawa walizokamatwa nazo ni za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo hazipatikani nchini na hazina matumizi yoyote.

      Kupitia taarifa rasmi zilionesha kuwa, Chemical bashirifu ndiyo aina ya dawa walizokamatwa nazo nchini humo, ambapo wasanii hao walikamatwa nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

      Akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam leo Kamishina wa Tume ya Kuratibu na Kuthibiti Dawa za Kulevya nchini, Christopher Shekiondo alisema kwamba kwa mujibu wa sheria za nchi, dawa walizokamatwanazo wasichana hao zinatumika kutengenezea dawa za kulevya, ambapo adhabu yao ni sawa na mtu aliyekamatwa na dawa za kulevya.

      Wasichana hao walikamatwa Julai 5, mwaka huu nchini humo wakiwa shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya sh. bilioni 6.8 wakitokea Tanzania.

      Shekiondo alisema dawa walizokamatwa nazo hazitumiki moja kwa moja kama dawa, bali zinatumika kutengenezea dawa za kulevya hivyo kwa mujibu wa sheria, adhabu zao zinakwenda sambamba na waliokamtwa na dawa za kulevya.

      "Dawa hizo hazitumiki moja kwa moja bali zinatumika kutengenezea dawa za kulevya, hivyo kama taarifa tulizopata ni sahihi juu ya aina ya dawa walizokamatwa nazo na dawa hizi hazitumiki sana nchini, bali zinatumika Afrika Kusini, Asia pamoja na Ulaya," alisema Shekiondo.

      Alisema kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu anayekamatwa na dawa hizo mara nyingi hukumbwa na adhabu ya kuhukumiwa miaka 20 au kifungo cha maisha.

      Akielezea kuhusu wasichana hao wawili kupanda kizimbana juzi, Kamishina huyo aliweka wazi kuwa hadi sasa hawajapata taarifa zozote rasmi, zaidi ya kupokea zile za awali za kushikiriwa na Jeshi la Polisi Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi.

      Kamishina huyo alisema inaonesha Watanzania wengi wamekamatwa na dawa za kulevya nchini Brazil ambao idadi yao inafikia 109, ambapo wengi wao wameshahukumiwa.

      Alisema watu hao wamekamtwa nchini humo, wakiwa na dawa aina ya cocain kwa ajili ya kusafirisha nchi nyingine, huku baadhi yao wamehukumiwa kunyongwa pamoja na kifungo cha maisha, ingawa idadi kamili ya watu hao bado haijafika rasmi.

      "Tumepokea taarifa jumla ya Watanzania 109 wamekamtwa nchini Brazil, ingawa bado tunasubiri kujua ni wangapi waliohukumiwa kifo, pamoja na kifungo cha maisha," alisema Shekiondo.

      Aliongezea kuwa baadhi ya nchi nyingine, ambazo Watanzania wanakamatwa na dawa hizo za kulevya wakiwa wanasafirisha ni China vijana 34, Kenya 30, Pakistani 16, Falme za Kiarabu ikiwemo Dubai 14, pamoja na nchi nyingine kama Japan, Argentina, Msumbiji, Afrika Kusini, Ureno, pamoja na Uingereza.

      Akizungumzia hukumu ambazo zimeshatolewa baadhi ya nchi walizokamatwa Watanzania hao,, Kamishina huyo alisema Brazil ambayo ndiyo Watanzania wengi wamekamatwa idadi kamili, bado hawajapata ingawa Kenya tayari wapo waliohukumiwa kifungo cha maisha, huku wengine wakiwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 hadi 40, nchi China wapo waliohukumiwa kifo na kifungo cha maisha.

      Shekiondo alisema Tanzania kwa sasa inajulikana kama ni njia ya kusafirisha dawa hizo.

      Alisema kuna baadhi ya watu wanatumia maji kusafirisha dawa hizo, yaani meli, jahazi pamoja na mitumbwi, hivyo wana mikakati ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya.

      SERIKALI YAOMBA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA ULINZI WA RASILIMALI NCHINI.



      Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na 
      “Wizara inaomba sote tuitafakari na kuitekeleza dhana ya Jeshi la Polisi 
      ya Ulinzi Shirikishi ni muhimu kila mwananchi mzalendo wa nchi hii ashiriki kikamilifu kudumisha amani na ulinzi wa nchi na rasilimali zake zote”Alisema Yustina. 
      Aidha Yustina alisema ulindaji wa rasilimali hizo hasa wanyama pori utasaidia kujenga na kuimarisha utalii wa nchi kutokana na zaidi ya asilimia 90 utalii unategemea wanyamapori na hivyo kuingizia nchi fedha za kigeni na pia kukuza uchumi.”Kwa hapa nchini zaidi ya asilimia 90 ya utalii unategemea wanyama pori hivyo, watalii wengi huja kuwaona, kuwapiga picha na kuondoka wachache huja kuwawinda kisheria na kuchukua nyara. Wanyamapori ndio wamebeba utalii katika Tanzania na kwa maana hiyo ndio, kwa kiasi kikubwa, wamebeba uchumi wa nchi hii” Alisema Yustina. 
      Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Kuzuia Ujangili kutoka wizara hiyo  Bw. John Muya aliwataka wananchi waliokatazwa kuishi maeneo ya njia za wanyama kutekeleza agizo hilo ili kuepuka uharibifu unaofanywa na wanyama hao kipindi cha uhamiaji.“Napenda kutoa wito kwa wananchi kuondoka kwenye yale maeneo ambayo ni mapito ya wanyama pindi wanapohama kuondoka ili kuondoa usumbufu na uharibifu wa mali” Alisema Muya.  
      Yustina aliwataka wananchi kuacha kuwatazama baadhi ya wanyama kama Fisi na Tembo kama kero kwa wananchi, badala yake tuwatazame wanyamapori kama benki kubwa na kama mkombozi wa nchi yetu kiuchumi.

      Cheki na Picha na ujumbe wa Diamond kwa haters wake


      Inaonekana Diamond amechoshwa na haters wanaosubiri aanguke kimuziki na kumcheka, ndio maana leo hii kupitia mtandao wa Instagram, ameamua kutupia picha inayomuonyesha anaanguka kutoka juu (angani) na kufikia chini kwa kichwa kwenye barabara ya lami. Picha hiyo iliyokuwa na maelezo yanayosema , "Najua hiki ndio mnachokisubiri, kwahiyo endeleeni kusubiri" na kuwa cc ma-haters 






      NANI ZAIDI KITAKWIMU: WAYNE ROONEY VS JUAN MATA



      Siku ya leo zilitoka taarifa kwamba Chelsea walituma ofa ya Paundi Millioni 10 pamoja na mchezaji mmoja aidha David Luiz au Juan Mata, ingawa muda mchache uliopita Chelsea walikanusha suala hilo - wakisema walituma ofa tu ya fedha.

      Pamoja na hayo tu kumekuwepo na mjadala kama ni sahihi kwa United kukataa ofa ya 10m + Mata? Kama ni kweli Chelsea walituma ofa hiyo. 

      Lakini ebu tujaribu kutazama kitakwimu kwa msimu uliopita ni nani zaidi baina ya wachezaji hawa wawili.

      source:shaffihdauda









      PAPIS CISSE AGOMA KUVAA JEZI ZA KUTANGAZA KAMPUNI YA MIKOPO - ASEMA DINI YAKE HAIMRUHUSU




      Hatma ya mchezaji PAPISS CISSE kuendelea kuwa ndani ya klabu ya Newcastle ipo shakani baada ya mshambuliaji wa kisenegali kujitoa kwenye safari ya kwenda Urenokwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.


      Kwa muda mrefu sasa mshambuliaji huyo amekuwa kwenye hali ya kutokuelewana na klabu yake kutokana na suala la kuvaa jezi zenye nembo ya kampuni ya mikopo ya riba ya Wonga.


      Cisse, 28, amegoma kuvaa jezi za mdhamini mpya wa Newcastle kwa sabau kampuni hiyo inafanya biashara ambayo ipo kinyume na imani ya dini yake. 

      Kutokana na suala hilo, mchezaji huyo aliomba avae jezi ambayo haina logo ya mdhamini huyo au jezi iwe na logo yoyote ya hisani ambayo haiendi kinyume na imani yake. 
      Wawikilishi wake wamekuwa kwenye mazungumzo na Newcastle wiki hii kuhusu suala la Cisse kulazimishwa kuvaa jezi za mdhamini - Wonga mazoezini na kwenye mechi. 

      Chama cha wanasoka wa kulipwa wa England pia kiliingilia majadiliano hayo lakini mpaka sasa hakuna maafikiano juu ya suala hilo, kitu kilichopelekea mshambuliaji huyo kuamua kubaki England wakati kikosi kizima cha Newcastle kikielekea Braga - Ureno.
      Cisse aliwajulisha mapema Newcastle kuhusu kuvaa jezi zenye nembo ya Wonga mara tu baada ya klabuhiyo kuingia mkataba na kampuni hiyo ya mikopo. Hata baadhi ya wachezaji wengine waislam wa Newcastle akiwemo kiungo Hatem Ben Arfa wemeendlea kuvaa jezi zenye nembo ya Wonga.
        
      Mchezaji wa zamani wa West Ham Frederic Kanoute - ambaye ni muislam pia - aliruhusiwa na klabu yake ya Sevilla kuvaa jezi isiyokuwa na nembo ya mdhamini ambayo ilikuwa kampuni ya kamari ya 888.com

      Newcastle na Wonga zilisaini mkataba wa udhamini wa jezi wenye thamani ya £24m mwishoni mwa msimu uliopita.

      SOURCE:SHAFFIHDAUDA

      SAKATA LA SISTA WA KANISA KATOLIKI ALIYEBAKWA NA KUNDI LA WANAUME WATATU



      Sista aliye mafunzoni ametekwa na kubakwa kwa wiki nzima na kundi la wanaume watatu katika kile kinachohisiwa kuwa ni shambulio la kulipiza kisasi, vyombo vya habari nchini India vimeripoti.

      Sista huyo mwenye miaka 22 alidaiwa kutekwa kwenye stesheni ya treni na binamu zake na kisha kushikiliwa mateka na kubakwa kwa zaidi ya siku kadhaa sababu waliishutumu familia yake kwa kifo cha baba yao.


      Ni tukio la karibu kabisa katika mfululizo wa mashambulio ya ubakaji nchini India mwaka huu tangu mwanafunzi alipobakwa na kundi la wanaume na kufa kutokana na majeraha yake ya kutisha ndani ya basi la Delhi Desemba mwaka jana.
       

      Sista huyo aliwaeleza polisi alikuwa akutane na binamu zake kwenye stesheni ya treni karibu na Chennai, huko Tamil Nadu, kusini mwa India, baada ya kudai kwamba mama yao alikuwa anaumwa.
       

      Hatahivyo, anasema alichukuliwa hadi kijiji cha jirani ambako alishambuliwa mara kadhaa.
       

      Watuhumiwa hao baadaye walimrejesha kwenye stesheni hiyo na kumwonya asiripoti tukio hilo.
       

      Binamu wa mwanamke huyo, Jotindra Sobhasundar mwenye miaka 30, na Tukuna Sobhasundar mwenye miaka 28, walikamatwa Jumapili, kwa mujibu wa ripoti.
       

      Mtuhumiwa wa tatu alikamatwa Jumatatu baada ya mfululizo wa makimbizano katika wilaya ya Kandhamal.
      Vyombo vya habari za mjini humo vilisema kaka wa Sista huyo alihojiwa kuhusiana na mauaji ya mmoja wa watuhumiwa. 

        
      Shambulio hilo lilidaiwa kutokea kati ya Julai 5 na 11 lakini likatangazwa hadharani wiki hii.

      Tukio hilo limelaaniwa vikali na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini India.

      Kardinali Oswald Gracias, alinukuliwa akisema: "Ubakaji huu wa makundi ni ugaidi wa kimwili na kihisia.

      Pia alizishutumu wakala za serikali kwa 'kukwepa wajibu wao'.

      SOURCE:MPEKUZI

      MZEE MANDELA ASHEREHEKEA MIAKA 95 LEO HUKU AKIWA MAHUTUTI HOSPITALINI



      Afrika Kusini leo wanasherehekea miaka 95 ya kuzaliwa kwa Mzee Nelson Mandela huku rais huyo wa zamani bado yuko mahututi hospitalini.

      Ilikuwa ikitabiriwa kwamba shujaa huyo wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi kwamba angeruhusiwa kwenda kusherehekea siku yake ya kuzaliwa lakini bado yuko hospitali kutokana na kurejea maambukizi kwenye mapafu.


      Kituo cha Kumbukumbu ya Nelson Mandela na makundi mengine yamewataka watu kujitolea kwa dakika 67 kwa kazi za hisani kukumbukia miaka 67 ambayo Mandela aliitumikia jamii yake.

      Umoja wa Mataifa pia umetambua mapambano ya Mandela dhidi ya ubaguzi wa rangi na kusema siku yake ya kuzaliwa ni fursa ya kuenzi urithi wake, na shughuli mbalimbali zimeandaliwa duniani kote.

      Siku ya kuzaliwa Mandela, Julai 18, ilitangazwa rasmi kuwa Siku ya Kimataifa ya Mandela na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2009 kama kutambua mchango wake kwa utamaduni wa amani na uhuru.

      Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon alisema Siku ya kuzaliwa Mandela mwaka huu imekuja katika wakati wa 'kuakisi kwa kina maisha yake na kazi ya Madiba, huku kiongozi huyo wa aina yake akiwa bado yuko hospitalini'
      Aliongeza: "Nelson Mandela alijitolea miaka 67 ya maisha yake kupigania haki za binadamu na haki kwa wote."


      Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ataadhimisha siku ya kuzaliwa Mandela kwa kutoa michango ya nyumba kwa familia masikini katika eneo la Pretoria.

      Mandela alilazwa hospitali mjini Pretoria Juni 8 kwa matatizo ya maambukizi kwenye mapafu yake.

      Mapema wiki hii, Rais mstaafu Thabo Mbeki alibashiri kwamba Mandela anaweza kuruhusiwa kutoka hospitali mapema na kwenda kupatia nafuu nyumbani.

      Marafiki ambao walimtembelea wamesema yuko kwenye mashine ya kusaidia maisha kwa ajili ya kusaidia tu kupumua kwa urahisi.
       

      Taarifa rasmi za hivi karibuni kabisa kuhusiana na afya yake zilisema Mandela alikuwa kwenye hali mbaya lakini inayoimarika.

      Lakini wote, mke wa Mandela, Graca Machel, na Rais Jacob Zuma wamesema hivi karibuni kwamba Mandela anaendelea vema na matibabu.

      Shujaa huyo wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi alitumikia miaka 27 gerezani kabla ya kuja kuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini mwaka 1994.

      RAIS KIKWETE AMTAKA RAIS WA SUDAN AWASAKE WATU WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA WANAJESHI WA TANZANIA HARAKA IWEZEKANAVYO



      Rais Jakaya Kikwete amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Sudan, Omar Bashir, kuhusu kuuawa na kujeruhiwa kwa askari wa Tanzania, walioko katika ulinzi wa kimataifa wa amani katika jimbo la Darfur.

      Taarifa ya Ikulu iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa katika mazungumzo hayo, Rais  Kikwete alimtaka Rais Bashir kuchukua hatua za haraka kuwasaka na kuwakamata waliohusika na kitendo hicho kiovu, na kuwafikisha mbele ya sheria haraka iwezekanavyo.

      Rais Bashir amekubaliana na Rais Kikwete na kumuahidi kuwasaka hadi kuwakamata wale wote waliohusika na kuwachukulia hatua za kisheria.

      Alimueleza Rais Kikwete kuwa binafsi anaamini waliohusika ni wahalifu, kusisitiza kuwa lazima watasakwa hadi kukamatwa na kuchukuliwa hatua.

      Alimpa pole Rais Kikwete kwa tukio hilo la kusikitisha, ambapo wanajeshi wa Tanzania walienda nchini Sudan kulinda amani na usalama wa wananchi wa Sudan.

      Awali Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon, alimpigia Rais Kikwete na kumpa pole kwa mkasa huo mkubwa na wa kusikitisha, ambao umewatokea Watanzania hao wakati wakitekeleza jukumu lao la kulinda amani nchini Sudan.

      Hadi sasa hakuna kikundi chochote kilichokiri kuhusika na shambulio hilo, ingawa kumekuwa na hali ya kutupiana lawama baina ya vikundi vya kiserikali na vya waasi katika jimbo la Darfur.

      Mapigano baina ya vikundi vya kikabila na koo mbalimbali, yamesababisha mapigano na uvunjifu mkubwa wa amani na usalama katika jimbo la Darfur kwa muda wa miaka 10 sasa.

      Mara nyingi mapigano na tofauti zao hizo zimesababisha vifo na uvunjifu wa amani kwa wananchi wa Sudan na wageni pia.

      Mwishoni mwa mwaka jana wanajeshi wanne kutoka Nigeria, waliuawa karibu na El Geneina, Magharibi mwa Darfur, ambapo pia inaelezwa na AU kuwa wanajeshi wapatao 50, wameuawa tangu kikosi hicho cha Umoja wa Afrika kinachoundwa kwa chini ya Umoja wa Mataifa (UNAMID), kianze operesheni yake mwishoni mwa 2007.
       

      Taarifa za UN pia zinaeleza kuwa kabla ya mashambulizi yaliyofanyika dhidi ya kikosi cha Tanzania Jumamosi iliyopita, wanajeshi sita wanaolinda amani waliuawa tangu Oktoba mwaka huu, ambapo pia inasadikiwa kuwa watu wapatao 300,000 wameyakimbia makazi yao. 
      Hata hivyo, kiini cha mgogoro huo inasadikiwa kuwa ni ugomvi wa ardhi na rasilimali zilizoko katika jimbo hilo nchini Sudan.

      Miili ya maaskari hao saba wa Tanzania, inatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa, Julai 19 kwa ajili ya maziko.

      HE LOVED IT & PUT A RING ON IT! CONGRATS HALLE BERRY.





      ACTRESS Halle Berry flashed her wedding ring as she arrived home with new hubby Olivier Martinez from their wedding in France.
      Halle, 46, showed off the chunky gold wedding band with a turquoise rock as she passed through LAX airport with Olivier and daughter Nahla, five.
      source:jestina-george

      WASTARA JUMA AANZA KUSAKA MUME WA KUMUOA BAADA YA KIFO CHA MUMEWE


       
      STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma amesema hana haraka ya kuolewa kwani anahitaji mume na si mwanaume  wa kupita

      Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Wastara alisema kwa sasa yupo huru kutoka na mtu yeyote ampendaye kutokana na sheria na dini inavyosema ila kwa sasa shughuli za kuigiza zimembana.
       

      ‘Nahitaji mume na si mwanaume  wa kupita,  awe mvumilivu, mchapakazi pia awe na hofu ya Mungu. Kwa sasa nafanya filamu zangu kama kumuenzi marehemu mume wangu,” alisema Wastara. 
        
      source:mpekuzi

      TINA TURNER WEDS ERWIN BACH IN A PRIVATE WEDDING CEREMONY.

      TINA Turner has married for the second time.
      The Private Dancer singer wed long-term partner Erwin Bach at a private ceremony in Switzerland, according to local reports.
      Municipal official Hannes Friess revealed the couple tied the knot in a quiet civil ceremony on the banks of Lake Zurich “a few days ago”.
      The 73-year-old star, who became a Swiss citizen in April, will celebrate the union in a Buddhist ceremony at the couple’s estate in Kusnacht on Sunday, with 120 guests.
      Tina has been dating the 57-year-old German record executive since the 1980s.
      She left her first husband, musical partner Ike Turner, in 1978 after years of abuse.
      source:jestina-george

      KAPOMBE ANAONDOKA KESHO MWANZA KWA SAFARI YA UHOLANZI, STARS YAENDELEA KUJIFUA KIRUMBA

      KIUNGO wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Shomary Kapombe anaondoka Mwanza kesho asubuhi kuja Dar es Salaam tayari kwa safari ya Uholanzi kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa huko.
      Kapombe amelazimika kuiacha kambi ya Stars mjini Mwanza inayojiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda wikiendi ijayo mjini Kampala, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za CHAN mwakani kwa ajili ya safari hiyo.
      Kiungo wa Taifa Stars, Frank Domayo akimtoka Shomary Kapombe kwenye mazoezi ya Stars jioni leo Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 

      Domayo anapasua...

      Chuji hajang'atuka; Kiungo Athumani Iddi 'Chuji' (wa tatu kushoto) aliyeripotiwa na gazeti moja kwamba ameng'atuka Stars akiwa mazoezini na wenzake leo

      Kapombe, anayechezea klabu ya Simba ya Dar es Salaam ataondoka nchini Ijumaa kwenda Uholanzi kujaribu bahati yake, ambako amealikwa na mtu aliyejitolea kumtafutia timu ya kuchezea huko.
      Stars inaendelea na mazoezi mjini Mwanza na kocha Kim Poulsen pamoja na kutoa ruhusa Kapombe aende Uholanzi, lakini hajaita mtu wa kuziba pengo lake. 
      Tayari kiungo wa Simba SC, Mwinyi Kazimoto ametoroka kwenye kambi hiyo na inadaiwa amekwenda Qatar kutafuta timu, lakini huyo pengo lake limezibwa na Mudathir Yahya wa Azam FC.

      source: binzubeiry

      "NIPO TAYARI KUPIGANA NA JACK WOLPER ENDAPO ATAENDELEA KULITUMIA JINA LANGU KUJIPATIA UMAARUFU"...BABY MADAHA



      Staa  wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph ‘Baby Madaha’ ameomba pambano la ngumi dhidi ya Jacqueline Wolper ili waweze kumaliza ubishi wa bifu lao.


      Akipiongea na  mwandishi wetu, Baby alisema amechoshwa kusikia tambo za mpinzani wake huyo hivyo kama kweli ni mwanamke, wakutane kwa  ngumi  ili amuoneshe cha mtema kuni.

       “Asiniambie mimi natafuta kiki, mimi ni msomi kuliko yeye, arudi shule au akauze vipodozi. Najua kuimba, kuigiza na ni msomi yeye anaweza hayo? 


      "Kimsingi naomba pambano nimtoe  manundu.Nipo  tayari  kupigana  naye  ili  nimshikishe  adabu,” alisema Baby Madaha. 

      source:mpekuzi

      22 CHILDREN DIE OF CONTAMINATED FREE FOOD PROVIDED BY THEIR SCHOOL IN BIHAR INDIA.

      Bodies of the children, who died in Chhapra after consuming contaminated mid-day meals, lying on ground. (HT Photo)

      The mid-day meal death toll in Bihar's Saran district rose to 22 with two more children falling victims on Wednesday after consumption of free food sparking violent protests amid suspicions by the state government it was poisoned.

      While 16 children, aged below 10 years and studying in Class I to V, had died in Chhapra itself, four others were declared dead on arrival at Patna Medical College Hospital (PMCH) late last night. Two died at the hospital this morning, official and PMCH sources said.
      Among the dead were two children of a woman cook of the mid-day meal project Panno Devi. Three children of another woman cook Manju Devi are under treatment at PMCH along with her.
      Twenty five others are under medical supervision in PMCH, Superintendent of PMCH Amarkant Jha Azad said. The Superintendent said the ailing children were admitted to ICU of paediatric department and senior doctors were attending to them round-the-clock.
      The tragedy took place at the government primary school in Dahrmasati Gandawan village at Mashrakh block, about 25 km from Chhapra and 60 km from state capital on Tuesday.

      BOSI MAN UNITED AONDOKA GHAFLA KAMBI YA TIMU AUSTRALIA KWENDA KUSHUGHULIKIA USAJILI WA FABREGAS

      MAKAMU Mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward ameondoka ghafla jana kwenye kambi ya maandalizi ya msimu ya klabu nchini Australia kwenda kushughulikia usajili wa kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas.
      United bado inajiamini itapata huduma za Fabregas, licha ya mchezaji huyo wa Barca kusema kwamba anataka kubaki Nou Camp na Arsenal inapewa kipaumbe cha kumsajili kwa Pauni Milioni 25 Nahodha wao huyo wa zamani.
      Vyanzo kutoka kambi ya mabingwa hao wa Ligi Kuu England vinasema Fabregas atajiunga nao, ingawa itawagharimu zaidi ya Pauni Milioni 26 walizotoa kama ofa ya kumtaka mapema wiki hii.
      Target: Manchester United want to add former Arsenal captain Cesc Fabregas to their midfield
      Anatakiwa: Manchester United inamtaka Nahodha wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas 
      Fabregas aliichezea Arsenal kuanzia mwaka 2003 hadi 2011, lakini amekuwa akiipenda klabu hiyo ya Old Trafford kwa muda mrefu.
      Akizungumza na gazeti la Sunday kuelekea Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Arsenal na United mwaka 2009, Fabregas alisema: "Mimi shabiki mzuri wa Man United. Sina tatizo kusema United ni moja ya klabu bora duniani – ingawa pia ninataka kuwafunga. Wao ni timu bora duniani kwa sasa – wa juu, timu ya juu na tunawaheshimu kwa kiasi kikubwa.'
      Kuondoka kwa Woodward kunakuja siku moja na kauli ya United kukataa ofa ya Chelsea kwa ajili ya mshambuliaji Wayne Rooney - mchezaji ambaye kocha David Moyes amesistiza hauzwi.
      Hadi sasa mchezaji pekee ambaye amesajiliwa ni beki kinda wa timu ya taifa ya Uruguay chini ya miaka 20,Guillermo Varela, ambaye hata hivyo hajaripoti kazini bado.
      Thiago Alcantara na Kevin Strootman, ambao wote walikuwa wanatakiwa sana United, wameamua kujiunga na Bayern Munich na Roma na kumuacha Moyes akiwa katika mahitaji ya kusaini viungo kikosini mwake.

      FEZA WA TANZANIA AGONGANISHA MABWANA BAADA YA KUINGIA KUONGA NA NJEMBA IKIWA UCHI BAFUNI





      Shemeji yetu Mbotswana, Oneal amechukizwa na kitendo cha Feza Kessy kwenda kuoga na mwanaume mwingine.


      Jana jioni, Feza ilimlazimu amuombe msamaha mpenzi wake huyo aliyeoneshwa kuumizwa roho na kitendo hicho.


      “Umefanya tena leo asubuhi. Umeniacha kitandani na kwenda kuoga na mwanaume aliye UCHI. I was so disappointed”, alisema Oneal ambaye hata hivyo hakumtaja mwanaume huyo.

      “What was wrong with this particular shower”, aliuliza Feza ambaye alijibiwa na Oneal,”He was naked”. 

      Wasiwasi wa Oneal ni kama vyombo vya habari vya Tanzania vikipata picha hizo zinazomuonesha Feza akioga na mwanaume mwingine bafuni na kuzitumia, jambo ambalo linaweza kutia doa mapenzi yao.



      Mrembo huyo wa Tanzania alimuomba msamaha mpenzi wake na kisha kumkumbatia na kumbusu huku wakijifunika shuka gubigubi, kitu kilichomaliza hasira za Mtswana huyo

      CHELSEA SASA WATANGAZA OFA YA PAUNI MILIONI 30 KWA ROONEY


      KOCHA Jose Mourinho amekiri wametoa ofa kwa ajili ya Wayne Rooney na habari zinasema wamesema wataipa Manchester United hata Pauni Milioni 30 wamnase nyota huyo.
      Ndani ya saa 24 tangu vyanzo vya karibu na Rooney kufichua kwamba ‘ana hasira na amechanganyikiwa’, mshambuliaji huyo yuko tayari kuwasilisha barua ya kuomba kuondoka, kwa sababu kocha David Moyes amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hatakuwa mshambuliaji chaguo la kwanza.
      Chelsea ilianza kupeleka ofa ya Pauni Milioni 22 ambayo ilikataliwa na United na sasa wanarudi na ofa iliyonenepa, Pauni Milioni 25— jumla Milioni 3 na inaweza kupanda hadi Milioni 30, ili tu wampate mkali huyo. 
      Ofa ya awali iliyofichuliwa na MailOnline na kukanushwa na Chelsea ilikuwa inahusi fedha na mchezaji kati ya Juan Mata na David Luiz.
      We want Roo: Mourinho chats with Chief Executive Ron Gourlay
      Tunamtaka Roo: Mourinho akizungumza na Mtendaji Mkuu, Ron Gourlay

      United imekataa ofa ya awali ya Chelsea na kuwaambia wasithubutu kurejea tena, kwa sababu Rooney hauzwi.
      Chelsea baadaye ikawatuhumu mabingwa hao wa Ligi Kuu England kwa kuvujisha taarifa za ofa ya awali.
      Taarifa kutoka Stamford Bridge ilisomeka: "Chelsea FC inathibitisha kwamba jana (juzi) imeandika barua rasmi ya ofa kwa Manchester United kwa ajili ya kumsajili Wayne Rooney.
      "Pamoja na hayo, vipengele vya ofa ni siri, kuepuka shaka na usumbufu uliotokana Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Sydney, mapendekezo ya dau hayahusishi uhamisho wa mkopo au mchezaji yeyote kutoka Chelsea kwenda Manchester United,". 
      Transfer tussle: Wayne Rooney's future remains unclear
      Sakata la uhamisho: Mustakabali wa Wayne Rooney bado tata

      WANASAYANSI WAGUNDUA NJIA ZA KUCHAJI SIMU KWA MKOJO


      Wanasayansi wa maabara ya Bristol Robotics Uingereza wamegundua njia ya kutumia mkojo kama chanzo cha kuzalisha umeme wa kuchaji betri za simu, na kudai kuwa wa kwanza kutengeneza “the world’s first microbial fuel cells (MFC) powered mobile phone”. 
       

      Watafiti hao walielezea juu ya ugunduzi wao kupitia jarida la ‘Physical Chemistry Chemical Physics’. 
      Dr Ioannis Ieropoulos amesema, huo ndio ugunduzi wa kwanza wa kuzalisha nguvu ya umeme kwa kutumia mkojo, na katika majaribio ya utafiti huo wamefanikiwa kuchaji simu ya Samsung. 
       

      Wanasayansi hao wanaamini kuwa teknolojia yao inaweza kutumika katika mabafu huko mbeleni kwaajili ya kuwashia mashine za kunyolea au kupasha moto maji ya kuoga na kuwasha taa.

      COMMENTS

      Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...