Taarifa ikufikie kwamba yule bondia mkongwe ambae ni mmoja
kati ya waliowahi kumiliki headlines za dunia sana Evander Holyfield
anatarajiwa kuja Tanzania.
PromotaMtanzania Jay Msangi kutoka Hall of Fame Boxing and Promotions Company ameongea
na jovinbachwa na kumwambia hiyo game imepangwa kuchezwa Uwanja wa
Taifa April 27 2014 Uwanja wa Taifa ambapo Evander atapigana na Francois
Botha wa South Africa aliewahi kuwa bingwa mara mbili.
Jay amesema haijawa ngumu kumpata Evander kwa ajili ya
pambano kwa sababu kampuni yake ina uzoefu wa miaka mingi na imeshaandaa
mapambano zaidi 30 kwenye jimbo la Ohio Marekani, ni kampuni ambayo iko
Marekani na hapa Tanzania.
Hata hivyo kwa mara ya kwanza hii kampuni August 30 2013
itamkutanisha bondia Francis Cheka na Mmarekani Derrick atakaekua bondia
wa kwanza Mmarekani kuja kupigana Tanzania.
Siku hiyohiyo ya August 30 pia mabondia Mada Maugo na Thomas Mashari watashuhudiwa wakizichapa live.
News, Events, Entertainment, Sports, Lifestyle, Fashion,politics, Beauty, Inspiration and yes... Gossip!
facebook likes
Friday, July 12, 2013
Huyu ndio staa mwingine wa dunia ataetua Tanzania muda mfupi ujao
Inaelekea President Obama kaacha upepo mzuri Tanzania manake taarifa zilizoifikia jovinbachwa.blogspot.com muda mfupi uliopita baada tu ya bondia Evander kuthibitishwa na yeye kuja Tanzania, staa huyu mwingine wa dunia nae anatarajiwa kufika Tanzania muda mfupi ujao.
Staa huyu mtangazaji Oprah Winfrey ambae amewahi kufanya interview na mastaa wengine kama marapper Jay Z, 50 Cent na mwimbaji Rihanna, unaambiwa kuna uwezekano mkubwa kabisa usimuone Dar es salaam au sehemu nyingine maarufu za town, atakwenda Serengeti moja kwa moja July 13 2013 kwa ajili ya mapumziko tu na kuondokea hukohuko.
Mwingine anaekuja kuitembelea Tanzania ni mwimbaji Lynda Turner…… endelea kukaa karibu na www.jovinbachwa.blogspot.com kwa info zaidi baadae…
IRENE UWOYA AFUNGUKA BAADA YA DIAMOND KUMLIPUA JANA
Kuna
saa najiuliza kwanin ukimwamin mtu ndio anageuka...kwanin ukiwa muwaz
watu wanakuchukulia vbaya? Leo nimeumia sanaaa kuliko
skuzote...sijaamini mtu niliye mwamini kumuona kama rafiki yangu anaweza
kuongea shit kuhusu mim...au najiuliza siruhusiwi kuwa na rafik wa
kiume? Lakin sa nyingine nakaa chin nasema God ...u know me better”
alifunguka Uwoya.
Sababu kubwa iliyodaiwa kumfanya Diamond atembee na Uwoya ni kitendo cha muigizaji huyo kudaiwa kumponda mara kwa mara na alikuwa hampendi Diamond ambaye alikuwa anafikishiwa habari hizo na marafiki zake Irine.
Sababu kubwa iliyodaiwa kumfanya Diamond atembee na Uwoya ni kitendo cha muigizaji huyo kudaiwa kumponda mara kwa mara na alikuwa hampendi Diamond ambaye alikuwa anafikishiwa habari hizo na marafiki zake Irine.
Kama hukufanikiwa kusoma habari hiyo iliyoripotiwa jana basi isome hapa http://www.jovinbachwa.blogspot.com
RAIS KIKWETE AWASHANGAA CHADEMA KUTAKA KAMBI YA KUJILINDA...DR. SLAA NAYE AWATAKA POLISI WAYAVUNJE MAKAMBI YA CCM
Rais wa Tanzania amewashangaa na kuwalaani CHADEMA kwa kutangaza kufundisha vijana namna ya kujilinda na kusema kuwa ni watu wa ajabu kama wamefikia huko.
Mh. Rais kayasema hayo katika kuhitimisha kongamano la amani huku bwana Cheyo nae akisema kuwa hata kama ni kutaka kuwa rais wa nchi CHADEMA wamefika kubaya....
Wakati mh. Rais akiwashangaa CHADEMA,Katibu Mkuu wa chama hiyo, Dr Wilbroad Slaa amelitaka jeshi la polisi kuvunja mara moja makambi yote ya CCM nchini yanayotoa mafunzo kwa vijana wanaoitwa Green Guards.
Kauli hiyo ya Dr. Slaa imekuja baada ya polisi kuwazuia CHADEMA kuanzisha kambi yoyote ya kujihami na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao endao watakaidi agizo hilo
Dk. Slaa, amesema kauli ya Jeshi la Polisi inadhihirisha namna wahusika wasivyofahamu sheria kwa kile alichoeleza kuwa wao hawaundi majeshi bali vikundi vya ukakamavu.
Alisema ni heri msemaji wa jeshi hilo angekaa kimya kuliko kulifedhehesha Jeshi la Polisi kwa tamko lisilokuwa na ushawishi wa kisheria.
“Nawashauri hawa waanze na Tendwa…ila kwanini wameanza leo sisi tulishayalalamikia makundi ya CCM kwa barua na hata walipomaliza mafunzo yao kule Igunga tukapiga na picha wao hawakuinua mdomo kuliongelea,” alisema Dk. Slaa.
Alisema katika miaka minne iliyopita CHADEMA ilikuwa ikionyesha kwa ushahidi namna vijana wa CCM wanavyopewa mafunzo ya kijeshi, ikwamo silaha kutoka nje ya nchi huku wahusika wakiendelea kukaa kimya.
Aliongeza kuwa hali hiyo ya kuamka baada ya kauli ya CHADEMA inatia nguvu shaka yao, aliyodai kuwa makundi ya CCM yanafanya mafunzo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Dk. Slaa alitolea mfano kundi la vijana wa CCM walioweka kambi katika shule ya wazazi katika Kata ya Ivumwe, Mbeya mjini na kisha kuwateka katibu wa CHADEMA Mbeya mjini na baadhi ya wanachama wake.
Alisema katika tukio la Ivumwe wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani wa hivi karibuni, CHADEMA walitoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi wa Mbeya ambaye aliwajibu kuwa wapeleke ushahidi kama vijana hao ni wahalifu.
Alibainisha kuwa CCM imekuwa na kawaida ya kukusanya vijana kutoka maeneo tofauti na kisha kuwapa mafunzo ya kijeshi na silaha kwa ajili ya kuwadhuru wapinzani na kutolea mfano Kambi ya Ulemo aliyosema ilikuwa na vijana waliopewa mafunzo ya kijeshi.
“Tunawasubiri tuone hatima yao ni nini, sisi tunajua Jeshi la Polisi limeshajitoa kulinda viongozi wa CHADEMA sasa kwanini tusijilinde wenyewe,” alisema Dk. Slaa.
Source: BBC, Tanzania Daima,Jamii Forum
PAJA LA WEMA SEPETU LAFANANISHWA NA NGOZI YA "KITI MOTO"
Wema Sepetu ni miongoni mwa wasanii walioathiriwa sana na Mikorogo.Matumizi ya madawa ya kujichubua yamemfanya msanii huyu maarufu nchini aharibike ikilinganishwa na jinsi alivyokuwa mwaka 2006 wakati aliponyakua taji la Miss Tanzania....
Athari za madawa hayo zilianzia mapajani na sasa zimekuwa zikipanda juu kuelekea usoni...
"Nimeshangaa sana kuliona paja la Wema.Ivi ni kwa nini anakubali kupiga picha kama hiyo wakati anajijua tayari keshakuwa kituko.?? Paja gani hilo? Linatofauti gani na ngozi ya nguruwe???"...Alifunguka mdau mmoja alipokuwa akipiga stori na mpekuzi wetu
UJUMBE:
>>Mkorogo ni hatari kwa afya yako.
>>Uzuri wa mwanamke si sura bali ni tabia
SERIKALI YATANGAZA VIWANGO VIPYA VYA CHINI VYA MISHAHARA KISEKTA
Serikali imetangaza viwango vipya vya chini vya mishahara kisekta ambavyo vinatofautiana kati ya sekta moja na nyingine ambavyo ni kuanzia Sh40,000 hadi Sh400,000 kwa mwezi kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema, watakaolipwa kima kidogo zaidi cha Sh40,000 ni wafanyakazi wa nyumbani ambao wameajiriwa na watu wa kawaida huku wakiishi kwenye nyumba za waajiri wao.
Kwa upande mwingine, katika viwango hivyo, kima kikubwa katika viwango hivyo cha Sh400,000 kitalipwa kwa wafanyakazi wa sekta za mawasiliano zikiwamo kampuni za simu, kampuni za kimataifa za nishati, madini na taasisi za fedha.
Katika viwango hivyo, mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na watu wa kawaida lakini ambao hawaishi kwenye nyumba za waajiri wao itakuwa Sh80,000.
“Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na mabalozi wa kigeni na wafanyabiashara maarufu wanatakiwa kulipwa Sh150,000 kwa mwezi,” ilisema taarifa hiyo.
Wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na maofisa wa Serikali watalipwa Sh130,000 kwa mwezi.
Kima cha chini cha mshahara katika huduma za kilimo ni Sh100,000 na huduma za afya Sh132,000.
Kwa upande wa wafanyakazi wa vyombo vya habari, posta na usafirishaji wa vifurushi ‘courier services’, kima cha chini kitaanzia Sh150,000.
Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa hoteli za kitalii kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ni Sh250,000, wakati kwa hoteli za kati ni Sh150,000 na migahawa, nyumba za wageni na baa ni Sh130,000.
Kampuni za ulinzi za kimataifa zitapaswa kulipa kiwango cha chini cha mishahara cha Sh150,000 kwa wafanyakazi wake sawa na kampuni ndogo za huduma za nishati. Kampuni ndogo za ulinzi zitatakiwa kulipa Sh100,000.
Kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga kitakuwa Sh300,000, sawa na wale wa utoaji na uingizaji wa mizigo. Wafanyakazi wanaofanya katika sekta ya usafirishaji wa majini, uvuvi na nchikavu wakitakiwa kulipwa Sh200,000.
Kima cha chini kwa kampuni za makandarasi daraja la kwanza kitakuwa Sh325,000, makandarasi daraja la pili hadi la nne Sh280,000 na makandarasi daraja la tano hadi saba Sh250,000
Wafanyakazi katika kampuni za uuzaji wa magari watatakiwa
kulipwa Sh300,000 na madalali wa bima watalipwa Sh200,000. Kampuni za
wachimbaji wadogo wa madini zitalazimika kulipa mshahara usiopungua
Sh200,000 kwa wafanyakazi wake.
Mishahara ya chini kwa wafanyakazi wa shule za awali, msingi na sekondari za binafsi ni Sh140,000 huku wafanyakazi wa viwandani wakipaswa kulipwa Sh100,000.
Taarifa hiyo ya Wizara ya Kazi imesema sekta ambazo hazijaorodheshwa, wafanyakazi wake watatakiwa kulipwa kuanzia Sh100,000.
Mwananchi
"KILA MTANZANIA NI LAZIMA ALIPIE SH. 1000 KWA AJILI YA KADI YA SIMU YAKE"....WAZIRI WA FEDHA AMESISITIZA TENA
SERIKALI imesisitiza kuwa itatoza Sh
1,000 kwa kila kadi ya simu inayotumika lakini pia inaangalia utaratibu
wa kufanya makato hayo kwa njia ambayo haitamuumiza mtumiaji wa simu.
Akizungumza jana jijini Dar es salaam,
Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa alisema kuwa kupitia tozo hizo
wanatarajia kukusanya Sh bilioni 160 kwa mwaka.
“Kupitia wawakilishi wenu na sisi
serikali kuwa sikivu, tulishauriwa na ikaonekana kwamba kuna uwezekano
wa kupata chanzo kingine cha mapato kupitia kadi za simu” alisema.
Alisema katika mapendekezo yaliyokuwa
yametolewa serikali ilishauriwa kutoza Sh 1,450 katika kila kadi ya simu
lakini baada ya kukaa na kushauriana serikali iliona ni vyema ikatoza
Sh 1,000 ili kila mwananchi aweze kumudu gharama ambapo kwa mwaka kila
mmiliki wa kadi ya simu atatozwa sh 12,000.
Alisema baadae serikali ilipokea
mapendekezo mbalimbali ili kuangalia kama hilo linaweza kutekelezeka na
walipita ngazi zote kabla halijapelekwa katika kamati za Bunge na
kushauriwa kwamba tozo hilo linaweza kufanyika kwa lengo la kukuza
uchumi hasa maeneo ya vijijini.
“Tathmini zote zimefanyika kikamilifu na
baadae suala hilo likafikishwa Bungeni ambapo pia napo lilikubalika...
inawezekana watu wanalalamika lakini ngazi zote suala hilo lilipopita
lilikubalika na ikaonekana ni sawa kutozwa sh 1,000 kwa kila kadi ya
simu” alisema.
Alisema kutokana na hilo kwa kutwa nzima
kadi ya simu itatozwa Sh 33.35 au Sh 100 kwa siku tatu ambapo serikali
inaangalia utaratibu mzuri ambao hautamuumiza mtumiaji wa simu.
Dk Mgimwa alisema fedha hizo
zitakazokusanywa zitaongeza upatikanaji wa maji vijijini, umeme pamoja
na kuboresha miundombinu katika maeneo ya vijijini.
Habari Leo
MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA BAADA YA KUMTUPA MTOTO WAKE CHOONI
Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni.
Tukio
hilo lilitokea Juni 14, Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto
waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo.
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
Ameongeza
kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo
tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
Rukia
Haruna (31) akitolewa nje na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje
ya Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela
Mwendesha
Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya
Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia
Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume
cha kifungu 218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.
Na Mbeya yetu
PREZZO AMPONDA DIAMOND.
Majigambo
ya Diamond kwenye vyombo vya habari kabla ya Tamasha la Matumaini
kufanyika kuhusu kumgalagaza Prezzo kwenye show hiyo hayajampendeza
Rapcellency na sasa ameamua kujibu.
Prezzo ambaye jina lake halisi ni Jackson
Makini alianza kwa kuweka picha ya gazeti inayowaonesha akiwa na
Diamond kwenye habari iliyohusu tamasha hilo na kuandika ‘Hahahaha
#DomoSeriously????
Rapper huyo hakuishia hapo aliweka picha
nyingine ya Diamond na kuandika: “U talkin money or u talkin nonsense au
anashindana na ndovu kun***a?
Mwisho alimalizia kwa kujibu tweet ya mtu
mmoja aliyemwambia kuwa huyo ni Diamond kwa kuandika: Unfortunately
only “diamonds” I know is the ones on ma neck fam.”
TANZANIA YAMJIBU RAIS KAGAME....YADAI IPO TAYARI KWA LOLOTE NA AKITHUBUTU ITAMCHAPA KAMA MTOTO
Kauli hiyo ya kwanza nzito imetolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa kufuatia taarifa ya matamshi makali yanayodaiwa kutolewa na Rais Paul Kagame wa Rwanda, dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na kutishia kuishambulia Tanzania.
Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa wizara hiyo, Mkumbwa Ally, alisema ingawa Serikali ya Tanzania hadi sasa inajua haina ugomvi wowote na Rwanda, lakini amekiri kuwapo kwa kile alichokiita ‘kupishana lugha’ kwa Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame.
Mkumbwa alikiri Serikali ya Tanzania kunasa matamshi yanayodaiwa kutolewa na Rais Kagame katika moja ya hotuba zake aliyoitoa Juni 30, nchini kwake wakati akihutubia katika hafla moja ya vijana.
Kwa mujibu wa hotuba hiyo, ambayo kwa wiki sasa imesambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii, Kagame anadaiwa kusikika akitoa matamshi ya vitisho dhidi ya Rais Kikwete, kwamba anamsubiri katika wakati aujuao na kumchapa.
Baadhi ya maneno yanayodaiwa Rais Kagame aliwaambia vijana waliokutana katika mkutano wao uliojulikana kama ‘Youth Konnect’ na kufadhiliwa na mke wake, Janet Kagame, yanasema: “Huyu mtu mliyemsikia akiwa upande wa Interahamwe na FDLR na akashauri majadiliano….majadiliano?”
Aidha, Kagame anadaiwa kusema kuwa hatakuwa tayari kujadili jambo hilo, isipokuwa atamsubiri Rais Kikwete sehemu muafaka na ‘kumtandika’.
“Sitapoteza muda wangu kumjibu Kikwete, inajulikana maana kuna mahali hataweza kuvuka…haiwezekani,” alikaririwa akisema Rais Kagame, akilenga kumtisha Rais Kikwete.
Mbali na Kagame, baadhi ya viongozi kadhaa wa serikali ya Rwanda wamekuwa wakimshambulia Rais Kikwete wakimpachika majina ya kejeli ya; “Rais mhurumia magaidi, wauaji wa kimbari, mkorofi na mwenye dharau.”
Mkumbwa hata hivyo alisema Serikali ya Tanzania haina sababu ya kuingia katika vita na Rwanda, kwa sababu tu ya ushauri alioutoa Rais Kikwete wa kuitaka ikutane na wapinzani wake wanaoishi ndani ya nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kujadiliana kuhusu amani ya nchi za Maziwa Makuu.
Alisema msimamo wa Tanzania utabaki kuwa uleule wa kuitaka nchi hiyo ikubali kukaa meza moja na wapinzani wake, ili kumaliza migogoro inayoendelea katika nchi hizo za maziwa makuu, ambao unaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa na SADC.
“Unajua mgogoro wa DRC na Rwanda hauwezi kumalizika bila ya nchi hizo kukaa meza moja na wapinzani wao ili kupata suluhu ya kudumu,” alisema Mkumbwa.
Aliwataka Watanzania kuwa watulivu na kuendelea na kazi zao kama kawaida, kwani serikali yao iko makini katika kulinda mipaka yake.
Chanzo cha mzozo Msuguano baina ya nchi hizi mbili ulianza siku chache tu baada ya kumalizika kwa kikao cha viongozi wa nchi za Maziwa Makuu na ambacho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, chini ya uenyekiti wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.
Rais Kikwete wakati akimtaarifu Rais Museveni kile walichokuwa wamekijadili katika kikao hicho kwa vile aliketi kwa muda kwa kuwa alichelewa kuwasili, alisema ni vema serikali za Rwanda na Uganda zifungue mlango wa mazungumzo na waasi wao na akaanza kutaja majina ya vikundi vya uasi vya nchi hiyo vilivyopo nchini DRC.
Habari zinasema kauli ya Rais Kikwete iliungwa mkono na Rais Museveni akisema: “Bila mazungumzo hatutafika popote pale”.
Hata hivyo, matamshi hayo yalijibiwa kwa ukali na serikali ya Rwanda, kiasi cha kumlazimu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kutoa tamko bungeni.
Kwa kauli yake, Membe alisema serikali ilikuwa imeshangazwa na shutuma hizo za Rwanda kwani halikuwa jambo baya kutoa ushauri uliolenga kuleta mapatano na kuepusha umwagaji zaidi wa damu wa wananchi.
Akaongeza kuwa, ilikuwa ni wajibu wa Serikali ya Rwanda kuupokea ama kuukataa, na wala si kutoa maneno ya kejeli na vitisho.
Kauli ya Zitto Akizungumzia kauli hiyo ya vitisho, mwanasiasa machachari hapa nchini na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, alisema ushauri wa Rais Kikwete kwa Rwanda ulikuwa wa busara mno na akashangaa kuona nchi hiyo jirani ikitoa vitisho, kejeli, dharau na ukosefu wa adabu kwa Kikwete.
Katika moja ya tamshi lake alilolitoa jana katika mitandano ya kijamii, Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) alisema Marekani wanaongea na waasi wa kundi la Taliban, hivyo hakuna dhambi kwa Rwanda pia kufanya hivyo.
“Pia kama hutaki ushauri si unakataa tu, sasa kuanza kurushiana maneno ya nini tena? Hutaki ushauri basi.
Maneno ya kila siku ya nini? Tangu Kikwete amesema kule Addis, hajasema tena. Membe (waziri) akajibu Dodoma Tanzania haijasema tena. Kigali inasema mambo haya kila siku kwa ajili ya nini?
“Taliban na Al Qaeda si wale wale? Wale watoto waliozaliwa mwaka 1994 na wakimbizi wa Kihutu waliopo Kongo nao ni wauaji? Tufikiri vizuri mambo haya. Kuna ‘genociders’ wasakwe, wakamatwe wahukumiwe. Kuna watu wana haki kabisa ya kutaka kushiriki kwenye siasa za Rwanda na wanazuiwa, wameshika silaha. Hawa lazima wakae meza moja wakubaliane,” alisema Zitto.
Mwanasiasa huyu alisema kwa sasa serikali za nchi hizo mbili zinatakiwa kuingia katika vita ya kupambana na kuondoa umasikini wa watu wake na si vita ya mtutu wa bunduki.
“Busara itumike kwa viongozi ‘neutral’ kama Uhuru Kenyatta kuwaweka pamoja Kagame na Kikwete wamalize tofauti zao. Haya maneno hayana maana yoyote,” alisema.
Alisema vita haitamuumiza Rais Kagame wala Rais Kikwete na familia zao, bali itaumiza wananchi wa kawaida wa mikoa ya Kagera na Kigoma na mikoa ya mpakani ya Rwanda.
“Vita itaturudisha nyuma sana kwenye juhudi za maendeleo. Vita itazima harakati za kujenga demokrasia nchini. Busara itumike tu,” alisema Zitto.
Tanzania Daima
Subscribe to:
Posts (Atom)