News, Events, Entertainment, Sports, Lifestyle, Fashion,politics, Beauty, Inspiration and yes... Gossip!
facebook likes
Saturday, July 6, 2013
Piga kura hapa kumuokoa Nando asitoke kwenye jumba la Big Brother The Chase.
Nando mmoja ya wawakilishi wa Tanzania kwenye jumba la Big brother the chase, wiki hii amekuwa nominated kwenye group la watu ambao wanaoweza kutoka kwenye jumba hilo. Mtu wangu wa nguvu una nguvu na nafasi kubwa ya kumuokoa Nando abakie kwenye jumba lile na aendelee kuiwakilia 254 vizuri. Hapahapa unaposoma hii story bonyeza HAPA na utaweza kupiga kura moja kwa moja na utamuokoa Nando wiki hii na pia kama ni bahati yako unaweza kushinda zawadi kutoka DSTV.
Usajili unaomiliki Headlines NBA !
Mchezaji
wa Los Angeles Lakers Dwight Howard hatimaye amefikia maamuzi ya timu
atakayoichezea baada ya kuwa kwenye hali ya utata kwa muda mrefu .
Howard ameamua kujiunga na Houston Rockets ambayo ilikuwa moja ya timu
tano zilizokuwa zinataka kumsajili.
Howard alijiunga na Lakers akitokea Orlando Magic msimu uliopita
ambapo alicheza Lakers kwa mkataba mfupi huku akiwa na uchaguzi wa
kusajiliwa na timu nyingine kwa muda mrefu .
Los Angeles Lakers walimtumia nyota wake Kobe Bryant kumshawishi
Howard kubakia na Lakers lakini mchezaji huyo alivutiwa na Houston
Rockets ambayo ilimuahidi kusajili wachezaji wengine nyota ambao wataipa
timu hiyo nafasi ya kuwania ubingwa.
Timu nyingine zilizokuwa zinamsaka Dwight Howard ni Dallas Mavericks,Golden State Warriors na Brooklyn Nets .
Howard amesaini mkataba wa miaka mitano na timu hiyo ambapo ataungana
na nyota wengine kama Jeremy Lin na James Harden huku Wakitarajia
kumuongeza Josh Smith toka Atlanta Hawks kuongeza nguvu.
Picha za Mtanzania @Wakazi akiwa Airport Dar kuelekea South Afrika kufanya show BBA kesho @BigBroAfrica
SH. 500/- SASA ITAKUWA SARAFU BADALA YA NOTI ILI KUIFANYA ISICHAKAE HARAKA
KUTOKANA na kuchakaa haraka kwa noti ya shilingi 500 na kiwango chake kudumu kwenye mzunguko kwa miezi sita tu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema inatarajia kubadili noti hiyo na kuwa ya sarafu.
Akizungumza na gazeti la Tanzania Daima juzi kwenye viwanja vya maonesho ya kimataifa ya biashara, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Abdul Dollah, alisema mabadiliko hayo yatafanyika hivi karibuni na sarafu hiyo itadumu kwenye mzunguuko kwa zaidi ya miaka 20 huku ikiwa na ubora wake.
Dollah alitaja sababu nyingine ya uchakavu huo ni kutokana na noti hiyo kushikwa na watu wengi kwenye mzunguko huku baadhi yao wakishindwa kuzihifadhi vizuri:
“Tofauti na noti nyingine kama vile zile za sh 5,000 na 10,000 hizi utakuta mara nyingi uchakavu wake si kama ule wa sh 500 kwa sababu noti hizi watumiaji wake wengi ni wale wenye akaunti benki.”
WAZIRI MAGUFULI ATAMANI KUWA RAIS WA TANZANIA......ANADAI KWAMBA YUPO TAYARI KUGOMBEA MWAKA 2015 ENDAPO ATAKIDHI MASHARTI
Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang’anyiro hicho.
Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos’, muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali.
Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015.
Licha ya kauli hiyo kusababisha minong’ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo.
Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge.
Alimshutumu hadharani aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa wilayani Mbogwe, Gervas Stephano, kuwa hana shukrani.
Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kuendelea na wadhifa huo.
“Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani…mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro…hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda…lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri,” alisema Dk. Magufuli.
“Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo…na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh. 3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana,” alisema.
Baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakilitaja mara kwa mara jina la Waziri Magufuli miongoni mwa watu wanaodhaniwa kutaka kugombea nafasi ya urais wa Tanzania mwaka 2015, ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha uvumi huo.
Mbali na Dk. Magufuli, wengine ndani ya CCM wanaotajwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anajiita mtaji wa urais; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ushirikiano wa Kimataifa –CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.
Nipashe:
OFFICIAL DSTV BIG BROTHER PARTY AT NYUMBANI LOUNGE
DSTV
pamoja na AIRTEL wanakuletea special Viewing party ya Big Brother
Eviction Show Kila Jumapili ndani ya NYUMBANI LOUNGE kuanzia saa mbili
usiku. Wiki hii Ndani ya Big Brother Rapper Mtanzania WAKAZI
atatumbuiza.
MWANACHUO WA MWAKA WA KWANZA ALAANI KITENDO CHA KUPIGWA "EXILE" NA MADENTI WENZIE
Hali imekuwa ni tofauti kidogo kwa mwanafunzi wa chuo kimoja hapa nchini ambaye yuko mwaka wa kwanza na anategemea kuingia mwaka wa pili.
Akiongea na mtandao huu kwa sharti la kutotajwa jina , mwanafunzi huyo amefunguka na kudai kuwa Exile imemuathiri sana kisaikolojia.Imemfanya aishi kama mtumwa huku taaluma yake ikiyumba kwa kasi.
Hili ni simulizi la mwanafunzi huyo:
"Maisha ya shule yana changamoto nyingi sana.Kwa mtu yeyote ambaye ni mcha mungu ni lazima itamuwia vigumu sana kukabiliana na hali hii.
"Nasema hivi kwa sababu ndani ya hosteli huwa tunaishi watu tofauti wenye malezi tofauti.Kasheshe ni kwetu sisi first year...
"Mazingira kwetu ni mageni na ndani ya hosteli tunaishi na mabraza wa miaka ya juu wenye wapenzi wao hapo hapo chuoni ambao huwaleta vyumbani na wakati mwngine hulala nao.
"Wanapokuja na wapenzi wao vyumbani ni lazima uwapishe wafanye mambo yao.Na ukiwapisha maana yake utoke kwa zaidi ya masaa matatu mpaka matano
"Ndani ya chumba changu tulikuwa tunaishi watatu, mmoja mwaka wa pili, mwingine wa tatu na mimi mwaka wa kwanza.Wote hao walikuwa na wapenzi wao hapo hapo chuoni.
"Siku zote za wikiendi walikuwa wamezigawana.Mmmoja ilikuwa ni jumamosi na mwingine jumapili.Yaani kwa kifupi ni kwamba sikuwa na uhuru wa kukaa chumbani siku za wikiendi na wakati mwingine hata siku za wiki.
"Nimeamua niwe muwazi maana hali hii imekuwa ni kero kwangu na imekuwa ikiniathiri sana kisaikilojia na kusababisha taaluma yangu iyumbe nikilinganisha na nilipokuwa naanza.
"Naomba nitoe ombi kwa wanafunzi wenzangu.Sote tuko vyuoni kutafuta maisha na zile hosteli tunazilipia kwa gharama sawa.Kwa nini umsumbue mwenzako wakati gesti zipo?..Yangu ni hayo tu"
AJALI MBAYA YA BASI LA SUMMRY YAUA WATU TISA NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA.
Basi la kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni Iku na kuuwa watu tisa na kujeruhi wengine hamsini na tatu.
Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa
sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 basi hilo lilipokuwa likitokea mjini
Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani Katavi likiwa na abiri waliokuwa
wametoka Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi
Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali hiyo ilihusisha basi aina ya
Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya kampuni ya Sumry lililokuwa
likiendesha na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane maarufu
kwa jina la Ntungu.
Alisema basi hilo lilipofika katika
daraja hilo lenye kona kali na mteremko dereva wake alishindwa kulimudu
na kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma kupanda juu ya
ukingo na kutumbukia mtoni ambapo dereva wa basi hilo aliweza kutoka na
kukimbilia kusikojulikana
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu
Rutengwe alitoa rambi rambi kwa wafiwa wote na kuwapa pole wahanga wa
ajali hiyo mbaya kutokea tangu mkoa huo uanze.
HABARI KWA HISANI YA http://lukwangule.blogspot.com
PICHA ZA SIKU: MASHINDANO YA MAGARI YA GHARAMA YASIYO RASMI YA WACHEZAJI WA MAN UNITED: ANDERSON KIBOKO AINGIA MAZOEZINI NA GARI LA MILLION 286
Anderson akiingia na gari yake aina ya Mercedez yenye thamani ya £168,395
Leo asubuhi wachezaji wa Manchester United walikuwa na mashindano yasiyo rasmi ya kuonyesha magari yao ya thamani wakati wakiwasili kwenye uwanja wao wa mazoezi AON Carrington. Mchezaji wa kibrazil Anderson pamoja na kutokuwa mmoja ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi sana na United - yeye ndio alikuwa mchezaji aliyekuja na gari la thamani zaidi Mercedez ambalo linauzwa kiasi cha millioni 286,271,500 za kitanzania.
Rio Ferdinand — Jaguar XJ Portfolio (£70,385)
Wayne Rooney — Range Rover Sport Autobiography (£84,895)
Nemanja Vidic — Mercedes M Class (£47,385)
Ryan Giggs — Range Rover Sport Autobiography (£98,395)
Phil Neville — Porsche Cayenne (£86,895)
Rafael and Fabio da Silva — Chevrolet Captiva (£32,000)
Michael Carrick — Mercedes M Class (£47,386)
Ashley Young — Range Rover Sport Autobiography (£68,995)
Alex Buttner — Chevrolet Camaro Coupe (36,785)
Msiba wa makeup Artist maarufu Nigeria
Waliokaribu na familia yake wamesema matatizo yaliambatana na blood pressure pamoja na BP ambapo alifariki asubuhi ya July 4 2013.. #R.I.P
HILI NDO GARI LA MBAO LILILO TENGENEZWA TANZANIA
Naibu
waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu mwenye suti akipewa
maelezo na afisa wa maliasili juu ya gari lililotengenezwa kwa miti
ambalo linawavutia wengi bandani hapo Simba kivutio cha banda (PICHA NA TULIZO KILAGA WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)
…………………………………………………………….
Hussein Makame-MAELEZO
GARI ya
mbao iliyobuniwa na mkazi wa kijiji cha Nyololo mkaoni Iringa, Keneth
Mwangoka imeokoa shilingi Bilioni moja kwa mwaka kwa kuhamasisha
kuhifadhi mazingira katika msitu wa Sao Hill ulioko mkoani humo.
Akizungumza
na MAELEZO katika viwanja vya Maonesho ya 37 ya Sabasaba jijini Dar es
Salaam jana, Afisa Misitu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka Msitu
wa Sao Hill mkoani Iringa, Fidelis Mwanalikungu alisema gari hiyo
ilibuniwa kwa kushirikiana na Kikundi cha Sanaa cha Imehe kilichopo
katika kijiji cha Nyololo.
Alisema
kikundi hicho kwa kutumia gari hiyo ambayo huvutia watu kuiangalia,
kinaeleimisha vijini 58 vinavyozunguka msitu wa Sao Hill kudhibiti
matumizi ya moto unawashwa na wakulima wakati wa kuandaa mashamba yao
kwa ajili ya kilimo.
Alifafanua
kuwa uhamasishaji huo umefanikiwa kupunguza moto kutoka matukio 143
yaliyokuwa yanasababisha hekta za misitu 500 hadi 1000 kwa mwaka hadi
kufikia matukiio manne tu kwa mwaka yaliyounguza hekta 17 za misitu.
“Ukiweka
hizo hekta 500 hadi 1,000 katika thamani ya fedha unakuta tulikuwa
tunapoteza kuanzia Milioni 840 mpaka Bilioni moja kwa mwaka kutokana na
kuungua kwa msitiu huo, sasa hii ni hasara kubwa” alisema Mwanalikungu.
Alisema
kutokana na elimu inayotolewa kushirikisha kikundi hicho, wameweza
kuhifadhi zingira ya msitu huo wa asili wa Serikali, vyanzo vya maji na
kuhifadhi mazingira ya vijiji hivyo.
Aliongeza
kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2009 uliobaini kuwa kutoka
mwaka 2010 kurudi nyuma miaka 11 kulikuwa kuna matukio mengi ya moto
yenye wastani wa matukio 143 kwa mwaka.
“Ilipofika
mwaka 2011 tukaangalia ni mikakati gani tunaweza kuichukua kwa
kuwashirikisha wanavijiji, ndipo tukagundua wazo la kusema tukiwa na
gari kama hili linalovutia watu, tukaweka mabango ya kuelimisha tunaweza
kufikisha ujumbe kwa urahisi zaidi” alisema Mwanalikungu.
Akizungumzia gari hiyo, Keneth Mwangoka gari hiyo aina ya Toyota Hiace aliinunua
kutoka kwa mtu ambaye alitaka kuiuza kama chuma chakavu na
aliitengeneza ili iweze kusaidia katika kuwavutia wanajiji na kupata
njia ya kuwapata kwa urahisia wanakijiji a kufikisha ujumbe.
Mwangoka
ambaye ni fundi wa gari hiyo, alisema gari hiyo ina injini ya Toyota
1S, robu tatu ya vitu vilivyotengeneza ni mbao na inatumia mafuta lita
moja kwa kilomita nane.
ALIYEFUNGWA PAMOJA NA MANDELA AMTEMBELEA MANDELA HOSPITALINI KUMJULIA HALI
BAADA YA JOYCE KIRIA KUSHAULIWA AMWAMBIE MUMEWE AACHANE NA SIASA na Hii ndo kauli na MSIMAMO wake kuhusiana na USHAURI HUO
Hapa kuna swala nahitaji kuliweka sawa, naamini tutaelewana fans zangu wote.
My Hubby Henry Kilewo.
My Hubby Henry Kilewo akiwa katika shughuli zake za kisiasa.
Nimeolewa na mwanasiasa, mume wangu Henry Kilewo ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Kinondoni, Ila mimi si mwanasiasa(nahudumia watu wote wenye vyama na wasio na vyama).
Our Wedding Day, Nikila kiapo, "KWA TABU NA RAHA"
Muda nakubali kuolewa naye nilifahamu fika kuwa yeye ni mwanasiasa, Ila nitamsupport mume wangu kwa kazi yake aliyoichagua, siwezi kumwambia AACHE SIASA, Hilo kwa kweli HALIWEZEKANI, Hata yeye hajawahi hata siku moja kuniingilia katika kazi yangu ya kutetea haki za wanawake na maendeleo ya wanawake kwa ujumla(WANAWAKELIVE) na kuniambia niiache.
Hubby Henry Kilewo kikazi zaidi.
Ila nina swali la kuuliza hapa "KILA MTU ANAPOPATA TATIZO KATIKA KAZI YAKE ANATAKIWA KUIACHA???" Mfano Daktari akipata tatizo katika kazi yake aache? Ama Mwalimu ama mtu yoyote yule kwa kazi anayoifanya akipata changamoto anatakiwa kuacha????
My family, Hubby Henry With Our Boys, Lincon na Linston.
source-http://www.joycekiria.com/
Hiki ndiyo kitu usichokijua kuhusu mchumba wa Mabeste ambaye anatarajia kupata mtoto na Mabeste hivi karibuni.
Kama hii ilikupita mtu wangu wa nguvu basi nakupa nafasi ya ujua kwamba msanii Mabeste hivi karibuni atakuwa baba na mchumba wake anaitwa Lisa William. Mabeste ambaye watu wengi wamemjua kupitia ngoma yake “Baadaye sana” na baadaye kufanya video ambayo pia ilifanya vizuri. Lisa William ambaye pia alikuwa video model wa ngoma ya “Sirudi tena” ya Mabeste anatarajiwa kujifungua hivi karibuni na pamoja kutengeneza familia na Mabeste.
Nakupa nafasi ya kuangalia video ya Sirudi tena umuone mama kijacho wa mtoto wa Mabeste akiwa kazini na baba kijacho wake Mabeste wa B Hits Music Group.
Kuwa wa kwanza kuona kionjo cha reality show ya Wema Sepetu.
Wema Sepetu alitangaza kwamba anaandaa reality show yake chini ya kampuni anayoimiliki “Endless Fame”. Muda umefika wa kuanza kuonyesha hiyo show yenyewe na Wema ameshatoa teaser au kionjo cha reality show hiyo ambayo inaonyesha baadhi ya vitu vinavyohusika kwenye show hiyo. Kwenye hii teaser inamuonyesha Wema anazungumzia kazi, mahusiano na katajwa Diamond humo,ziara za Wema na maisha ya nyumbani.
MTANGAZAJI DIDA SHAIBU (WA KIPNIDI CHA MITIKISIKO YA PWANI) AOLEWA NA SASA NI MRS EZDEN JUMANNE.
Superman Dwight Howard kuitosa L.A Lakers?
Dwight Howard mchezaji wa ligi ya NBA nchini marekani kwenye timu ya Los Angels Lakers akiwa na mkali mwezake kama Kobe Brayant, inasemekana anataihama timu hiyo hivi karibuni. Dwight Howard ambaye aliwahi kutembelea Tanzania na kutoa misaada kwenye shule ya sekondari Kipok huko Arusha mbele ya waziri mkuu kwa wakati hule mheshimiwa Edward Lowassa, alitokea timu ya Orlando Magic msimu uliopita na kujiunga na Lakers ili kuunganisha nguvu na Kobe, lakini wamepata matokeo mabaya sana msimu huu ulioisha. Mategemeo makubwa ya washabiki wa Lakers ilikuwa ni kumuona Howard akitengeneza pacha na Kobe kama ilivyokuwa kwa Kobe na mkali mwingine aliyestaafu Shaq Oneil.
DWIGHT HOWARD AKIMZAWADI JEZI YAKE RAIS KIKWETE IKULU YA DAR ES SALAAM
Tetesi zinasema kwamba huenda Dwight Howard akahamia
Huston Rockets ambapo kuna wakali wengine kama James Harden. Kama
akihama litakuwa pigo kubwa sana Lakers kwasababu Howard atakuwa
ameitumikia timu hiyo kwa msimu mmoja tu.Kwa mujibu wa mtandao wa
kuaminika wa NBA ambao umeongea na wakala wa mchezaji huyu, amesema
kwamba mteja wake bado hajafanya maamuzi wapi pakwenda lakini atatoa
maamuzi yake hivi karibuni.
DWIGHT HOWARD AKIKABIDHI MSAADA WA MILLIONI 90 HUKO ARUSHA
DWIGHT HOWARD AKIWA NA MHE LOWASSADWIGHT HOWARD AKIPAMBANA NA HASHEEM THABEET UWANJANI
DWIGHT HOWARD NA KOBE BRAYANT
Umezisikia taarifa za Rais Kikwete kuwa refa wa Simba na Yanga jumapili hii?
Naona hii ni historia kabisa aisee….. yani Rais Jakaya Kikwete anaweza hata kuingizwa kwenye kitabu cha kumbukumbu za dunia kwa kukubali mwaliko wa kuwa refa na kuchezesha mechi ya Wabunge wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania wa timu za Simba na Yanga jumapili July 7 2013.
Taarifa ambayo nimepewa na Global Publishers ambao ndio waandaaji, ni kwamba Rais amekubali kuwa refa kwenye Tamasha la Matumaini litakalofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambalo sehemu ya mapato yake yatasaidia elimu Tanzania.
Ni mara ngapi tunamuona President wetu kwenye sehemu rasmirasmi akiwa mgeni rasmi? ni mara ngapi tunatamani kuona upande wake wa pili kwenye ishu kama hizi? basi Jumapili hii itakua burudani na pia vichekesho… yani ukijaribu kutengeneza picha President na umri wake, na umbo lake, na cheo chake alafu apulize filimbi?????
Yani anakuwa refa na jezi zake kabisa…. na tumeshamzoea siku zote huwa anatokelezea hivi yani….
Subscribe to:
Posts (Atom)