facebook likes

Tuesday, July 9, 2013

"JACK WOLPER ANATAFUTA UMAARUFU KUPITIA JINA LANGU....KAMA SANAA IMEMSHINDA BASI AKAJIUZE AU AKAUZE VIPODOZI"...BABY MADAHA




MWIGIZAJI wa kike na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Baby Madaha Joseph amemshukia mwigizaji mwenzake wa kike Jack Wolper kwa kudai kuwa amekuwa akitumia vyombo vya habari kumsema na baadae kujifanya anamuomba msamaha huku hana dhamira ya kweli.

Akiongea na FC , msanii huyo amesema kuwa  Jack  Wolper anatumia jina lake ili apande na kuwa Maarufu (nyota ).

“Mimi ni mwanamke mpigaji na ninajua ninachofanya katika maisha yangu...

"Kuna wanawake hawajui misingi ya sanaa.Ni wanawake ambao  wamevamia fani na kutuharibia  sifa  zetu  kama  wasanii..

"Mimi siwezi kugombana na mtu mwenye fani moja ,tena  ya kubebwa . Jack hana cha kufanya akifeli kuigiza labda arudie kazi yake ya kuuza vipodozi...Atafanya nini kingine hapa mjini zaidi  ya  kujiuza?,”alisema Baby Madaha  na  kuongeza:

“Jack anataka kukiki kwa kunichafulia jina langu, lakini mimi ni Star mwenye vision na najua nafanya nini katika Industry..

"Mimi ni kiongozi mtarajiwa .Nategemewa niongoze watu , sasa nikianza kugombana na watu itaniharibia  ndoto zangu za kisiasa,” 

HUYO NDO "MELLIS EDWARD" ALIYEKAMTWA NA MADAWA YA KULEVYA AKIWA NA "AGNESS MASOGANGE


Picha  ya  Mrembo Mellis Edward  aliyedakwa  na  madawa  ya  kulevya  Afrika  kusini  akiwa  na  Agness Masogange
Mellis Edward
Inahisiwa kuwa  huyu mwanamke wa pili aliyetajwa na Kamanda Nzowa kwa jina la “Melisa Edward”  ni mdogo wake na Agnes ambaye katika akaunti ya facebook anayo tumia jina la (MELLIS EDWARD) , Agnes amemuweka katika orodha ya family kama ‘sister’ katika akaunti yake ya Facebook.
 Kamanda  Gofrey  Nzowa - Kitengo  cha  Madawa ya Kulevya


 Agness Masogange  akiyahesabu  "MAPESA" yake.Picha  hii aliiweka  siku  chache  zilizopita

AGNESS MASOGANGE AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA AFRIKA KUSINI


  HATIMAYE  wale Wanawake wawili walionaswa  na  madawa ya  kulevya  Afrika  kusini wametambuliwa kuwa  ni  mabinti  wa  KITANZANIA ..

Mabinti  hao  wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza na mwandishi wetu  jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.

Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE)  ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.

Jumapili iliyopita mtandao huu  ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.

Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.

Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.

Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi. Tukio hilo linatoka takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.

Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.

Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.

Pinda alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.
 

Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.

Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani.

Melezo Kwa hisani ya Nipashe.

NANDO NA FEZA KESSY WAENDELEA KUPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA NDANI YA BIG BROTHER......HAKUNA ALIYEINGIA KIKAANGONI


 
Wiki hii Watanzania na mashabiki wa shindano la Big Brother Africa hawana haja ya kuwa wasiwasi ya kuwaokoa washiriki wao kwakuwa Nando na Feza Kessy wako safe. 



Kilichobaki ni kuvuta tu viti virefu na kuendelea na bata huku tukiwaangalia wengine wakihaha kuokoa washiriki wao.



Hata hivyo Evictions ya wiki hii inatarajiwa kuwa ya aina yake tangu show ianze hasa kwakuwa waliotajwa kuondoka ni washiriki ngangari.

 Ni nani kati ya Cleo, Natasha, Pokello, Selly, Melvin na Annabel anayeweza kubwaga manyanga kwenye mchezo huo wa ‘kufukuzana’? Afrika itaamua.

UGOMVI WA NDOA WASABABISHA MWANAMKE AVAMIWE NA KUKATWA MIKONO YAKE



Mwanamke mmoja Sumayi Girandi mkazi wa kijiji cha Kunzugu wilayani Bunda amepoteza vidole vitatu vya mkono wa kulia na kiganja cha mkono wa kushoto kukatwa baada kushambuliwa kwa mapanga na watu wasiojulikana kisa kikidaiwa kuwa kutaka kunyang’anywa mali zake.

Uhodari wa mama huyo wa kutafuta mafanikio ya familia yake hasa baada ya kutengana na mume wake umeishia hapo baada ya watu wasiojulikana kumvamia nyumbani kwake na kumshambulia kwa mapanga na kisha  wakamkata kiganja cha mkono wa kushoto na kuanguka.


Kwa sasa Sumayi Girandi anatibiwa katika Hospitali teule ya wilaya.
Vitendo vya kujeruhi na kuua wanawake mkoani Mara kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya ndugu kutaka kuwanyang’anya bado vinaendelea.
Katika tukio lingine wilayani Bunda dereva mmoja wa pikipiki ameuawa na watu wasiojulikana ambapo taarifa zinasema kuwa kabla ya kuuawa kwa dereva huyo wa bodaboda inadaiwa alikodiwa na watu wawili.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mara Ferdinand Mtui amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na tayari watu wanne wamekamatwa wakiwemo watu wanaotuhumiwa kumkatakata mapanga mwanamke Sumayi Girandi.
Emmanuel Amas, TBC Mara.

GENEVIEVE AKABIDHI JUMBA KWA WAZAZI WAKE



ZAENI matunda mema! Ndivyo wanavyoweza kusema wazazi wa mwigizaji maarufu nchini  Genevieve Nnaji baada ya kukabidhiwa nyumba ya kifahari na mtoto wao.

Mioyo ya wazazi hayo iko poa baada ya mwanadada huyo mwenye mvuto kuwahamishia katika jumba la kifahari lililopo eneo la watu maarufu jijini Lagos. Eneo hilo linajulikana kama Lekki.


Awali familia hiyo ilikuwa ikiishi eneo la Egbeda, ambako huishi watu wa kariba ya kawaida. Mama wa msanii huyo ameshagota umri wa miaka 60 na mshua ana miaka 70.


Kwa mujibu wa watu walio karibu na familia hiyo, ilikuwa furaha ya aina yake kwa wazee hao kupata makao mapya yenye hadhi inayostahili.


Genevieve, ameamua kutoa nyumba hiyo kwa wazazi kama sehemu tu ya shukrani. Lakini pia kuwahamishia eneo hilo kutarahisisha upatikanaji wa huduma za msingi kama vile matibabu.Imeripotiwa kuwa baba yake anashindwa kutembea umbali mrefu kwa sababu ana matatizo ya miguu.



Awali wazazi hao walikuwa katika mazingira yasiyoridhisha pamoja na ukweli kwamba binti yao ana uwezo wa kuwatunza.Lakini ukweli wa mambo ni kwamba hii si mara ya kwanza kwa binti huyo kuwakumbuka wazazi wake. Kila kipato chake kinapoongezeka, amekuwa na tabia ya kuboresha mazingira ya familia yake.


Majirani wanasema wazazi wa msanii huyo ni watulivu na wachamungu na kwamba huwezi amini kuwa binti yao ni staa anayekubalika katika mengi ndani na nje ya Afrika

MARIAH CAREY VIATU VYAMUUMBUA



MUIMBAJI mwenye sauti yenye mvuto nchini Marekani Mariah Carey ajikuta katika wakati mgumu na aibu ya aina yake baada ya viatu virefu maarufu kwa jina la 'high heels' kumdodosha wakati akicheza shoo ya video ya nyimbo inayojulikana kwa jina la 'Beautiful'

Viatu virefu ni moja ya vitu ambavyo muimbaji huyo huvipenda lakini huenda hatotaka tena kuvisikia kutokana na hali iliyompata kudondoshwa na viatu hivyo na kumsababishia maumivu makali na hatimaye kukimbizwa hospitali .


Mtu wakaribu wa mwanamuziki huyo aliiambiwa chanzo kimoja cha habari kuwa ajali hiyo ilitokea wakati wa utengenezaji wa video ya remix ya 'Beautiful' iliyokuwa ikiongozwa na muwewake Nick Canno, ndipo muimbaji huyo alidondoka na kusababisha maumivu ya bega.


Wakati huo huo chanzo kingine kiliuambia mtandao wa New York Post kuwa ajali hiyo ilitokana na viatu virefu alivyokuwa amevaa wakati anacheza video hiyo.

JAY Z NA KANYE WEST WANAKUJA NA WATCH THE THRONE PART TWO



Kanye West’s engineer reveals that Jay-Z and Kanye will be back in the studio for another collaboration. Kwa kupitia mtandao wa kijamii wa twitter, Mike Dean ambaye ametengeneza album mpya ya Kanye West “Yeezus” amefunguka kwamba Jay Z na Kanye West wapo tayari kufanya watch the throne part two.
Kama unaweza kukumbuka album ya Watch The Throne ilifinya vizuri sana katika mauzo hasa upande wa itunes.. Album hiyo ilikuwa na nyimbo kali kama Niggas in paris, church in the wild na nyingine nyingi.


OLOYA KUTUA DAR AGOSTI 28


Moses Oloya kazini.

FILAMU ya Klabu za Simba na Yanga kuwania saini ya mshambuliaji anayecheza soka la kulipwa nchini Vietnam katika Klabu ya Thuan Xang Saigon, sasa inaelekea kunoga baada ya mchezaji huyo kuelezwa kuwa atatua jijini Dar, Oktoba 28, mwaka huu.
Taarifa zinaeleza kuwa Simba ambayo ndiyo ilikuwa ya kwanza kumuwania mchezaji huyo, inakamilisha mipango ya kumsajili na ndiyo ambayo imepanga kumleta nchini siku hiyo, lakini Yanga nayo inamhitaji na tayari ilishatuma mtu Vietnam.
Inaelezwa kuwa wakati Simba ikikamilisha mpango huo wa kumleta nchini Agosti 28, tayari Yanga nayo imeanza mipango ya kuwapiga bao wapinzani wao hao, kama ilivyofanya kwa Mbuyu Twite, msimu uliopita.
Chanzo makini cha habari kutoka Simba kimesema kiungo huyo aliyebakiza mkataba wa miezi miwili nchini Vietnam, anasubiri ligi kuu ya nchini humo imalizike kabla ya kutua Msimbazi.
Chanzo hicho kilisema klabu hiyo itafanya jitihada zote ili isimkose kiungo huyo raia wa Uganda, kwani haitaki kushuhudia akitua kwa wapinzani wao hao wa jadi, Yanga.
“Mara baada tu ya mchezaji huyo kuwasili, tutaanza kushughulikia ITC (Hati ya Uhamisho wa Kimataifa) yake ili tuweze kummiliki rasmi,” kilisema chanzo hicho na kuendelea:
“Ligi yao ya Vietnam inamalizika Agosti 27, kisha siku moja baadaye ataondoka kuja huku, tayari ameshaomba release (ruhusa) kwenye klabu yake ili aje nchini kwa ajili ya kukamilisha usajili wake.
“Unajua Yanga wamekuwa wakituingilia katika masuala yetu ya usajili, hivyo tunafanya hivyo ili kukamilisha dili mapema.”
Licha ya kuwepo na taarifa za kukanusha juu ya Yanga kufanya mazungumzo na mchezaji huyo, Championi lina uhakika kuwa kigogo wa Yanga alitua nchini Vietnam wiki ya juzi na kuzungumza naye lakini hawakufikia muafaka, hivyo atakapotua hapa nchini siku hiyo, ndiyo kila kitu kitakuwa wazi.

Massari ft. French Montana - Shisha

M2theP azungumzia tattoo yake ya chozi na mpango wake wa kuchora tattoo ya sura ya marehem Ngwea

Baada ya kuondokewa na kipenzi chake cha karibu (Ngwea), M2thep amesema yuko mbioni kuchora tattoo kubwa yenye sura ya Ngwea mgongoni katika kumkumbuka kwake, na kwasababu alipokuwa nae South Africa mara ya mwisho alimtakia kuwa anataka kuchora tattoo.

"Tattoo ya chozi hii niliichora kwasababu ya kuondokewa na mama yangu mzazi, hii inaashiria nilipoondokewa na mama yangu, then niliweza kuchora tattoo hii ya chozi, yaah nikachora tattoo hii ya chozi, nikachora tattoo ya music mkononi, ambapo mi ni blood ambae napenda sana music, nikachora melody kwenye shingo,then nataka kuchora tattoo kubwa ngongoni yenye picha yake, nadhani itakuwa ndio kumbukumbu yangu kubwa, ambayo ntaichora mgongoni, kichwa kizima cha Albert nitakichora, yaani nategemea hicho kitu kukifanya, yaani ntakapo tulia nadhani, ntakapotulia ntaweza kufanya hicho kitu, kwasababu sasa hivi yenyewe ndio nimeanza ku recover, na natoka toka sasa hivi na vitu vingi vinanihusu studio nini, ila nikipata muda ndio ambacho cha muhimu, yaani hata yeye mwenyewe kwanza kipindi anakuja soth africa alisema mwenyewe anataka kuchora tatto, lakini kwa bahati mbaya mpaka anaondoka hajaweza kuchora hiyo tatto ambayo alikuwa anaitarajia yeye wenyewe kuichora, ambacho mi ndio nitakachokifanya kumuenzi, ntachora tattoo kubwa mgongoni ambayo itakuwa na picha yake" amesema M2thep.

Baada ya kupiga show BBA sasa Wakazi kushoot video South Africa na kampuni mpya ya mtoto wa makamba



Baada ya kufanya show kali siku ya Jumapili ndani ya BBa evection night, Rapper Wakazi sasa anatarajia kushoot video ya wimbo wake unaoitwa "The Touch" nchinu humo (South Africa) akiwa chini ya management ya kampuni inayosimamiwa na mtoto wa Makamba, Thuwein Makamba "Cervon".

"My kid brother Thuwein Makamba is @Wakazi's manager, both are here in J'burg and will shoot Wakazi's  single TOUCH video this week.Thuwein runs a new talent management company called CERVON-be the winner! and @Wakazi is his first artist"

Licha ya statkent hiyo iliyotolewa na dada wa Thuwein "Mwamvita Makamba" kupitia ukurasa wake wa twitter, Wakazi amesema sio tu kampuni hiyo itakuwa ikisimamia kazi zake, bali yeye pia ni patner kwenye kampuni hiyo.

Mtanzania Omary Sykes auwawa kwa kupigwa risasi nchini Marekani


POLISI wametambua mwili wa mwanafunzi wa Howard University aliyeuawa kwenye jaribio la uhalifu Alhamisi usiku. Omar Sykes, 22, na mwanafunzi mwenzake walikuwa  wanatembea maeneo ya 700 block of Fairmont Street NW kabla ya saa 5.30 usiku walipofuatwa na watu wawili. 

Polisi wanaamini kulikuwa na jaribio la uhalifu ila yalitokea mabishano kabla mmoja ya wale watu kutoa bastola na kumuua Sykes. Alifikia mauti kwenye hospitali ya maeneo ya jirani.

“Tunadhani ilikuwa jambo la ghafla na hatuna uhakika kama wanafunzi hao waliibiwa mali yoyote” alisema Kapteni Bob Alder wa kituo cha polisi DC  alipohojiwa na News4. Mwanafunzi mwingine alipigwa na kitako cha bastola na kujeruhiwa kichwani ingawa hana majeraha makubwa. 


“Wanafunzi wengi wamepatwa na hofu ya kutoka na kutembea usiku kwani hali hii inaogopesha sana,” alisema mwanafunzi mmoja alipohojiwa na Megan McGrath kutoka News4.

Maelezo kamili kuhusu watuhumiwa bado hayajapatikana. Kulikuwa na matukio mengi ya kujumuisha watu wakati wa tukio hivyo polisi wanatumaini kuwa haitawia vigumu kwa wahalifu hao kujulikana. Sykes alipenda uandishi na mara ya mwisho aliandika makala kwenye mtandao unaoitwa Our Black Pages  mnamo tarehe 11 Juni. Wasifa wake unaonesha  kwamba alikuwa anasomea Marketing na Public Relations. Mkesha wa sala kwa ajili ya marehemu utafanyika shuleni  kwao Jumamosi kuanzia saa 1 usiku.
 Howard University imetoa maelezo yafuatayo kuhusiana na kifo cha Alhamisi:
“Tuna huzuni kubwa kufuatia kifo cha mmoja wa wanafunzi wetu kilichotokea nje ya shule. Mwanafunzi mwingine alijeruhiwa kwenye tukio hilo na anaendelea na matibabu…. Polisi wa Howard University wanashirikiana polisi wa mji ili kupeleleza tukio hili hatari. Tunawapa pole familia, shule na wale wote walioguswa na tukio hili kwa namna moja au nyingine. Huduma ya ushauri nasaha itapatikana masaa 24 kwa wanafunzi wote watakaohitaji msaada katika kipindi hiki kigumu.
habari kutoka michuzijr blog 

Usajili mwingine ulio-Make Headlines NBA.


Utah Jazz v Atlanta HawksHuku zikiwa zimepita siku mbili tu  baada ya kuhusishwa kwenye usajili wa mchezaji Dwight Howard kwenye timu ya Houston Rockets ambapo jina la Josh Smith lilitajwa kwenye ahadi zilizomvuta Howard kwenye timu ya Houston mchezaji wa Atlanta Hwaks Josh Smith ameripotiwa kujiunga na timu ya Detroit Pistons na sio Houston Rockets kama ilivyotarajiwa na wengi .
Josh mwenye umri wa miaka 27 ambaye alicheza Atlanta Hawks kwa muda wa miaka tisa amesaini kuichezea pistons kwa miaka minne ambapo atalipwa jumla ya dola milioni 56 katika kipindi chote hicho .
hawks.0326 7
Josh ni mmoja kati ya wachezaji wachache walioingia kwneye NBA wakitokea shule ya sekondari tofauti na wachezaji wengine ambao mara nyingi huanzia vyuoni kwenye shindano maarufu la kukuza vipaji vinavyokuja kufanya vizuri kwenye NBA la NCAA ambapo alisajiliwa na Atlanta Hawks akitokea shule ya sekondari ya Oakhill Academy huko Atlanta .
Kwa muda mrefu Josh ambaye anafahamika kwa jina utani la J-Smoove alikuwa mchezaji bora kwenye timu ya Atlanta Hawks na ujio wake ndani ya Detroit utaiongezea nguvu timu hiyo ambapo anatarajiwa kuungana na wachezaji kama Andre Drummond na Gregg Monroe huku Atlanta Hawks alikoondoka akirithiwa na Paul Millsapp ambaye amesajiliwa toka Utah Jazz.

Barcelona wafikia makubaliano ya kumuuza striker huyu.


david_villa_barca
Taarifa zilizoibuka kwenye mitandao kadhaa ya vyombo vya habari nchini Hispania zinadai kuwa Klabu za Fc Barcelona na Atletico Madrid zimefikia makubaliano juu ya mshambuliaji David Villa . Makubaliano haya ambayo ni ya kimsingi yasiyo rasmi yatamshuhudia David Villa akijiunga na Atletico kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni tano ambapo Madrid watalipa euro milioni mbili kwa mkupuo wa kwanza , Euro milioni mbili nyingine endapo Villa atabakia na timu hiyo msimu ujao na ziada ya Euro milioni moja endapo atakuwepo kwa msimu wa pili. Pamoja na mauzo hayo Barca watakuwa na haki ya kuvuna asilimia hasmini ya fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo ya mchezaji huyo endapo Atletico itaamua kumuuza .
david_villa_lujoso04
Villa amekuwa kwenye wakati mgumu ndani ya kikosi cha Barcelona ambapo ameshindwa kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza hali inayomlazimu kwenda mahali kwingine . Villa ana malengo ya kuwemo kwenye kikosi kitakachoiwakilisha Hispania kwenye michuano ya kombe la dunia mwakani huko nchini Brazil hali inayoleta ulazima wa kuondoka kwake ili azidi kumshawishi kocha Vicente Del Bosque kumuweka kwenye mipango yake ya kombe la dunia .
Villa alijiunga na Barca akitokea Valencia misimu mitatu iliyopita ambapo alinunuliwa kwa zaidi ya Euro milioni 30 wakati huo ambapo alifunga mabao 23 kwenye msimu wake wa kwanza lakini amekuwa akishuka kwenye orodha ya washambuliaji wa timu hiyo siku hadi siku.

SABABU TANO ZILIZOWAFANYA CHADEMA WAGOME KUSHIRIKI "KONGAMANO LA AMANI" LINALOANZA KESHO


Ndugu waandishi wa habari,
Tumewaiteni hapa mchana huu kwa dharula, kutokana na kujitokeza kwa jambo moja muhimu sana katika mustakabali wa chama chetu na taifa kwa ujumla. Jambo lenyewe ni hili:

Kwa muda wa siku mbili, kuanzia kesho– tarehe 9 Julai 2013 hadi 10 Julai – kutakuwa na “KONGAMANO LA AMANI” lililoitishwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania – Tanzania Center For Democracy (TCD).

Kongamano hilo linatajadili na kutafakari Amani ya Taifa, litafanyika kwenye hoteli ya White Sands ya jijini Dar es Salaam. Litafuguliwa na Mwenyekiti wa TCD, Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Mheshimiwa James Mbatia na litafungwa na Rais Jakaya Kikwete.

Baadhi washiriki ni pamoja na mawaziri, viongozi wakuu wa vyama vyenye wabunge ambavyo ni wanachama wa TCD – Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), United Democracy Party (UDP), Tanzania Lebour Party (TLP), NCCR- Mageuzi na Chadema.


Aidha, chama cha UPDP nacho kitashiriki mkutano huo kwa niaba ya vyama vingine ambavyo havina wabunge.

Ndugu waandishi wa habari,
Chadema kikiwa mmoja wa wadau wakubwa wa TCD, kimepokea mwaliko wa kutano huo. Hata hivyo, tunapenda kutumia nafasi hii, kupitia kwenu, kuutangazia umma na wote wanaotutakia mema na kulitakia mema taifa, kwamba hatutashiriki mkutano huo kwa sababu zifuatazo:

Kwanza, Mwenyekiti wa TCD, Mheshimiwa Mbatia kwa makusudi amekiuka maazimio ya kikao ya kuteuwa muwezeshaji wa mkutano huo na badala yake akafungamana na CCM kuteuwa watu anaowataka wao.


Pili, Chadema haitashiriki mkutano huo kwa kuwa Amani haijadiliwi. Amani inatengenezwa na kuwapo kwa mazingira ya haki na usawa; na kwamba aliyebobea katika uvunjaji wa haki hizo, ni serikali yenyewe.

Katika mazingira haya, Chadema inaona hakuna umuhimu wa kushiriki kwenye mkutano ambao washiriki ni wale wale wanaotuhumiwa kuvunja haki za binadamu.


Tatu, Amani siyo ya vyama vya siasa pekee yake. Amani inahusisha wadfau mbalimbali wakiwamo viongozi wa kidini, taasisi za kiraia na mashirika yasiokuwa ya kiserikali. Taarifa zilizopo, ni kwamba mkutano huu haukushirikisha viongozi wa kidini, na hivyo, tunadhani kuwa siyo jambo zuri kama kweli tunataka kutafuta amani ya taifa.

Nne, Chadema haitashiriki mkutano huo kwa kuwa aliyepanga, aliyefadhiri na aliyeitisha mkutano huo kwa mgongo wa TCD, ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mizengo Kayanza Peter Pinda, ambaye ndani ya nafasi yake, haonekani kuwa na dhamira ya dhati ya kuwapo amani katika taifa letu.

Ndugu waandishi wa habari;
Ninyi ni mashahidi wa jinsi Waziri Mkuu Pinda alivyo mstari wa mbele katika kuhubiri kauli za chuki, uhasama, uchochezi, ubabe na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini.

 Siyo mara moja wala mbili, Waziri Mkuu Pinda amesikika, tena ndani ya Bunge, akihamasiha vyombo vya usalama kuvunja sheria kwa kupiga, kuteka na kung’oa meno watu wanaotumia haki zao za kikatiba kushinikiza serikali kuchukua hatua dhidi yamaovu.

Tano, Chadema haitashiriki katika mkutano huo kwa kuwa Serikali ya CCM inayofadhiri mkutano huu, imejaa unafiki kwa kuhubiri amani mchana, wakati usiku inachochea uhasama wa kidini, kisiasa na inawagawa Watanzania kwa misingi ya imani za kidini na vyama.
 

Chadema inao ushahidi usio na chembe ya mashaka, kwamba mifarakano mingi inayotokea kwenye jamii, mapigano katika koo mbalimbali, ugomvi wa kugombea ardhi kati ya wakulima na wafugaji, machafuko kwenye mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani, sababisho kuu ni CCM kuvitumia vyombo vya dola, kutaka kukibeba chama hicho.

Tunataka umma utuelewe, kwamba tuna dhamira ya dhati ya kuona Tanzania inakuwa kisiwa cha amani, lakini hatutakubali kushiriki katika vikao ambavyo wanaoviongoza hawana dhamira hiyo.

 Ili amani iweze kupatikana, ni sharti tuwe kuwepo mijadala inayoingia kwenye viini vinavyosababisha amani ikosekane na hatua hiyo ianze kuchukuliwa na ione inachukuliwa na serikali.

Chadema kiko tayari, kufanya kazi ya kutafuta amani na wale wanaopenda demokrasia. Chadema haifanyakazi na wanafiki wa amani.

Imetolewa na:
Benson Singo Kigaila,
Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo,
Dar es Salaam

MKOMBOZI KAFIKA: VING'AMUZI VYA AZAM KUANZA KUSAMBAA KARIBUNI

KAMPUNI YA SSB KUPITIA AZAM WANATARAJIA KULETA KING'AMUZI KIPYA NA CHA BEI POA AMBACHO KITAUZWA TSHS 30,000 NA MALIPO YAKE KWA MWEZI NI TSHS 2000. Kwasasa nasikia kipo kwenye majaribio kwa baadhi.

WANAFUNZI WAAMUA KUKESHA BAA WAKINYWA POMBE MARA BAADA YA WALIMU KUGOMA KUFUNDISHA HUKO KENYA...



 
Wazazi waliofika kuwatafuta watoto wao waliokuwa wametoweka
 
POLISI wa Kenya wamewakamata zaidi ya wanafunzi elfu moja baada ya kupatikana wakiwa walevi mjini Nairobi wikendi hii. Polisi waliendesha msako katika baa anuai na vilabu vya burudani baada ya kupokea malalamishi kwamba watoto wa shule wamekua wakifurika kwenye burudika tangu mgomo wa walimu uanze.

Taarifa zinasema kwa sasa wanafunzi wengi hawako shuleni baada ya waalimu wa Kenya kugoma wakitaka Serikali kuwalipa marupurupu yao kutokana na ahadi iliyotolewa kwao na Serikali mapema miaka ya themanini. Mgomo huo umeingia wiki ya tatu sasa hali iliyofanya wanafunzi kukosa cha kufanya na hivyo kuanza kwenda kwenye vilabu vya burudani nyakati za usiku. Katika kuzima tabia hii polisi mjini Nairobi mwishoni mwa wiki walifanya msako mkali katika mabaa na sehemu za burudani na kuwanasa watoto zaidi ya 1,000. Polisi walianza kuwa na wasiwasI wakati visa vya unyang’anyi vilipoongezeka katika mji mikubwa nchini Kenya

. Wasiwasi ulizidi wakati walalamikaji walipokuwa wakidai kuwa wanaowapora na kuwapiga kabari ni kundi la watoto wanaodhaniwa kuwa ni wa shule. 

Na mabaa na maeneo ya burudani ilipoanza kufurika polisi wakaona ni wakati muafaka wa kuchukua hatua. Polisi sasa wametoa onyo kwa wenye mabaa nchini kenya kuheshimu sheria za biashara. Baada ya wanafunzi kukosa kurudi nyumbani na wengine kuripotiwa kutoroka katika shule zao za mabweni wazazi walifurika katika vituo mbali mbali vya polisi kujua hatma ya watoto wao.
Lakini wengi wa wazazi waliokuwa wamefurika katika kituo cha polisi cha Central jijini Nairobi walielekeza lawama zao kwa mgomo wa sasa wa walimu unaoendelea. Polisi wanasema mtindo huu mpya wa watoto kutoroka madarasani na kuvamia maeneo ya burudani na ma baa sio tatizo la Nairobi pekee bali limeenea katika miji mingi ya Kenya.
Na kabla mambo hayaja haribika zaidi wazazi wanamtaka rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuingilia kati mgomu huo wa walimu kuhusu mishahara na marupurupu mbalimbali.

HIZI NDO JEZI MPYA ZA TOTTENHAM HOTSPUR WAKIWA WANADHAMINIWA NA "HP"


Hali ya taharuki yatanda nchini Misri : NI HUZUNI NA MAJONZI...ANGALIA PICHA ZA MAITI WALIOKUFA VURUGU ZA MISRI


Maafisa wa Afya Misri wamesema takriban watu 42 wameuawa kwa kupigwa risasi mjini Cairo nje ya kambi ya kijeshi ambapo wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi walikua wamekusanyika na wanaamini anazuiliwa hapo. Watu wengine 300 wamejeruhiwa.
Kundi la Muslima Brotherhood limewataka raia wa Misri kuwapinga wale linawaita wanaopokonya raia uhuru na demokrasia. Brotherhood imelaumu jeshi kwa kuwaua raia wake.
Katika kikao na waandishi wa habari, wafuasi hao walimlaani vikali mkuu wa jeshi Abdel Fattah Al-Sisi na kumtaja kama muuaji aliyewashambulia raia wenzake.
Haya yanajiri huku ghasia zikiendelea baada ya kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa rais Mohammed Morsi.
Waandamanaji hao wanasema vikosi maalum viliwafyatua risasi baada ya swala ya fajir huku wengine wakishambuliwa walipokusanyika nje ya makao ambako bwana Morsi anadhaniwa kuzuiliwa wakitaka watawala kumwachilia huru.
Msemaji wa chama cha Muslim brotherhood amesema kuwa idadi ya waliofariki katika ghasia hizo imefikia 30 huku zaidi ya watu 500 wakijeruhiwa.
Lakini katika taarifa yake, jeshi la nchi hiyo limesema kuwa kundi moja la kigaidi lilikuwa likijaribu kuingia katika kambi hiyo na kumuua mwanajeshi mmoja.
Limeongezea zaidi ya watu 200 walitiwa mbaroni wakimiliki silaha kama vile visu.
Duru kutoka wizara ya afya zilisema kuwa afisaa mmoja wa jeshi aliuawa.
Bwana Morsi, aliyekuwa rais wa kwanza wa kiisilamu kuchaguliwa kidemopkrasia Misri, aling'olewa mamlakani na jeshi, siku ya Jumatano baada ya kufanyika maandamano makubwa.
Mmoja wa waandamanaji Mahmud al-Shilli, aliambia shirika la habari la AFP kuwa wanajeshi waliwarushia gesi ya kutoa machozi lakini kikundi cha wanaume waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia ndio waliwafyatulia risasi.
Katika taarifa iliyosomwa kwenye vyombo vya yhabari vya serikali, jeshi lililaumu kikundi cha watu wlaiokuwa wamejihami ambao limesma ni mgaidi waliokuwa na njama ya kuvamia kambi ya jeshi.







MAAJABU ...HUYU ndo MWANAMKE MZEE KULIKO WOTE DUNIANI ALIZALIWA MWAKA 1885 ANA MIAKA 125 NA BADO YU HAI

 
Oldest woman of worldA chinese woman born in 1885 and still alive! -127 year old.

IRENE UWOYA AMWAGIWA MATUSI YAA NGUONI NA MASHABIKI WA BONGO FLEVA BAADA YA KUMFANANISHA 'DIAMOND PLATINUMZ' NA 'MICHAEL JACKSON':

MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya, amelowa mvua ya matusi baada ya kumfananisha mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na aliyekuwa mwanamuziki mkubwa duniani, marehemu Michael Jackson.
Wikiendi iliyopita, Uwoya aliandika kwenye ukurasa wake katika mtandao wa Instagram kuwa msanii huyo anayefanya vizuri katika Bongo Fleva ndiye staa atakayemrithi mkali huyo wa Pop, maandishi ambayo yalizua matusi hayo ya nguoni.
Baadhi ya mashabiki wa mastaa hao walitoa maoni kuwa jambo hilo ni sawa na kufananisha vitu ambavyo havina uwiano hasa ukizingatia Michael Jackson alishafariki dunia Juni 25, 2009.
“Sasa hiyo ni akili gani ya ki…(tusi) kumfananisha mtu aliyeko hai na marehemu?” alihoji Mishish, mmoja wa mashabiki wa Uwoya katika mtandao wa Facebook baada ya ishu hiyo kuwa gumzo mitandaoni.
“Kweli wewe Irene (Uwoya) ni …(tusi) au kwa sababu Diamond amesha…(tusi) ndiyo maana unamsifia kiasi hicho,” aliandika shabiki mwingine kwenye Twitter na kupisha wengine kuendelea kumporomoshea Uwoya matusi ya nguoni

KWA WALE WAPENZI WA KUNYOA VIDUKU,SASA KUNA HII STYLE NYINGINE INAITWA KABANG:

Wabongo wataiga na hii style eti!

SERA YA MAVAZI KWA WANAFUNZI CBE YAONGEZA UFAULU

IMG 9385 599a8
Mhadhiri Msaidia wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Mariam Ally Tambwe akizungumza na mteja aliyetembelea banda la Wizara ya Viwanda na Bishara sehemu ya chuo hicho katika viwanja vya Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Sababasa jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki hii.

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...