Habari zilizopatikana majira ya saa kumi kasoro robo alasiri jana zinafahamisha kuwa, Mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha na mmiliki wa hoteli amepigwa risasi na watu wasiojulikana bado katika eneo la Mijohoroni upande wa kulia (punde tu baada ya Boma Ng’ombe ukitokea Moshi kuelekea Arusha), mchana wa leo, alipokuwa ameitikia wito alioitiwa wa mazungumzo ya kibiashara ya madini.
....SOMA ZAIDI.....
Habari zilizopatikana majira ya saa kumi kasoro robo alasiri jana zinafahamisha kuwa, Mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha na mmiliki wa hoteli amepigwa
risasi na watu wasiojulikana bado katika eneo la Mijohoroni upande wa
kulia (punde tu baada ya Boma Ng’ombe ukitokea Moshi kuelekea Arusha),
mchana wa leo, alipokuwa ameitikia wito alioitiwa wa mazungumzo ya
kibiashara ya madini.
Taarifa zinasema marehemu amepigwa risasi kati ya 6 - 12 katika paji la uso na maeneo mengine ya mwilini.
Mtu mmoja aliyewahi kufika kwenye eneo la tukio baada ya kusikia milio ya risasi anasema alimkuta mtu mmoja wa fanani ya Kimasai ambaye alishuhudia tukio zima na kumsimulia kuwa aliona watu
wanapiga risasi na kisha wakaondoka kwa pikipiki kuelekea porini huku akielekeza mkono kuonesha walikokimbilia. .
No comments:
Post a Comment