facebook likes

Wednesday, July 17, 2013

Mzee Magali wa Bongo Movie aingia kwenye Bongo Flava



Surprise zinaendelea na sasa inakuja bombshell nyingine. Kwa mujibu wa mtangazaji wa Take One ya Clouds TV, Zamaradi Mketema, muigizaji wa filamu nchini maarufu kama Mzee Magali ametupa karata yake kwenye muziki.

Paundi Milioni 40 zitatosha kumng’oa huyu jamaa Liverpool.


Wakala Pere Guardiola ambaye ni mdogo wa Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola ameziambia klabu za Real Madrid na Arsenal kuwa ofa ya paundi milioni 40 itatosha kumtoa mshambuliaji huyo Liverpool .
Pere Guardiola amesema kuwa ana imani kuwa ofa ya paundi milioni 40 haitakutana na pingamizi lolote toka Liverpool na hivyo kufanya kazi ya kumuuza mchezaji huyo (Suarez) kuwa nyepesi .

Klabu ya Arsenal imepeleka ofa mbili za paundi milioni 30 na paundi milioni 35 kwa ajili ya Suarez ambapo Liverpool imezikataa ofa hizo . Klabu hiyo yenye maskani yake huko Anfield haiko tayari kumuuza Suarez kwenda klabu nyingine ya England na inasemekana kuwa inasubiri ofa toka kwa Real Madrid ambayo ni moja ya timu zinazotaka kumsajili Suarez.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay Suarez amesema kuwa anataka kuondoka Liverpool ambapo ametaja kucheza Ligi ya mabingwa na kuandamwa na vyombo vya habari kama sababu za kutaka kuondoka .54-liverpoolsuarez-paw

Baada ya Jay Z na P.Diddy kufanya vizuri..rapper mwingine mkubwa aingia kwenye dunia ya fashion na brand ya nguo zake

Kama ulikua hujui mtu wangu wa nguvu chukua hii, lebo ya nguo Sean John ambayo inamilikiwa na P.Diddy inachangia kiasi kikubwa sana cha utajiri wa jamaa huyu ambaye kwa sasa amehamia kwenye Tv channel akiwa na channel yake inayoitwa Revolt. Rapper mwingine ambaye amefaidika sana na biashara ya mavazi ni Jay Z alivyokuwa anamiliki Roca Wear kabla hajaiuza. Rapper mwingine mkubwa ambaye kwa sasa yupo kwenye harakati za uwekezaji sana ni Nas. Hivi karibuni na ameanzisha lebo yake ya mavazi ya kiume na kuipa jina la HSTRY, kama ulikuwa haujapata story nyingine ya Nas ni kwamba yuko mbioni kufungua duka lake la sneakers pia. Kwenye brand yake ya mavazi Nas unaambiwa ameshiriki kwenye ku-design mavazi hayo ambayo yana material tofauti lakini ngozi imechukua nafasi kubwa sana hasa kwenye makoti. Tarehe moja mwezi wa nane ndiyo siku ambayo mavazi hayo yataingia sokoni.Hizi picha ni baadhi ya nguo za HSTRY ya Nas.


wenn33606711-e1332766608260
look4
look3
look2
look1
1

Kuwa wa kwanza kujua ratiba ya “Magna Carta World Tour” ya Jay Z


jay-z-wireless-festival




















Mtu wangu wa nguvu najua umesha enjoy kusikiliza album mpya ya Jay Z ambayo imefika Platinum baada ya wiki moja tangu aitoe. Hivi sasa Jay Z ambaye ni baba wa mtoto Blue Ivy, ametoa ratiba ya world tour yake. Hivi sasa Jay Z  ametoa ratiba ya tour hiyo kwenye bara la Ulaya. Jay Z anatarajiwa kufanya show kwenye majiji kama Manchester,Paris.Oslo na sehemu nyingine. Jay Z ana show zaido ya 20 barani Ulaya na hii ndiyo ratiba yenyewe jinsi show zitakavyoenda na bado tunasubiri kwa hamu kama Jay Z ataileta tour yake Africa hasa Tanzania.
jay-z-europe-tour-475x671 copy
“Magna Carta World Tour” – European Dates
October 3 – Manchester, UK – Manchester Arena
October 4 – Manchester, UK – Manchester Arena
October 6 – Dublin, Ireland – O2 Arena
October 8 – UK, Birmingham NIA Arena
October 10 – London, UK – O2 Arena
October 11 – London, UK – O2 Arena
October 12 – London, UK – O2 Arena
October 14 – London, UK – O2 Arena (Birmingham NIA)
October 15 – London, UK – O2 Arena (Leeds/Newcastle/ Sheffield Arena)
October 17 – Paris, France – Bercy
October 18 – Paris, France – Bercy
October 20 – Zurich, Switzerland – Hallenstadion
October 21 – Antwerp, Belgium – Sportpaleis
October 23 – Oslo, Norway – Spektrum
October 25 – Stockholm, Sweden – Globe
October 27 – Hamburg, Germany – O2 World
October 28 – Cologne, Germany – Lanxess Arena
October 29 – Amsterdam, Netherlands – Ziggo Dome

Breaking News ,Man United yaiambia Chelsea No!!!!!


rooneyMabingwa wa kombe la UEFA Europa League Chelsea The Blues wamekuwa klabu ya kwanza kuwa na maombi rasmi ya kumsajili mshambuliaji Wayne Rooney ambapo Manchester United imekataa ofa ya paundi milioni kumi pamoja na mchezaji mmojawapo kati ya Juan Matta na David Luiz kwa ajili ya mshambuliaji huyo.

Chelsea imekuwa ikifuatilia hali ya Wayne Rooney ambaye amekuwa kwenye wakati mgumu hivo karibuni huku mustakabali wake ukiwa haujapata ufumbuzi . Mshambuliaji huyo hapo jana aliripotiwa na magazeti ya huko England kukerwa na kauli ya kocha wake mpya David Moyes ambaye alisema kuwa Rooney atacheza kama mbadala wa mshambuliaji chaguo la kwanza Robin Van Persie .

Rooney kwa muda mrefu ameonyesha kutofurahishwa na kitendo cha kutopangwa kwenye nafasi anayoipenda ya ushambuliaji wa kati ambapo amekuwa akibadilishwa mara kwa mara kwenye nafasi tofauti kuanzia pembeni hadi nafasi ya kiungo cha kati.
Msimu uliopita Sir Alex Ferguson alitoa taarifa kuwa Wayne amemtaarifu kuwa anataka kuondoka , taarifa ambayo hata hivyo ilikanushwa baadaye . Hata hivyo David Moyes baada ya kusisitiza kuwa Rooney hatouzwa alionekana kwenda mbali kwa kauli aliyoitoa ambapo alisema kuwa hataruhusu mshambuliaji huyo kuonekana mkubwa kuliko klabu nzima ya United.

CHELSEA YATHIBITISHA KUTUMA OFA YA KUMSAJILI WAYNE ROONEY - LAKINI YAKANUSHA KUTAKA KUWATOA AIDHA MATA AU LUIZ KWENYE DILI HILO

Masaa kadhaa baada ya kutoka kwa taarifa kwamba klabu ya Chelsea imetuma ofa ya paundi millioni 10 pamoja na mchezaji mmoja aidha David Luiz au Juan Mata kwa Manchester United ili kumsajili Wayne Rooney, sasa mabingwa hao wa Europ League wamethibitisha kutuma ofa kwa ajili ya kumsaini Rooney.

Lakini pamoja na kuthibitisha kutuma ofa hiyo, Chelsea wamekanusha taarifa kwamba ofa hiyo ilikuwa ni ya kiasi cha fedha pamoja kutoa mchezaji wao mmoja ili kuweza kumsaini Rooney.

Katika taarifa iliyotolewa na mtandao rasmi wa Chelsea - klabu imekiri kwamba jana usiku ilituma ofa kwenda United lakini haikuwa inahusisha mchezaji wao yoyote kuhusishwa na dili hilo.
 

LULU AKABIDHIWA TUZO YAKE YA ZIFF .



Hatimaye Lulu amepokea ile tuzo yake aliyo shinda kweNye ZIFF kule Zanzibar kama msanii bora wa kike katika filamu za kiswahili. Hongera sana Lulu.

BIFU LA DIAMOND NA PREZOO LACHUKUA SURA MPYA HABARI KAMILI HII HAPA



Rapcellency, Prezzo amesema hawezi kumuomba msamaha Diamond kwenye Twitter kwakuwa anaamini hakuna alichomkosea na ni jambo la kitoto.

Akiongea Jana  mchana kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen, kinachoendeshwa Mzazi Willy M. Tuva, Prezzo amesema Diamond ndiye aliyemchokoza baada ya wasanii hao kutumbuiza mwanzoni mwa mwezi huu kwenye tamasha la Matumaini.

 Prezzo anadai aligundua kuwa Diamond alimponda kwenye magazeti ya Tanzania kuwa hamwezi kwa lolote kwenye muziki.
“Mimi sipendi kuwa na adui kwa sababu muziki unafaa kuleta muungano, sa me nikashangaa mbona huyu brother ananiingilia na huku sikumbuki kumkosea wala hatujawai kukutana ana kwa ana,” alisema Prezzo.
“Mtu yeyote anamjua Prezzo ni kama rattle snake, ukimchokoza you have to get prepared to be bitten.
 
Rapper huyo aliendelea kudai kuwa alimpigia simu Diamond lakini hakupokea na ndio maana aliamua kumdiss kwenye Twitter.
“Jamaa hakupokea simu nikaona ah! Basi liwalo na liwe, nikadecide ku-air my views.”
Hata hivyo Prezzo amesema hawezi kumuomba msamaha Diamond kwenye Twitter kama anavyomtaka afanye.
“Unaona kwa saa hizi akianza kusema aende kwa Twitter aniombe msamaha, maisha huwa hayaendi hivo…kwa hivyo vitu vingine naona ni kama ni utoto unaingilia kati, kwani yeye kusema niombe msamaha kwa Twitter….niombe msamaha kwa kosa gani? Kusema ukweli,unajua mimini msema ukweli, mimi kuomba msamaha kwa Twitter naona kidogo ni utoto.”
Hata hivyo Prezzo amesema hataki beef na Diamond kwasababu anamheshimu na amemshukuru Willy Tuva kwa kujaribu kuwasuluhisha.

KIONGOZI MKUU WA MADAWA YA KULEVYA AKAMATWA

 
Vita dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya ni ya dunia nzima ambapo kila nchi inafanya kila liwezekanalo kutafuta vyanzo vya mitandao mikubwa inayofanya biashara hiyo. Serikali ya Mexico imefanikiwa kumkamata kiongozi wa mtandao mkubwa wa matukio ya kihalifu na usambazaji wa dawa za kulevya nchini humo unaofahamika kama ‘Zest’ aliyekuwa akisakwa kwa udi na uvumba Taarifa iliyoripotiwa na Reuters inasema mtuhumiwa huyo anayejulikana kwa jina la Miguel Angel Trevino aka Z-40, alifanikiwa kukamatwa jana (July 15) baada ya askari kuifuatilia gari yake ya Pickup kwa helicopter.

Msemaji wa serikali ya Mexico Eduardo Sanchez amesema, Trevino ( 40), alikamatwa akiwa na washirika wake wengine wawili kufuatia operesheni ya miezi mingi ya kumsaka, na alikutwa akiwa na pesa taslim zaidi ya $2 million.
Kukamatwa kwa Z-40 ni ushindi mkubwa kwa serikali ya Mexico kutokana na ukubwa wa mtandao huo wa Zetas ambao umekua tishio nchini humo kutokana na vitendo vya matukio ya mauaji yaliyofanywa na magenge ya mtandao huo unaojihusisha pia na biashara haramu ya dawa za kulevya, vitendo ambavyo vimechafua jina la nchi hiyo kiasi cha kuwapa hofu watalii na wawekezaji.

AONDOLEWA FUVU LA KICHA UPANDE MMOJA BAADA YA KUSHAMBULIWA NA RAFIKI YAKE .......MAPENZI NDIO CHANZO

KUSHOTO: John Eccles baada ya kuondolewa sehemu ya fuvu lake. KATIKATI: Eccles akiwa hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji wa fuvu lake. KULIA: Andrew Dodds.
Mtu mmoja alilazimika kuondolewa theluthi moja ya fuvu lake baada ya kuwa ameshambuliwa na rafiki yake wa zamani aliyegeuka mshindani wake katika mapenzi.
Wafanyakazi wa matibabu walilazimika kupachika kipande cha bati katika kichwa cha John Eccles baada ya kupondwa fuvu lake ukutano katika makabiliano hayo yaliyomwacha akiwa hajitambui kwa wiki mbili.
Mtu huyo mwenye miaka 35 alisema aliachwa kama alikuwa 'kagongwa na gari' wakati mwishowe alipozinduka hospitali hapo, ambako alilazimishwa kukaa kwa miezi sita.
Pale kwanza alipopata fahamu kufuatia tukio hilo dhidi ya rafiki yake wa zamani, Andrew Dodds, hakuwa akiweza kukumbuka kilichokuwa kimetokea.
Wanaume hao wawili walihitimisha urafiki wao wa zaidi ya miaka 20 pale Dodds alipoanza mahusiano na mpenzi wa Eccles na mama huyo wa binti yake.
Eccles aligonga kichwa chake ukutani baada ya kuwa amepigwa ngumi na Dodds nje ya klabu moja ya usiku mjini Consett, huko County Durham, Aprili mwaka jana, na kumwacha akiwa taabani.
Dodds alifungwa jela miaka mitatu Agosti, mwaka jana kwa kujeruhi kinyume cha sheria katika Mahakama ya Durham.
Eccles, ambaye anafanya kazi ya meneja wa zamu katika kituo cha kupumzikia, ameendelea kupata nafuu lakini anasumbuliwa na matatizo ya kupoteza kumbukumbu, kupooza upande wake wa kulia na kufanyiwa mazoezi ya viungo kusaidia aendelee kufanya shughuli zake za kawaida.
Akielezea kuzinduka kutoka kwenye shambulio hilo kwa mara ya kwanza, Eccles, mkazi wa Blackhill, karibu na Consett, alisema: "Sikufahamu kilichokuwa kikiendelea. Siwezi kukumbuka kilichotokea. Familia yangu ilibidi wanieleze."
Eccles alisema kwamba angeweza kufa kufuatia shambulio hilo lakini alisema alikuwa anaweza kurejea kufanya kazi.
Alisema: "Nina mkutano na watu wa afya sehemu za kazi wiki hii hivyo nitaona watakachosema, lakini ningependa kurejea kufanya kazi mapema iwezekanavyo.
"Nimekuwa nikielezwa inaweza kuwa miezi 18, inaweza kuwa miaka mitano au sita, lakini nataka kurejea sasa.
Eccles alitibiwa kufuatia kuvuja damu nyingi kwenye ubongo na akaendelea kukaa kwenye chumba cha uangalizi maalumu katika Hospitali ya Royal Victoria mjini Newcaste kwa miezi baada ya tukio hilo.
Sasa Eccles na mdogo wake, Mark mwenye miaka 32, wamekusanya takribani Pauni za Uingereza 1,000 kwa ajili ya kitengo hicho kufuatia usiku wa hisani kwenye Klabu ya Number One mjini Consett.

HUYU NDIYE MCHUMBA WA T.I.D "KINANA SEIF".....SOON KUFUNGA NDOA

Kila utakayemuuliza kuhusiana na relationship status ya artist wa singo za “Zeze”, “Kiuno” na “Make Me Higher” ambaye pia ni prezidaa wa Top Band atakuambia jamaa is engaged to his long time girlfriend aitwaye Kinana Seif.
Siku chache baada ya TID whose real name is Khalid Mohamed baada ya kumvisha pete demu wake huyo, ali-hoolar kupitia kwenye BLOG HII kwamba wedding bells kati ya wawili hao zingesikika very soon but unaambiwa hadi sasa yakaribia miaka miwili kukiwahakuna cha ndoa wala nini.

Mnyama TID alipovutiwa waya na muwindaji wetu ili kujua kama ndoa ipo au imeyeyuka hata kabla ya vikao this is what he said, “Mzee hakuna kitu kama hicho, watu wanaongea mitaani kuwa
nilikuwa naigiza kumvisha sukari wa moyo wangu Kinana pete, I wanna tell them that the girl is mine, wanataka kuona ndoa kwa kunipangia au? Waambie sipangiwi, I always arrange my moves na si vingnevyo”.
And alipoulizwa harusi lini ilikuwa hivi, “Kwa sasa Kinana anamalizia semester yake ya Sheria kule Urusi and natarajia kwenda kuungana nae kwenye graduation yake mwezi wa tisa na
tutakaporejea tu michakato ya kuoana itakuwa inapamba moto na Insha’Allah kama Allah ataajalia mwishoni mwa mwaka huu naweka kitu ndani”, TID .

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...