|
||
|
News, Events, Entertainment, Sports, Lifestyle, Fashion,politics, Beauty, Inspiration and yes... Gossip!
facebook likes
Wednesday, February 6, 2013
Mzee Majuto amwomba JK trekta
Kova afafanua sakata la wizi wa mil. 150/-
|
||
|
LUKUVI AFUNGUKA ,CHADEMA NAO WAMWAKIA SPIKA MAKINDA
Rufaa hizo ni pamoja na ile ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kulitaka Bunge lisitishe uamuzi wa kupewa ujaji wa Mahakama Kuu, jaji mmoja kwa madai kuwa hana vigezo vya kuwa na nafasi hiyo.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alitoa msimamo huo jana baada ya Spika Makinda kueleza bungeni kuwa Lissu ndiye kinara wa vurugu, huku ikielezwa kuwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itamchukulia hatua za kinidhamu.
Kabla ya Spika Makinda kuahirisha Bunge, kulitokea mvutano kati yake na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari baada ya Makinda kumweleza kuwa hajui kanuni hivyo atulie.
Hata hivyo, alimruhusu kuzungumza na ndipo Nassari alipopinga Kamati ya Uongozi ya Bunge kufuta hoja binafsi za wabunge akieleza ni kinyume cha kanuni za Bunge kufanyika kitu hicho.
Kabla ya Spika Makinda kujibu, Lissu alisimama na kuomba mwongozo wa Spika akisema; “Mheshimiwa Spika tunataka utueleze tutaendelea kukata rufaa hadi lini, wakati una rufaa zetu 10 kuanzia mwaka juzi na hujazitolea uamuzi, naomba mwongozo wako Mheshimiwa Spika,” alisema Lissu na kujibiwa na Spika Makinda kuwa, “Rufaa hizo zinafanyiwa kazi na zitatolewa uamuzi.”
Makinda aliliahirisha Bunge kwa kile alichosema kukithiri kwa vitendo vya utovu wa nidhamu ndani ya Bunge hilo na kufuta hoja binafsi ambazo hutolewa na kuchangiwa baada ya kipindi cha maswali na majibu.
Makinda alisema: “Waheshimiwa wabunge, tangu Januari 30, hadi jana (juzi) Februari 4, 2013 tuliamua kuwasilisha bungeni hoja binafsi za wabunge ambazo ziliahirishwa katika mkutano wa tisa wa Bunge kwa nia njema ya kujadiliana masuala makubwa ya kitaifa na kuishauri Serikali nini kifanyike ili kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayowahusu wananchi.
“Hata hivyo, imelazimu kuahirisha mijadala yote ya hoja binafsi kutokana na tabia iliyojitokeza ya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wabunge na hivyo kuamua kwa makusudi kuanzisha vurugu na kulifanya Bunge kupoteza heshima yake,” alisema Spika Makinda.
Alisema kutokana na hali hiyo, Kamati ya Uongozi imekubaliana kuwa suala hilo lipelekwe kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili ilichunguze na kuwasilisha mapendekezo yake kabla ya mkutano unaoendelea kumalizika na kwamba hoja zote binafsi zisiwasilishwe kutokana na utovu wa nidhamu ambao ungeweza kujitokeza katika hoja zilizobakia.
Hata hivyo, Lissu alisema kuwa kelele za kutetea taratibu na kanuni ndizo zinamfanya aonekane kuwa ana utovu wa nidhamu.
“Spika anaonyesha upendeleo wa waziwazi, anakiuka kanuni kwa makusudi. Mimi nitasema, sitaogopa kamati, hata nikiitwa nitasema... Sasa tunachokifanya, tumekutana leo (jana) na tumeandaa taarifa ya kutaka Spika aondolewe yeye na naibu wake, hii tutaiwasilisha kama taarifa kati ya kesho (leo) na keshokutwa (kesho),” alisema Lissu.
Juzi Naibu Spika, Job Ndugai naye aliahirisha kikao cha Bunge kilichokaa kwa dakika 43 ikiwa ni muda mfupi zaidi baada ya kutokea vurugu zilizoanzishwa na kambi ya upinzani ikiongozwa na wabunge wa Chadema waliodai kuwa hawatendewi haki.
Akizungumzia hoja ya Mnyika, Spika Makinda alisema, “Kulingana na maelezo hayo ya utangulizi, hoja ya Mnyika, ilikidhi vigezo na alipewa nafasi na akawasilisha hoja yake.
Baada ya hoja hiyo kuwasilishwa na kwa mujibu wa kanuni ya 53(6) (c), Waziri wa Maji ambaye ndiye Msemaji wa Serikali kuhusu hoja husika, alipewa nafasi ya kuwa mchangiaji wa kwanza na kutoa maoni ya shughuli za Serikali.”
Alisema maoni hayo ya Waziri wa Maji yalizingatia Kanuni ya 57(1) (c) inayoruhusu kuingiza au kuongeza maneno mapya kwenye hoja.
Makinda alisema: “Kwa masikitiko makubwa sote tulishuhudia vurugu zilizojitokeza katika Bunge hili hasa wakati wa mjadala wa hoja binafsi za wabunge. Kimsingi huu ulikuwa ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu kutokea katika historia ya Bunge letu.”
Dk Slaa amshukia
Akizungumza hukusu matukio hayo, Dk Slaa alisema amewazuia wabunge wake kuonana na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kama wakiitwa hadi hapo rufaa zao 10 zitakazotolewa uamuzi.
“Tumeshawaeleza wabunge wetu wasiende kwenye kamati hiyo hadi Spika wa Bunge na Naibu wa Spika watakapotoa uamuzi wa rufaa zetu 10 mbele ya Bunge letu la Jamhuri ya Muungano,”alisema Dk Slaa.
Dk Slaa alisema wanalaani kitendo cha Spika wa Bunge, Naibu wa Spika na wenyeviti wa Bunge kwa kitendo cha ubaguzi wa wazi kwa wabunge wa upinzani, kinyume na Kanuni ya 8 ya Bunge inayotaka watende haki, uadilifu bila chuki kwa wabunge wote.
Alilaani kitendo cha Naibu Spika Ndugai kuleta ubaguzi wa kutopitisha hoja binafsi ambazo zingeleta tija kwa wananchi zilizowasilishwa bungeni na Mnyika.
“Jana ilitokea fujo bungeni hivyo Naibu Spika alitakiwa asitishe Bunge kwa muda hadi utulivu utakaporejea, lakini alichokifanya ni kafuta hoja ya Mnyika aliyoiwasilisha bila ya kuwahoji wabunge. Huu ni ukiukwaji wa kanuni za Bunge zinavyosema,” alisema Dk Slaa.
Alisema alishangazwa na uongo wa Spika Makinda bungeni akieleza kuwa Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe alisimama kwa kifungu 53 (c) wakati alisimama kwa kutumia kifungu 51(c) akipendekeza kuondolewa bungeni kwa hoja binafsi ya Mnyika.
“Spika amekuwa mpotoshaji, muongo na kumsemea, Waziri wa Maji amesimama kwa kutumia kanuni ya 53(c) wakati alitumia kanuni ya 51 (c), kanuni inataka kama hoja imefikishwa bungeni isiondolewe. Kilichotokea hoja imeondolewa,”alisema Dk Slaa.
Nasari alalama hoja
kuzimwa
Nassari aliyekuwa awasilishe hoja yake, kuhusu mwenendo wa Baraza la Mtihani la Taifa unavyoathiri elimu nchini, alisema kuwa atakata rufaa kupinga uamuzi wa Spika.
“Nitakata rufaa Kamati ya Uongozi, hoja yangu iliahirishwa mkutano uliopita, halafu leo inaondolewa bila sababu, kweli sikubali kwa sababu hoja yangu haihusiani na vurugu zilizotokea,” alisema.
Lukuvi apigilia msumari
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisema: “Kamati ya Uongozi ndiyo inayopanga shughuli za Bunge na ndiyo inayomshauri Spika inapoona kuna tatizo kabla, wakati na baada ya Bunge.
“Sasa, imeamriwa hivyo kufuta hoja na iko katika kanuni...Unajua Kamati ya Uongozi, mimi naingia kwa nafasi yangu pamoja na Mwanasheria Mkuu,.Sasa hizi hoja binafsi ilikuwa ni ‘favour’ (fadhila) tu sasa tunaona zinakoelekea siko na uamuzi tuliofikia ni kuziondoa.”
SOURCE Habari LEO
REBECCA ADLINGTON WA UINGEREZA AJIUZULU KUOGELEA
Rebecca Adlington akitangaza kujiuzulu mashindano ya kuogelea mbele ya waandishi wa habari.
Rebecca Adlington akiwa katika picha ya pamoja na wazazi wake, muda
mfupi kabla ya kutangaza kujiuzulu mashindano ya kuogelea mbele ya
waandishi wa habari.
Rebecca Adlington katika akiwa na washindi wengine baada ya kujitwalia medali katika mchezo wa kuogelea.
Rebecca Adlington katika akiwa na washindi wengine baada ya kujitwalia medali katika mchezo wa kuogelea.
Rebecca Adlington akipozi akiwa ameshikilia medali ya dhahabu na bendera ya taifa ya Uingereza.
Rebecca Adlington akionesha tuzo ya OBE aliyotunukiwa na Malkia Elizabeth wa II wa Uingereza.
LONDON, England
'Nalichukia sana neno nastaafu. Napenda
sana kuogelea, lakini kufanya hivyo kiushindani kwa sasa sitoendelea, nimefikia
tamati. Daima nitendelea kuogelea hata nikiwa na umri wa miaka 90'
BINGWA
wa medali mbili za dhahabu za michuano ya Olimpiki katika mchezo wa kuogelea, Rebecca
Adlington leo amethibituisha rasmi kustaafu katika katika uogeleaji wa
ushindani.
Majaaliwa
na ya muogeleaji huyo kijana mwenye umri wa miaka 23 katika mchezo huo yalizua
maswali makuu, tangu mkali huyo alipotwaa Shaba mbili za Olimpiki ya majira
ya joto mwaka jana jijini hapa.
Akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari jana jijini hapa, Rebecca mzaliwa wa Mansfield alithibitisha
kuhitimisha zama zake katika mchezo huo, akiwa ametwaa ubingwa wa Olimpiki,
dunia, Ulaya na michuano ya Commonwealth.
'Nalichukia
sana neno
nastaafu. Napenda sana
kuogelea, lakini kufanya hivyo kiushindani kwa sasa sitoendelea, nimefikia
tamati. Daima nitendelea kuogelea hata nikiwa na umri wa miaka 90.'
Rebecca
akaongeza kuwa: 'Kwa hakika siwezi kushinda nao (waogeleaji vijana). Siwezi
kushinda tena katika ngazi hiyo, nahitaji kujiweka mbali kidogo wakati huu hali
yangu ikitengemaa.
'Ilikuwa
muda huo. Beijing
ilibadili maisha yangu yote, kila mmoja alitaka kujifunza kuhusu mimi. Ulikuwa wakati
bora zaidi katika zama zangu mchezoni. Nina furaha sana kuona rekodi yangu ya dunia ingali
imesimama,' alisema Rebecca katika mkutano wake huo.
……The Sun……
Kuondokewa hoja binafsi bungeni ni kuwasaliti wananchi
TABIA ya kujadiliwa
kwa hoja za Mawaziri wa Elimu, Mafunzo na Ufundi Shukuru Kawambwa, na
wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na hatimae kuungwa mkono na Wabunge wa
Vyama vyao, zimetafsiliwa kama ni Kuwasaliti wananchi waliowapa Kura.
Sababu ya
kutafsilika hivyo, kumetokana na kwamba mara zote zimekuwa zikipendekeza
kuondolewa bungeni kwa hoja binafsi zilizowasilishwa mapema na wabunge
wa upinzani, ambazo wananchi wanaona zina dhima ya Mustakabali wa Taifa.
Hoja binafsi
zilizohasimiwa na mawaziri hao ziondolewe ni pamoja na Udhaifu wa Sekta
ya Elimu iliyowasilishwa na Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia-NCCR
Mageuzi, na ya Maji ambayo mapema iliwasilishwa na Mbunge wa Ubungo
(Chadema), John Mnyika.
Kinachopelekea
tafsiri hizo, ni pamoja na Mawazi wa Wizara zingine kutoweka pingamizi
la kuondolewa kwa Hoja binafsi ya Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi
Mwigulu Nchemba kuhusu mikopo ya Elimu ya Juu.
Hoja
nyingine ni ile ya Mbunge wa Nzega Dk. Hamisi Kigwangala ya mpango
maalumu wa kukuza ajira kwa vijana kwa kuanzisha mfuko wa mikopo
ya vijana wanaowekeza kwenye kilimo na viwanda vyenye uhusiano wa moja
kwa moja na kilimo kwa hoja Mbadala za
Kama
ilivyofanyika kwa Mbatia alipowasilisha Hoja ya Udhaifu wa Sekta ya
Elimu, ndivyo ilivyofanyika kwa Mnyika katika hoja yake aliyokuwa
akitaka Bunge liazimie kuitaka Serikali ichukue hatua za haraka ya
kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa majitaka katika
Jiji la Dar es Salaam.
Hapa
ndipo nilipoona umuhimu wa wa bunge hili la kichama na kishabiki kuwa
ni kubadilisha utaratibu katika katiba mpya, spika na naibu wake wasiwe
wabunge na wasiwe na chama chochote cha siasa, na mawaziri nao wasiwe
wabunge.
Sikubaliani
kwamba kila kinachoongelewa na upinzani ni cha kubeza, ieleweke kuwa,
ukiyakataa mapendekezo ya upinzani si kana kwamba umewapinga wao bali
unakuwa umewapinga wananchi walioko nyuma yao.
Kilicho
mbele yetu, tunatakiwa tuweke Utaifa kwanza na kasha ndipo vyama vyenu
baadae. Lakini nimehuzunishwa sana na mwenendo wa Bunge letu, ambalo
sasa naona limekuwa halina utaifa kwa baadhi ya wabunge, bali
limegubikwa na uvyama.
Wananchi sasa
tunaamini kwamba, kila inapotolewa hoja ya manufaa kwa wananchi hasa
inapotolewa na wapinzani, Spika au Naibu Spika wa Bunge anaizima, hivyo
kwa tabia na muktadha huo, tunajua wabunge wa chama cha cha mapinduzi
(CCM), wameamua kututesa wananchi , Je. Hawajui mwaka 2015 uko
mlangoni?.
Kiukweli
mpaka sasa, Bunge limewaonesha wananchi kwamba halina maadili, na
lawama zote lazima tuwatupie wasimamizi wa Bunge wakiongozwa na Spika
na Naibu Spika. Lazima ifike mahali wabunge waogope na kuona jinsi
wapiga kura walivyopigwa Jua na Mvua ili kuwafanya wawe wawakilishi wao,
kuliko hivi wanavyoisimamia Serikali kinafiki.
Hivi
wabunge; Je,mmesahau kabisa kwamba kuna watu wanakufa huku na nchi iko
katika hali mbaya kwa njaa,,, migogoro ya kijamii na kidini, elimu haina
mwelekeo wala haimuandai mtanzania kujitegemea zaidi ya kuwa mtumwa wa
ajira
Aidha
najihoji moyoni Je, baadhi yenu mtapataje uchungu kama mishahara yenu
imefikia million tatu nukta sita ukiondoa marupurupu!! Basi kama tatizo
ni siasa,,,Rais Kikwete licha ya juhudi zake zinazosemekana ni
nyingi ili atakapokabidhi kijiti aweze kukumbukwa, Wabunge hawa ndio
watu uliopewa na wananchi ili wakusaidie kutokomeza Umasikini, Ujinga na
Maradhi.
KUTOKA BUNGENI LEO
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia (kushoto) January Makamba wakibadilishana mawazo na Ahmed Shabiby(Gairo) katika viwanja vya Bunge .(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
wanafunzi wa Shule ya Independence kutoka Dar es Salaam wakitambulishwa Bungeni leo.
Salehe Pamba (kulia) amkisikiliza Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya sola ya Rex Energy Francis Kibhisa jinsi ya matumizi mbalimbali
ya umeme wa Sola. Maonyesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Bunge
mjini Dodoma.(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
MOURINHO AKERWA WACHEZAJI REAL MADRID KUIPOTEZEA LA LIGA NA KUIKAMIA MECHI YA LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA DHIDI YA MAN U…!
José Mourinho aliona ni kitu gani kingetokea kwa timu
yake ya Real Madrid kabla ya mechi yao ya ugenini dhidi ya Granada. Na hicho
ndicho kilichomfanya atumie dakika kadhaa kwenye vyumba vya kuvalia kabla ya
kuchezwa kwa mechi hiyo waliyolala 1-0, akiwakumbusha wachezaji wake kuwa kadri
wanavyocheza vizuri katika La Liga, Ligi Kuu ya Hispania ndivyto wanavyojiwekea
mazingira mazuri ya kufanya vyema katika mechi yao ijayo ya Ligi ya Klabu Bingwa
Ulaya dhidi ya Manchester United na pia ya marudiano kwenye Kombe la Mfalme dhidi
ya Barçelona.
"Mnapaswa kuzingatia fahari ya weledi wenu kwa
kucheza katika kiwango chenu cha juu katika kila mechi. Mnapaswa kujituma sana
na siyo kubweteka, tena katika kila michuano."
Huo ndiyo ujumbe alioutoa Mourinho kwa wachezaji wake bila
kupindisha maneno, muda mfupi kabla ya mechi yao dhidi ya Granada.
"Kuwa wa pili ni bora kuliko kushika nafasi ya tatu,
na kuwa nyuma ya Barca kwa pointi tano au sita ni bora kuliko kuachwa kwa pointi
15 au 16", ulikuwa ni ujumbe mwingine wa kocha huyo Mreno kwa wachezaji
wake.
Kwahiyo, kuhuzunika kwa Mreno huyo kufuatia kichapo
walichopata kutoka kwa Granada kilitokana zaidi na namna timu ilivyocheza na
siyo matokeo.
"Matokeo hayakunisumbua sana, lakini kiwango cha timu
katika kipindi cha kwanza hakikunifurahisha kabisa; kilikuwa cha hovyo. Tulitawala
katika kipindi cha pili na kupata nafasi chache za kufunga na kusawazisha, lakini
hilo peke yake halikutosha kunipa furaha," alisema Mourinho.
Real Madrid watashuka dimbani Jumatano ijayo kucheza
nyumbani mechi yao ya kwanza ya hatua ya 16-bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
dhidi ya Man U na Februari 27 watarudiana na Barcelona katika mechi yao ya ugenini
ya nusu fainali ya Kombe la Mfalme kwenye Uwanja wa Camp Nou. Katika mechi yao
ya kwanza dhidi ya Barca, matokeo yalikuwa sare ya 1-1.
WALCOTT ALILIA KUCHEZESHWA KATIKATI ENGLAND
LONDON, ENGLAND
THEO Walcott amemwambia kocha wa England, Roy Hodgson: “Nichezeshe fowadi nitawasambaratisha Wabrazil Jumatano.”
Staa
huyo wa Arsenal, amemwambia Hodgson kwamba yu tayari kumaliza tatizo la
majeruhi kwenye kikosi, na kuanza kwenye safu ya ushambuliaji katika
mechi hiyo ya kirafiki itakayopigwa Wembley.
Kukosekana
kwa Jermain Defoe na Daniel Sturridge kwa kuwa majeruhi, na Danny
Welbeck anayehangaika kumaliza tatizo la nyonga, Hodgson amebaki na
Wayne Rooney akiwa mshambuliaji pekee aliye fiti kikamilifu.
Walcott
amekuwa kwenye kiwango kizuri Arsenal akiachwa kucheza kulia kwa
washambuliaji watatu, lakini ameeleza kwamba amejifua kucheza mbele
akiwa na Rooney mazoezini kwenye Uwanja wa St George's Park mwanzoni mwa
wiki, na yu tayari kuongoza mashambulizi dhidi ya Brazil.
NEYMAR AITAKA ENGLAND ISAHAU KUTWAA KOMBE LA DUNIA, KISA? ETI NI TIMU YA MTU MMOJA …ROONEY
MSHAMBULIAJI
wa Brazil, Neymar amsema England isahau kuhusu kutwaa kombe la dunia
kwa vile ni timu inayomtegemea mtu mmoja, Rooney.
Amesema:
“England ni timu nzuri yenye baadhi ya wachezaji wazuri sana lakini
siwachukulii kama wapinzani wetu wakubwa katika Kombe la dunia.
“Nadhani
wanamtegemea sana Rooney, ukimuondoa yeye sioni mwingine anayeweza kuwa
muuaji. Lakini Brazil tuna wachezaji wengi wanaoweza kufanya hivyo.
“England ina wachezaji wazuri lakini kamwe siwezi kuwalinganisha na Hispania au Argentina.
“Itazame Argentina. Kama Messi asipokuwa kwenye hali nzuri ya kimchezo, bado wapo Aguero na Teves.
“Na Hispania, asipong’ara Iniesta kuna Xavi na Villa.”
Flaviana Matata ala shavu, ashiriki kwenye matangazo ya Diesel + Edun
Mwanamitindo wa kimataifa kutoka nchini Tanzania Flaviana Matata ameshiriki katika kampeni za matangazo makubwa ya makampuni ya nguo ya DIESELna EDUN. Kampeni ya DIESEL + EDUN ilianzishwa mwaka jana mwezi wa kwanza ambapo muanzilishi wa kampuni ya DIESEL – Renzo-Ali hewson walisafiri hadi nchi ya Uganda na Mali kuangalia wakulima wa pamba na wakaamua kutengeneza nguo kwa kutumia hizo pamba ili kuwanufaisha hao wakulima.
Mfungwa ampa mimba askari magereza mwanamke
NEW YORK (AP) — A federal prison guard was charged Tuesday with having an illegal affair with an inmate convicted in one of New York's most notorious police killings, later becoming pregnant with his child.
Nancy Gonzalez, 29, was arrested Tuesday on charges she intentionally engaged in a sex act with Ronell Wilson while working the night shift at the Metropolitan Detention Center in Brooklyn. She became pregnant in June, a few months into the affair, according to court papers. Gonzalez appeared in court Tuesday visibly pregnant and crying, her hair pulled back in a ponytail, and was released on $150,000 bond.
"She's had a very tragic life," said her attorney, Anthony Rico. "She has long-term issues that affected her life and judgment."
Her family didn't comment as a swarm of photographers and television cameras surrounded them outside federal court. Gonzalez buried her head in Rico's shoulder while he spoke to reporters.
"These are very serious charges," he said, adding he wouldn't say whether Wilson pressured Gonzalez into the affair.
Wilson, 30, was a young gang member on Staten Island when he was convicted in the point-blank shootings of undercover officers James Nemorin and Rodney Andrews in a 2006 illegal gun sting gone awry. The officers were both shot in the back of the head. Wilson was sentenced to death, but the sentence was thrown out in 2010 by an appeals court based on prosecutorial error.
Wilson could still face death; a new jury will decide his fate. But the replay of the trial's penalty phase has been put off as Wilson's lawyers seek to convince a judge that he's ineligible for the death penalty because he's mentally disabled.
In November, a hearing was held on the claim, and a decision from Judge Nicholas Garaufis is pending, though it's unclear how Gonzalez's arrest will affect the motion.
Wilson was moved to solitary confinement in August while the reports of the relationship were investigated.
According to court papers, Gonzalez was seen by other inmates going in and out of Wilson's cell starting in March, meeting him in a vacant activity room next to his cell when other inmates were supposed to be sleeping.
"I took a chance because I was so vulnerable and wanted to be loved and now I am carrying his child," Gonzalez said, according to court papers.
She said she "kind of got sucked into his world," and that she "felt like, well, why not give him a child as far as giving him some kind of hope."
She confessed her relationship with Wilson to a different boyfriend, another inmate who had been under her supervision at the federal prison but is now housed at a state facility. She said it was over with Wilson, and that she was worried she would get into trouble.
After she became pregnant, Wilson's mother made contact, requesting a sonogram photo, according to court papers. Gonzalez said she was worried about the calls because she feared authorities would catch her.
"I know what's to come. I know what is going to be said about me," she said, according to court papers. "How am I going to explain this to this little boy? Mommy was in the military ... Mommy was a C.O., Mommy got wrapped up ... And then the opposite end is with a person who took lives. So how do you explain that?"
Mhariri Nipashe Amchana Spika & Serikali - Haikubaliki kuligeuza Bunge kibogoyo
Haikubaliki kuligeuza Bunge kibogoyo
Katika mkutano wa 10 unaoendelea mjini Dodoma tangu wiki iliyopita, umma umepigwa na butwaa kuingiwa na fazaa kubwa kutokana na mwenendo wa mambo ndani ya chombo hicho kikubwa na muhimu cha uwakilishi wa wananchi chenye wajibu wa kutunga sheria na kuisimamia serikali.
Fazaa hii siyo ya bure ila ni kutokana ukweli kwamba ama kumekuwa na mbinu za kufanya chombo hicho kisitekeleze wajibu wake kupitia mbunge mmoja mmoja kwa sababu moja tu, ushabiki wa kisiasa ambao hauna tija. Huu ni ushabiki ambao tunathubutu kusema wazi kuwa unadimimiza siyo demokrasia tu bali pia umejikita kuilinda serikali isiwajibishwe ndani ya chombo hicho muhimu.
Wakati mkutano huu ukianza mjini Dodoma Jumanne Januari 29, mwaka huu, yaani wiki iliyopita, tulimkumbusha Spika wa Bunge kuwa ana mzigo wa viporo vya kazi ambazo ama alizitaka mwenyewe ziwasilishwe kwake kwa maamuzi, au wabunge walizipeleka kwake kwa maamuzi kutokana ama mambo kutokwenda sawa au kumtakiwa atoe maelekezo yake. Viporo hivi ni vingi na vipo tangu Bunge hili linaanza kazi mwaka 2011.
Tulimkumbusha Spika juu viporo hivyo ili kuvitolea uamuzi, nia ikiwa ni kumkumbusha tu ili kwa kukaa kimya juu yake watu wasijekuanza kuhoji juu uimara wa kiti chake, uadilifu wa kuendesha shughuli za Bunge na utendaji wa haki kwa wabunge wote pasi na itikadi zao kwa kuwa wote wamechaguliwa na wananchi na wanatokana na mfumo halali wa kisiasa ambao taifa hili limeamua kufuata.
Tunajua mkutano wa sasa utaahirishwa Ijumaa hii, yaani keshokutwa, na inavyoelekea ni vigumu kwa maamuzi ya viporo vyote kutolewa maamuzi, lakini wakati viporo hivyo vikisumbua vichwa vya wananchi wengi huku wakihoji juu ya mwenendo mzima wa Bunge letu, mkutano huu umeshuhudia tena mambo ya aibu kubwa yakifanyika.
Ijumaa iliyopita, Jumatatu na jana, wabunge wamesema wazi mbele ya Spika kwamba kiti chake kinayumba, hakitendei haki kambi ya upinzani, kanuni za Bunge zinapindishwa ili tu kupotosha mambo, kuilinda serikali isiwajibishwe hali ambayo ni sawa na kusema kupora wajibu wa kibunge wa kuisimamia serikali.
Sakata la sasa lilianza na hoja ya Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Mageuzi), James Mbatia, juu ya uadilifu wa sekta ya elimu ambayo ilikuwa nzito, yenye maana na ambayo kwa kweli ilikuwa inalenga kutafuta uwajibikaji ndani ya serikali juu ya mustakabali wa elimu ya taifa hili.
Kisha ikafuata ya Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, ambayo ililenga pia kutafuta uwajibikaji serikalini katika suala zima la upatikanaji wa maji safi na uondoaji wa maji taka katika jiji la Dar es Salaam, huku mabilioni ya fedha yaliwa yemetumika bila kuwako kwa huduma yoyote ya maana ya maji, lakini pia ipo ya Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari, ambayo ilitaka kujielekeza kwenye suala la utendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani. Kwa bahati mbaya sana hoja hii haikuwasilishwa kabisa, ni kama ikienguliwa juu kwa juu.
Kiti cha Spika katika sakata lote hili kinayooshewa kidole kwamba kimeshindwa kusimamia haki, kwamba kimeyumba kiasi cha kuegemea upande mmoja; ni hatari kubwa inapofikia hatua ya wabunge kwa ujasiri mkubwa wanathubutu kutuhumu kiti kuyumba kiasi cha kusababisha kukosekana kwa maelewano ndani ya Bunge.
Ni hatari kweli kweli!
Kwa wale walioangalia Bunge Jumatatu jioni watashuhudia walichokiona kwamba siyo taswira njema kwa taifa linalojitapa kuheshimu utawala wa sheria, demokrasia na kuheshimu kanuni, miiko na maadili yanaokubalika kijamii na kitaifa.
Kwa bahati mbaya sana tangu kuanza kwa Bunge la sasa mwaka 2010 kufuatia uchaguzi mkuu wa 2010, kumekuwa na hisia kwamba uimara wa kiti cha Spika umetiliwa shaka kubwa hasa katika suala zima la kutenda haki sawia kwa wabunge wote bila kujali wanatokana na chama gani cha siasa wanapowasilisha hoja zao.
Tunachukua wasaa huu kuweka wazi kwamba kama Bunge likigeuzwa kuwa sehemu ya muhimili wa utawala ama kwa dhahiri au hata kwa mlango wa nyuma ni wazi hakuna tena haja ya kuwako kwa chombo hicho, ni kwa maana hii tunamshauri Spika awe mvumilivu na asimame kidete kuhakikisha kwamba muhimili anaousimamia unatekeleza wajibu wake mkuu wa kikatiba kulingana na ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania wa kuisimamia na kuishari serikali ili iwajibike ipasavyo kwa wananchi wake. Yanayoendelea mjini Dodoma kwa sasa hakika ni juhudi za kutaka serikali ilale na kukoroma na wabunge waangalie tu. Hii haikubaliki na haitakubalika asilani.
ends
CHANZO: NIPASHE
My take:
Media fraternity yote inatakiwa ku-rally behind opposition camp na umma wote kwa ujumla kupinga abuse ya kiti cha uspika unaosababishwa na siasa chafu na umangimeza wa CCM
Tundu Lissu hana fujo, kiti cha spika ndio kinapwaya!
Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania amemtaja mbunge wa singida mashariki Mhe Tundu Lissu kuwa ni mbunge anae ongoza kwa fujo na msumbufu bungeni! Hii ni mara ya kwanza katika historia ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kumsikia spika wa bunge akitaja orodha ya majina ya wabunge wenye fujo na wasumbufu. Nikiri kuwa sijawahi kumsikia spika yoyote kabla ya mama Makinda akifanya kama alivyo fanya mama huyu!
Baada ya mama Makinda kumtaja Tundu Lissu kuwa ndiye mbunge msumbufu na mwenye fujo kuliko wabunge wote mjengoni, Nimejikuta najiuliza maswali kadhaa.
1. Je ni kweli Tundu Lissu ni mbunge msumbufu na mwenye fujo bungeni kwa maana ya halisi ya usumbufu na fujo?!
2. Je kuzisimamia, kuzifuata na kuzijua kanuni za bunge huku akitaka kiti cha spika kizisimamia na kuzifuata kanuni hizo pale kinapo yumba ndio usumbufu au fujo?
3. Je, ulio itwa usumbufu na fujo za Tundu Lissu bungeni una tija kwa wananchi wanao fuatilia bunge na unawakera wananchi hao au unakikera tu kiti cha spika?
4. Je, kiti cha spika kimeonyesha umahiri wa kiutendaji kwa maana ya utendaji wa haki usio egemea itikadi wala kuegemea chama tawala bila kuwakwaza wananchi na wabunge wa upinzani?
5. Je usumbufu na fujo za Tundu Lissu bungeni na maamuzi ya kiti cha spika ni kipi kina athiri na kuwasumbua watanzania katika mfumo na aina ya bunge tulilo nalo leo?!
MTAZAMO WANGU.
Mimi kama mwananchi wa kawaida ninae fuatilia bunge naona fujo na usumbufu alio batizwa Tundu Lisu unafaa uelekezwe kwenye kiti na mamlaka dhaifu ya spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kwa nini?
1. Mpaka sasa kiti cha spika kimeonyesha udhaifu na kimeonekana kuyumba huku kikionyesha upendeleo wa wazi wazi kwa wabunge wa ccm na kukandamiza wabunge wa upinzani. Ushahidi ni yanayoendelea bungeni kuanzia kwenye hoja ya Lema kuhusu waziri mkuu kulidanganya bunge hadi kwenye hoja binafsi za wabunge wa upinzani kuzuiliwa huku za wabunge wa ccm kuruhusiwa kusomwa.
2. Mpaka sasa rufaa 10 za wabunge wa upinzani hasa Chadema hazija patiwa majibu huku wabunge haohao wengi wakitegemewa kuitwa kwenye kamati ya maadili na nidhamu ya bunge kwa kile kilicho itwa kuvunja kanuni za bunge. Jiulize kwa nini ni miaka takribani miwili sasa hakuna rufaa hata moja iliyo jibiwa wakati nyingine zina majibu ya wazi kabisa mfano ile ya Pinda kuongea uwongo bungeni kuhusu mauwaji ya waandamaji wa Chadema mkoani Arusha?
3. Mpaka sasa wabunge wengi wa upinzani ndio wamelalamikia kuonewa na kiti cha spika kuliko wabunge wa ccm. Mara kadhaa hata wanaharakati wameonyesha hisia zao waziwazi kuwa kiti cha spika kina pwaya na kimeonyesha udhaifu wa kiutendaji.
4. Wananchi wengi wa kawaida wameonyesha waziwazi kutokuwa na imani na kiti cha spika kwa jinsi kinavyo endesha bunge. Wana ona kuna tofauti kubwa ya uendashaji wa bunge wa kati wa kipindi cha Mzee Sitta na kipindi hiki cha Anna Makinda.
5. Kuahirishwa kwa bunge hivi karibuni kutokana na ubabe wa kiti cha spika kusababisha vurugu zilizotokea bungeni nao ni ushahidi mwingine kuwa kiti cha spika kina sababisha fujo kutokana na wabunge kutetea haki zao zinazo pokwa na kiti hicho.
HITIMISHO.
Udhaifu na kupwaya kwa kiti cha spika ndio kuna sababisha fujo na vurugu kutokana na kukandimiza upinzani kwa maslahi ya chama tawala na kulinda udhaifu na ombwe la serikali. Tundu Lissu hana fujo na usumbufu unao athiri watanzania kama jinsi maamuzi mabovu ya kiti cha spika yanavyo weza na kuendelea kutuathiri watanzania.
Ulio itwa usumbufu na fujo za Tindu Lissu bungeni hauja zima hoja ya kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka wala kuzima hoja za sakata la gesi ya Mtwara, fujo na usumbufu wa Tundu Lissu hauja zima hoja makini ya elimu iliyo tolewa na Mbatia wala hoja ya tatizo la maji ya John Mnyika.
Udhaifu na ombwe la kiti cha spika ndio chanzo cha kumuona Tundu Lissu ni msumbufu kwa kuwa ana kisulubu kiti kusimamia na kuzifuata kanuni.
Waziri wa elimu amuumbua James Mbatia, awasilisha mtaala wa elimu nchini
waziri
wa elimu Mh.shukuru Kawambwa amewasilisha mtaala halisi wa elimu wa mwaka
2005 hapa nchini ambao umegawanyika katika sehemu tatu.
1.mtaala wa elimu ya chekechea
2.mtaala wa elimu ya msingi
3.mtaala wa elimu ya sekondari.
mtaala huo unaenda kukaguliwa na kuthibitishwa na timu ya wabunge wakiwemo Mbatia,Magret Sitta na wabunge wengine waliobobea katika masuala ya elimu.
Ikumbukwe kuwa Mbatia ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na rais aliapa kuwa endapo serikali itawasilisha mtaala huo bungeni yeye ataijuzulu ubunge wake.
MY TAKE; MBATIA ATAJIUZULU UBUNGE????
1.mtaala wa elimu ya chekechea
2.mtaala wa elimu ya msingi
3.mtaala wa elimu ya sekondari.
mtaala huo unaenda kukaguliwa na kuthibitishwa na timu ya wabunge wakiwemo Mbatia,Magret Sitta na wabunge wengine waliobobea katika masuala ya elimu.
Ikumbukwe kuwa Mbatia ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na rais aliapa kuwa endapo serikali itawasilisha mtaala huo bungeni yeye ataijuzulu ubunge wake.
MY TAKE; MBATIA ATAJIUZULU UBUNGE????
Immigrants in the United States 40.4 Million, 13% of 311.6 Million USA population
Five hundred and twenty five people, coming from more than
75 countries, were sworn in as US citizens
at the 27th annual naturalization ceremony
at the Seattle Center in Washington on July 4, 2011
.Definitions
"Foreign born" and "immigrants" are used interchangeably
and refer to persons with no US citizenship at birth.
This population includes naturalized citizens,
lawful permanent residents, refugees and asylees,
persons on certain temporary visas, and the unauthorized.
According to the most recently available data, how many immigrants are in the United States?
According to estimates from the 2011 ACS, The US immigrant population stood at almost 40.4 million, or 13 percent of the total US population of 311.6 million.
Between 2010 and 2011, the foreign-born population increased by 422,000, or 1 percent. This increase is lower than year-to-year changes in the first half of the 2000s.
What are the historical numbers and shares of immigrants in the United States?
Data on the nativity of the US population were first collected in the 1850 decennial census. That year, there were 2.2 million foreign born in the United States, or almost 10 percent of the total population.
Between 1860 and 1920, immigrants as a percentage of the total population fluctuated between 13 and 15 percent, peaking at nearly 15 percent in 1890 mainly due to European immigration. By 1930, immigrants' share of the US population had dropped to less than 12 percent (14.2 million).
The share of foreign born in the US population continued to decline between the 1930s and 1970s, reaching a record low of approximately 5 percent in 1970 (9.6 million). However, since 1970, the percentage has increased rapidly, mainly due to large-scale immigration from Latin America and Asia.
The foreign born represented 6 percent (14.1 million) of the total US population in 1980. By 1990, their share had risen to 8 percent (19.8 million), and by the 2000 census they comprised 11 percent (31.1 million) of the total US population. In 2011, immigrants comprised 13 percent (40.4 million) of the total US population.
How do the top source countries with the largest share of immigrants compare to those 50 years ago?
Together, immigrants from these ten countries made up close to 60 percent of all foreign born residing in the United States in 2011.
The predominance of immigrants from Latin American and Asian countries in the late 20th and early 21st centuries starkly contrasts with the trend seen in 1960 when immigrants tended to be from European countries. Italian-born immigrants made up 13 percent of all foreign born in 1960, followed by those born in Germany and Canada (accounting for about 10 percent each). In 1960s no single country accounted for more than 15 percent of the total immigrant population.
75 countries, were sworn in as US citizens
at the 27th annual naturalization ceremony
at the Seattle Center in Washington on July 4, 2011
.Definitions
"Foreign born" and "immigrants" are used interchangeably
and refer to persons with no US citizenship at birth.
This population includes naturalized citizens,
lawful permanent residents, refugees and asylees,
persons on certain temporary visas, and the unauthorized.
According to the most recently available data, how many immigrants are in the United States?
According to estimates from the 2011 ACS, The US immigrant population stood at almost 40.4 million, or 13 percent of the total US population of 311.6 million.
Between 2010 and 2011, the foreign-born population increased by 422,000, or 1 percent. This increase is lower than year-to-year changes in the first half of the 2000s.
What are the historical numbers and shares of immigrants in the United States?
Data on the nativity of the US population were first collected in the 1850 decennial census. That year, there were 2.2 million foreign born in the United States, or almost 10 percent of the total population.
Between 1860 and 1920, immigrants as a percentage of the total population fluctuated between 13 and 15 percent, peaking at nearly 15 percent in 1890 mainly due to European immigration. By 1930, immigrants' share of the US population had dropped to less than 12 percent (14.2 million).
The share of foreign born in the US population continued to decline between the 1930s and 1970s, reaching a record low of approximately 5 percent in 1970 (9.6 million). However, since 1970, the percentage has increased rapidly, mainly due to large-scale immigration from Latin America and Asia.
The foreign born represented 6 percent (14.1 million) of the total US population in 1980. By 1990, their share had risen to 8 percent (19.8 million), and by the 2000 census they comprised 11 percent (31.1 million) of the total US population. In 2011, immigrants comprised 13 percent (40.4 million) of the total US population.
How do the top source countries with the largest share of immigrants compare to those 50 years ago?
- In 2011, Mexican-born immigrants accounted for approximately 29 percent of the nearly 40.4 million foreign born residing in the United States, making them by far the largest immigrant group in the country.
- China (including Hong Kong but not Taiwan) was the second largest at almost 5 percent of the foreign born, closely followed by
- India (also nearly 5 percent).
- Immigrants from the Philippines accounted for 4 percent of the total immigrant population.
- El Salvador,
- Vietnam,
- Cuba, and
- Korea (each 3 percent), as well as the
- Dominican Republic and Guatemala (2 percent each) also were among the top ten countries of origin.
Together, immigrants from these ten countries made up close to 60 percent of all foreign born residing in the United States in 2011.
The predominance of immigrants from Latin American and Asian countries in the late 20th and early 21st centuries starkly contrasts with the trend seen in 1960 when immigrants tended to be from European countries. Italian-born immigrants made up 13 percent of all foreign born in 1960, followed by those born in Germany and Canada (accounting for about 10 percent each). In 1960s no single country accounted for more than 15 percent of the total immigrant population.
TAARIFA KUHUSU KICHINA KUFUNDISHWA CHUONI DODOMA.
Chuo kikuu cha Dodoma
kimethibitisha kwamba Kozi ya lugha ya kichina itaanza kutolewa kwenye
chuo hicho ambapo makamu mkuu wa chuo Profesa Idris Kikula amesema
uamuzi huo umetokana na kukua kwa ushirikiano wa wafanyabiashara wa
China na wafanyabiashara wa Tanzania.
thecitizen.co.tz wameripoti kwamba Profesa kasema chuo chake kilikua na malengo ya kuandaa walimu ambao watakua wakifundisha lugha ya kichina kwenye shule za sekondari Tanzania pamoja na taasisi nyingine za elimu.
Info za uhakika ni kwamba mwaka 2006 wageni kutoka nchi mbalimbali duniani wasiozidi laki mbili walikwenda China kujifunza kichina, na wakati huohuo watu wapatao milioni 20 sehemu mbalimbali duniani wameshajifunza lugha ya kichina
thecitizen.co.tz wameripoti kwamba Profesa kasema chuo chake kilikua na malengo ya kuandaa walimu ambao watakua wakifundisha lugha ya kichina kwenye shule za sekondari Tanzania pamoja na taasisi nyingine za elimu.
Info za uhakika ni kwamba mwaka 2006 wageni kutoka nchi mbalimbali duniani wasiozidi laki mbili walikwenda China kujifunza kichina, na wakati huohuo watu wapatao milioni 20 sehemu mbalimbali duniani wameshajifunza lugha ya kichina
SENTENSI 6 KUHUSU TAARIFA YA MSANII MRISHO MPOTO KUTANGAZA KUGOMBEA UBUNGE.
Jumatatu february 4 2013 msanii
Mrisho Mpoto alitangaza kwa mara ya kwanza kupitia AMPLIFAYA ya CLOUDS
FM kwamba mwaka 2015 ataingia kugombea Ubunge kwenye jimbo lolote
Tanzania ambalo mbunge wake analegalega.
Baada ya taarifa yake kusikika alipokea simu 80 zikiwemo 12 za wanasiasa pamoja na sm 400 kutoka kwa watu mbalimbali ambao wamempongeza na wengine wakimuuliza maswali huku wabunge wakiongea nae kuhusu kujiunga nao.
Namkariri akisema “ni wazo ambalo limetoka kwa wananchi wenyewe wakisema nadhani tumekosea kupeleka mwakilishi, nadhani mwakilishi wetu ni wewe kwa hiyo ile demand ya wananchi imekua kubwa, nikasema hapana sasa lazima niende mwenyewe.
Amesema “nimekua mwakilishi wa wananchi kwa muda mrefu upitia nyimbo zangu lakini watu hawataki kusikia wala kubadilika, tunapozungumzia maisha tunazungumzia madirisha manne, kuna dirisha la kwamba wananchi wanajua wewe hujui, la pili mwananchi anajua wewe hujui, la tatu mwananchi hajui na wewe hujui, la nne wewe unajua mwananchi anajua kwa hiyo dirisha hili wawakilishi wetu wamekua wakitumia vibaya sana wanafikiri wananchi hawajui wao ndio wanajua, ile dhana ya kuona wananchi hawajui ila wao ndio wanajua tunataka tukaionyeshe, tumezungumza sana” – Mpoto
“Hebu angalia mfano mzuri wa pale Mtwara, leo mpaka watu wanakufa mtu anasema siwezi kwenda kusaidia kule kwa sababu mimi mbunge wa jimbo lako, jimbo gani? wewe ni mbunge wa wananchi, unapokua mbunge ni mbunge wa Watanzania wote, watu hawataki kushughulika nao mpaka viongozi wanakuja kutoka huko ndio wanakwenda kule kuzungumza, haya mambo kama yanaweza kuzungumzwa yangetokea? alafu unasema amekufa mtu mmoja tu watu wawili? ile pia ni roho, ile pia ni damu, tumeshindwa kusikilizwa hapa tutasikilizwa tukiwa kulekule ndani ” – Mpoto
Mpoto amesema mpaka sasa anayo kadi ya chama japo hataki kutaja ni chama gani lakini ahadi yake ni kwamba ndani ya wiki chache zijazo atatangaza Exclusive kupitia AMPLIFAYA ni chama gani atakachogombea nacho huku akisisitiza kuwa wananchi wanahitaji vitu vitano tu ambavyo atavieleza wakati utakapofika.
Baada ya taarifa yake kusikika alipokea simu 80 zikiwemo 12 za wanasiasa pamoja na sm 400 kutoka kwa watu mbalimbali ambao wamempongeza na wengine wakimuuliza maswali huku wabunge wakiongea nae kuhusu kujiunga nao.
Namkariri akisema “ni wazo ambalo limetoka kwa wananchi wenyewe wakisema nadhani tumekosea kupeleka mwakilishi, nadhani mwakilishi wetu ni wewe kwa hiyo ile demand ya wananchi imekua kubwa, nikasema hapana sasa lazima niende mwenyewe.
Amesema “nimekua mwakilishi wa wananchi kwa muda mrefu upitia nyimbo zangu lakini watu hawataki kusikia wala kubadilika, tunapozungumzia maisha tunazungumzia madirisha manne, kuna dirisha la kwamba wananchi wanajua wewe hujui, la pili mwananchi anajua wewe hujui, la tatu mwananchi hajui na wewe hujui, la nne wewe unajua mwananchi anajua kwa hiyo dirisha hili wawakilishi wetu wamekua wakitumia vibaya sana wanafikiri wananchi hawajui wao ndio wanajua, ile dhana ya kuona wananchi hawajui ila wao ndio wanajua tunataka tukaionyeshe, tumezungumza sana” – Mpoto
“Hebu angalia mfano mzuri wa pale Mtwara, leo mpaka watu wanakufa mtu anasema siwezi kwenda kusaidia kule kwa sababu mimi mbunge wa jimbo lako, jimbo gani? wewe ni mbunge wa wananchi, unapokua mbunge ni mbunge wa Watanzania wote, watu hawataki kushughulika nao mpaka viongozi wanakuja kutoka huko ndio wanakwenda kule kuzungumza, haya mambo kama yanaweza kuzungumzwa yangetokea? alafu unasema amekufa mtu mmoja tu watu wawili? ile pia ni roho, ile pia ni damu, tumeshindwa kusikilizwa hapa tutasikilizwa tukiwa kulekule ndani ” – Mpoto
Mpoto amesema mpaka sasa anayo kadi ya chama japo hataki kutaja ni chama gani lakini ahadi yake ni kwamba ndani ya wiki chache zijazo atatangaza Exclusive kupitia AMPLIFAYA ni chama gani atakachogombea nacho huku akisisitiza kuwa wananchi wanahitaji vitu vitano tu ambavyo atavieleza wakati utakapofika.
HII NI VIDEO YA DAKIKA 2 ZA RAIS OBAMA AKIONGEA KISWAHILI MWANZONI NA MWISHONI KWENYE MSG YAKE KWA WAKENYA.
Hii ni mara yangu ya kwanza kumsikia Rais Barack Obama wa Marekani akizungumza Kiswahili, ni kwenye hii video hapa chini mwanzoni na mwishoni… pamoja na kwamba ameizungumzia kidogo familia yake nchini Kenya lakini pia amesisitiza Wakenya kuungana pamoja na kuufanya uchaguzi mkuu wa March 2013 kuwa wa amani na wa kidemokrasia.
SABABU ZA ETOO KUSHINDWA KUJA TANZANIA KUICHEZEA CAMEROON FEB 6.
Mwandishi wa habari Shaffih
Dauda ameripoti kwamba nahodha wa timu ya Taifa ya Cameroon Samuel Etoo
amejiondoa kwenye kikosi chake kitakachocheza na Taifa Stars kwenye
mchezo wa kimataifa wa kirafiki february 6 2013 uwanja wa Taifa jijini
Dar Es Salaam.
Mwanzoni Kocha wa Cameroon alisikika kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM akiomba radhi kutokana na baadhi ya wachezaji wake kuchelewa kufika Tanzania na akatoa ahadi kwamba mpaka february 6 asubuhi ana imani wachezaji wote watakua wamewasili.
Sababu hasa ambazo zimemfanya Etoo kushindwa kuja Tanzania safari hii ni matatizo ya mgongo unaomsumbua kwa sasa.
Kwenye line nyingine kocha wa Cameroon kasema sababu zilizofanya wachezaji wengine kuchelewa kufika Tanzania ni nchi za mbali wanapofanyia kazi, wanacheza Ulaya hivyo ni safari ambayo sio fupi.
Mwanzoni Kocha wa Cameroon alisikika kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM akiomba radhi kutokana na baadhi ya wachezaji wake kuchelewa kufika Tanzania na akatoa ahadi kwamba mpaka february 6 asubuhi ana imani wachezaji wote watakua wamewasili.
Sababu hasa ambazo zimemfanya Etoo kushindwa kuja Tanzania safari hii ni matatizo ya mgongo unaomsumbua kwa sasa.
Kwenye line nyingine kocha wa Cameroon kasema sababu zilizofanya wachezaji wengine kuchelewa kufika Tanzania ni nchi za mbali wanapofanyia kazi, wanacheza Ulaya hivyo ni safari ambayo sio fupi.
Subscribe to:
Posts (Atom)