RIPOTI ya Wiki imegundua kuwa, fedha ni hatari kwa afya ya binadamu kwani huweza kusababisha madhara makubwa.
Katika uchunguzi, ilibainika kuwa fedha za noti na zile za sarafu huweza
kukusanya na kusambaza vimelea vya magonjwa hatari kutoka kwa mtu mmoja
kwenda kwa mwingine.
.....SOMA ZAIDI....
Kuhakikisha ukweli wa jambo hilo, Ripoti ya Wiki ilifanya mahojiano na
mtaalam wa magonjwa mbalimbali, Dk. Richard Marise na kusema kuwa tafiti
mbalimbali duniani zimeripoti kuhusu vimelea vinavyoweza kusafirishwa
kupitia fedha ambavyo ni Staphylococcus Aureus, Escherichiacoli,Fecal
Bacteria na sumu nyingine.
“Tafiti nyingi zilizofanywa katika nchi zilizoendelea, zimegundua kuwa
vimelea hatarishi kwenye fedha hasa za noti ambapo vingi hutokana na
uchafu utokao kwa mwanadamu mwenyewe kwa mfano; kinyesi, mkojo na jasho.
“Vimelea hivyo kwa pamoja husababisha magonjwa kama boils (magonjwa ya
ngozi) pneumonia, toxic shock syndrome (homa za sumu mwilini), diarrhea
(kuharisha), gum diseases (magonjwa ya fizi), homa za vipindi na
meningitis (uvumbi wa bongo) ambao kama hakuna matibabu huweza
kusababisha kifo,” alisema Dk. Richard.
No comments:
Post a Comment