facebook likes

Thursday, August 8, 2013

BAADA YA KUKWAMA KWA LUIS, BARCELONA SASA WAMGEUKIA AGGER.


KLABU ya Barcelona ya Hispania sasa imemgeukia beki mahiri wa klabu ya Liverpool, Daniel Agger baada ya ofa yao ya kumtaka beki wa Chelsea David Luiz kukataliwa. 
....SOMA ZAIDI....Chelsea aliweka bayana baada ya kukataa ofa ya Barcelona ya paundi milioni 34.5 kwa kuwaambia kuwa wasijisumbua kuleta ofa nyingine kwani beki beki huyo wa kimataifa wa Brazil hauzwi. Ujumbe huo wa Chelsea umeonekana kuwaingia Barcelona ambapo sasa kuna tetesi kuwa wamegeuzia majeshi yao Liverpool kwa kupelekea ofa ya paundi milioni 17 kwa ajili ya beki huyo wa kimataifa wa Denmark. Ofa hiyo itamuweka meneja wa Liverpool Brendan Rodgers njia panda kutokana na sakata linaloendelea kuhusu uhamisho wa Luis Suarez huku akisisitiza kuwa hawana nia ya kuuza mchezaji wowote kwa kipindi hiki.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...