MSANII
wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ ameswekwa rumande kwa
kudaiwa kuchoma nyumba ya baba wa msanii mwenzake ‘Geez Mabovu’, Mashaka
Mrisho.
Tukio hilo lilitokea Agosti 1, mwaka huu ambapo mwenye nyumba sambamba
na polisi walimkamata Dudu Baya na mkewe Mariam kwa madai ya kuchoma
moto nyumba kwa makusudi na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi
Oysterbay.
“Mkewe alitupia mkaa wa moto katika sofa, likashika moto kabla majirani
hawajanisaidia kuuzima. Baada ya kuwauliza kulikoni wakanitishia maisha
ndipo nikawapeleka polisi na kupewa RB namba OB/RB/13485/2013 na kuja
kumkamata,” alisema Mashaka.
Dudu Baya alipotafutwa na mwandishi wetu, alikiri kukamatwa na kuwekwa
sero kwa saa sita kabla ya kuwekewa dhamana na shemeji yake aliyemtaja
kwa jina la Vero.
“Vyumba vyake na vyangu haviingiliani kabisa, tumetenganishwa na ukuta
hivyo shutuma zake hazina ukweli dhidi yetu ila naamini uchunguzi wa
polisi ndiyo utatoa majibu,” alisema Dudu baya
No comments:
Post a Comment