News, Events, Entertainment, Sports, Lifestyle, Fashion,politics, Beauty, Inspiration and yes... Gossip!
facebook likes
Tuesday, February 19, 2013
JOKATE AZUNGUMZIA MAPENZI YA DAIMOND NA PENNY
Jokate aka kidoti
BAADA
ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupata demu mpya, Penniel Mungilwa
‘Penny’, Jokate Mwegelo ametoa baraka zake kwa jamaa huyo aliyewahi
kudaiwa kuwa mpenzi wake akisema haoni tatizo wawili hao kuwa pamoja
kama kweli wamependana na kuridhiana.
Akizungumza
katika mahojiano maalum alipobanwa kuhusiana na uhusiano wa wapenzi
hao huku ikifahamika kuwa Penny alikuwa shosti wake, Jokate ambaye ni
Miss Tanzania namba 2, 2006/07 alisema kwamba yeye na mrembo huyo
walikuwa washikaji tu na wala hawakuwa na urafiki wa karibu kama baadhi
ya watu wanavyoamini.
Jokate
ambaye pia ni mtangazaji wa Runinga ya Channel O alifunguka kuwa
anawatakia kila la heri na baraka zote Diamond na Penny katika uhusiano
wao mpya wa kimapenzi endapo tu watakuwa wamependana na kuridhiana kwa
dhati.
“Japokuwa sipendi kumuongelea Diamond lakini ukweli sioni tatizo kwa wao kupendana, mimi naona poa tu,” alifunguka Jokate ambaye pia ni bonge la mwigizaji.
Kabla ya kutoka kimapenzi na Penny ambaye naye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Diamond aliwahi kuviteka vyombo vya habari akiripotiwa kuwa na Jokate, kabla ya mambo kwenda mrama.
MATOKEO FORM IV: IDADI YA WALIOFAULU NA WALIOFELI IKO HAPA.
Wizara ya elimu na mafunzo ya
ufundi february 18 2013 imetangaza matokeo ya kidato cha nne 2012 ambapo
yameonyesha kiwango cha kufaulu kimeshuka kwa asilimia kubwa
ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Waziri wa wizara hiyo Dr. Shukuru Kawambwa amesema kati ya wanafunzi laki nne na elfu 56 waliofanya mtihani, wanafunzi laki mbili na elfu 40 sawa na nusu ya wote waliofanya mtihani, wamefeli kwa kupata sifuri ambapo pia matokeo yameonyesha shule binafsi zimeendelea kufanya vizuri ikilinganishwa na shule za serikali huku idadi ya kufaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu nayo ikishuka kwa zaidi ya asilimi 50.
Namkariri Dr Kawambwa akisema “Tathmini ya awali iliyofanywa kuhusu ufaulu wa Watahiniwa katika shule mbalimbali inaonyesha kuwa shule zilizofanya vizuri zaidi ni zile ambazo zina mahitaji yote ya msingi ikiwemo walimu wa kutosha, miundombinu iliyokamilika, vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya kutosha, shule zenye ufaulu wa chini ni zile ambazo zina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukosa walimu wa sayansi na hisabati kwa shule za vijijini, kutokuwepo kwa maabara kwa shule zenye mkondo wa sayansi na kutokuwepo kwa maabara kwa ajili ya kujisomea”
Waliopata division 1 ni wavulana elfu moja na sabini na tatu, wasichana ni mia tano 68 ambapo jumla yao ni 1641, division two wavulana ni elfu 4 mia 4 na 56 na wasichana ni elfu 1 mia 9 na 97 jumla yao ni elfu 6453, division three wavulana na elfu 10 mia 8 na 13 na wasichana ni elfu 4 mia 6 na 13 jumla yao ni elfu 15 mia 4 na 26, ukijumlisha divisio one mpaka three wavulana ni 16342 na wasichana 7178.
Katika mtihani huo jumla ya wanafunzi 728 wamefutiwa majibu ya mtihani wao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya udanganyifu pamoja na kutoa lugha chafu.

SABABU ZA DRAKE KUZUIWA NA MABAUNSA KUINGIA CLUB
Mtandao wa TMZ umeripoti kwamba
rapper Drake alizuiwa kuingia kwenye club moja ya usiku huko Hollywood
Marekani weekend iliyopita.
Sababu hasa ni kwamba hasimu wake, staa mwenzake ambae mwaka jana walirushiana chupa kwenye club moja ya usiku, mwimbaji Chris Brown tayari alikua ameshaingia ndani kwenye club hiyo hivyo mabaunsa walifanya kile walichoelekezwa cha kutoruhusu hizo sura mbili kuingia kwenye club hiyo kwa wakati mmoja.
Club nyingi sasa hivi zinahofia kuwaruhusu wawili hao kuwepo sehemu moja ili kuepuka yaliyotokea kwenye club waliyorushiana chupa ambayo ilifungwa kwa muda, pamoja na watu mbalimbali kudai fidia za kuumizwa kwenye ugomvi wa mastaa hao wawili ambao inaaminika ulikua ni wa kumgombania Rihanna.

Subscribe to:
Posts (Atom)