Rais
Jakaya Kikwete akiwa na Mke wake Mama Salma Kikwete wakizungumza na
Rais Mstaafu wa Marekani Mheshimiwa George Bush wakati wa kikao cha wake
wa Marais wa Afrika kinachofanyika katika hoteli ya Serena hapa Dar es
Salaam.
Rais
Jakaya Kikwete akizungumza na Rais Mstaafu wa Marekani Mheshimiwa
George Bush muda mfupi kabla ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa wake
wa Marais wa Afrika unaofanyika Serena hotel.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Marekani
Mheshimiwa George Bush wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wake wa Marais
na wakuu wa nchi za Afrika unafanyika Dar es Salaam kwa ufadhili wa
Taasisi ya George Bush.
Rais
Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa
Marekani Mheshimiwa George Bush na baadhi ya wake wa marais na wakuu
wa nchi za Afrika muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kuufungua rasmi
mkutano huo kwenye hoteli ya Serena.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete (kkulia) Mke wa Rais wa Marekani, Michelle
Obama (katikati) na Mke wa Rais Mstaafu wa Marekani, Mama Laura Bush,
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wake wa Marais barani Afrika
unaofanyika kwenye hoteli ya Serena.
======== ========= =========
MAMA OBAMA AMPONGEZA MAMA KIKWETE KWA KAZI KUBWA ANAYOFANYA YA KUWASAIDIA WATOTO WA KIKE
Mke
wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama amempongeza Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutoa elimu bure
kwa watoto Wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira
hatarishi .
Mama
Obama alizitoa pongezi hizo jana wakati wa majadiliano baina yake na
Mama Laura Bush kwenye mkutano wa wake Wa Marais Wa afrika unafanyia
katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mama
Obama alisema kuwa wake Wa Marais wanakazi kubwa ya kuhakikisha kuwa
wanawasaidia wanawake na watoto hasa katika upatikanaji Wa elimu na
mahitaji mengine muhimu.
"Juzi
nilitembelea makumbusho ya taifa, nilikutana na watoto ambao baadhi
yao walikuwa ni wale wanaosomeshwa na Mama Kikwete , niliongea nao
watoto hawa wanapatiwa bure elimu, chakula na maladhi hakika nampongeza
sana kwa kazi nzuri anayoifanya", alisema Mama Obama.
Akiongea
wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mama Kikwete alisema kuwa wake wa
Marais waliohudhuria mkutano huo wanawawakilisha wanawake wa Afrika
ambao wanahitaji kusaidiwa katika mambo ya afya, elimu na
ujasiriamali.
Mama
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) alisema kuwa katika mkutano huo washiriki watapata nafasi ya
kubadilishana ujuzi wa kazi na kutembelea hospitali ya Kansa ya Ocen
Road,kituo cha Mabinti na hospitali ya CCBRT ambako watajionea jitihada
kubwa zinazofanywa na watanzania za kuisaidia jamii inayowazunguka.
Alisema
kuwa baada ya kumalizika kwa mkutano huo anaamini kuwa washiriki
watarudi katika nchi zao na kuweza kukubaliana na Serikali zao pamoja na
wadau Wa wengine kuwekeza zaidi kwa wanawake ili kuimarisha bara la
Afrika.
Mkutano
huo wa siku mbili umeandaliwa na Taasisi ya Rais mstaafu wa Marekani
George Bush na kuhudhuriwa na baadhi ya wake Wa Marais wa Afrika na Mke
wa Waziri mkuu mstaafu Wa Uingereza Cherie Blair.
Mada
kuu ni wekeza kwa wanawake imarisha Afrika lengo l ikiwa ni kuimarisha
upatikanaji wa Afya kwa wanawake, upatikanaji Wa elimu na uchumi katika
Afrika.
Credit: Michuzi.