facebook likes

Thursday, August 8, 2013

TUZO ZA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA KUFANYIKA LAGOS MAPEMA MWAKANI.


SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limetangaza kuwa sherehe za utoaji tuzo kwa wachezaji wa Afrika zitafanyika Januari 9 mwakani jijini Lagos, Nigeria. 
...SOMA ZAIDI....
Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa Lagos kuwa mwenyeji wa sherehe hizo toka mwaka 2008 wakati Emmanuel Adebayor aliposhinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka akiwashinda Mohamed Abou Treika wa Misri na Michael Essien wa Ghana. Sherehe za tuzo hizo zitakuwa zimegawanyika katika makundi 13 huku tuzo mchezaji bora wa mwaka wa Afrika ikiongoza orodha hiyo. Kiungo wa mahiri wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Manchester City, Yaya Toure ndio mshindi wa tuzo hiyo kwa miaka miwili iliyopita.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...