Kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas hatimaye amevunja ukimya kuhusu
suala la Manchester United kutaka kumsajili kwa kusema anataka kubaki
nchini Spain.
Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal akiongea kwenye mkutano wa
waandishi wa habari jijini Kuala Lumpur mahala ambapo Barcelona wapo
kwa ajili ya maadalizi ya msimu mpya.
Fabregas alisema: 'Ndoto yangu siku zote imekuwa kuichezea Barcelona
na hakuna kilichobadilika. Nina furaha sana kuwa hapa na sijawahi
kufikiria kuhusu kuondoka.
"Sijawahi kuwa na shaka juu hilo. Haijanigharimu chochote kurudi Barcelona na sasa nataka kuwa mshindi nikiwa hapa.
'Siku zote nimekuwa nikitambua ninavyothaminiwa na klabu. Kila mut
ameniambia namna anavyonitegemea, sijwahi kupata ishara yoyote tofauti
ya kuhisi sihitajiki.
'Sikutaka kusema lolote huko mwanzo kwa sababu kwangu mimi kila kitu
kilikuwa wazi kwamba nilikuwa nataka kuendelea kubaki hapa. Niliiambia
klabu nitaongea itakapofika zamu yangu.
'Kuna baadhi ya vitu vilitengenezwa, lakini havikuwa vya kweli - hasa
la kusema kwamba nimeomba kuongezewa mkataba,' alisisitiza Cesc
Fabregas
No comments:
Post a Comment