LIVERPOOL imeonyesha inaweza kuishi bila
Luis Suarez anayetaka kuondoka, baada ya kuendelea vema na mechi zake
za kujiandaa na msimu.
Pamoja na habari za Luis Suarez kuondoka
kuwa ajenda kuu kwa sasa, kikosi cha Brendan Rodgers leo kimeifumua
valeranga mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Ullevaal, mjini Oslo, Norway katika mchezo wa kirafiki.Ushindi: Liverpool imeifunga Valerenga 3-1 kwenye Uwanja wa Ullevaal, Oslo leo
Shukrani kwao wafungaji wa mabao ya leo,
Luis Alberto, Iago Aspas, Martin Kelly na Raheem Sterling katika mchezo
wa leo, Liverpool ikishuhudiwa na mmiliki wake, John W Henry kwa mara
ya kwanza baada ya miezi 13 ikiweka rekodi ya kushinda mechi ya sita.
Alberto alifunga dakika ya 31, Aspas
dakika ya 42, Kelly dakika ya 54 na Sterling dakika ya 90, wakati bao la
wenyeji lilifungwa na Giancarlo Gonzalez dakika ya 35.
Kikosi cha Liverpool leo kilikuwa: Jones/Mignolet
dk46, Alberto/Coutinho dk46, Aspas/Borini dk46, Henderson/Gerrard dk46,
Coates/Toure dk46, Downing/Sterling dk46, Spearing/Kelly dk46,
Allen/Lucas dk46, Flanagan/Enrique dk46, Ibe/Assaidi dk46 na Wisdom.
Valerenga: Kongshavn/Knutsen dk85,
Larsen/Wawrzynkiewicz dk51, Gonzalez, Hogh, Lecjaks, Ogude/Nasberg dk62,
Zajic/Haested dk57, Holm/Zahid dk57, Fellah, Berre/Borven dk67 na
Calvo.
Joe Allen akishuhudia shuti la Luis Alberto (hayupo pichani) likitinga nyavuni
Iago Aspas akiifungia Liverpool kabla ya mapumziko
Mashabiki wa Liverpool mjini Oslo wakionyesha kumuunga mkono kocha Brendan Rodgers na timu yake
Joe Allen akitoa pasi huku akizongwa na mchezaji wa Valerenga, Mohamed Fellah
Kwenye kipaza: Gwiji wa Liverpool, Ian Rush akifanyiwa mahojiano wakati wa mapumziko
No comments:
Post a Comment