facebook likes

Tuesday, July 16, 2013

SAKATA LA DIAMOND NA UWOYA LUIZA MBUTU AWAPA SOMO


Kiongozi  na mwimbaji mkongwe  wa bendi ya 'Twanga Pepeta' luiza Mbutu amefunguka na kuonyesha  kukerwa kwake na tabia ya baadhi ya wasanii wa filamu na bongofleva wanaojihusisha na skendo za kimapenzi na kuamua kuwafunda ka kuwapa somo kali.Akizungumza na mwandishi wetu kwenye  hivi karibuni luiza alidai kwamba wasanii wa fani zote ni kioo cha jamii hivyo kitendo cha baadhi ya wasanii kujihusisha na mambo yasio kubalika kwenye jamii wakati wao ni kioo cha jamii  ni sawa na kuipotosha jamii hiyo inayowatazama.

BREAKING NEWS: BAADA YA MAN UNITED KUPELEKA OFA BARCA - FABREGAS ASEMA ANATAKA KUENDELEA KUBAKI CAMP NOU


Siku chache baada ya kumkosa Thiago Alcantara inaonekana sasa Manchester United ipo njiani kumkosa mchezaji mwingine kutoka FC Barcelona, Cesc Fabregas. Hii inakuja baada ya kocha wa klabu hiyo  Tito Vilanova kusema kwamba ameongea na kiungo huyo wa Spain na ameambia na mchezaji huyo kwamba anahitaji kuendelea kubaki Camp Nou. 

Jana jumatatu iliripotiwa kwamba United walituma ofa ya kwanza ya kiasi cha £25.9 million  kwa ajili ya kumsajili Fabregas, ambaye amefeli kupata nafasi katika kikosi cha kwanza tangu aliporudi akitokea Arsenal.
Lakini akiongea na waandishi wa habari leo mchana, Vilanova amesema wazi kwamba Fabregas bado anataka kubaki kwenye klabu yake hiyo ya utotoni, na hana mawazo ya kuondoka kwa sasa.
 "Ninafahamu kwamba tumepokea ofa kadhaa kutoka kwa vilabu tofauti. Niliongea na Cesc na ameniambia kwamba anataka kubaki.
"Cesc hana mawazo ya kuondoka kwenda klabu nyingine. Anajua ushindani ni mkubwa hapa na ana ndoto za kuendelea kuwa hapa na kufanikiwa.


AUNT EZEKIEL AMTOSA MUMEWE KIPINDI HIKI



Wengi  walitegemea  kuwa  Aunt  Ezekiel ataungana  na  mumewe Sunday  katika  kipindi  hiki  cha  mwezi  mtukufu wa Ramadhani  lakini  hali  imekuwa  ni  tofauti....
Aunt  anayetumia  jina  la  Rahma  baada  ya  kubadili  dini  ili  aolewe  na  mwanaume  huyo,   amemtosa  mkaka  huyo  na  kuendelea  kula  bata  nchini  huku  akidai  kuwa  mumewe  hana  mengi.


"Sina  mpango  wowote  wa  kuondoka  nchini  kumfuata  mwanaume.Yeye  ni  mume  wangu, ntamkuta  tu  hata  nikienda  mwakani.

"Kwanza  mume  wangu  hana  mengi  na  si  mkorofi  na  anajua  wazi  kwamba  sipendi  kubanwa.Kwa  sasa  nina  mambo  mengi  likiwemo  hili  la  kuisambaza  filamu  yangu  mpya  ya  Scola  mwezi  ujao"...Alisema  aunt  Ezekiel
 
source: thechoicetz

Ney wa Mitego, baada ya ujauzito wa GF wake kutoka: Namuachia Mwenyezi Mungu, tutajaaliwa mwingine nafkiri may be ndio itakuwa rizki yetu.


 
Girlfiend wa Rapper Ney wa Mitego "Siwema" ambae alikuwa na ujauzito wa Rapper huyo, bad news ni kuwa mimba hiyo imetoka mara baada ya kuanguka akiwa bafuni baada ya kusikia kizunguzungu. Ney wa Mitego ameeleza kisa kilivyotokea.

"Alianguka nini bahati mbaya ndio kama hivyo, namuachia mwenyezi mungu, tutajaaliwa mwingine nafkiri may be ndio itakuwa rizki yetu.
Ilikuwa ijumaa mida ya mchana mchana, alikuwa kazini akasema kichwa kama kinamuuma hivi,akaniambia bana mi natoka hapa sijiskii vizuri acha nirudi home, alivyorudi home akawa ameingia kuoga, alivyoingia kuoga aakajiskia kizungu zungu akadondoka bafuni, akawa amepoteza fahamu kama siku nzima, kwahiyo mwisho wa siku nikawa naongea na Dr, akawa anafight katika juhudi zake zote kasema hapa lazima tuokoe kimoja, kwahiyo tuangalie tufanye nini, tufanya maamuzi ya kitu uzima, kwahiyo tukajua, tukasema no way out inabidi tu afanye tu anachokiweza yeyey Dr." amesema Ney wa Mitego.

Nu Video: Sina Imani Shettah feat Rich Mavoco






 

















Ile video ya wimbo wa Shettah ambao wengi wanauita usilete ukimwi nyumbani ila jina lake halisi ni "Sina Imani" imekamilika, mkono wa producer akiwa ni Adam Juma (kabla hajaacha kutengeneza video za mziki) kutoka Next Level..

Nu video: Love Me by Izzo Bizness Feat Barnaba na Shaah





















 Ile video iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Izzo tangu ilipodondoshwa ngoma, leo hii iko tayari kwa ajili ya macho yako. video imefanywa na Emedia chini ya Nick Dizzo

GERRARD KUSAINI MIAKA MIWILI ZAIDI LIVERPOOL.


NAHODHA wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na klabu hiyo baadae leo. Mazungumzo baina ya wakala wa Gerrard na mkurugenzi mtendaji wa Liverpool Ian Ayre yamekuwa yakiendelea toka mwishoni mwa msimu uliopita na pande hizo mbili zimefikia makubaliano ambaye yatamuweka Gerrard Anfield katika kipindi cha miaka miwili ijayo. Mkataba wa sasa wa Gerrard unamalizika mwishoni mwa msimu ujao lakini meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amemuhakikishia kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 kuendelea kuwepo hapo siku zijazo. Ni zaidi ya miaka 14 toka Gerrard alipoanza kuchezea kikosi cha kwanza cha Liverpool na mkataba mpya atakaosaini utamuhakikishia kumaliza soka lake katika klabu hiyohiyo. Liverpool imeanza ziara yake ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi huku Australia na barani Asia.

Hawa ndio Watanzania wawili walioingia kwenye hii list ya Mamilionea 10 wa kutazamwa Afrika 2013

Patrick Ngowi 

Ninao uhakika kwamba hii ni ripoti nyingine ya kutoa nguvu kwa vijana ambao wamekata tamaa au bado hawaamini katika kile wanachoweza kukifanya kwa nguvu zao na akili zao, vijana ambao bado fikra zao ziko kwenye imani kwamba Matajiri wote wa sasa walianza kuingiza mamilioni mwezi wa kwanza tu baada ya kuanza biashara…. hawa hapa chini ni vijana chini ya umri wa miaka 39, wote ni kutoka Afrika na kila mmoja ana stori yake ya kuanzia mbali kimaisha…
Kwa mara nyingine tena kijana wa Kitanzania Patrick Ngowi (28) ametokelezea kwenye list ya Jarida maarufu la Forbes lakini kwa sasa katajwa kwenye 10 bora ya vijana wa Kiafrika mamilionea wa kutazamwa mwaka 2013 ambapo kampuni yake ya Helvetic Solar inayojishughulisha na ishu za umeme wa Solar inatarajiwa kuingiza dola za Kimarekani milioni saba kabla ya mwaka 2013 kumalizika.
Ni Mtanzania ambae aliwahi kusota sana kwenye kuzitafuta pesa, biashara yake ya kwanza ilikua ni vocha lakini kwa uvumilivu na malengo aliyokua nayo, kutokukata tamaa na kuota kuzifanyia kazi fikra za mbali ambazo vijana wengi wanazo ila hawajui jinsi ya kuzifikia, ndio kumempa haya mafanikio aliyonayo leo.
Ngowi
Mtanzania mwingine alietajwa kwenye hii list ni Mbunge wa Singida mjini (CCM) Mohammed Dewji a.k.a Mo Dewji mwenye umri wa miaka 38 ambae pia ni Young Global Leader kwenye World Economic Forum akiwa ni CEO wa METL ambayo unaambiwa imeajiri zaidi ya watu elfu 24
Mo Dewji Forbes
Dewji
Wengine ni Gerald Wamalwa (28) wa South Afrika, Sibongile Sambo, South Africa , Khanyi DhlomoSouth Africa , Colin Thornton, South Africa, Alan Knott-Craig Jr.South Africa, Igho Sanomi, Nigeria, Quinton van der Burgh, South Africa, Gerald Wamalwa, Kenya
na Ken Njoroge mwenye umri wa miaka 37 ambae ni Mkenya pia.

Barcelona kumpoteza nyota wake mwingine?

Cesc Fabregas akiwa na washkaji zake Gerard Pique na Sergio Busquets.
Cesc Fabregas akiwa na washkaji zake Gerard Pique na Sergio Busquets.
Zikiwa zimepita saa karibu 24 tangu ilipotangazwa kuwa Bayern Munich wamekamilisha usajili wa Thiago Alcantarra , Barcelona huenda wakalazimika kupoteza mchezaji mwingine wa safu ya kiungo baada ya  klabu ya Manchester United kutuma ofa ya kumsajili kiungo Cesc fabregas . United wakiugulia machungu ya kumkosa Thiago wametuma ofa ya paundi milioni 26 kwa ajili ya Fabregas wakiwa kwenye harakati za kuimarisha kikosi chake hasa nafasi ya kiungo ambayo kocha mpya David Moyes anaiona inahitaji kuongezewa nguvu .

Je Cesc ataungana na mshkaji wake wa nguvu wa enzi hizo RVP ndani ya Old Traford?
Je Cesc ataungana na mshkaji wake wa nguvu wa enzi hizo RVP ndani ya Old Traford?
United baada ya kutangaza hapo jana kuwa wana fedha za kufanya usajili wa nyota yoyote ambaye Moyes atamhitaji kwenye kikosi chake walipata pigo la kwanza baada ya taarifa ya Thiago kwenda Bayern kutoka rasmi baada ya mchezaji huyo kuripotiwa kuwa kwenye rada za David Moyes ambaye amekuwa akimtazama kama mrithi wa muda mrefu wa kiungo Paul Scholes ambaye amestaafu .
Usajili wa Fabregas hautakuwa rahisi kwani mchezaji huyo aliwahi kuichezea Arsenal siku za nyuma na klabu hiyo (Arsenal) ina chaguo la kwanza la kumsajili au kukataa kumsajili Cesc kwa mujibu wa mkataba wake wakati alipouzwa toka Arsenal kwenda Barca misimu miwili iliyopita .
Ugumu mwingine unatokana na ukweli kuwa Fabregas ana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Barca na haitakuwa rahisi kwa klabu hiyo kuruhusu kiungo mwingine kuondoka baada ya Thiago . Hata hivyo maisha ya Fabregas tangu arejee Barca toka Arsenal hayajakuwa mepesi kama ilivyotarajiwa na wengi na kocha aliyeondoka Pep Guardiola aliwahi kupendekeza kuuzwa kwa mchezaji huyo baada kutoridhishwa na na kiwango chake .

KALI YA LEO: SHABIKI WA MAN UNITED AMBAYE HAJAWAHI KUKOSA MECHI OLD TRAFFORD TANGU MWAKA 1974 - ALIIKOSA HARUSI YA NDUGU YAKE NA KWENDA KUIONA UNITED




Shabiki wa Manchester United Bwana Peter Bolton inawezekana ndiye mshabiki namba moja wa timu hiyo.
Bolton mwenye miaka 56 ambaye anatarajiwa kukwea pipa kuifuata United kwenye ziara ya pre-season tour barani Asia na Australia, hajawahi kukosa mchezo hata mmoja wa United ndani ya Old Trafford tangu mwaka 1974 na Bolton aliwahi hata kuamua kukosa harusi ya kaka kwa ajili ya mechi ya United. 

 ‘Nilipokutana na mke wangu mwaka 1976 kwenye ukumbi wa disco, aliniuliza kama ningeenda tena wiki ijayo. Nilimjibu “Hapana, nitaenda kuangalia mechi dhidi ya Spurs White Hart Lane, tangu siku hiyo aligundua maisha yangu yanazungukwa na soka. Mwaka 1979, tulikuwa tumepanga kufunga ndoa na ilibidi nichague mwezi wa sita - kwa sababu nilijua hakuna soka mwezi huo!’
Present and correct: Man United super-fan Peter Bolton with the World Club Cup in a photograph from 2008

‘Wakati kaka yangu alipokuwa anaoa, alipanga tarehe ambayo iliangukia wikiendi katikati ya msimu. Nilibaki njia panda kwa sababu kulikuwa kuna mechi ya United ikicheza.... baadae niliamua kwenda kuangalia mechi Old Trafford na usiku nikaenda kwenye party ya harusi. Kaka yangu hakukasirika, alifahamu namna ninavyopenda kuiona United ikicheza.’

Wiki hii, Bolton anakwea pipa kwenda Sydney kwa ajili ya kuiangalia timu yake aipendayo ikijiandaa na msimu mpya - hakuenda Bangkok lakini sasa atakuwa na wiki tatu zenye mihangaiko kuliko akisafiri maili 30,000 na kutumia masaa zaidi ya 50 hewani kuifuata timu ya David Moyes kwenye pre season. 
Bolton, ambaye anaishi maili kadhaa kutoka Old Trafford huko Timperley, anasema: ‘Nina mashaka kama nitabakiza chochote katika hizi £5,000 ndani ya kipindi cha wiki 3 zijazo. Ni vigumu kusema, kwa sababu huwezi kutabiri matumizi ya fedha lakini sina cha kujutia kwa sababu naenda kuiangalia timu yangu.
'Nina fahamu namna safari yangu itakavyokuwa, nitasafiri kwa umbali wa maili 30,000 na masaa kama 55 hewani. Tatizo ni kwamba hakuna hata ndege moja itakayokuwa ikienda moja kwa moja. 
Club legend: Gary Neville stands next to Bolton's One Love United flag
 Gary Neville akisimama na bendera ya bwana Bolton yenye maandishi ya 'One Love'
‘Nitatoka Manchester mpaka Sydney kupitia Dubai. Then Sydney mpaka Yokohama kupitia South Korea. Halafu nitachukua treni mpaka Osaka kabla ya kuelekea Hong Kong kupitia Shanghai. Halafu nitakuwa narudi nyumbani Manchester kupitia Dubai na baada ya hapo safari itakuwa inaelekea Stockholm Sweden. Lakini hata kutokea kurudi nyumbani itabidi nipitie Oslo!'
Bolton, ambaye ameshahudhuria mechi za United za nyumbani zaidi ya 1,000 mfululizo na amekuwa akishabikiwa United tangu mwaka 1962, pia amekuwa akifuatilia mechi za timu ya vijana ya United pale Old Trafford.
‘Niliangalia michezo 120 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Ikiwa timu ya wakubwa haichezi, najaribu kufuatila timu ya vijana na timu ya reserve pia nyumbani na ugenini. Mwaka uliopita nilienda kuangalia wakicheza na Swansea na Southampton ugenini nikiisapoti timu ya vijana.
‘Mke wangu anajua ninavyopenda soka na kuna siku nyingi ndani ya mwaka ambazo ninatumia kuwa nae na familia kiujumla. Kwangu mimi soka ni kama kilevi changu, kwangu mimi ni familia na soka ndio vitu muhimu.'
Brilliant trip: Bolton and his flag in the San Mames - he says Athletic Bilbao are the most welcoming fans
Bolton na bendera yake ya akiishangilia United. Amesema kwamba mashabiki wa Atletico Bilbao ndio wastaarabu kuliko wote ambao amewahi kukutana nao. 

KIKOSI CHA KWANZA CHA WACHEZAJI WAHALIFU WA KISHERIA: MESSI, SUAREZ, DE GEA NA WENGINEO


Siku chache zilizopita mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutuhumiwa kukwepa kodi. Alifunguliwa kesi lakini mwishowe akaamua kulipa kiasi cha $19m kumaliza kesi hiyo nje ya mahakama.

Makala hii inajaribu kupanga kikosi cha wachezaji ambao wameshawahi kutuhumiwa na makosa ya kisheria. Kinawahusisha wanasoka ambao wameshawah kutuhumiwa na kukutwa na hatia ya makosa ya ubakaji, wizi, na hata kupigana. 

Golikipa: David De Gea - Manchester United
 Mapema mwaka 2011, baada ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na United David De Gea alikutwa na tuhuma za kuiba maandazi katika supermarket ya Tesco. Alijitetea kwamba aliondoa kwenye supermarket na kuenda kwenye gari ili kufuata fedha za kulipa, lakini tayari taswira yake iliharibiwa na tuhuma hizo. 

Beki wa Kulia: Micah Richards - Manchester City. 
Huyu alikutwa na hatia ya kukimbia kulipa fedha za kupaki gari lake, pia alikutwa na makosa ya kuendesha gari kwa kasi sana. Kijana huyu anayelipwa mamilioni ya fedha na waarabu wa City kwa sasa anatumikia adhabu ya kutoendesha gari gari. 

Beki wa kati: Titus Bramble - Sunderland.

 Huyu inawezekana ni mmoja wa mabeki wabovu wa premier league, anatuhumiwa na kesi ya ubakaji. Yeyey na mdogo wake Tesfaye Bramble wote walithumiwa kumbaka msichana mmoja lakini kwa bahati nzuri kwake alikutwa hana makosa na mdogo wake akifungwa kwa kosa hilo. 

Beki wa kati: John Terry - Chelsea. 
Terry ametuhumiwa na makosa makubwa mawili. Alikutwa na hatia na FA kwa kosa la kumtukana kibaguzi Anton Ferdinand na alipewa adhabu ya kusimamishwa mechi kadhaa. Pia aliwahi kukiri kulala na mke wa mchezaji mwenzie wa Chelsea Wayne Bridge.

Beki wa kushoto: Danilo Larangeira - Udinese. 
Huyu ni mbaguzi wa rangi. Alimuita mchezaji mweusi 'nyani' na akashtakiwa kwa kosa hilo na kukutwa na hatia - akapewa adhabu ya kulipa faini na kusimamishwa mechi kadhaa.

Kiungo wa kati: Joey Barton - QPR. 

Inawezekana ndio mchezaji ambaye ametuhumiwa kwa makosa mengi kuliko wote kwenye kikosi hiki.  Kuendesha gari kwa kasi kubwa, Kupigana, Kuendesha huku amelewa, kupigana na mapolisi na listi inaendelea zaidi. Mwaka huu alijaribu hata kuwatukana Neymar na Thiago Silva kuwaita majina ya ajabu ajabu.Njia pekee ya kumzungumiza huyu ni kumuita kichaa. 

Kiungo wa kati:  Lee Catermole - Sunderland.

 Huyu hafahamiki sana, lakini amekuwa akishikwa sana na mkono wa kisheria. Amekuwa akipigana sana kwenye mabaa na ameshakaa sana rumande, kwa sasa yupo kwenye program iitwayo 'PubWatch' kumuangalia kila anachokifanya akiingia kwenye mabaa.

Winga wa kulia: Jermaine Pennant - Stoke City.

Aliwahi kushtakiwa kwa kutumia madawa ya kulevya, pia amekuwa na sifa ya kupigana kwenye mabaa, aliwahi kufungwa kwa kosa la kuendesha huku amelewa na kusababisha ajali. Amewahi kuvitumikia vikosi vya Arsenal na Liverpool.

Winga wa kushoto: Frank Riberry - Bayern Munich.

Winga huyu wa Bayern Munich anatuhumiwa na kesi ya ubakaji kwa kufanya mapenzi na changudoa ambaye ana umri mdogo. Alikuwa kwenye timu ya taifa ya Ufaransa na akaagiza aitiwe changudoa chumbani kwake ndipo alipokutana na binti huyo mdogo. 

Mshambuliaji: Luis Suarez - Liverpool

Hapa nilipata mtihani kidogo kuchagua kati ya Suarez au Balotelli, lakini mshambuliaji huyu wa Liverpool ameweza kushinda kuchukua jukumu la mshambuliaji wa kati. Ameshakutwa na hatia katika kesi za ubaguzi, kung'ata wachezaji wenzie, pamoja na kuwapiga. Ni mshambuliaji mkali lakini ana vituko mno.  

Mshambuliaji: Marlon King. 
Aliwahi kukaa jela miezi 18. Alikutwa na hatia kwa kumpiga kichwa mchezaji mwenzie Dean Windass wakiwa casino. Aliiba gari la BMW. Kwa ujumla ameshawahi kukutwa na hatia ya makosa ya jinai, likiwemo la kumpiga ngumi ya kichwa msichana wake, kuendesha kwa kasi huku akiwa amelewa. 

Huyu anastahili nafasi mbele ya Lionel Messi mwenye kesi ya kukwepa kodi, na mtukutu Balotelli.

Status ya Chidi Benz kuhusu dawa za kulevya.

.

.
Hii ni status ya July 15 2013 kwenye facebook ya Rapper Chidi Benz ambae mwaka 2011 alitangaza kuachana na uvutaji wa bangi ambao alikiri ulimfanya afanye mambo mengi yasiyo mazuri na hata kutoa picha mbaya kwa watu mbalimbali iliyotokana pia na ukorofi wa kupiga watu mara kwa mara. Chidi Benz on dawa za kulevya July 15 2013 Chidi Benz on dawa za kulevya July 15 2013 COMMENTS Chidi Benz on dawa za kulevya July 15 2013 COMMENTS 2

DRC kuwa uwanja wa 'VITA WAKALA' (Proxy War) Kati ya Tanzania na Rwanda?



Proxy War au Proxy Warfare ni vita inayopiganwa kwa kupitia sehemu nyingine. Katika vita 'ya kawaida' mapigano huwa kati ya nchi na nchi.Kwa mfano, Vita ya Kagera ilkuwa kati ya Tanzania na Uganda, na mapambano yalitokea katika nch zote mbili.

Katika proxy war hali ni tofauti. Nchi A inaweza kupigana vita na nchi B katika nchi C.Yaani kwa ufasaha zaidi, kwa mfano, kuna mapambano katika nchi C kati ya jeshi la nchi hiyo na waasi, kisha nchi A inapeleka askari wake kuilisaidia jeshi la serikali la nchi C, na nchi B inapeleka askari wake (au inasaidia kwa siri) kusaidia waasi wanaopigana na serikali ya nchi C.

Naomba ieleweke kuwa mie sio nabii wa waangamizi, kwa kimombo 'prophet of doom.' Ninachoongelea hapa kinatokana tu na hali halisi ilivyo kwenye mapigano yanayoendelea nchi DRC kati ya jeshi la Serikali ya nchi hiyo na kikundi cha waasi cha M23.

Nchi yetu imetoa wanajeshi kadhaa kushirikiana na Malawi na Afrika Kusini kuunda kikosi cha kulinda amani nchini DRC. Lakini kuna taarifa kuwa waasi wa M23 wanapewa sapoti na Rwanda (kama ni kweli au la,mie sina hakika...lakini lisemwalo lipo...kwanini Rwanda ituhumiwe na si Kenya au Msumbiji?)

Sasa tukiangalia hali ya uhusinao kati ya Tanzania na Rwanda katika siku za hivi karibuni, na tukijikumbusha kauli ya Rais Paul Kagame kuwa "atamsbiri (Rais Jakaya) Kikwete mahala mwafaka kisha mtandike" kuna uwezekano "mahala hapo mwafaka" kuwa ni DRC. 

Kwanini ninasema hivyo? Uwezekano wa Rwanda kuivamia Tanzania au Tanzania kuivamia Rwanda ni mdogo sana,kutokana na sababu mbalimbali. Lakini nchi hizo mbili zinaweza 'kupigana vita kirahisi' kupitia mapigano yanayoendelea kati ya Jeshi la DRC linalosaidiwa na 'Kikosi cha Kimataifa' (kinachojumuisha Jeshi la Tanzania) na waasi wa M23 (wanaodaiwa kusaidiwa na Rwanda.)

Vyovyote itakavyokuwa, vita ni kitu kibaya, natunapaswa kuombea kistokee kwa gharama yoyote ile.Mwanafalsafa mahiri wa 'Sanaa ya Vita' (Art of War), Mchina SUN TZU anatahadharisha kuwa "vita ni suala la uhai na kifo, barabara inayoelekea kwenye usalama au maangamizi..."

Kuna wanaojidanganya kuwa Rwanda "ni kijinchi kidogo kisicho na uwezo wa kupambana na Tanzania." I wish wangekuwa sahihi.Kwa mujibu wa SUN TZU, ushindi katika vita yoyote ile unategemea sana matumizi ya mashushushu (wapelelezi) wa ndani na wa nje.Hivi tunafahamu kuwa tuna Wanyarwanda wangapi Tanzania ambao wapo mahsusi katika kufanikisha azma yoyote ile ya nchi yao?Kwa maafisa wetu uhamiaji ambao bia mbili tatu tu wapo tayari kumpa mtu passport ya Kitanzania, tuna maadui wangapi wanaotengeneza idadi yetu kukaribia milioni 50? 

Soma hapa http://suntzusaid.com/book/13 kufahamu zaidi kuhusu matumizi ya mashushushu katika vita, kwa mujibu wa SUN TZU.(na jaribu kupigia mstari uhusiano wetu wa Malawi na uwezekano wao kuwa mojawapo ya aina hizo za mashushushu)

Anyway, kama nilivyobainisha hapo awali, mie sio nabii wa majanga.Ningependa sana askari wetu waliokwenda huko DRC watimize jukumu lao haraka na kurejea nyumbani wakiwa salama WOTE. Nilichoeleza kuhusu PROXY WAR ni uchambuzi tu unaozingatia hali halisi.
 
source: jiachie

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...