facebook likes

Thursday, July 4, 2013

Picha 11 za jinsi huyu anaetuhumiwa kuwa tapeli anaetumia jina la Jokate Mwegelo alivyokamatwa


.
.
Aliefanikisha huyu jamaa kukamatwa ni mrembo mmoja model Blessing ambae alishiriki Miss Morogoro 2013 ambapo namkariri akisema “wiki mbili zilizopita nilipata msg kwamba Kidoti hair na Mzinga Planet wanahitaji mamodo kwa ajili ya kutengeneza matangazo kwa ajili ya nywele za kidoti, tulikua Morogoro kwa ajili ya Miss Morogoro tukaja Dar mpaka Mzalendo Pub msg ilipotuelekeza lakini nilivyoingia sikuona mtu ambae anahusiana na Jokate, niliona watu ambao nawajua lakini sio kuhusu nywele’
‘Nikampigia kaka mmoja anaitwa Johnson kwa sababu najua anafahamiana na Jokate, nikampigia kumfokea kumwambia nyinyi vipi mbona mmetangaza audition alafu sioni hata mtu mmoja ambae anahusika? naona watu ambao kampuni zao zipo majumbani kwao? baada ya dakika zaidi ya 10 kina Jokate wakawa wameshafika japo baadhi ya mamodo wengine walikua wameshaondoka lakini baadhi ya viongozi kama Majaji wa kike walikuepo na walipoulizwa wakasema tumsubiri Mpeka ambae ndio muhusika na pia Mkurugenzi wa Mzinga Planet” – Blessing
Baada ya kina Jokate kufika Mpeka alipigiwa simu ili arudi Mzalendo Pub, japo alisita sana mtuhumiwa huyu alikuja kwenye eneo la tukio na kukutana uso kwa uso na Jokate na timu yake, baada ya hapo akaanza kusingizia kwamba yeye hausiki ila kuna watu wengine ndio wanahusika ila alipotoa namba zao wakapigiwa simu, kila mmoja alionekana kutaharuki kwa sababu hawajui chochote kuhusu hiyo Mzinga Planet.
Baada ya Jokate na timu yake kukaa na Mpeka na kumuuliza kistaarabu bila kutoa ushirikiano wa kutosha, uamuzi ulitoka kwamba apelekwe Polisi Osterbay ili kuendelea na taratibu nyingine za kisheria.
Mpeka alikua anaonekana analia wakati mwingie na hiyo ilikua ni baada ya kumpiga huyu msichana shuhuda aitwae Blessing kwa sababu alimchomea mpaka akakamtwa.
.
Msg alizotumia watu kwenye facebook na msg za simu za mkononi.
.
Huyu dada hapa kushoto alikua mmoja wa majaji, anasema alikua hajui lolote kama ni utapeli ulikua unafanyika.
.
Mzalendo Pub.
.
.
.
.
.
Hapa ni wakati Jokate alipoamua kukaa na Mpeka kistaarabu kuongea nae kabla ya hatua za kisheria
Jokate amesema “miongoni mwa mabinti waliowahi kutapeliwa na matapeli wanaotumia jina la Jokate Mwegelo au Kidoti ni pamoja na mrembo mmoja alipelekwa kwenye hoteli Arusha ambapo mwanaume alimwambia kama atalala nae hotelini atapata fursa ya kuwa model wa Kidoti, alilala nae siku tatu hotelini alafu baadae mwanaume akaondoka ghafla na kuiba simu za huyu mrembo na laptop na hata bili akamwachia yule msichana ndio alipe”
Hii audition aliyoifanya Mpeka, usaili mdogo ambao ni Wasichana takribani arobaini walijitokeza, ‘mtu akisikia tangazo kama hili au kama nikiwa na kitu ofcourse watu watakisikia kwenye Amplifaya au millardayo.com na pia niko twitter @JokateM kwa hiyo itakua ni rahisi kutambua kweli kama hiki kitu kimetoka kwa Jokate’
.
.
.
Polisi Osterbay.
.
.


Ryan Giggs si amepewa cheo kipya Manchester United leo aisee.. ni cheo gani?



ryan-giggs-football-sport-celebrity
Kiungo/winga wa muda mrefu wa klabu ya Manchester United Ryan Giggs ameteuliwa kuwa kocha mchezaji ndani ya klabu hiyo ambapo atakuwa akisaidiana na kocha David Moyes pamoja na makocha wengine wasaidizi .
Mchezaji huyo ambaye amekuwa na United kwa misimu 23 akiwa ameichezea klabu hiyo tangu akiwa na umri wa miaka 14 amekuwa akisomea ukocha kwa muda mrefu ambapo tayari amepata shahada mbalimbali za UEFA huku akiwa anamalizia shahada yake ya mwisho ambayo ni UEFA Pro License .
Giggs akiwa na umri wa miaka 40 ni mchezaji mwenye umri mkubwa kuliko wote ndani ya United na ana rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyefunga mabao kwenye kila msimu wa Ligi kuu ya England tangu ilipoanzishwa mwaka 92 na uteuzi wake unamaanisha kuwa atakuwa akifanya kazi yake kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo huku akibakia kuwa mhezaji baada ya kusaini nyongeza ya mkataba wa mwaka mmoja mwezi wa nne mwaka huu.
Akiwa amecheza zaidi ya 1000 za United kwenye kiwango cha juu uzoefu wa Giggs utakuwa silaha muhimu kwa kocha mpya David Moyes ambaye ndio kwanza ameanza kazi ya kuifundisha United Jumatatu ya wiki hii akiwa ameteuliwa kuchukua nafasi ya Sir Alex Fergusson aliyestaafu baada ya msimu uliopita akiwa amekaa kwenye benchi la United kwa miaka 26 .
Uteuzi huu unaweza kuwa mwanzo wa maisha mapya ya Giggs kwenye tasnia ya ukocha  pale atakapoamua kustaafu kucheza soka kwani amekuwa akisomea ukocha kwa muda mrefu na tayari ana vyeti vya kutosha na nafasi hii mpya itamuongezea uzoefu ambao utamfanya kuwa moja ya mahaguo ya kwanza kurithi nafasi ya David Moyes pale atakapofikia mwisho wake kama kocha .
Zaidi ya Giggs mchezaji wa zamani wa United ambaye alikuwa nahodha wa Everton wakati David  Moyes akiwa kocha mkuu Phil Neville anatarajiwa kujiunga na benchi la ufundi la United baada ya kutangaza kustaafu kucheza soka msimu uliopita.
Neville naye ana uzoefu wa ukocha akiwa amewahi kufanya kazi kama mmoja wa makocha wasaidizi wa timu ya taifa ya England kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 21 na kama Giggs amekuwa akisomea kozi kadhaa za ukocha ambazo amefuzu akiwa anashikilia shahada za UEFA B na UEFA A  . Neville mwenye umri wa miaka 36  aliichezea United kwa muda wa miaka 10 tangu mwaka 1995 mpaka 2005 ambapo alicheza mechi 263 kabla ya kuhamia Everton alikocheza kwa miaka 10 alipocheza mechi 242 kabla ya kustaafu mwishoni mwa msimu uliopita .

Ebwana Brazil wamepanda kwenye viwango vya soka Duniani, Tanzania je?



.
.
Ushindi ilioupata timu ya taifa ya Brazil kwenye michuano ya kombe la mabara mwishoni mwa wiki iliyopita umeisaidia timu hiyo kupanda zaidi ya nafasi kumi kwenye viwango vya ubora vya soka vya FIFA.
Brazil ilianza michuano hiyo ikiwa inashika nafasi ya 22 ambayo ni nafasi ya chini kuwahi kushikiliwa na timu hiyo lakini ushindi kwenye michezo yake mitano kuanzia hatua ya makundi, nusu fainali na fainali umeipandisha Brazil hadi kufikia nafasi ya tisa .
Bado Hispania wameendelea kushika nafasi ya kwanza wakifuatiwa na Ujerumani huku Colombia,Argentina na Uholanzi zikikamilisha orodha ya timu tano bora za dunia.
Italia ambao walifika hatua ya nusu fainali kwenye kombe la Mabara wanashika nafasi ya sita mbele ya Ureno walio kwenye nafasi ya saba huku Croatia , Brazil na Ubelgiji wakishika nafasi za nane, tisa na kumi .
.
.
Timu ya taifa ya Ivory Coast ambayo mchezo wake wa mwisho wa kimataifa ulikuwa dhidi ya Taifa Stars ya Tanzania ambapo Tembo hao walishinda kwa 4-2 wanabakia kuwa timu inayoshika nafasi ya kwanza kwa Afrika wakiwa wameshika nafasi ya 13 kwenye viwango vya dunia wakifuatiwa na Ghana walioko kwenye nafasi ya 24.
Mali ndio timu ya tatu kwa ubora Afrika wakiwa  wanawafuatia na Ghana  kwenye nafasi ya 28 huku tano Bora ikikamilishwa na Algeria na Nigeria wanaoshika nafasi za 4 na 5 wakiwa wameshika nafasi za 34 na 35 kimpangilio kwenye viwango hivyo.
Kwenye ukanda wa CECAFA ambako Tanzania iko ,Uganda wako kwenye nafasi ya juu wakiwa wanashikilia namba 19 kwa Afrika na 80 kidunia wakifatiwa na Ethiopia walio nafasi ya 25 kwa Bara la Afrika na nafasi ya 90 Duniani.
Tanzania inashika nafasi ya 35 kwenye orodha ya nchi 54 za Afrika huku ikiwa kwenye nafasi ya 121 Duniani.

Kuhusu usajili wa Gonzalo Higuain kwenda Arsenal

Usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina kuelekea klabu ya washika Bunduki wa Huko London kwenye uwanja wa Emirates Arsenal utakamilika hivi karibuni kwa mujibu wa baba yake mzazi pamoja na kaka yake ambaye pia ni wakala wa mchezaji huyo . Jorge Higuain amesema kuwa mwanaye atakuwa mchezaji wa Arsenal ndani ya siku chache zijazo baada ya kupata ruhusu toka kwa Real Madrid ya kuzungumza rasmi na Arsenal .
Taarifa zaidi ambazo zimethibitishwa na wakala wa mchezaji huyo Nicolas Higuain ni kwamba mdogo wake angeweza kuwa amekamilisha usajili wake ndani ya Arsenal tangu wiki iliyopita lakini ilishindika kwa kuwa klabu ya Real Madrid haikuwa imetoa ruhusa kwa wakala kuzungumza na Arsenal . Jorge Higuain kwa upande wake amesema kuwa siku zote hawaweza kufanya makubaliano na klabu nyingine pasipo kupata ruhusa ya klabu anayochezea mtoto wake na ukubali wa Real kutoa ruhusa unamaanisha kuwa Gonzalo atatambulishwa kama mchezaji mpya wa Arsenal ndani ya siku chache zijazo .
Usajili wa Higuain kwenda Arsenal umekuwa ukizungumzwa kwa muda mrefu na baadhi ya mashabiki walikuwa wameanza kukata tamaa hasa ukizingatia ukweli kuwa klabu hiyo imewahi kukaribia kuwasajili wachezaji wengi hapo awali huku mipango ikiharibika mwishoni . Tayari kumekuwa na makubaliano ya msingi baina ya Arsenal na wawakilishi wa Higuain pamoja na makubaliano baina ya Real na wakala wa mchezaji mwenyewe lakini hakukuwa na makubaliano rasmi ya kutoa ruhusa kwa Arsenal kuzungumza na Gonzalo .Gonzalo-Higuain61
Tayari Real Madrid walishaweka wazi azma yao ya kumruhusu mchezaji huyo kuondoka baada ya kuwa ameichezea klabu hiyo kwa muda wa miaka 6 tangu aliposajiliwa akitokea River Plate ya Argentina .
Gonzalo Higuain mwenyewe ameonekana akiwa kwenye uwanja wa Ndege wa Heathrow huko London ambako inaaminika alikwenda kukamilisha mipango ya awali ya kujiunga na Arsenal ambao wameripotiwa kuwa tayari kuwalipa Real paundi milioni 22 kwa ajili ya mchezaji huyo.

Chelsea wamemsajili huyu nyota wa Uholanzi aisee




Marco Van Ginkel.
Marco Van Ginkel.
Klabu ya Chelsea imefikia makubaliano rasmi ya kumsajili nyota wa timu ya taifa ya Uholanzi kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21 Marco Van Ginkel toka klabu ya Vittesse Arnherm . Nyota huyo atathibitishwa kuwa mchezaji wa Chelsea ndani ya siku chache zijazo baada ya ofa toka kwa The Blues ya Euro milioni 10.5 kukubaliwa na klabu ya Vittesse.
Usajili wa Van Ginkel utakamilika baada ya mchezaji huyo kufaulu vipimo vya afya pamoja na makubaliano binafsi baina yake na Chelsea vitu ambavyo kuna uhakika kuwa havitamzuia nyota huyo kuwa mchezaji mpya wa Chelsea .
Kiungo mshambuliaji  huyo aliibuka na kutengeneza vichwa vya habari baada ya kufanya vizuri kwenye msimu wake wa kwanza kwenye klabu yake ambapo alifuga mabao nane kabla ya kufanya vizuri kwenye fainali za Mataifa ya Ulaya kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21 na kabla ya hapo alipewa tuzo ya ‘mchezaji mwenye kipaji bora wa mwaka” yaani Talent Of The Year kwenye tuzo za wachezaji bora wa uholanzi kwa msimu ulioisha jambo lililomfanya kocha wa timu ya Taifa ya wakubwa Louis Van Gaal kumuita kwenye kikosi chake ambapo amecheza mechi moja .
Klabu ya Chelsea imepata wepesi wa kumsajili Marco Van Ginkel kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya klabu hiyo na klabu ya Vittese Arnherm ambapo siku za nyuma Chelsea imewahi kuwapa Vittese wachezaji ambao walicheza kwenye klabu hiyo kwa mkopo kama Gael Kakuta na Patrick Van Aanholt.
Van Ginkel anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Chelsea chini ya utawala wa kocha mpya aliyerejea kwa mara ya pili Jose Mourinho baada ya Andre Schurle toka Ujerumani huku wachezaji wengine kama Edinson Cavanni na Wayne Rooney wakihusishwa na usajili ndani ya Chelsea.


COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...