Mji mzima ulikuwa katika
maombolezo jana baada ya Lolong, mamba mkubwa kabisa duniani kufa katika
Ziwa lake la kujengwa kutokana na kuumwa ghafla.
Mamba huyo
majichumvi mwenye urefu wa futi 21 na uzito wa tani moja, ambaye
alikamatwa miezi chini ya 18 iliyopita na timu ya wanaume majasiri
kusini mwa Philippines, alikutwa akiwa amelala chali katika eneo lake
kwenye hifadhi ya biashara ya utalii.
Lolong, anaaminika kuwa na
zaidi ya miaka 50, aliana kuumwa baada ya kumeza mfuko wa plastiki
takribani wiki tatu zilizopita. Baada ya hapo akabaki akiharisha
mfululizo, limeripoti gazeti la The Philippine Star.
Lolong, amepewa
jina hilo na mwindaji maarufu wa Philippines, amekuwa akilaumiwa kwa
vifo vya vya wavuvi kadhaa kabla ya kukamatwa kiaina kwenye ziwa lenye
matope karibu na mji wa Bunawan (wenye wakazi 35,000), maili 515 kusini
mashariki mwa Manila.
Wanaume 30 walitumia wiki tatu kujaribu
kumkamata mnyama huyo mkubwa kabla mwishowe kufanikiwa Septemba 2011 kwa
kutumia mzoga wa nguruwe kama chambo na kutupa nyaya juu kuzunguka
mwili wake.
Ilibidi litumike trekta kumvuta hadi kwenye trela -
lakini hapo kabla umati mkubwa wa watu ulimzingira kwa ajili ya kupiga
picha na mamba huyo aliyevunja rekodi.
Tangu hapo, Lolong amekuwa
kivutio nyota kwenye hifanyi ya kitalii na madiwani wa mji wametangaza
kwamba mji wao mdogo hatimaye umepata nafasi kwenye ramani ya dunia.
Lakini
jana, wengi wa wakazi wa mji huo walikuwa wakilia baada ya kugundua
kwamba Lolong amekufa ndani ya mwaka na nusu tangu kuhamishiwa kwenye
makazi yake mapya.
"Hatufahamu kilichomtokea," alisema Meya Edwin
Elorde aliyeshitushwa mno na kifo hicho, ambaye aliripotiwa kumshika
mnyama huyo kabla hajafa.
"Nimetokea kumpenda mamba yule. Ameleta umaarufu na hazina kwenye mji wetu na, katika njia ndogo, kuelekea Philippines."
Elorde
alisema kwamba baada ya kukamatwa kwa mamba huyo - ambaye alitawala
vichwa vha habari kwenye vyombo mbalimbali vya habari duniani - hifadhi
maalumu ya utalii wa kibiashara ilitengenezwa kumhifadhi.
Wakazi wa
nchi hiyo na watalii wa nje wamefanya safari maalumu kwenye jamii hiyo
inayofikika kwa shida kushuhudia kiumbe huyo wa ajabu.
"Tulikuwa
tumepanga kujenga barabara maalumu kuelekea kwenye hifadhi hiyo sababu
tumekuwa tukipata watalii wengi, lakini sasa sina hakika kama
tutaendelea na mipango hiyo," alisema Meya huyo.
"Pengine mipango
itaendelea kama tutaweza kukamata mammba zaidi - kuna wengine wengi
kuzunguka eneo hilo - lakini siwezi kusema kama wanaweza kufikia ukubwa
kama wa Lolong.
Uchunguzi ulitarajiwa kufanyika jana kujua sababu za kifo chake.