MSHABULIAJI nyota wa
kimataifa wa Senegal na klabu ya AC Milan, Mbaye Niang amekataa mwito wa
majukumu katika timu yake ya taifa ambayo inakabiliwa na mechi ya
kirafiki ya kimataifa dhidi Zambia Agosti 14 mwaka huu.
Niang
ambaye alizaliwa nchini Ufaransa, amekuwa akitakiwa na nchi zote mbili
Ufaransa na Senegal lakini kufuatia kufungiwa kwa mwaka mmoja Novemba
mwaka jana kucheza katika timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka
21, kocha Teranga Lions aliamua kumjumuisha katika kikosi chake. Mechi
hiyo kati ya Senegal na Zambia inatarajiw akuchezwa huko Saint-Leu
karibu na jiji la Paris ambapo Senegal watawakosa pia nyota wake wengine
ambao ni Demba Ban a Papiss Cisse. Pamoja
na kuwakosa nyota hao, wachezaji wengine wanne wapya wameitwa kuongeza
nguvu katika kikosi hicho ambao ni Issa Cissokho na Pape Djilobodji
wanaocheza klabu ya FC Nantes, Alfred Ndiaye anayecheza Sunderland na
Henry Saivet wa Bordeaux. Senegal
wanaongoza kundi J la kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la
Dunia 2014 wakiwa na alama tisa wakati Zambia wao wanashika nafasi ya
pili katika kundi D wakitofautiana alama moja na na vinara wa kundi hilo
Ghana.
No comments:
Post a Comment