facebook likes

Monday, July 22, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFANYA ZIARA YA KUKAGUA SHUGHULI ZA USAFI WA MAZINGIRA MKOA WA DAR ES SALAAM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Viongozi wa Kata ya Ukonga kuhusu usafi wa mitaro ya maji machafu, wakati alipokuwa kwenye ziara yake kutembelea na kukagua shughuli za usafi Mkoa wa Dar es Salaam leo Julai 21, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Soko la vyakula la Buguruni, wakati alipokuwa kwenye ziara yake kutembelea na kukagua shughuli za usafi Mkoa wa Dar es Salaam leo Julai 21, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa Matango katika Soko la Buguruni, wakati alipokuwa kwenye ziara yake kutembelea na kukagua shughuli za usafi Mkoa wa Dar es Salaam leo Julai 21, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka kutembelea Bwawa la maji machafu Buguruni wakati alipokuwa kwenye ziara yake kutembelea na kukagua shughuli za usafi Mkoa wa Dar es Salaam leo Julai 21, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Mtaro wa maji machafu uliopo Mayfear Plaza Mikocheni wakati alipokuwa kwenye ziara yake kutembelea na kukagua shughuli za usafi Mkoa wa Dar es Salaam leo Julai 21, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mmoja wa Wakazi wa Msasani baada ya kutembelea kuona Mitaro ya maji machafu ya eneo hilo, wakati alipokuwa kwenye ziara yake kutembelea na kukagua shughuli za usafi Mkoa wa Dar es Salaam leo Julai 21, 2013

TOP 100 YA WAFUNGAJI BORA WA LIGI KUU YA ENGLAND - THIERRY HENRY NA HASSELBAINK NDIO WACHEZAJI WA KIGENI PEKEE WALIO NDANI YA TOP 10 -



Wakati zikiwa zimebaki takribani siku 30 kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England - hii ndio listi ya wafungaji bora wa muda wote wa ligi kuu ya England.
Inayoongozwa na Alan Shearer ambaye amefunga jumla ya mabao 260, akifuatiwa na Andy Cole na mfaransa Thierry Henry akishika nafasi ya 3 - huku yeye na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Jimmy Floyd Hasselbaink wakiwa ndio wachezaji pekee kutoka nje ya United Kingdom kuwemo ndani ya Top 10.


HIZI NDIO BEI ZA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014: YA BEI YA CHINI KABISA NI $220 MECHI YA UFUNGUZI - FAINALI NI $440


Bei za tiketi kwa ajili ya mashabiki wa kutoka nje ya Brazil watakaokwenda nchini Brazil kuangalia fainali za kombe la dunia zitaanzia bei ya $90 (£59, 69 euros) kwa mechi za makundi.
FIFA imetangaza kwamba tiketi ya bei rahisi kabisa kwa mashabiki wataokwenda Brazil kwa ajili ya mchezo wa fainali ya michuano hiyo itaanzia $440 (£288) na ya bei ghali kabisa itakuwa kiasi cha  $990 (£650) ambayo ni sawa na 1,603,800 kwa fedha za madafu.

Michuano hiyo itaanza mnamo tarehe 12 June mwaka ujao, huku mechi ya kwanza ya ufunguzi ikichezwa jijini Sao Paulo.
Tiketi zitaanza kuuzwa mnamo 20 August mwaka huu.
Mashabiki wana muda mpaka 10 October kutuma maombi ya kununua tiketi na utafanyika uchaguzi wa kuamua maombi yapi yamepita.


Kuna jumla ya tiketi millioni 3 ambazo zipo kwa ajili ya maombi ya manunuzi ya mashabiki.

BEI ZA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA (Mashabiki wa nje ya Brazil)

MatchesCategory 1Category 2Category 3

Opening Match$495$330$220
Group Matches$175$135$90
Round of 16$220$165$110
Quarter Finals$330$220$165
Semi Finals$660$440$275
3rd / 4th Place Match$330$220$165
Final$990$660$440

Kwa raia ya wa Brazil tiketi ya bei rahisi kabisa itaanzia kwenye kiasi cha $15. Hizi zinapatikana kwa wanafunzi tu, na wale watu wenye umri zaidi ya miaka 60 ambao wapo kwenye mipango ya kusaidia jamiii. Kwa wabrazil wengine wote bei ya chini kabisa itaanzia kiasi cha $30.

Bei ya chini kabisa ya tiketi katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 nchini South Africa ilikuwa ni  $20, na pia ilikuwa kwenye mechi za  makundi.
FIFA mwanzoni ilisema kwamba tiketi za kombe la dunia mwaka 2014 zitakuwa za bei rahisi kuliko zote.

Katika mtandao rasmi wa kuuza tiketi wa FIFA kutakuwepo na ramani ya ya uwanja inayokuonyesha sehemu za kukaa kutokana na bei ya tiketi yako.
Hi inamaanisha kwamba hakutakuwa na kuhangaika katika kujua ni wapi unapaswa kukaa, alisema mkurugenzi wa masoko wa FIFA  Thierry Weil, ambaye ndio anayehusika na masuala ya yote tiketi.

Mashabiki wanaweza kuomba angalau siti nne kwa mechi, na kwa mechi saba tu.
Amesema pia kutakuwa na mfumo wa kuuza tena tiketi ikiwa watu waliomba au kununua tiketi kabisa na wakashindwa kufika uwanjani.
Angalau tiketi 400,000 zitawekwa maalum kwa mashabiki wa nchi mwenyeji, hukukaribia tiketi 50,000 zikiwa maalum kwa ajili ya wajenzi wanaojenga viwanja vitakavyotumika kwenye michuano hiyo.

KWA NDUGU ZANGU WABONGO MNAOTAKA KUOMBA KUNUNUA TIKETI UNAWEZA KUINGIA KWENYE MTANDAO HUU - www.ticket.org/WorldCup

BAADA YA KUWATWANGA 7-0 MSIMU ULIOPITA - JUPP HEYNCKES AJIONDOA KWENYE LISTI YA MAKOCHA WANAOTAJWA KUIFUNDISHA BARCELONA


Kocha wa zamani wa Bayern Munich Jupp Heynckes amejiondoa kwenye listi ya makocha wanaodhaniwa watapewa kazi ya ukocha wa kuinoa klabu ya FC Barcelona. 

Kocha huyo mwenye miaka 68, alishinda makombe matatu na Mabavaria msimu uliopita pamoja kumaliza utawala wa FC Barca kwa kuwapa kipigo cha 7-0 katika mechi mbili za nusu fainali ya klabu bingwa ya dunia, amekuwa akitajwa na vyombo vya habari na mashabiki wa Barcelona kama ndio mtu sahihi kurithi mikoba ya Tito Vilanova, ambaye alijiuzulu kutoka na matatizo ya kiafya.

Lakini, kocha huyo wa zamani wa Real Madrid amejiondoa kwenye listi ya makocha wanaowania jukumu la kuinoa Barca msimu unaokuja na kusisitiza kwamba siku zake za kukaa kwenye bechi la ufundi zimeisha.

"Najiweka bize kwa kufanya vitu vyangu nivipendavyo na kufuatilia michezo. Nina wanyama wangu kwenye bustani," aliiambia Sky Sports News HD. "Nadhani itakuwa haiwezekani kwangu mimi, baada ya kufanya kazi na Bayern Munich, sasa niende kuchukua jukumu kwenye klabu nyingine.

"Nimeelewa ishara za mwili wangu na njihisi nipo vizuri, na nafurahia maisha nje ya soka."

MIAKA 10 TANGU RONALDINHO ASAJILIWE BARCELONA - ANGALIA MABAO YAKE BORA YALIYOTEULIWA NA MTANDAO RASMI WA BARCA


Siku kama ya leo miaka 10 iliyopita FC barcelona iliwapiga bao Manchester United na kumsajili mbrazil Ronaldinho Gaucho. Usajili wa mbrazili huyu ndio ulikuwa mwanzo wa mapinduzi ya utawala wa soka nchini Hispania na barani ulaya. Leo ikiwa ni miaka 10 tangu Ronaldinho atue Nou Camp - FC Barcelona imeamua kumkumbuka gwiji wa klabu hiyo Gaucho kwa kuandaa video za mabao yake bora wakati akiichezea timu hiyo.Ziangalie video hizi zinazomuonyesha mchawi huyu wa soka wa kibrazili.

VIDEO: MBWANA SAMATTA AIBEBA TP MAZEMBE UGENINI DHIDI YA ES SETIF - AFUNGA BAO PEKEE NA KUIPA SARE MAZEMBE



Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya TP Mazembe ameendelea kung'ara kwenye timu hiyo baada ya juzi kuifungia bao muhimu la ugenini klabu yake ilipokuwa ikicheza na klabu ya ES Setif ya Algeria katika mchezo wa kombe la CAF.

Samatta alifunga bao hilo kutoka na mpira wa faulo uliotemwa na kipa wa Setif na yeye akaumalizia bila kupoteza nafasi katika dakika ya 81. Dakika moja baadae Setif wakiwa na sapoti kubwa ya mashabiki wao walirudisha bao hilo kupitia mchezaji M. Delhoum. Kutokana na matokeo hayo timu zote za kundi B zinabaki pointi moja moja, baada ya CA Bezertin ya Tunisia kutoka sare na FUS Rabat ya Morroco.


TeamPldWDLGFGAGDPts
Tunisia CA Bizertin10101101
Democratic Republic of the Congo TP Mazembe10101101
Algeria ES Sétif10101101
Morocco FUS Rabat10101101

HII NDIO RATIBA YOTE YA RAUNDI YA KWANZA YA LIGI KUU MSIMU UJAO - YANGA KUANZA KUTETEA UBINGWA DHIDI YA ASHANTI - SIMBA DHIDI YA RHINO RAGERS YA SHINYANGA


Simba kuanzia ugenini dhidi ya Rhino - Yanga nyumbani dhidi ya Ashanti


ASILIMIA 48.3 YA WANAUME TANZANIA WAMEBAMBIKIWA WATOTO NA WAKE ZAO



Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali nchini imesema karibu nusu ya watu waliojitokeza kupima vinasaba (DNA) ili kubaini uhalali wa watoto wao, vipimo vimeonesha si wazazi halisi wa watoto waliopimwa.

Takwimu hizo ni kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2010, ikionesha kuwa, asilimia 48.32 ya wazazi 'wanalea' watoto wasio wa kwao wakati asilimia 51.68 ndio wazazi halali.

Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Jinai, Vinasaba na Baiolojia wa ofisi hiyo, Gloria Machuve katika mkutano na wanahabari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dar es Salaam.

Ingawa hakutaja idadi kamili ya waliojitokeza kupima DNA, alisema idadi hutofautiana mwaka hadi mwaka. Ili kufanya vipimo vya DNA, wazazi hulazimika kulipia Sh 100,000.

Machuve alisema kazi ya DNA si kutambua watoto halali na wasio halali pekee, bali vipimo hivyo vina umuhimu mkubwa kwa jamii.
 
Alitoa mfano kuwa, matumizi ya Teknolojia ya vinasaba vya binadamu yamewezesha kesi mbili za mauaji ya vikongwe na albino kutolewa hukumu katika mikoa ya Shinyanga, Kagera na Sumbawanga baada ya kufanyika kwa uchunguzi katika matukio manane.

Aidha, alisema katika majanga mbalimbali yaliyokumba nchi ikiwa pamoja na milipuko ya mabomu yaliyotokea Mbagala, Dar es Salaam mwaka 2010 walitambua mabaki ya askari sita ambao baadaye walichukuliwa na ndugu zao na kuzikwa.

Alitolea pia mfano wa tukio la moto katika Shule ya wasichana ya Idodi mkoani Iringa ambako licha ya kuungua vibaya, miili ya wanafunzi 12 ilitambuliwa hivyo makaburi yao kutambuliwa. Katika Jengo la ghorofa lililoporomoka mtaa wa Kisutu mwaka huu, marehemu 23 walitambulika.

Aidha, katika ajali ya Ndege ya Comoro mwaka 2010 mabaki ya miili ya marehemu 25 ilitambuliwa huku katika masuala ya uhamiaji teknolojia hiyo ilitumika kudhihirisha hawana uhusiano na wananchi wa Tanzania.

Machuve alisema katika masuala ya ubakaji na mimba za utotoni  teknolojia hiyo imesaidia kuwa fikisha wahusika mahakamani pamoja na katika wizi wa kutumia silaha.

SERIKALI YALEGEZA MSIMAMO KUHUSU KODI YA LINE....WAZIRI WA FEDHA AKUBALI KUWAPELEKEA WABUNGE WAJADILI UPYA



Wakati Serikali imeeleza nia yake ya kuangalia upya utozaji wa kodi ya kila mwezi kwenye laini za simu za mkononi, imeeleza pia mpango wa kufunga mtambo maalumu ili kubaini malalamiko ya kampuni za simu kudaiwa kuiba fedha za watumiaji.

Katika kile kinachoonesha kusikiliza kilio cha wananchi, Serikali imesema inapitia maoni na mapendekezo yaliyotolewa na wadau ili kuiangalia upya sheria hiyo ya kutoza kodi ya Sh 1,000 kwa kila laini kwa nia ya kuwapunguzia wananchi mzigo huo.

Serikali imetoa kauli hiyo Dar es Salaam jana kupitia kwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Waziri wa Fedha,  Dk  William Mgimwa walipozungumza na waandishi wa habari.

Dk  Mgimwa alisema hatua hiyo imekuja baada ya Serikali juzi kukutana na watoaji wa huduma za mawasiliano nchini waliofika kuwasilisha maoni yao juu ya tozo hiyo kwa nia ya kuwapunguzia wananchi wa hali ya chini ukali wake.

Hata hivyo alipoombwa na waandishi wa habari kuyaeleza mapendekezo yaliyotolewa na watoa huduma hao wa mawasiliano, Dk Mgimwa hakuwa tayari kuyataja hadharani zaidi ya kusema ni mapendekezo mazuri na rafiki kwa wananchi wa chini.


"Tulijadiliana nao mambo mengi ambayo yatatusaidia mbele ya safari namna tunavyoweza kupunguza makali hasa kwa watu wa kipato cha chini," alisisitiza Dk Mgimwa.

Alisema mbali ya maoni hayo ya watoa huduma za mawasiliano, pia Serikali imepokea maoni na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na kuona umuhimu wa kuyapitia maoni hayo na kuyatolea majibu.

"Serikali imepokea maoni na mapendekezo mbalimbali na sasa tunakwenda kuyafanyia kazi na baadaye tutakuwa na taarifa ya kuwaeleza wananchi ni nini tulichokiona juu ya kodi hii.


"Tunajua wananchi wa chini wanaweza kuumia lakini si nia ya Serikali kumuumiza mtu yoyote," alisema Dk Mgimwa.

Hata hivyo kutokana na suala hilo kuwa la kisheria kutokana na kupitishwa na Bunge, Dk Mgimwa alisema Serikali itatoa majibu ya nini kimekubaliwa baada ya suala hilo kurejeshwa tena bungeni na kuamulia vinginevyo.


"Suala hili ni la kisheria, jambo lolote likipita bungeni likawa sheria hata mimi Waziri siwezi kulibadilisha lazima lifuate mkondo uleule. Vikao vya Bunge vitakaa hivi karibuni na jambo hilo litajadiliwa huko," alisisitiza Dk Mgimwa.

Makato hayo ya kodi kwa kila mtumiaji wa simu ya Sh 1,000 yalitakiwa kuanza kukatwa kuanzia Julai mosi mwaka huu, lakini Dk Mgimwa alisema kuwa kodi hiyo haijaanza kukatwa kutokana na mfumo wake kutokamilika.

Alisema nia ya Serikali katika kodi hiyo ni kuboresha huduma za maji, umeme na barabara hasa vijijini ili wananchi wawe na uwezo wa kufikisha mazao yao haraka sokoni na kwamba kodi hiyo si pekee kwani Serikali ilipokea mapendekezo 67 ya kodi lakini  baadhi yalionekana kutotekelezeka.

"Wazo hili lilitoka katika Kamati za Bunge kwa wabunge wenyewe na sisi hatuchuji peke yetu mawazo hayo, bali kuna Kamati ya Kodi na Kamati ya Bunge lenyewe ambazo pia zilihusika katika kutoa mapendekezo ya mwisho."

COMPUTER ZA USHAHIDI ZILIZOTUMIKA KWENYE UWIZI WA ATM ZAIBIWA NDANI YA KITUO CHA POLISI - MAKAO MAKUU MWANZA



Siri za wizi uliotokea Makao Makuu ya Polisi mkoani Mwanza zimeanza kuvuja ambapo imebainika kuwa kompyuta aina ya laptop zilizoibwa ndani ya chumba cha vielelezo zilikuwa za ushahidi wa kesi ya wezi wa mashine za kuchukulia fedha(ATM). 


Katika wizi huo wa benki ambao ulifanyika kwenye mashine za ATM mbalimbali na watuhumiwa watatu kunaswa Februari 10, mwaka huu saa 6 usiku wakiiba kwenye ATM za NMB,Tawi la PPF Plaza, Polisi walinasa vitu vingi vya watuhumiwa hao ikiwa ni pamoja na kompyuta mbili ambazo zinadaiwa kuibwa kituoni hapo juzi.



Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Polisi zimeeleza kwamba katika wizi huo uliotokea katika maghala ya Polisi, moja kati ya vifaa vilivyoibwa ni mafaili mbalimbali ya vielelezo kadhaa vya kesi zinazochunguzwa na polisi ikiwa ni pamoja na laptop hizo ambazo zilikuwa ni ushahidi kwa kesi hiyo ya wizi wa ATM.



Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ernest Mangu alipoulizwa kuhusiana na vielelezo vilivyoibwa Polisi, alikanusha kwamba laptop hizo zilikuwa kielelezo cha kesi za wizi wa fedha katika ATM lakini pia hakuwa tayari kueleza zilikuwa za kesi gani.



Wakati Kamanda huyo akikanusha baadhi ya askari ambao wanahusika na uchunguzi huo wamedai kuwa wizi huo uliendeshwa na maofisa wa polisi wasio waaminifu na kubainisha hakuna wizi unaoweza kufanywa na watu kutoka nje ya polisi.

SHILOLE ATANGAZA BIFU LA NGUMI BAADA YA SINTAH KUMPONDA KUWA ANAUWEZO MDOGO KIMUZIKI



MWIGIZAJI wa kike wa filamu na muziki Bongo zuwena Mohamed ‘Shilole’ amemtangazia hali ya hatari msanii mwenzake wa filamu na mtangazaji wa televisheni Christina John ‘ Sintah’ kuwa popote atakapomkuta lazima amchape kwa kipigo ambacho hatasahau katika maisha yake...

Shilole  ametoa kauli hiyo kufuatia kuandikwa na mwanadada huyo katika mtandao wake akimbeza kwa kejeli. .
“Ni kweli sisi wanawake hatupendani na kuwa na wivu wa kijinga, mtu anakurupuka anakotoka bila hata kufanya utafiti na kunibeza eti sina uwezo wa kuimba na JLO (Jenifer Lopez) ....

"Kuna mtu aliyetegemea mimi kwenda kufanya show Marekeni!Sasa ninachomwambia ninamtafuta nikikutana naye nimtapa kipigo cha Mbwa mwizi,”aliongea kwa hasira Shilole.

Katika mtandao wake Sintah aliandika kwa kusema Shilole ni sawa na mtu anayeota ndoto za mchana, na kumkejeli kwa kusema kuwa aendelee kuota anaweza baadae kurudi katika hali yake...

  Sehemu ya maneno yanayomkera Shilole ni haya:
“Shilole bwana hii week katujia na kali kuliko eti ameongea na Benny Medina (Jlo’s Manager) ili aweze kufanya collabo na my sister, heee yes inawezekana maana hakuna lisilowezekana chini ya jua lakini swali ni?? wataimbaje?? yule dada yake na mie ni RnB na music wa Shilole bado sijaujua ni chakacha ama nini sasa naomba msaada kwenye tuta wadau wa music, hili linauwezekano??,”

“ Chakacha na RnB?? Kwa sababu Shilole nyimbo zake sawa na Snura wa majanga, kidogo Linah angeniambia ana collabo na my sisy ningeelewa sasa Shilole?? Ndoto za mchana ila si vibaya kuota maana ukishtuka unarudi ktk reality,”

Shilole anasema kuwa hajawahi kumuona mwanamke mwenye roho dhaifu kama Sintah, anajifanya anambabaikia Jlo wakati hata hajulikani....

“Mimi sikuwa nimeenda Marekani kwa ajili ya kuomba kumshirikisha J-lo kuimba naye,  lakini baada ya meneja wake kuja kuniona na kumpelekea video za muziki wangu  JLO alikubali kufanya kazi na mimi...

"Ilitakiwa nionane naye siku ya Jumapili lakini ndio siku niliyoondoka na ninarudi huko kwa ajili ya kazi hiyo, sijui nikifanya naye kazi atajificha wapi?,” anasema Shilole.

Shilole anasema Mungu ni mkubwa hata kama kuna mtu anayemchukia kwa mafanikio yake bado Mungu ana nafasi kubwa kuwazima watu wenye roho mbaya wivu kama Sintah ambaye anaonekana yupo tayari kwa ajili ya kuwaombea matatizo watu wanaojituma kwa ajili ya kuendesha maisha yao.

LADY JAYDEE NA JUMA NATURE WAJIPANGA KUTOA NGOMA YA PAMOJA



Baada ya kumpa shavu The Heavy Weight MC Profesa Jay kwenye joto hasira, Lady JayDee a.k.a Anaconda anaendeleza utamaduni wa kuwapa mashavu wasanii wakongwe na wakali..hivi karibuni alirekodi wimbo na Q chilah, and guess Who’s next, ni Juma Kassim Nature Kiroboto.


Kupitia akauunti yake ya twitter Anaconda amewapa fans wake good news kuhusu ujio wa ngoma yake na Juma Nature, huku akitaka kujua kama wako tayari kuipokea. 
fans wengi waliipokea habari hiyo kwa shangwe lakini Jide aliwaeleza kuwa sio kwamba kila wimbo anaorekodi sasa hivi atauachia sasa hivi.



“Tunarekodi tu nyimbo ili ziwepo ila haimaanishi zote zitatoka kwa wakati mmoja zitapeana muda. Wakati ukipata hisia lazma uingie Studio.” Alitweet Lady JayDee.


Kwa upande mwingine Mkali huyo aliweka wazi kile kinachomnyima amani katika maisha yake ‘kimuziki’ kuwa ni kiu ya kufanya wimbo na malkia wa mipasho Khadija Kopa. 

MSANII SHETTA AMALIZA BIFU NA BABA YAKE BAADA YA KUZINGUANA TANGU AKIWA NA MIAKA 7


 Baraka za mwezi Mtukufu wa Ramadhan zimeitembelea familia ya Baba Qayllah, Shetta Bilal. Baada ya miaka mingi ya maelewano hafifu na baba yake mzazi, leo baba na mwanae wameamua  kusameheana

Kupitia Instagram, Shetta amepost picha (hiyo juu) akiwa na baba yake mzazi Mzee Bilal ambaye ni Sheikh, pamoja na mdogo wake Awab na kuandika: Wit my daddy n my young broda Awab….. #happyday baada ya miaka mingi kuwa na tofauti na mzee tangu nina miaka 7 leo yameisha #bassawa #Ramadankareem.”

Mwandishi wetu amezungumza kwa simu na Shetta kutaka kupata maelezo zaidi ya kwanini alikuwa haelewani na baba yake.
“Basi tu tulikuwa tunakosana, nahisi situations zangu na maisha yangu vilikuwa haviko sawa. Kazi yangu ninayofanya na nini kwasababu yeye ni mtu wa dini sana, baba yangu ni Al Haj, Sheikh. Kwahiyo nahisi hilo lilikuwa tatizo kwa upande wake..”


Shetta amesema kwa muda wote huo baba yake alikuwa hamfahamu mke wake pamoja mwanae, Qayllah lakini sasa anafuraha kwakuwa wameyamaliza baba  yake amemuelewa.

JOSEPH LUDOVICK AFUNGUKA....ADAI KWAMBA MATESO YOTE ANAYOYAPATA NI KWA AJILI YA CHADEMA



SIKU chache baada ya Mahakama kumuachia kwa dhamana mshitakiwa mwenza wa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, Joseph Ludovick, amefunguka na kuelezea tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake, ikiwamo uhusiano wake na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba.

Ludovick, ambaye anadaiwa kurubuniwa na Nchemba na hivyo kumrekodi Lwakatare wakipanga mipango ya kumdhuru Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Denis Msaky, alijitokeza juzi katika mtandao wa kijamii wa Mabadiliko na kuomba kuulizwa jambo lolote, kwa kile kilichoonekana kutaka kujibu tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa dhidi yake.

Maswali na majibu yake ilikuwa ni kama ifuatavyo;

KUHUSU UHUSIANO WAKE NA MWIGULU

Akielezea uhusiano wake na Mwigulu baada ya kuulizwa swali na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Abdul Dello, Ludovick alisema ni wa kawaida na kwamba haufikii kama ule wa Lwakatare na Maggid Mjengwa.

“Tumejuana kwenye mitandao ya kijamii na tukadevelop ukaribu, ilitokana na mimi kukosoa mijadala yake na kumpinga.

“Ninayo mahusiano na watu wengi tu nje ya Chadema. Mfano ni huyo Mwigullu, Sixtus Mapunda, Mbunge Kangi Lugora, nk.na sidhani kama ni dhambi hii. Wapo wengi tu wenye uhusiano kama huu. Wote hawa katika nyakati tofauti tumesaidiana mengi.

Katika swali lake lingine, Abdul Dello alihoji: “Ludo, Mwigulu Nchemba alithibitika kukutumia m-pesa ya elfu 50 ilikuwa ya kazi gani?

Ludovick alijibu akieleza kuwa: “Nilikuwa na tatizo binafsi la kifamilia, nilihitaji msaada.”
KUHUSISHWA NA USALAMA WA TAIFA
Mtu mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Hamis Hamad alimuuliza akisema:

“Ludo, unasemwa sana mtaani kuwa wewe ni TISS Agent (wakala wa usalama wa taifa) uliyepachikwa pale Chadema kwa ajili ya kuiua kifo cha kawaida na ndiyo maana unafanya kazi nyingi za kujitolea badala ya kwenda kufundisha kama taaluma yako ya ualimu inavyokuruhusu, kweli?

Majibu ya Ludovick yalikuwa hivi: “Nchi hii tunapenda majungu tuuu, na magazeti yetu yamebobea kusambaza majungu na kupakazia watu. Huwezi kuelewa dhana hii hadi ikukute. Juu ya kazi ni tofauti za kimtazamo, so wengine wanapenda kuajiriwa na wengine hawapendi, so haicount hii. Ni uamuzi tu. Niliijua Chadema 2006 na kujiunga rasmi 2009. Hakuna aliyenipachika huko. Ni by conviction, nakuhakikishia hata matatizo yote ninayoyapata ni kwa sababu ya Chadema.”

AELEZA ANAVYOMFAHAMU LWAKATARE

Boniface Magessa alimuuliza hivi: “Ludovick, elezea kidogo unavyomfahamu Lwakatare. Siku ya tukio la kurekodiwa ulikuwa wapi? Kama mlikuwa wote siku hiyo, ulikaa mbele yake au nyuma yake?

Ludovick: “Magessa, Lwakatare tumekutana Bukoba 2010 wakati wa kampeni. Tumefahamiana kwa sababu ya Chadema tu. Na ameendelea kuwa rafiki yangu na kiongozi wangu.

Siku ya tukio la kurekodiwa nilikuwa nyumbani kwake Lwakatare. Siyo muhimu juu ya location”.

MASWALI MENGINE
Leila Sheikh alimuuliza hivi; “Ludo, eti uliwahi kuruka ukuta usiku fulani?

Ludovick: “Da Leilah umefunga wewe? Sasa haya ya kuruka ukuta usiku fulani ni nini tena? Teh teh, hebu fafanua? Marcois, siku hizi kibwagizo changu ni kuwa natazama yote haya nayo ni ubatili mtupu, ni sawa na kufukuza upepo”.

Swali lake lingine lilisomeka hivi: “Kama wewe ni mwanachama hai wa Chadema kwa nini umeitwa 'msaliti' na shabiki wa Chadema kuwa ile kanda ya Lwakatare ulitumwa na Mwigulu kuipiga? Je, ile kanda ni ya kweli?

Inadaiwa kuwa ile kanda inaonesha nia/mpango wa kumuumiza Msacky.

Katika majibu yake Ludovick naye alijibu “Leila, mimi ni Mwanachadema hai. Kuitwa msaliti ni hali halisi ya sasa. Lakini inawezekana kuwa mimi wanayeniita msaliti, siku moja wakaona kuwa ndiye mwokozi.
 
Fikiria kama ningekuwa natumika kama mnavyosema, kwa nini kesi ya ugaidi imefutwa? Si ningesema tu kuwa kulikuwa na watu wengine kadhaa? Kama ninatumika, kwa nini nikamatwe Iringa na kusafirishwa usiku tena chini ya ulinzi mkali? Leila teh teh kwamba nilitumwa kurekodi ile kanda!!! Yaani na Lwakatare naye akatumwa ili aongee haya tunayotuhumiwa kuyapanga?


Na je, suala hili ikionekana kuwa ni kweli Lwakatare alilifanya, nani atakuwa msaliti kwa Chadema? Je, chama chetu kinazo sera za kudhuru waandishi? Sasa msaliti ni yule anayechafua chama kwa kupanga mambo yasiyoendana na sera za chama? Au ni yule anaye kilinda chama? Haya si nyote mnajua concept ya whistle blowers? Hamtegemei wawemo ndani ya Chadema?

Na je, kama Mahakama itaamua kuwa tuhuma zetu ni kweli bila chembe ya shaka, ninyi mtaendelea kusema nini, kuwa mimi msaliti au wote sasa tutakuwa wasaliti? Naomba tuachie mahakama suala hili. Kuitwa msaliti wakati unaumia kwa ajili ya hao wanaokuita wasaliti, kibinadamu inaumiza sana. Na hilo ndilo linanitokea.

Kuhusu kwa nini watu wote wananilaumu, si kweli. Wapo wasioona hivyo, ila in a great party propaganda chafu za CCM na za Chadema zimenifanya muhanga wa mambo haya. Uhusiano wangu na Lwakatare kwa sasa ni wa mashaka sana.

Swali jingine la Sheila ni hili: “Je, wewe bado mwanachama wa Chadema? Kama ndiyo, mbona walikutema kwa muda ukakaa rumande bila dhamana? Kwa nini wewe ambaye ni volunteer wa Chadema ulikanwa pale baada ya kushikiliwa na polisi? Huo ndiyo u****wa kafara.

Alijibu hivi: “Mimi ni mwanachama wa Chadema na nakuhakikishia mateso yote ninayoyapata ni kwa sababu ya Chadema.

Masharti ya dhamana hayakuwa wadhamini wawekwe na Chadema, bali watu wawili. Sasa sidhani kama Chadema walikuwa na kesi mahakamani hadi watafute wadhamini. Kuhusu kuwa volunteer wa Chadema ni majungu niliyoyazungumza. Sijawahi kuwa volunteer wa Chadema. Mimi ni mwanachama wa kawaida.

Nyoni Magoha alimuuliza hivi: “Wewe bado una imani na Chadema? Utaendelea kuwa mwanachama hai au umeshajitoa/utajitoa?

Majibu ya Ludovick: “Ninayo imani kubwa sana na isiyotetereka kwa Chadema. Nitaendelea kuwa mwanachama hai”.

Hata hivyo, Ludovick ambaye anatajwa kuhusika na tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alikwepa kuzungumzia jambo hilo na hata alipoulizwa baadhi ya maswali yenye mwelekeo huo.

Kuhusishwa Ludovick na tukio la Kibanda kunatokana na utata wa kauli na mwenendo wake siku ambayo Mhariri Mtendaji huyo alijeruhiwa.

 source: Mtanzania: 

WATOTO WAWILI WABAKWA NA BABA ZAO JIJINI DAR



Ukatili wa kutisha umewakuta watoto wawili wa familia tofauti wakidaiwa kubakwa na wazazi wao huku mmoja akifanyiwa unyama huo na baba yake mzazi na mwingine baba yake mdogo.

Habari zilizopatikana kutoka kwa ndugu, wazazi na majirani wa watoto hao zilisema kuwa wote walifanyiwa ukatili huo siku moja kwa nyakati na mazingira tofauti wilayani Temeke, Dar hivi karibuni.

Watoto hao ambao wote walifikishwa siku moja katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke kwa matibabu, walieleza jinsi walivyotendewa unyama huo wa kusikitisha ambao mzazi au mlezi hapaswi kumtendea mwanaye.

Wakwanza ni Anifa (8) ambaye alieleza kuwa alibakwa na baba yake mdogo aliyemtaja kwa jina moja la Amani.
Wapili ni Prisca ambaye alimweleza mwanahabari wetu kuwa alibakwa na baba yake mzazi aliyemtaja kwa jina moja la Charles.

Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti wakiwa wodini hospitalini hapo wakiuguzwa majeraha, watoto hao waliokuwa sambamba na mama zao, walieleza kwa kina kile walichofanyiwa na wazazi wao.

Anifa alisema mara nyingi baba yake mdogo alikuwa akimpa pipi na akimuonesha muvi za picha za utupu na kumshawishi wafanye uchafu huo.

“Kuna wakati alikuwa akiniambia atanipa pesa lakini pia alinitisha kwa kisu au panga ili nimpe, nikawa nakataa lakini siku hiyo usiku alinibaka huku amenishikia kisu,” alisema mtoto Anifa kwa huzuni.

Kwa upande wake, Prisca alisema baba yake alimwambia atampa pesa ili wafanye mapenzi na wakati anamwingilia alikuwa ameshika noti ambayo hata hivyo alishindwa kusema ilikuwa na thamani gani.

Moja kati ya mambo yaliyoibua maswali ni kama kweli wabakaji wa watoto hao ni baba zao?

Ili kupata majibu  mwandishi wetu alizungumza na watoto hao kwa kina juu ya ukweli kama wahusika wanawafahamu vizuri ambapo katika mahojiano hayo yaliyorekodiwa, kila mmoja alikiri kuwa wanawajua fika wazazi wao hao.

Bila kupepesa macho wala kuogopa, mtoto Anifa alikiri kuwa mbakaji wake ni baba yake mdogo ambaye mara nyingi alikuwa akimtishia ili afanye naye mapenzi bila mafanikio hadi siku aliyopata nafasi usiku.

Kilichowashangaza wengi ni umri mdogo wa watoto hao kwani mtoto Anifa ana miaka nane huku mwenzake akiwa na umri wa miaka mitano.

“Mwanangu ana miaka mitano tu, sasa najiuliza huyu baba yake alikuwa anatafuta nini kwake, kwa kweli imeniuma sana na nimechanganyikiwa kwa kitendo alichofanyiwa na baba yake,” alisema mama wa Prisca huku mama wa Anifa akithibitisha umri wa mtoto wake kuwa ni miaka minane akiwa ni denti wa darasa la tatu katika shule ya msingi (jina kapuni).

Mama mzazi wa Prisca aliyejitambulisha kwa jina moja la Maria, alisema alishitushwa na taarifa za mumewe kumbaka mtoto wao.

“Nimeshaachana na mume wangu na sasa ameoa mwanamke mwingine, kwa kweli niliumia sana baada ya kupata habari za mwanangu kubakwa na baba yake.

“Nilikwenda Polisi Chang’ombe (Dar) nikamfungulia jalada la kesi namba CHA/RB/6028/2013-UBAKAJI ambapo mtuhumiwa alikamatwa na sasa yupo mahabusu katika Gereza la Keko akisubiri kesi yake kusikilizwa,” alisema mzazi huyo.

Kwa upande wa Anifa, shangazi yake aitwaye Wamoja alisema kuwa mtuhumiwa wa ubakaji wa Anifa alikamatwa mara alipokwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali mgonjwa.

“Alijifanya hajui chochote akaja hospitali kwa kuwa Anifa alishamtaja kule polisi, ndipo akakamatwa na kufikishwa polisi Chang’ombe akisubiri kufikishwa mahakamani,” alisema Wamoja.

Baadhi ya mashuhuda wa matukio hayo, walishangazwa na madai ya watoto hao kubakwa na wazazi wao ambapo walisema kuwa siyo bure, lazima kuna kitu nyuma ya pazia.

source:GPL 

MAJUNGU YAWAFANYA "SCORPION GIRLS" WAZINGUANE



MEMBA wa Kundi la Scorpion Girls, Isabela Mpanda ‘Bela’ na Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ wametofautiana hadi kufikia hatua ya kutukanana na kutupiana nguo nje.

Mpango mzima ulitokea hivi karibuni Kijitonyama jijini Dar, nyumbani kwa Isabela ambapo chanzo cha ugomvi huo ni baada ya Isabela kumsifi a mtandaoni X-memba wa kundi lao, Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’ kwa kununua gari, ndipo Kabula  alipokasirika na kuanza kumtukana Bela na mama yake matusi ya nguoni.

“Sikumuelewa kabisa Jini, kumsifi a Jack kuhusu kumiliki gari ndiyo kumemfanya anitukane? Iliniuma sana na sitamsamehe, bora kila mtu achukue hamsini zake, nguo zake nilimtupia nje,” alisema Bela na kusisitiza kufanya muziki peke yake kwa sasa.

Justine Timberlake, Macklemore na Rayan Lewis waongoza kinyang'anyiro tuzo za MTV VMA 2013



Justine Timberlake, Macklemore na Ryan Lewis wameongoza kutajwa katika kinyang'anyiro tuzo za MTV VMA, 2013 ambapo kila mmoja ametajwa kuwa nominated mara sita, Bruno Mars, Robin Thicke, Kendrick Lamar na Drake pia wametajwa kuwa nominated mara nyingi katika tuzo hizo (Video Music Awards)

Mirror ya Justin Timberlake kutoka kwenye album yake (The 20/20 Experience),imekuwa nominated kwenye category ya Video of the Year, Best Male Video, Best Pop Video na Best Editing, wakati video yake ya “Suit & Tie” with Jay-Z, imechaguliwa katika Best Collaboration na Best Direction. 

Macklemore na Ryan Lewis, wanagombania category kubwa sana ambayo ni tuzo ya Video bora ya mwaka kwa hit yao “Thrift Shop,”wakati goma yao “Can't Hold Us” imeingia kwenye Best Hip Hop Video, Best Cinematography, Best Direction na Best Editing.Video ya “Same Love” imechaguliwa kwenye category  Best Video yenye meseji ya kijamii (Social Message). 

Kendrick Lamar na Drake ni wawili kati ya ma Rapper waliochaguliwa zaidi kwenye 2013 VMAs. Wote wawili wapo kwenye category ya Best Hip Hop video.“Started From The Bottom”  ya Drake pamoja na “Swimming Pools." ya Kendrik Lamar. 
MTV 2013 Video Music Awards inatarajiwa kufanyika live siku ya Jumapiliis  ya tarehe 25, 9 pm EST.

Video of the Year
Justin Timberlake – “Mirrors”
Macklemore & Ryan Lewis feat. Wanz – “Thrift Shop”
Bruno Mars – “Locked Out of Heaven”
Robin Thicke feat. T.I. and Pharrell – “Blurred Lines”
Taylor Swift – “I Knew You Were Trouble”

Best Hip Hop Video
Macklemore & Ryan Lewis feat. Ray Dalton – “Can’t Hold Us”
Drake – “Started From The Bottom”
Kendrick Lamar – “Swimming Pools”
A$AP Rocky feat. Drake, 2 Chainz and Kendrick Lamar – “F–kin’ Problems”
J. Cole feat. Miguel – “Power Trip”

Best Male Video
Justin Timberlake – “Mirrors”
Robin Thicke feat. T.I. and Pharrell – “Blurred Lines”
Bruno Mars – “Locked Out of Heaven”
Ed Sheeran – “Lego House”
Kendrick Lamar – “Swimming Pools”

Best Female Video
Rihanna feat. Mikky Ekko – “Stay”
Taylor Swift – “I Knew You Were Trouble”
Miley Cyrus – “We Can’t Stop”
Pink feat. Nate Ruess – “Just Give Me A Reason”
Demi Lovato – “Heart Attack”

Best Pop Video
Bruno Mars – “Locked Out of Heaven”
Justin Timberlake – “Mirrors”
Fun. – “Carry On”
Miley Cyrus – “We Can’t Stop”
Selena Gomez – “Come and Get It”

Artist To Watch (Formerly Best New Artist)
Twenty One Pilots – “Holding On To You”
Zedd feat. Foxes – “Clarity”
Austin Mahone – “What About Love”
The Weeknd – “Wicked Games”
Iggy Azalea – “Work”

Best Collaboration
Justin Timberlake, feat. Jay-Z – “Suit & Tie”
Pitbull feat. Christina Aguilera – “Feel This Moment”
Calvin Harris feat. Ellie Goulding – “I Need Your Love”
Robin Thicke feat. T.I. and Pharrell – “Blurred Lines”
Pink feat. Nate Ruess – “Just Give Me A Reason”

Best Video With A Social Message
Kelly Clarkson – “People Like Us”
Macklemore & Ryan Lewis – “Same Love”
Snoop Lion – “No Guns Allowed”
Miguel – “Candles in the Sun”
Beyoncé- “I Was Here”

Best Rock Video
Imagine Dragons – “Radioactive”
Fall Out Boy – “My Songs Know What You Did in the Dark (Light Em Up)”
Mumford & Sons – “I Will Wait”
Thirty Seconds To Mars – “Up in the Air”
Vampire Weekend – “Diane Young”

Best Art Direction
Capital Cities – “Safe and Sound”
Thirty Seconds To Mars – “Up in the Air”
Janelle Monae feat. Erykah Badu – “Q.U.E.E.N”
Lana Del Rey – “National Anthem”
Alt-J – “Tesselate”

Best Choreography
Chris Brown – “Fine China”
Ciara – “Body Party”
Jennifer Lopez feat. Pitbull – “Live It Up”
will.i.am feat. Justin Bieber – “#thatPOWER”
Bruno Mars – “Treasure”

Best Cinematography
Thirty Seconds To Mars – “Up in the Air”
Lana Del Rey – “Ride”
Yeah Yeah Yeahs – “Sacrilege”
Macklemore & Ryan Lewis feat. Ray Dalton – “Can’t Hold Us”
A-Trak & Tommy Trash – “Tuna Melt”

Best Direction
Justin Timberlake feat. Jay-Z – “Suit & Tie”
Macklemore & Ryan Lewis feat. Ray Dalton – “Can’t Hold Us”
Yeah Yeah Yeahs – “Sacrilege”
Fun. – “Carry On”
Drake – “Started From The Bottom”

Best Editing
Pink feat. Nate Ruess – “Just Give Me A Reason”
Calvin Harris feat. Florence Welch – “Sweet Nothing”
Macklemore & Ryan Lewis feat. Ray Dalton – “Can’t Hold Us”
Justin Timberlake – “Mirrors”
Miley Cyrus – “We Can’t Stop”

Best Visual Effects
Capital Cities – “Safe and Sound”
Duck Sauce – “It’s You”
Flying Lotus – “Tony Tortures”
Skrillex feat. the Doors – ”Breakn’ a Sweat”
The Weeknd – “Wicked Games”

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...