MAPOKEZI
wa Mshambuliaji Mpya wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga aliyetokea timu
ya Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA),Yayo Lutimba kwenye uwanja wa
Ndege Mkoani Tanga jana yalikuwa ya aina yake kutokana na kulakiwa na
wingi wa mashabiki,viongozi na wanachama wa timu hiyo.
Mapokezi
hayo yalianza saa mbili asubuhi na mchezaji huyo kutua saa nne katika
uwanja wa ndege akiwa na Meneja wa timu hiyo Akida Machai ambaye alikuwa
ameambatana naye kutoka nchini Uganda.
(picha kwa hisani ya binzubeiry)
Mshambuliaji
wa Mpya wa klabu ya Coastal Union ya Tanga Yayo Lutimba akitoka uwanja
wa Ndege wa Tanga mara baada ya kutua akitokea nchini Uganda kushoto
kwake ni Meneja wa timu ya Coastal Union Akida Machai ambaye alimfuata
nchini humo.
Awali
aliripotiwa katika gazeti la Uganda New Vision la jana (juzi)
liliripoti kuwa mchezaji huyo alisajiliwa na Yanga ya Tanzania.
Akizungumza
katika mapokezi hayo,Katibu wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga,Kassim
Eli Siagi alisema wameingia mkataba wa miaka miwili na mchezaji huyo
ambaye ataitumia timu hiyo kuanza msimu mpya wa ligi kuu utakaoanza
Agosti 24 mwaka huu.
El Siagi alisema kuwepo kwa mchezaji huyo katika kikosi kuteleta chachu na upinzani mkubwa na hivyo kuipa mafanikio timu hiyo.
Katibu
Mkuu wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga, Kassim El Siagi kulia mwenye
shati la mistari meupe katikati ni Mshambuliaji huyo Yayo Lutimba na
kulia ni shabiki wa timu hiyo Miraji Wandi.
Awali
akizungumza mara baada ya kuwasili uwanjani hapo,Lutimba alihaidia
kucheza kwa kujituma ili kuweza kuipa mafanikio timu hiyo pamoja na
kushirikiana na wachezaji wenzake ili kutimiza malengo yao.
No comments:
Post a Comment