facebook likes

Thursday, August 8, 2013

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA: NDUGU WAGOMA KUZIKA MAREHEMU WAKIAMINI MGANGA ATAMFUFUA NDUGU YAO




Dereva wa boda boda Cheni Abed akiwa chini baada ya pikipiki yake

 kugonga na baiskeli kwenye makutano ya barabara za Mafisa,Kichangani.
Dereva wa boda boda Aliyejulikana kwa jina Bw Cheni Abed kufariki dunia 
baada ya kugongana na baiskeli huku dereva wa baiskeli hiyo ambaye pia alimpakia mwanawakiwa salama salmini.
....SOMA NA ANGALIA PICAHA ZAIDI...Cheni ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mchuma kata ya Kichangani mkoani hapo  alipoteza maisha baada ya kugongana na baiskeli hiyo na kuangukia kichwa  kwenye makutano ya barabara za Msamvu,Mafisa,Mwembesongo huku dereva  wa baiskel hiyo ambaye alimpakia mwanae wakisalimika kwenye tukio hilo.

Umati wa watu ukishuhudi tukio hilo la aina yake

Kufuatia mazingira ya tukio hilo familia ya dereva boda boda huyo iliamua 
kusafiri hadi wilaya ya mvomero kwenda kwa mganga wa kienyeji kuchunguza  mazingira ya kifo hicho ambapo Sangoma Hamis Masai mkazi wa kijiji cha  Changarawe kata ya Mzumbe Wilaya ya Mvomero mkoani hapo alimueleza baba  wa mzazi wa marehemu huyo Bw Abed Shabani kwamba mama yake mzazi ndiye  alimuua mjukuu wake huyo kwa kumchukua msukule na kwamba Sangoma huyo  alimhakikishia Mzee Shabani kwamba alikuwa na uwezo wa kumrejesha dunia  mwanae huyo aliekuwa nguvu muhimu kwenye familia hiyo.

Kufutia kauli hiyo Mzee Shabani aliludi Morogoro mjini na kusitisha mazishi ya 
kijana wake kwa siku nne akisubiri mganga huyo amfufue, kufuatia taarifa hizo  majirani ambao tayari walishaanza kutoa msaada wa kuchimba kaburi na kuchanga  michango ya mtaa walizuiwa kufanya shughuri hizo kwa maelezo kwamba Cheni  angefufuliwa.
Habari za kufufuka kwa boda boda huyo zilizagaa kwa kasi kubwa kama

 kile
 kimbunga cha sunami na kwamba siku ya nne aliyoahidi mganga huyo 
kumfufua boda boda huyo ilipofika umati wa watu kutoka kona zote za mji wa  morogoro walifuka nyumbani kwa mzee Shabani akiwemo waandishi wa habari hizi  kwa lengo la kushuhudia maajabu hayo. Na Dustan Shekidele..


Familia hiyo na wananchi hao walisubiri toka saa mbili asubuhi hadi 
saa moja usiku bila kushuhudi boda boda huyo akifufuliwa na kwamba  Sangoma huyo alipoulizwa na familia hiyo alidai kwamba kuna mashariti  yalivunjwa
 na familia hiyo hivyo asingeweza tena kumfufua marehemu wao na kwamba 
baada
 ya kauli hiyo watu walitawanyika na kurudi siku iliyofuta kumzika boda boda
 huyo.
Katika mazishi hayo kuliibuka mambo kadhaa ambapo miongoni mwa mambo 
hayo ni mashekhe wote wa kata ya kichanga kugoma kwenda kumsalia marehmu  huyo wakiitaka familia hiyo kwenda kumwita mganga huyo wa kiennyeji  wanayemuami aje kumsalia marehemu wao.


Familia hiyo baada ya kuona viongozi hao wa dini wamevuta 'Hend Breck' 
wameamu kukodi boda boda na kwenda kumfuata shekh Mageta ambaye ana  undugu na familia hiyo na kwamba kwenye mawaidha yake Shekh Mageta akiipiga  madongo familia hiyo kwa kuabudu mambo ya kishirikina.

"Nimepata habari mashekh wenzangu wa eneo hili wamesusia kuja 
kwenye msiba huu kwa mambo yetu ya kijinga ya kuabudu ushirikina kijana  wetu amekufa kwa ajari na ameangukia kichwa damu nyingi zimetoka leo  mnaenda kuangua kwa mganga kuchunguza kifo chake na mnadanganywa  eti mganga huyo naweza kumfufua mtu mbona ameshindwa kumfufua naomba
siku nyingine msiludie jambo hili" alisema Shekhe mageta kwenye mawaidha yake.
Mwenyekiti wa mtaa huo wa chuma Bw Nathanael Chacha ambaye alikiri 
kupokea taarifa za familia hiyo kumfufua kijana wao alijaribu kuwaambia  wajumbe wake waliokuwa kwenye zoezi la kuchanga pesa za pole kuacha  zoezi hilo.
Jambo la tatu lililojiri kwenye msiba huo ni kwamba kwenye akaunti ya simu

 ya marehemu kulikutwa pesa taslimu shilingi laki sita na kwamba dada za 
marehmu walihangaika kuzitoa pesa hizo bila mafanikio baada ya kushindwa  kuitambua namba ya siri ya marehmu huyo licha ya kujari kuweka namba ya  siri ya mwaka wa kuzaliwa wa maremu huyo.
Baba mzaza wa marembu Mzee Abed Shabani alipohojiwa na mtandao huu 
alikiri simu ya mwanae huyo kuwa na kiasi hicho cha fedha na kudai kwamba  wanashindwa kuzitoa baada ya kutoitambua namba ya siri, habari ambazo  mtandao huu umezinasa zilidai kwamba mchumba wa boda boda huyo ambaye  amezaa naye mtoto mmoja ndiye pekee anayejua namba za siri za simu ya  mpenzi wake na kwamba kuna habari zinadai kwamba wifi zake kwa sasa  wamemficha jambo hilo naye amedai kwamba kamwe hawezi kuwatajia  namba hizo za siri mpaka atakapohakikishiwa mgao wa fedha hizo kwa yeye na
 mtoto wake.
 
Mwendelezo wa tukio hili kwa picha za mazishi usikose kutemebea mtandao huu  kujua mengi juu ya tukio hili ikiwemo ya bibi huyo wa marehemu aliyetumia uchawi  naye kufariki duni kwa Sangoma huyo

Pikipiki yake ikiwa safi haijaaribika popote kama inavyoonekana 

Polisi wakimpakia kwenye gari boda boda huyo kwa lengo la kumpeleka 
hospitali ambapo kabla ya kufika hospitali boda boda huyo alifia njiani.





Mungu ni mkubwa dereva wa baiskeli hiyo alimpakia mwanae ambaye 
hakuumia popote kwenye ajari hiyo

Gari ya polisi ikielekea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...