facebook likes

Friday, February 8, 2013

PICHA YA SIKU

Msanii Rama D ambaye hivi sasa anafanya poa na ngoma ya 'Kuwa na subira' akiwa na familia yake nchini Australia.Kwenye Picha ni mama wa mke wake(Mama Mkwe) anayeenda kwa jina la Michelle,mke wake Jazz na mtoto wake wa kike anayeenda kwa jina la Abigail

PREZZO NA GOLDIE KUFUNGA PINGU ZA MAISHA FEBRUARI 9



Kutokana na mitandao mbalimbali nchini Nigeria, rapper Jackson Makini aka Prezzo anatarajia kufunga ndoa na mwanamuziki wa Nigeria Goldie February 9.


Habari hiyo pia imeandikwa na website ya Big Brother Africa. Harusi hiyo itafanyika jijini Lagos, Nigeria.

Katika hatua nyingine mwakilishi wa mwaka jana wa Nigeria kwenye shindano la Big Brother Africa, anatarajia kuanzisha Reality TV show yake.Goldie anaanzisha show hiyo iitwayo ‘Tru Friendship’. ‘Tru Friendship’ itaonesha maisha ya kila siku ya muimbaji huyo wa Skibobo, Goldie, yote kama mtu maarufu na kama Susan Harvey.

Show hiyo itaanza kuonekana mwishoni mwa mwezi huu.

me

http://i1323.photobucket.com/albums/u599/Jovin_Edward_Bachwa/23e4c3ff-040a-42aa-b8f0-16b4da282048_zpsa0a58e2d.jpg

Angalia Picha....MV VICTORIA ILIVYONUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO

Maafisa wa kikosi hicho walijitosa kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria ambapo walifanikiwa kuuzima huku ukiwa tayari umeteketeza magodoro yote pamoja na mito ya makochi iliyokuwa katika chumba cha kuhifadhia mizigo.
Juhudi zikiendelea kwa maafisa wa kikosi…

"SITAPOTEZA MUDA WANGU KUMJIBU NIKKI MBISHI...NAWEZA KUMLEA NA AKAISHI VIZURI"...NEY WA MITEGO



Rapper na hitmaker wa ‘Nasema Nao’ Ney wa Mitego amefunguka kuwa hana mpango wa kumjibu Nikki Mbishi aliyeandika wimbo wa kumdiss uitwao ‘New wa Mitego’. 
 Miongoni mwa mashairi kwenye wimbo huo yanasema, “’Ney wa mitego, anagawa ndogo ka gay mwenye pepo’.


Pia February 6, Nikki alitweet, ‘I am deeply in love with this shawty named @Nay wa mitego’.Mwandishi wetu ameongea na Ney kuhusiana na issue hiyo ambaye amesema hana mpango wa kumjibu Nikki kwakuwa anatafuta pa kutokea.
“Anatafuta pa kutokea mimi sitaki kuongea lolote kuhusu yeye. Mimi sitaki kufuatilia kwasababu nimeshagundua kuwa ni upuuzi, yeye anatafuta njia ya kupita mimi sitaki kuzungumza chochote, hata interview yoyote kuhusu yeye sitaki, yaani nalizungumza hili kwasababu nyinyi ni wanangu lakini nimekataa, nimekataa kabisa, sitaki kabisa kumzungumzia huyo mtu,” amesema Ney.
“Kama kuna wananchi ambao ni matahira wanaweza kuelewa hicho alichokifanya it’s okay. Mimi huwa namuimba mtu kwa kitu ambacho kila mtu anakiona na ndio maana nimekuwa na mashabiki wengi sana kwasababu mimi huwa naongea ukweli. 
Nikisema Chidi Benz katoboa pua ni kweli katoboa pua, sijawahi kumuimba mtu kwa matusi au nini kwahiyo siwezi kubishana na mtu wa aina hiyo. Kwanza hajulikani, hajui anafanya nini, kwanza yeye mwenyewe hajielewi, kujielewa hakuna mwanaume anasuka hata Ulaya kwenyewe waliacha, mtu wa design hiyo ni mtu ambaye hata nauli ya kwenda studio hana, ana matatizo.”
“Angekuja kuongea na mimi ningemwambia andika lyrics hizi ni poa zaidi hata wananchi watakuelewa.Siwezi kumjibu Nikki Mbishi hata siku moja. Yeye anahustle ili atoke kwenye muziki lakini mimi mwenzake naishi bila muziki so mimi naweza nikamlea yeye na akaishi vizuri, nikamtengenezea nywele zake anazosuka, nikamkodishia na salon kwenda kusuka kila anapohitaji. Sio mara ya kwanza, alishaniimba kabla ya hapa mimi nikachukulia poa,” alisisitiza Ney wa Mitego.

RAIS KIKWETE ASISITIZA KUWA VITAMBULISHO VYA TAIFA HAVITAUZWA....


Rais Jakaya Kikwete amesema serikali itagharamia gharama zote za mamlaka ya vitambulisho vya taifa nchini NIDA ili kuondokana na changamoto zilizojitokeza awali huku akiwataka watendaji wakuu na watumishi wa NIDA wawe wazalendo na waaminifu kwa kuepuka kutoa vitambulisho kwa watu wasiostahili.

SAMATTA: GOLI LANGU DHIDI YA CAMEROON NI OMBI LANGU LA MSAMAHA KWA WASHABIKI NA NAAMINI WAMENISAMEHE

MBWANA Samatta amesema kuwa anaamini goli la ushindi alilofunga dhidi ya Cameroon linatosha kumsafisha kwa mashabiki wake.
 

Hiyo imekuja baada ya mashabiki wa soka kuwazomea pamoja na Thomas Ulimwengu wakati Stars ikicheza na Zambia, mwaka jana kwenye uwanja wa Taifa.
 

Nikutokana na kuchelewa kuripoti kambini kujiwinda na mchezo huo wa kirafiki na Chipolopolo mwakajana.
 

Kitendo hicho kilimkasirisha kocha Kim Poulsen ambaye aligoma kuwapanga kwenye kikosi ambacho kilicheza mtanange huo.
 

Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0. Bao hilo pekee, likizamishwa na Mrisho Ngassa kwa shuti la mwendo mrefu.
 

"Naamini ushindi huu utakuwa umewafurahisha mashabiki na kurudisha imani kwetu." alisema Samatta.
 

Alisema haikuwa lengo leo kuchelewa kujiunga na kambi ya timu isipokuwa ni mambo tu yaliingiliana.

SALAAM KUTOKA KWA DIAMOND PLATNUMZZ NA VALENTINE DAY......KIGOMA ALL STAR

LADIES & GENTLEMAN NAPENDA KUWATAARIFU
KUWA VALENTINE YANGU YA MWAKA HUU
NTAILIA MWANZA....HABARI NYC KWA
BALLERZ N DIVAZ KUWA SUKARI YA
WATOTO NTAKUWEPO NA CREW NZIMA YA
WASAFI KUAKIKISHA NAWALEWESHA USIKU
MZIMA MPAKA KESHO.....!!!
NA KWA MARA YA KWANZA  NTAMVISHA PETE
SEXY DIVA ATAKAEPENDEZA KULIKO DIVAZ
WOTE NDANI, PIA MWANAUME ATAKAE
PENDEZA KULIKO BALLERZ WOTE
PLATNUMZ NTAMVALISHA SAA
KALI....
USIKU HUO UTAHAPPEN NDANI YA
GOLDEN CREST,MWANZA TAREHE
14/2/2013 KUANZIA SAA 2 USIKU
HADI MAJOGOOOO...
PIA SINTOKUWA PEKEE YANGU...
THE QUEEN OF AFRO POP DARLEEN,
MAKOMANDO NA LAMECK DITTO......
WATAKINUKISHA VILIVYO....
SIPAKUKOSA KWA KIINGILIO CHA
20,000/= TU....
WAAAAASAAAFIIIIII.....!!!!

KURASA ZA MWANZO NA MWISHO ZA MAGAZETI FEB 8 2013 NDIO HIZI.


0
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

ALICHOANDIKA MH. ZITTO KABWE FACEBOOK KUHUSU BUNGENI LEO @ZittoKabwe

.

FEZZA KESSY KUICHIA SINGLE YAKE MPYA TAREHE 11

Mwanadada ambaye aliwahi kutwaa taji la Miss Dar City Center maarufu kama Fezza Kessy baada ya kuona rafiki yake kipenzi Vanessa Mdee kuingia katika tasnia ya muziki,basi na yeye amekuja na single yake mpya"Amani ya Moyo"ambayo anatarajia rasmi kuiachia siku ya Jumatatu tarehe 11 mwezi huu.
Baada ya kutuma hii cover ya single yake mpya katika e mail yetu aliandika ujumbe mfupi na kusema "Music is My job,My life,my everthing......!!!!!!!

OMMY DIMPOZZ:SIDHANI KAMA USHIRIKINA UNAFAIDA KATIKA MUZIKI

Baada ya taarifa kuenea katika mitandao kuhusu Diamond anatumia mganga wa jadi katika kazi zake za muziki.
Leo kupitia Clouds Fm double XXL katika jiwe la wiki rafiki yake wa karibu 'Ommy Dimpoz' aliweza kusema kwa upande wake hadhani kama vitu vya ushirikina vinaleta faida katika upande wa muziki na wala hajawahi kujihusisha navyo maishani mwake.
Swali:Mara ya mwisho baada ya kukutana na Diamond Platinum hamjawahi kuzungumzia mambo ya ushirikina"Kusema kweli mara mwisho nakumbuka nilikutana naye na tukazungumzia kuhusu show yangu lakini mambo mengi hatujazungumza.Ommy Dimpoz alisema

ELIMU YA U DJ YAANZA RASMI DAR ES SALAAM

HII TAARIFA MAALUM KUTOKA TAASISI BINAFSI AMBAYO ITAKUWA INATOA MAFUNZO MAALUM KWA WATU WOTE WENYE UMRI KUANZIA MIAKA 18 AMBAO WANANIA YA KUWA  MA-DJ MAARUFU HAPA NCHINI
TCH DJ ACADEMY
  PO BOX
  DAR ES SALAAM
  TANZANIA
  TEL: + 255/ 0712 580 859

   KOZI TUNAZOFUNDISHA:

 

 INTRODUCTION TO THE DJ INDUSTRY (KOZI YA 1)

1.Set up Machine
2.Mixer Operation
3.Pioneer Operation
4.Basic Mixing
5.Beat Count
6. Beat to Beat mixing
7.Acapella Mixing
Kozi hii mwanafunzi atajifunza kwa muda wa miezi mitatu (3)

ADVANCE TO THE DJ INDUSTRY ( Kozi ya 2)

1. Sound and Level
2. Turntable Operation
3. Perfect mixing
4. Scratching
5. Creative mixing and Techniques
Kozi hii mwanafunzi atajifunza kwa muda wa miezi miwili (2) baada ya kumaliza kozi ya kwanza ya Introduction to the dj I ndustry.
Kozi zote mbili Introduction to the dj industry na Advance to the dj industry zitafundishwa kwa muda wa miezi sita (6).
Fomu ni Tsh 10,000/= tu na utaratibu wa ada za kozi zote utapatikana kwenye form.
Walimu watakao fundisha ni          DJ ZERO
                                              DJ PQ
                                                     DJ D OMMY
                                           Na wengine wengi
                              Mafunzo yameanza rasmi tarehe 4 feb 2013

PICHA 10 ZA MAPOKEZI YA KUNDI LA PAH ONE CONGO DRC.


Haya ni mapokezi ya raia wa Congo DRC ambako kundi la wakali wapya kwenye muziki Tanzania Pah One limekwenda kwa ajili ya kufanya show, endelea kupita on jovinbachwa.blogspot.com kupata info kamili.









COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...