Batulli ambaye ni mmoja wa waigizaji wa kike warembo nchini na ambaye jina
lake halisi ni Yobnesh Yussuph aka Nesh, amefunguka kwenye Twitter kuwa
licha ya soko la movie kupanuka, waigizaji wengi hawana kitu.
........SOMA ZAIDI......... “Wasanii wengi wa filamu huwa tunaamka asubuhi hata hatujui tutakula
nini. Accounts zetu hazina kitu wakati tuna film nyingi sana sokoni,”
ametweet.
“Wenzetu huamka na mipango kamili ya siku iliyopo lakini wasanii wa
film huwa tunaamka huku tukiwaza ni nani wa kumpiga kibomu siku iende.
"Jina kubwa umejibana umepata gari yako 1 tena used, siku ikiipeleka
garage unashinda na wewe huko huko garage kazi zote unasimamisha
#Huruma.”
Batulli ameilalamikia pia mikataba mibovu iliyopo kwenye filamu.
“Mikataba ya kazi za film Tanzania ukiisoma unaweza ukajuta kwanini
uliamua kuwa muigizaji, unauza movie yako na haki miliki kwa miaka 50.
"Hakuna anaependa ndio maana tunalia na serikali mikataba ibadilishwe
tupewe kipaumbele movie niuze leo nimiliki baada ya 50 yrs?
"Unapoenda
kuuza kazi halafu tajiri anakupangia bei ya kuinunua pasipo kuangalia
gharama ulizotumia ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.”
No comments:
Post a Comment