KIPA wa zamani wa Simba, Juma Kaseja, ameendelea kukumbana na mikasa
lukuki baada ya paspoti yake kuibwa katika hali ya utatanishi huku rais
wa Klabu ya FC Lupopo, Victor Kasongo Ngoy, akimtaka aende DR Congo wiki
hii.
.....SOMA ZAIDI,....
Habari
za uhakika zinaeleza kuwa, paspoti hiyo ya Kaseja iliibwa wakati akiwa
kambi ya timu ya taifa hali iliyomlazimu kwenda kuripoti katika kituo
cha polisi.
“Baada ya kutoa taarifa, Kaseja alianza kufanya mpango wa kupata pasi
nyingine, kitu ambacho kiliwashangaza wengi ni kwamba chumba chake
kilikuwa kimefungwa. Inaonekana kama kuna watu wanaomfuatilia.
“Maana walitaka asicheze mechi dhidi ya Stars, lakini hata yule wakala
aliyetumwa na FC Lupopo kumfuata Kaseja, amekuwa akipata misukosuko
kibao bila sababu, hali inayoonyesha kuna watu hawataki kuona
anafanikiwa,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Alipoulizwa Kaseja kuhusiana na kupotea kwa paspoti yake, alisema yupo
katika mikakati ya kupata paspoti mpya lakini akataka kuendelea kukaa
kimya.
“Ni kweli, lakini ningependa niendelee kukaa kimya na mambo yaendelee yanavyokwenda,” alisema.
Taarifa nyingine zinaeleza, kipa huyo atasafiri kwenda DR Congo kuonana
na rais wa timu hiyo kama atafanikiwa kupata haraka pasi hiyo ya
kusafiria.
Kipa huyo amekuwa akiingia katika misukosuko mfululizo hali inayoashiria
kwamba kuna watu walitaka kuona hachezi katika kikosi cha timu ya taifa
na ikiwezekana asipate timu ya kuichezea.
Kaseja yupo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba na FC Lupopo.
No comments:
Post a Comment