WAFUASI
52 wa Shekhe Ponda Issa Ponda, waliohukumiwa adhabu ya kifungo cha
mwaka mmoja jela, wamekata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,
wakipinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyowatia hatiani.
.......READ MORE.....
Katika rufaa yao hiyo, wafungwa hao, kupitia kwa wakili wao, Mohamed
Tibanyendela, wanapinga hukumu ya Mahakama ya Kisutu, ambapo pamoja na
mambo mengine, wanadai kuwa hakimu alikosea kisheria kuchambua ushahidi
wa pande zote uliowasilishwa mahakamani hapo.
Pia wanadai kuwa katika hukumu hiyo, hakimu alijikanganya kwa kumwachia
huru mmoja wa washtakiwa na kuwatia hatiani washtakiwa wengine.
Rufaa
hiyo imepangwa kusikilizwa leo na Jaji Salvatory Bongole, mahakamani
hapo. Machi mwaka huu Hakimu Sundi Fimbo wa Mahakama ya Kisutu
aliwahukumu washtakiwa hao wa kesi ya kula njama na kufanya maandamano
isivyo halali kwenda jela mwaka mmoja baada ya kuwatia hatiani katika
mkosa yaliyokuwa yakiwakabili.
Washtakiwa hao walidaiwa kutenda makosa hayo Februari 15, mwaka huu.
Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Salum Makame, Said Idd na Ally
Nandumbi, Makame, Idd na Nandumbi, Hussein Athumani, Seif Rwambo, Abdull
Ally, Waziri Swed, Naziru Waziri, Ahmad Rashid, Jumanne Kayogola, Hamis
Tita, Amri Diyaga, Salum Said, Rajabu Mpita na Haji Sheluhenda, Abdul
Ahmed, Bakari Mwambele, Ramadhani Fadhili na Awadh Juma.
Wengine ni Omari Mkwau, Kassim Chobo, Abubakari Bakari, Ramadhani
Milambo, Hamis Ndeka, Athuman Juma, Abdallah Salum, Juma Makoti, Bashir
Kakatu, Imam Omari, Rashid Lukuta, Bakari Athumani, Mbwana Kassim,
Nurdin Ahmed, Mustapha Mide, Rajabu Kifumbo, Zuberi Juma.
Wengine ni Omari Mkandi, Idrisa Katulimo, Sawali Mola, Said Dudu,
Ramadhani Juma, Mussa Sinde, Issa Sobo, Yahaya Salum, Jabil Twahil,
Shomari Tarimo, Hashim Bendera, Waziri Toy, Athuman Yahaya, Yasin
Seleman, Shaban Malenda, Yasin Mohamed, Khatib Abdallah na Rajabu Rashid
wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.
Awali, ilidaiwa kuwa katika siku ya tukio, wilaya ya Ilala, jijini Dar
es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama za kufanya
maandamano isivyo halali.
Shtaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza,
washtakiwa walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kusababisha
uvunjifu wa amani.
Shtaka la tatu ilidaiwa kuwa washtakiwa wote kwa pamoja walikiuka amri
ya Jeshi la Polisi ya kutoa zuio la kufanya maandamano na kufanya
mkusanyiko ulisababisha vurugu na uvunjifu wa amani.
Katika shtaka la nne, ilidaiwa kuwa mshtakiwa Makame, Idd na Nandumbi,
waliwashawishi wananchi kwa kuwasambazia vipeperushi vya kuhamasisha
kufanya maandamano yasiyo halali.
No comments:
Post a Comment