Kenya
itakuwa nchi ya 100 ya kigeni kuwa na mchezaji anayekipiga kwenye ligi
kuu ya England wakati kiungo wa kimataifa wa nchi hiyo Victor Wanyama
atakapocheza mechi yake ya kwanza akiwa na Southampton.
Na
yote haya yasingewezekana kama isingekuwa kwa mama wa watoto sita,
ambaye ametumia maisha yake yote akifanya kazi ya mkuu wa kitengo cha
michezo katika shule moja jijini Nairobi.
Wanyama,
22, alianza kufahamika vizuri kwenye ulimwengu wa kimataifa wa soka
mwezi November mwaka jana wakati alipofunga goli katika mechi kati ya
klabu yake ya zamani na FC Barcelona na kuisadia klabu hiyo ya Uskochi
kushinda 2-1 katika mechi ya makundi ya Champions League.
Kiungo
huyo mwenye kimo cha 6ft 2in anayecheza kiungo cha ulinzi alivivutia
vilabu vya Manchester United, Arsenal na Everton miongoni mwa vingine
vingi lakini hatimaye mwishoni alisaini kuichezea Southampton kwa ada ya
uhamisho iliyovunja rekodi ya klabu hiyo £12.5million wakati wa dirisha
la usajili hili lilipofunguliwa.
Sehemu wanazotoka wachezaji wanaokipiga kwenye EPL |
Wachezaji
kutoka Albania mpaka Zimbabwe na nchi zingine 98, ukiachana na mataifa
manne yaliyomo ndani ya ya mipaka ya UK, yameshakuwa na wawakilishi
katika misimu 21 tangu ulipoanzishwa rasmi mfumo wa Premier League mnamo
1992 - lakini Wanyama anakuwa mchezaji wa kwanza kuiwakilisha nchi yake
ya Kenya.
Akiwa
na miaka 22 sasa lakini tayari ameshachezea vilabu vya juu kwa maana ya
professional clubs katika nchi tano tofauti, kuanzia AFC Leopards ya
nyumbani kwao akiwa na miaka 15, akaenda Helsingborgs huko Sweden akiwa
na miaka 16, Beerschot ya Belgium akiwa na miaka 17, Celtic ya Scotland
akiwa na miaka 20 na sasa yupo Southampton.
Lakini
bila uangalizi na kujitoa kwa mwalimu wa michezo Sophie Makoba, 48,
ingekuwa vigumu kwa Wanyama kutambua na kukiendeleza kipaji chake.
Kwa
msaada wake, Wanyama aliweza kujiendeleza na kuwa mtu muhimu katika
nchi yenye wakazi 44 million kwa kuwa mkenya wa kwanza kucheza kwenye
ligi kuu ya England.
'Premier
League ni ligi bora na ndio inayofuatiliwa kwa kiasi kikubwa nchini
Kenya na najua watapata mashabiki wengi sasa hivi wakiwa wamemsajili
Victor,' alisema Makoba katika mahojiano na gazeti la Daily mail.
'Watu
wa Kenya wana shauku kubwa ya msimu mpya wa EPL. Watu wengi wanaangalia
mechi za EPL japo sio wote wanaoweza kuangalia kwenye TV zao kwa sababu
ni gharama kubwa kulipia.'
Akiwa
bado mdogo Wanyama alikuwa na bahati nzuri ya kujiunga na shule ya
sekondari - Kamukunji High School, ambapo mwalimu amekuwa akifanya kazi.
"Hakuwa na akili sana darasani lakini ndio mchezaji mzuri zaidi
kiwanjani, aliweza kupata nafasi kwenye timu ya kwanza ya shule akiwa
amezidiwa na wenzie umri wa miaka mitatu alipokuwa na miaka 13,' anaelezea mwalimu Makoba.
Makoba
alikuwa mwanamichezo wa kweli, aliwahi kucheza michezo ya gymnastic
akiwa mdogo na pia akajaribu kucheza netball na riadha kabla ya hajaenda
kucheza basketball katika ngazi ya taifa.
Angeweza
kuendelea na michezo lakini kwake elimu ilikuwa ni bora zaidi, na hivyo
alipopata nafasi ya kusoma chuo akaamua kuachana na micheoz na kujiunga
na chuo.
'Wakati
nilipomaliza chuo mwaka 1990, nilikuwa nina miaka 25 na nikaamua
kufanya kazi katika shule ya Kamukunji kama mkuu wa kitengo cha michezo
shuleni. 'Niliona kwamba kuna wanafunzi ambao hawakuwa vizuri kimasomo
darasani ambao wangeweza kupata mafanikio kupitia michezo na kuanzia
hapo tukaanza kitu ambacho kimekuwa utamaduni wa kuendeleza michezo
mashuleni.'
Kamukunji
hakukuwa na mazingira mazuri. Ilikuwa ni kama shule nyingine tu za
kawaida jijini Nairobi, ambapo wananchi wa maisha ya kawaida ambao wana
uwezo wa kupata kiasi kisichozidi £1,000 kwa mwaka na pia vifaa vya
ufundishaji shuleni hapo vilikuwa vya kawaida.
Makoba
amekuwa mpenzi mkubwa wa soka kwa muda mrefu sana. Anaisapoti klabu ya
Manchester United na wachezaji kama George Best, Robin van Persie ndio
anawapenda lakini Roy Keane ndio zaidi.
Familia
yake yote inapenda soka. Mumewe ni shabiki mkubwa wa Arsenal, watoto
wake wawili wa kiume wote wanashabiki a Man united kama mama yao, lakini
mtoto mwingine wa kiume yeye ni shabiki wa Chelsea.
Pamoja na kuwa na mapenzi na mchezo lakini Kenya haina vifaa vizuri vya michezo.
'Hatukuwa
na uwanja pale Kamukunji hivyo nilikuwa naandaa mpango timu yangu
kufanya mazoezi katika uwanja wa kuazima uliopo karibu na shule,'
alisema Makoba. 'Uwanja wa kuazima ulikuwa unatumika jioni hivyo
ilitubidi kuanza mapema, kabla ya wenye uwanja wenyewe hawajafika. Hivyo
tulipendelea kufanya mazoezi asubuhi alfajiri mpaka kulipokucha kwa
ajili ya watoto kurudi shule.'
Kujitoa
kwa Makoba kulianza kulipa miaka 15 baadae wakati Kamukunji ilipoanza
kukuza vipaji vya makinda ambao walienda kupata nafasi kwenye vilabu
barani ulaya katika ligi tofauti.
Baadhi
ya vipaji vilivyokuzwa katika shule ya Kamukunji chini ya uangalizi wa
Makoba, miongoni mwao ni mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya Dennis
Oliech, 28, anayekipiga Ajaccio inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa,
mshambuliaji mwingine Patrick Oboya, 26, ambaye amewahi kuchezea vilabu
tofauti nchini Czech Republic na Slovakia, pia wapo wachezaji
wanaokipiga kwenye ligi ya nyumbani kama Kevin Ochieng, winga ambaye
ameshavichezea vilabu kadhaa vya Kenya.
Bila
shaka majina makubwa katika soka la Kenya kwa hivi sasa ni Wanyama na
kaka yake McDonald Mariga Wanyama, 26, kiungo wa ulinzi wa Inter Milan
ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Parma.
Mariga
angeweza kuwa mkenya wa kwanza kucheza katika ligi kuu ya England mnamo
mwaka 2010, wakati Roberto Mancini alipojaribu kumnunua kwenda
Manchester City, lakini alikosa kibali cha kufanya kazi nchini humo.
Japo
suala hilo liliingiliwa kati na waziri mkuu wa Kenya wa wakati huo
Raila Odinga, ambaye alitumia masaa kadhaa kuzungumza na waziri mkuu
Gordon Brown na maofisa wengine, lakini ilishindikana kumpatia Mariga
kibali.
'Siku
zote niliamini Victor angeenda mbali,' anasema Makoba. 'Mara zote
amekuwa mtaratibu, mpole na mwenye heshima. Mama yake Mildread na baba,
Noah, walikuwa wakifanya kazi kwenye shirika la reli la Kenya wakati
Victor akiwa mdogo.
Walikuwa
maskini, wakiishi na watoto nane katika nyumba ndogo sana. Mildred
anaishi kwenye nyumba nzuri sana, kwenye eneo zuri. Wanaendesha magari
mazuri kama Hummer na Cadillac. Nina furaha sana na mafanikio ya vijana
wangu.'
Makoba
alihama kutoka Kamajunji mwaka jana na kuhamia kwenye shule ya
wasichana watupu, ambapo jukumu lake ni kuendeleza vipaji vya soka na
basketball kwenye shule.
chanzo:shaffihdauda
No comments:
Post a Comment