Kocha
wa Manchester United David Moyes kwa mara nyingine tena amesisitiza
kwamba Wayne Rooney hatouzwa msimu huu,
Chelsea tayari wameshatuma ofa mbili
ambazo zimekataliwa kwa ajili ya Rooney - huku kocha wa timu hiyo Jose
Mourinho akiapa kutokata tamaa mpaka siku ya mwisho ya dirisha la
usajili litakapofungwa.
Pamoja na yote hayo, Moyes amesisitiza kwamba hakuna kilichobadilika.
"Wayne Rooney hauzwi," Boss huyo wa
United aliwaambia waandishi wa habari baada ya mchezo wa ngao ya hisani
jumapili jana. "Hakuna kiichobadilika kwenye suala hilo hivyo hakuna
majibu yoyote ya zaidi kuhusu suala hili."
"Baadhi yenu hamtopenda kusikia kuhusu
suala hili kwa sababu mmendika habari zisizokuwa na ukweli. Sijagombana
na Wayne. Alifanya mazoezi na wachezaji wa kikosi cha ziada kwa sababu
aliomba iwe hivyo yeye mwenyewe."
Moyes pia alizungumzia kauli yake
kwamba Rooney atakuwa fiti kuichezea England dhidi ya Scotland katikati
ya wiki lakini sio kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya
Swansea City siku ya jumamosi. (HM)
"Nataka ajiunge na England. Bado
hajapata usawa wa kimwili tayari kucheza mechi ya ushindani. Hajacheza
mechi yoyote tangu aumie. Hivyo huwezi kudhani mtu wa namna hiyo kucheza
mechi ya ushindani kwa muda mrefu.
"Nimeongea na Roy Hodgson kwa muda wa
masaa mawili kwa muda tofauti. Itakuwa jambo zuri kwa Manchester United
ikiwa atapata nafasi ya kucheza."
Chanzo: sportmail
No comments:
Post a Comment