facebook likes

Monday, August 12, 2013

"JAPO NILITUHUMIWA KUGAWA PENZI GESTI, LAKINI NIMEPIMA NA SINA UKIMWI.... NANI MJANJA??"...ROSE NDAUKA

Mwanadada Rose Ndauka ambaye hivi karibuni aliingia katika skendo ya kimapenzi na Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayechipukia, ameamua kuwa mmoja wa wasanii wachache wa Sanaa ya Filamu nchini kuamua kuanika wazi majibu ya vipimo vyake vya gonjwa hatari la ukimwi nchini. 

.......SOMA ZAIDI.....Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmmoja wa kijamii, Rose aliweka majibu ya vipimo hivyo vilivyochukuliwa wiki kadhaa zilizopita katika hospitali ya TMJ iliyopo jijini Dar es salaam, vikionesha kuwa mwanadada huyo yu SALAMA kabisa na safi kiafya ama HIV NEGATIVE kwa mujibu wa vipimo hivyo.

Katika picha hiyo Rose ndauka aliandika anamshukuru Mungu sana kwa majibu hayo.


No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...