facebook likes

Monday, August 12, 2013

Manchester United yashinda Ngao ya Jamii



CS 1

Kocha wa Manchester United David Moyes  August 11 2013 ameanza rasmi kazi yake kama kocha wa timu hiyo kwenye mechi ya ushindani baada ya kuiongoza timu hiyo kupata ushindi wa mbili bila kwenye mechi ya kuwania ngao ya jamii dhidi ya Wigan Athletic.
...ANGALIA PICHA NA MAGOLI...... HAPA

United ilipata magoli yake kupitia kwa mfungaji bora wa ligi kuu ya England kwa msimu uliopita Robin Van Persie ambae ndio alifunga hizo goli zote mbili ambapo club hii iliyoanza kuitwa Manchester United mwaka 1902 iliingia kwenye hii mechi bila mkali wao Wayne Rooney ambae hakuchaguliwa kwa sababu ni majeruhi.
Pamoja na hiyo sababu ya majeraha yake, bado ishu ya Rooney ndani ya Manchester United ni kama kitendawili.
Unaambiwa Manchester United ndio club ya kwanza England kushinda European Cup mwaka 1968 chini ya management ya Matt Busby.
CS3

Beki wa Manchester United ambae pia ni nahodha msaidizi wa timu hiyo Mfaransa Patrice Evra, alikuwa mchezaji bora wa mchezo huo baada ya kucheza kwa kiwango cha juu kwa kuchangia kwenye ufungaji wa goli zote mbili.
Taji la ngao ya Jamii linakuwa taji la kwanza kwa kocha mpya David Moyes tangu alipoteuliwa kurithi nafasi ya kocha wa zamani Sir Alex Ferguson mwishoni mwa msimu wa ligi uliokwisha ambapo Moyes ataanza rasmi kampeni ya utetezi wa ubingwa wa ligi kuu ya England kwa klabu yake wiki ijayo wakati Manchester United watakapokutana na Swansea City kwenye mechi ya kwanza ya ligi.

 Tazama magoli hapa:

 Umati wa mashabiki wa soka ukiwa unaingia ndani ya Uwanja wa Wembley jijini London, kuangalia pambano la Ngao ya Hisani kati ya Manchester United na Wigan Athletic, ambapo United imeshinda kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Robin van Persie (Picha kwa Hisani ya Gazeti la Daily Mail la Uingereza)
Man United (kulia) nma Wigan (kushoto), wakiwa wamejipanga kabla ya kuanza kwa pambano la Ngao ya Hisani kwenye dimba la Wembley jijini London. Mechi hiyo inayohusisha mabingwa wa Ligi Kuu na wale wa Kombe la FA, ni kiashiria cha ufunguzi wa msimu wa 2013/14 wa Ligi Kuu ya England.
On form: Van Persie scored a double as Manchester United beat Wigan 2-0 at Wembley
Kwenye kiwango cha juu: Robin Van Persie aliifungia Man United mabao yote mawili (moja kila kipindi), kuipa timu yake ubingwa wa Ngao ya Hisani na ushindi wa kwanza kwa kocha mpya David Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson.
Early blow: Robin van Persie headed Manchester United into the lead in the sixth minute
Bao la mapema: Robin van Persie akijitisha mpira kufunga kwa kichwa, kuipa Manchester United bao la uongozi katika dakika ya sita ya pambano holo Wembley.
In action: Manchester United's Atonio Valencia takes the ball away from Wigan's Jordi Gomez
Kikazi zaidi: Winga wa Manchester United, Atonio Valencia akimtoka beki wa Wigan, Jordi Gomez.
Ahead: The Dutchman arrived late in the penalty area to head Patrice Evra's cross into the bottom corner
Joy: United celebrate Van Persie's early goal at Wembley
Raha ya ushindi: Nyota wa Man United wakishangilia bao la mapema la Van Persie kwenye dimba la Wembley.
New signings: United's Wilfried Zaha, (left) competes with Wigan Athletic's James McClean
Usajili mpya Old Trafford: Nyota mpya wa Man United, Wilfried Zaha, (kushoto) akichuana na mchezaji wa Wigan Athletic, James McClean.
Elusive: United's new winger Wilfried Zaha escapes the attention of Ben Watson
Nakutoka hivi: Winga mpya wa Man United, Wilfried Zaha akichanja mbuga kumtoka Ben Watson.
Vocal: David Moyes and Owen Coyle shout out instructions to their teams
Maelekezo ya makocha: David Moyes wa Man United (kushoto) na Owen Coyle wa Wigan Athletic, wakitoa maelekezo kwa wachezaji wao.
Advantage doubled: Van Persie net's Manchester United's second goal just before the hour mark
Natikisa hivi nyavu: Van Persie akiifungia Manchester United bao la pili kuipa ushindi wa mabao 2-0.
Challenge: Manchester United's Nemanja Vidic comes under pressure from Shaun Maloney
Mchuano dimbani: Beki wa Manchester United, Nemanja Vidic akichuana na Shaun Maloney wa Wigan Athletic.
Race: Chris Smalling (left) competes with McClean to reach the ball
Mbio dimbani: Beki Chris Smalling (kushoto) wa Man United, akishindana mbio kuwania mpira na McClean wa Wigan Athletic.
The heat is on: Manchester United and Wigan walk out onto the pitch at Wembley
From the front: Manchester United manager Moyes leads his team out at Wembley
Bosi kazini: Kocha mpya wa Manchester United, Moyes akiongoza nyota wa kikosi chake katika mechi hiyo.
New toy: Fourth official Michael Oliver tests out the Goal Decision System before the match
Majaribio GLT: Mwamuzi wa akiba, Michael Oliver akifanyia majaribio mfumo mpya wa Goal Line Technology (GLT), ulioanza kutumiwa katika mechi hiyo ya Ngao ya Hisani na kutarajiwa kutumiwa katika Ligi Kuu ya England.
Iconic walk: Fans make their way down Wembley Way for the Community Shield
Twenzetu!!! Mashabiki wakiingia Uwanja wa Wembley.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...