Francois Bozize - Africanarguments.org |
Rais aliyeondolewa madarakani kwa mapinduzi ya mwezi machi mwaka huu
nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati, Francois Bozize amesema yupo tayari
kurejea madarakani na kuiondoa serikali ya mpito inayoongozwa na kundi
la waasi wa Seleka.
Baada ya kuwa nje ya nchi yake kwa zaidi ya miezi minne, Bozize amesema
atatumia njia za kidemokrasia kufanikisha lengo hilo na ikishindikana
atalazimika kutumia nguvu.
Akiwa katika mahojiano na Radio France International RFI jijini Paris
Ufaransa, Bozize ameituhumu nchi jirani ya Chad kwa kuwaunga mkono waasi
wa Seleka waliofanikisha kuuangusha utawala wake.
Katika hatua nyingine, Bozize amesema ameanzisha chama chake ambacho
anaamini kitamsaidia kufanikisha malengo hayo na ameiomba Ufaransa
kusaidia Taifa lake ili suluhu ya kisiasa iweze kupatikana.
Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki-moon alilitaka
Baraza la Usalama la UNSC kuwawekea vikwazo baadhi ya viongozi wa Seleka
kutokana na kutajwa kuhusika na uvunjifu wa haki za binadamu nchini
mwao.
Aidha Ban alihimiza uundwaji wa tume ya kutafuta ukweli itakayochunguza
matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea kushuhudiwa nchini
Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Via kiswahili.rfi.fr
No comments:
Post a Comment