BENKI Kuu ya Tanzania
(BoT) Kanda ya Kaskazini, Arusha imewatahadharisha wananchi kuhusiana na tatizo
la noti bandia nchini,
....SOMA ZAIDI.... anaripoti Richard Konga, Arusha.Akizungumza
wakati wa Maonesho ya Wakulima Nane nane yaliyomalizika hivi karibuni, Meneja
wa Fedha na Utawala wa BoT, Evena Ndesingo, alisema benki hiyo imeanza kutumia
maonyesho ya wakulima kutoa elimu ya utambuzi wa noti zake.
Alisema wananchi wanatakiwa kuwa makini wakati
wa kutoa au kupokea fedha ili kuepuka kufilisika na kuyumbisha uchumi wa
taifa.
“Benki imeanzisha utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi ili watambue noti
bandia kupitia alama halisi zilizoko kwenye noti halali,” alisema.
Hata hivyo, alisema
matumizi ya noti bandia ndani ya jamii yanapungua kila mwaka kutokana na jamii
kuwa na uelewa wa noti halisi na bandia na hivyo kupunguza kasi ya mzunguko wa
noti bandia hizo.
Alisema BoT kupitia
matawi yake nchini imejidhatiti kuwaelimisha wananchi juu ya utambuzi wa noti
mpya na alama zake ili jamii izielewe na kutofautisha noti hizo.Alisema noti
bandia iwapo zitaachwa ziendelee kuwepo kwenye mzunguko wa matumizi ya kawaida
ipo hatari kwa jamii kufilisika na taifa kuyumba kiuchumi.
Ndesingo aliwataka
wananchi kuwa makini wanapofanya malipo ya noti mpya kwa kuchunguza kwa makini
alama hizo kabla hazijapelekewa matumizi ya noti hizo kwa mtu mwingine.
No comments:
Post a Comment