DIWANI wa Kata ya Chonyonyo
(CCM) wilayani Karagwe, Arnold Rweshekerwa, amenusurika kuuawa na kundi la
majambazi waliomteka nyara katika eneo la Kyanyamisa kabla ya kuwatoroka akiwa
amewafungia ndani ya gari lake katika Pori la Kimisi.
...SOMA ZAIDI.........
Tukio hilo limetokea siku chache
tangu Rais Jakaya Kikwete, atoe siku 14 kwa majambazi katika mikoa ya Kagera,
Geita na Kigoma kusalimisha silaha na kuacha vitendo hivyo kabla ya msako wa
nyumba kwa nyumba kuanza.
Pia
agizo hilo la Rais Kikwete liliwahusu wahamiaji haramu waliopo katika mikoa
hiyo kuwa wameondoka ndani ya kipindi hicho.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mjini hapa na kuthibitishwa na Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Kagera, Phillip Kalangi, tukio hilo lilitokea Agosti 10,
mwaka huu saa 2.00 katika eneo lenye kibao kinachoonesha sehemu ya hifadhi ya
akiba katika pori la Kimisi kuelekea wilayani Ngara.
Baada ya
kunusurika kuuawa na majambazi hayo, waliteketeza gari la diwani huyo kwa kitu
kinachodhaniwa bomu. Habari hizo zinaeleza kuwa, Diwani huyo alikuwa ameenda
Kijiji cha Kyanyamisa kumtembelea bibi yake mzaa mama, ambapo wakati akirudi
nyumbani alikutana na watu wawili njiani, wakiwa na bastola, ambapo baada ya
kumsimamisha walimtaka ageuze gari kurudi alikokuwa anatoka.
Wakati
wa harakati za kugeuza gari hilo, huku majambazi hao wakiwa wamekaa ndani ya
gari lake hilo alikutana na watu wengine tena.
Alisema
watu hao walikuwa na mifuko minne iliyojaa bunduki, magazine na risasi, ambapo
akiwa anawaendesha kwenye gari lake, watu hao walikuwa wanaingiza risasi kweye
magazine.
Walipofika
mbali jirani na hifadhi ya akiba walimwamuru diwani huyo kusimamisha gari na
kuzima taa, huku wakiendelea kuingiza risasi kwenye magazine kwa tochi.
Wakiwa
katikati ya Pori la Kimisi alifunga milango ya gari kisha kuruka kwa kupitia
dirishani kutokomea porini.
Habari
hizo zinaeleza kuwa diwani huyo alitembea zaidi ya kilomita mbili akirudi
Karagwe, ambapo aliona pikipiki moja ikiwa na watu wawili wenye silaha
wakitokea Kyanyamisa kwenda Ngara.
Inadaiwa alishindwa kuwasimamisha kwa kuhofia huenda wakawa ni wenzao,
wakati alipokuwa ametekwa aliwasikia wakiwasiliana na watu wengine.
Baadaye
alipata usafiri wa Hiace iliyokuwa ikitoka Benako wilayani Ngara saa 3.30.
Alipanda gari hilo ambapo alianza kuwasimulia abiria kilichotokea. Habari zaidi
zilieleza kuwa abiria hao walimwambia kuwa waliona gari likiteketea kwa moto.
Kamanda
Kalangi alisema; “Tukio hilo lipo na gari limeteketezwa kweli,
lakini suala la utekaji wa diwani huyo, inakuwa ngumu kulithibitisha kwani
wakati likitokea, alikuwa peke yake.”
Katika tukio , watu hao hawakuweza kumdhuru diwani huyo, bali walimpora
simu, sh.100,000 na viatu vyake alivyokuwa amevaa.
Diwani huyo amelazwa Hospitali Teule
ya Nyakahanga baada ya kupoteza fahamu
No comments:
Post a Comment