facebook likes

Monday, August 12, 2013

ALIYEMVUTISHA MADAWA YA KULEVYA (UNGA) RAY C AKAMATWE..!

WIKI iliyopita, sexy lady wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ au ‘Kiuno Bila Mfupa’ alifunguka juu ya mwanaume aliyekuwa akimvutisha madawa ya kulevya ‘unga’ bila kumtaja hivyo kuibua mzozo katika majukwaa ya kisheria kuwa mtu huyo akamatwe mara moja.

....SOMA ZAIDI...

Mara baada ya Ray C kufunguka kuhusu ishu hiyo kupitia Clouds TV, habari hiyo iligeuka gumzo hasa kwenye mitandao ya kijamii ikisemekana kuwa mhusika anafahamika.

Ray C alisema mwanaume aliyekuwa akimuwekea unga bila yeye kujua alikuwa ni boyfriend wake ambaye alitengana naye mwaka 2010 ili kujinusuru na balaa hilo.

Alisema: “Nilimpenda kwa moyo wangu wote ila nikalazimika kuachana naye.

“Ilibidi aende kwa sababu yeye ndiye aliyeniletea balaa lote. Nikasema vyovyote vile Mungu naomba unisaidie, nampenda huyu kijana ila hayupo sawa. Tukatengana 2010 lakini tatizo lilikuwa limeshaota mizizi.”

Kwa mujibu wa baadhi ya wanasheria waliozungumza na gazeti hili, katika maelezo ya Ray C, mhusika ana kesi mbili za kujibu, kwanza kuwa na huo unga na pili kumuwekea mtu madawa ya kulevya bila kujua au hata angejua, yote ni makosa ya jinai.

“Ukiangalia watu kama Rais Jakaya Kikwete na Ruge Mutahaba walivyojitahidi kumwokoa Ray C utagundua ni jinsi gani walivyohangaika wakati aliyesababisha yupo!

“Kinachotakiwa kufanyika ni Ray C kumtaja mhusika ‘theni’ sheria ifuate mkondo wake.

Ni vema ishu hii ya Ray C ikatumika kama fundisho kwa mastaa wengine na jamii nzima hasa linapokuja suala la aina ya mpenzi unayekuwa naye,” aliandika mmoja wa wachangia mada mtandaoni.

Historia inaonesha kuwa mwanadada huyo ambaye anarejea upya katika muziki aliwahi kuwa na wanaume wawili waliofahamika kila kona Bongo.

Mmoja ni staa wa Big Brother Africa, Mwisho Mwampamba ambaye alikuwa mara tu baada ya kutoka kwenye shindano hilo mwaka 2003 ambaye Ray C aliwahi kukiri kuwa walidumu hadi mwaka 2006.

Mwingine ni aliyekuwa rapa wa N2N Soldiers kwa sasa yuko kwenye Kruu ya Weusi, Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ waliyehitilafiana mwaka 2008.

source:peruzibongo

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...