Sakata la klabu ya Yanga kugomea
kukubaliana na mkataba wa kati ya kamati ya Ligi na Azam Media wa kuipa
haki za matangazo ya televisheni ya mechi za ligi kuu kituo cha Azam TV
limechukua sura mpya baada ya Rais wa shirikisho la soka la nchini TFF
Leogdar Tenga kuingilia kati.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi mtandao
huu ulizozipata ni kwamba Tenga amewaandikia barua Yanga akiwaambia
kwamba amepata malalamiko yao dhidi ya mkataba wa urushwaji wa matangazo
ya mechi za ligi kupitia Azam TV.
Pia Tenga amewaambia Yanga kwamba
ameiomba kamati ya ligi kumpatia maelezo namna mchakato mzima wa ugawaji
wa tenda hiyo ulivyofanywa mpaka kufikia maamuzi ya kuingia makubaliano
na Azam TV.
Tenga amewaomba Yanga kuwa wavumilivu
ili kushughulikia malalamiko yao kuhakikisha muafaka unafikiwa kwa ajili
ya manufaa ya soka la Tanzania.
Chanzo: shaffihdauda
No comments:
Post a Comment