facebook likes

Monday, August 12, 2013

AJALI MBAYA YATOKEA BARA BARA KUU YA MOSHI-ARUSHA ENEO LA KWA SADALA

 Gari la shirika la umeme Tanzania (Tanesco) imepinduka jana usiku baada ya kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Corola katika eneo la 
Kwa Sadala barabara kuu ya Moshi-Arusha. 
.......SOMA ZAIDI.....
 Kwa mujubu wa shuhuda wa ajali hiyo, gari la Tanesco lilikuwa limepakia wafanyakazi wa shirika hilo wapatao 18 wakitokea eneo la KIA kuelekea mjini Moshi. 
 
 Amesema dereva wa gari dogo alikuwa akijaribu kuzipita gari kadhaa zilizokuwa zikielekea Arusha ndipo akakutana na Loli hilo kabla ya kurudi  upande wake.
Ndipo gari magari hayo yakagongana na kisha gari la Tanesco kupinduka.
 
 Shuhuda  amesema majerhi wa ajali hiyo walikimbizwa hosptali ya KCMC huku dereva wa gari hilo dogo akiingia mitini na kutokomea kusiko julikana. 
                                    Toyota Corola lililosababisha ajali hii
             Askari wa usalama barabarani na gari la tanesco lililopinduka
                                           Wadau eneo la  tukio

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...