Burudani ya mchezo wa timu mbili ziliminyana vikali kwenye mchezo wa
kirafiki mjini Washington D.C nchini Marekani na kushuhudia timu ya
Chelsea kushinda mabao 2-1 dhidi ya Rome,
Bao la kwanza: Mshambuliaji hatari wa Rome Erik Lamela alipofunga goli la kujishtukizia. Photo Credits: dailymail.co.uk
Rome ndio walioanza kufungua dimba mnamo dakika ya 20 baada ya ya kipa
wa timu ya Chelsea Mark Schwarzer kufanya kosa ndani ya lango kwa mpira
uliorudishwa nyuma na beki wake wa kushoto Ryan Bertrand huku kipa
akitaka kuremba mpira uliorudishwa nyuma matokeo yake kujikuta mpira
umemcheza na kugonga mwamba bila ya kuweza kuudhibiti hapo mshambuliaji
wa timu ya Roma Erik Lamela akijikuta kupata mwanya wa kufunga goli la
kiubwete ndani ya lango la timu ya Chelsea kipindi cha kwanza.
Furaha za goli: Kiungo wa timu ya Chelsea Frank Lampard akisherehekea bao la kusawazisha. Photo Credits: dailymail.co.uk
Timu
ya Chelsea katika kipindi cha pili iliingia uwanjani na nguvu mpya za
matumani ya ushindi kwa mpambano wa vuta ni kuvute dhidi ya timu ya
Rome kutoka nchini Italy, bao la kusawazishwa lilifungwa dakika ya 60 na
mshambuliaji hatari Frank Lampard baada ya kuachi kombara kali njee ya
18 na kujikuta Rome kuelimewa duru la pili dhidi ya Chelsea iliokua
ikipiga makombora ya mbali.
Rome
walijitahidi sana kimchezo pamoja na kushambulia kipindi cha pili,
wakipapatuana na kila mmoja kutaka usindi wa mchezo huo, mnamo dakika ya
89 ilikua vuta nikuvute katika lango la Rome ndipo mshambuliaji hatari
wa Chelsea Romelu Lukaku alipopata mwanya wa kuipatia timu
yake bao la pili, hadi muamuzi wa mpambano waburudani hiyo, Amando
Villarreal alipopuliza pinga yake ya mwisho, na kujikuta timu ya
Chelsea Roma inatoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Rome ndani
uwanja cha RFK Stadium, Washington, D.C
Mshambuliaji w wa bao la ushindi Romelu Lukaku alipotingisha nyamvu za Rome Siku ya Jumamosi , Aug 10, katika uwanja cha RFK Stadium, Washington, D.C. Photo Credits: dailymail.co.uk
Wapenzi wa timu zote mbili
waliofurika katika burudani ya mpambano kati ya Chelsea na Rome ya Italy
Siku Jumamosi , Aug 10, katika uwanja cha RFK Stadium, Washington, D.C
ANGALIA VIDEO HAPA
No comments:
Post a Comment