...SOMA ZAIDI......
Mkutano huo ambao ulifanyika Dar es Salaam kuanzia Juni 28 hadi Julai
Mosi mwaka huu ulindaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa hivi karibuni, ulihusisha viongozi wakuu wa Afrika.
Akizungumza na Mwananchi jana, Utouh alisema kuwa, ukaguzi wa fedha
hizo utaanza kufanyika Oktoba mwaka huu, huku ukienda sambamba na
ukaguzi wa matumizi za wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2013/14.
“Tutafanya ukaguzi maalumu wa Sh8 bilioni zilizotumika katika mkutano
wa Smart Partnership Dialogue ili tuweze kubaini matumizi ya fedha
hizo,”alisema Utouh.
Aliongeza, kwa mujibu wa sheria, CAG anapaswa kukagua matumizi ya
fedha zote za Serikali zinazotumika katika Wizara, Taasisi na Mashirika
ya Serikali ili waweze kubaini uhalali wa matumizi ya fedha hizo kwa
kila ibara.
Alisema, kwa sasa zoezi la kufunga hesabu linafanyika Septemba mwaka
huu, kila wizara ikiwamo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa zitatakiwa kuwasilisha taarifa hizo ofisini wake kwa ajili ya
kuanza ukaguzi ambao utafanyika Oktoba mwaka huu. Kusoma zaidi bofya
“Kwa sasa wizara nyingi ikiwamo Wizara ya Mambo ya Nje inakamilisha
zoezi la kuhakiki hesabu zao, na kwamba wakimaliza wanatupa taarifa ili
tuweze kukagua hesabu zao za mwaka, jambo ambalo linaweza kutusaidia
kubaini matumizi mabaya ya fedha za serikali kwa mwaka,” aliongeza.
Aliongeza ikiwa fedha hizo zimetumika kinyume na taratibu,
zitabainika na kwamba watawalisha taarifa hiyo serikalini kwa ajili ya
kuwachukulia hatua watu watakaobainika wametumia vibaya fedha za
Serikali.
Hivi karibuni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta
alimtaka CAG kufanya ukaguzi wa Sh8 bilioni zilizotumika wakati wa
Mkutano wa Smart Partnership uliofanyika jijini Dar es Salaam. Alisema
baada ya kukamilika uchunguzi huo, watakaobainika kuhusika wachukuliwe
hatua madhubuti na stahiki.Hata hivyo, Utouh alisema mbali ya Waziri Sitta kumtaka kufanya uchunguzi, lakini mpaka sasa hajapewa agizo hilo kwa maandishi kuhusiana na tuhuma hizo.
“Mimi nilisoma kwenye vyombo vya habari vya kunitaka nifanye uchunguzi kuhusiana na ubadhirifu wa fedha hizo, lakini mpaka sasa hakuna barua yoyote iliyowasilishwa ofisini kwangu ikinitaka nifanye hivyo,”alifafanua.
Alisema kutokana na hali hiyo, atafanya ukaguzi kwa mujibu wa sheria na taratibu za kazi zake ili aweze kubaini tatizo hilo.
Hivi karibuni, Waziri Sitta alisema kuwa wizara hiyo imetumia kiasi cha Sh8 bilioni katika mkutano wa Smart Partnership Dialogue, kutokana na kuzikabidhi kampuni tatu hewa ambazo zililipwa fedha wakati hazijasajiliwa kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela).
Chanzo :mwanachi.
No comments:
Post a Comment