Mwakilishi
wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman (katikati)
akipata maelezo ya kazi mbalimbali za Shirika hilo kutoka kwa Afisa
Habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama wakati alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho
ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Mkufunzu
wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) Marwa Wambura (katikati)
akimuonyesha Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO)
Diana Templeman (kulia) malighafi za ngozi zinazotumika kutengeneza
bidhaa mbalimbali na wanafunzi wa Chuo hicho ambapo mafunzo hayo
yanadhaminiwa na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza
viwanda Duniani (UNIDO).
Mwakilishi
wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman akiangalia
viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na wanafunzi wa Chuo cha DIT kwenye
banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na Wanafunzi wa Chuo cha DIT cha Mwanza.
Mwakilishi
wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman
akizungumza na waandishi habari ambapo amefafanua changamoto mbalimbali
zinazoikabili dunia katika mabadiliko ya tabianchi ambapo wao kama Umoja
wa Mataifa wanafanya kazi ya kuelemisha Umma, Wakulima, Wafanyabiashara
na Wasindikaji jinsi ya kuelelewa mabadiliko ya tabianchi katika
kukabiliana na tatizo la uhaba wa njaa duniani na upatikanaji wa
chakula. Kulia ni Mratibu wa kazi za vijana vijijini katika masuala ya
Kilimo, Uvuvi na Ufugaji wa FAO Bw.Eliamoni Lyatuu.
Afisa
habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Usia
Nkhoma Ledama akitoa ufafanuzi wa vipeperushi mbalimbali
vinavyozungumzia kazi zinazofanywa na shirika hilo hapa nchini kwa
baadhi ya vijana na watoto waliotembelea banda hilo leo kwenye maonesho
ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar.
Baadhi ya watoto waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa wakifurahia picha.
No comments:
Post a Comment