facebook likes

Saturday, July 6, 2013

BAADA YA JOYCE KIRIA KUSHAULIWA AMWAMBIE MUMEWE AACHANE NA SIASA na Hii ndo kauli na MSIMAMO wake kuhusiana na USHAURI HUO

   IMENUKULIWA MOJA KWA MOJA TOKA KWA JOYCE KIRIA

Hapa kuna swala nahitaji kuliweka sawa, naamini tutaelewana fans zangu wote.




My Hubby Henry Kilewo.


My Hubby Henry Kilewo akiwa katika shughuli zake za kisiasa.


Nimeolewa na mwanasiasa, mume wangu Henry Kilewo ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Kinondoni, Ila mimi si mwanasiasa(nahudumia watu wote wenye vyama na wasio na vyama).



Our Wedding Day, Nikila kiapo, "KWA TABU NA RAHA"

Muda nakubali kuolewa naye nilifahamu fika kuwa yeye ni mwanasiasa, Ila nitamsupport mume wangu kwa kazi yake aliyoichagua, siwezi kumwambia AACHE SIASA, Hilo kwa kweli HALIWEZEKANI, Hata yeye hajawahi hata siku moja kuniingilia katika kazi yangu ya kutetea haki za wanawake na maendeleo ya wanawake kwa ujumla(WANAWAKELIVE) na kuniambia niiache.


Hubby Henry Kilewo kikazi zaidi.

Ila nina swali la kuuliza hapa "KILA MTU ANAPOPATA TATIZO KATIKA KAZI YAKE ANATAKIWA KUIACHA???" Mfano Daktari akipata tatizo katika kazi yake aache? Ama Mwalimu ama mtu yoyote yule kwa kazi anayoifanya akipata changamoto anatakiwa kuacha????


My family, Hubby Henry With Our Boys, Lincon na Linston.

Fans Wangu wote naamini mtakuwa mmenielewa na mtaendelea kuwa nami all the way, Msimamo wangu ni huu, Nitasimama upande wake na kuendelea kumsupport mume wangu Henry, SIASA ni kitu anachokipenda SIWEZI KUMWAMBIA AACHE

source-http://www.joycekiria.com/

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...