facebook likes

Saturday, July 6, 2013

Superman Dwight Howard kuitosa L.A Lakers?


dm_130620_dwight_howard_image
Dwight Howard mchezaji wa ligi ya NBA nchini marekani kwenye timu ya Los Angels Lakers akiwa na mkali mwezake kama Kobe Brayant, inasemekana anataihama timu hiyo hivi karibuni. Dwight Howard ambaye aliwahi kutembelea Tanzania na kutoa misaada kwenye shule ya sekondari Kipok huko Arusha mbele ya waziri mkuu kwa wakati hule mheshimiwa Edward Lowassa, alitokea timu ya Orlando Magic msimu uliopita na kujiunga na Lakers ili kuunganisha nguvu na Kobe, lakini wamepata matokeo mabaya sana msimu huu ulioisha. Mategemeo makubwa ya washabiki wa Lakers ilikuwa ni kumuona Howard akitengeneza pacha na Kobe kama ilivyokuwa kwa Kobe na mkali mwingine aliyestaafu Shaq Oneil.
2

DWIGHT HOWARD AKIMZAWADI JEZI YAKE RAIS KIKWETE IKULU YA DAR ES SALAAM
Tetesi zinasema kwamba huenda Dwight Howard akahamia Huston Rockets ambapo kuna wakali wengine kama James Harden. Kama akihama litakuwa pigo kubwa sana Lakers kwasababu Howard atakuwa ameitumikia timu hiyo kwa msimu mmoja tu.Kwa mujibu wa mtandao wa kuaminika wa NBA ambao umeongea na wakala wa mchezaji huyu, amesema kwamba mteja wake bado hajafanya maamuzi wapi pakwenda lakini atatoa maamuzi yake hivi karibuni.
howard1 DWIGHT HOWARD AKIKABIDHI MSAADA WA MILLIONI 90 HUKO ARUSHA howardDWIGHT HOWARD AKIWA NA MHE LOWASSAdwight-howard-hasheem-thabeet-2009-10-12-21-40-47DWIGHT HOWARD AKIPAMBANA NA HASHEEM THABEET UWANJANIkobe-dwight-howard-lakers
 DWIGHT HOWARD NA KOBE BRAYANT

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...