Basi la kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni Iku na kuuwa watu tisa na kujeruhi wengine hamsini na tatu.
Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa
sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 basi hilo lilipokuwa likitokea mjini
Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani Katavi likiwa na abiri waliokuwa
wametoka Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi
Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali hiyo ilihusisha basi aina ya
Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya kampuni ya Sumry lililokuwa
likiendesha na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane maarufu
kwa jina la Ntungu.
Alisema basi hilo lilipofika katika
daraja hilo lenye kona kali na mteremko dereva wake alishindwa kulimudu
na kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma kupanda juu ya
ukingo na kutumbukia mtoni ambapo dereva wa basi hilo aliweza kutoka na
kukimbilia kusikojulikana
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu
Rutengwe alitoa rambi rambi kwa wafiwa wote na kuwapa pole wahanga wa
ajali hiyo mbaya kutokea tangu mkoa huo uanze.
HABARI KWA HISANI YA http://lukwangule.blogspot.com
No comments:
Post a Comment