Nelson
Mandela ameendelea kuwekwa hai kwa msaada wa mashine za kumsaidia
kupumua na anakabiliwa na 'anakaribia kifo,' nyaraka za mahakama
zimefichua.
Afya
ya rais huyo wa zamani ni 'yenye hatari kubwa,' kwa mujibu wa nyaraka
zilizowasilishwa mahakamani kwenye kesi ambayo imepelekea mabaki ya
miili ya watoto wake watatu kuzikwa upya Alhamisi kwenye makaburi yao ya
awali.
Nyaraka
za mahakama za Juni 26 zilisema: "Matarajio hayo ya kukaribia kifo
chake yanaegemea katika uhalisia na uthabiti,' zilisema nyaraka hizo za
mahakama.
Mandela,
ambaye alilazwa hospitali Juni 8, ameendelea kuwa mahututi lakini hali
inayoimarika, kwa mujibu wa Ofisi ya Rais Jacob Zuma, ambaye
alimtembelea kiongozi huyo wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi
Alhamisi.
Ikulu
ya Afrika Kusini imekanusha kwamba Mandela yuko kwenye 'hali ya kulala
tu', na kurejea taarifa zake zilizopita kwamba kiongozi huyo mpendwa
yuko mahututi lakini katika hali inayoimarika.
Ikulu hiyo ilitoa taarifa 'inayofafanua' hali ya Mandela, imeripotiwa.
Walisema: "Tunathibitisha taarifa zetu za zilizotolewa awali ... baada ya Rais Jacob Zuma kumtembelea Madiba hospitalini."
Mandela
yuko chini ya uangalizi wa karibu wa timu ya wauguzi, ikulu hiyo
ilisema, masaa kadhaa baada ya ripoti hizo za kusisimua za mahakama
kufichuka.
Nyaraka
hizo zilisomeka: Wanasema hali ya rais wa kwanza mweusi wa nchi hiyo ni
'yenye hatari kubwa'. "Matarajio ya kukaribia kifo chake yanaegemea
katika uhalisia na uthabiti,' ziliongeza. Nyaraka hizo za kisheria
zinahusiana na mapambano makali ya kisheria yenye chuki kati ya makundi
yanayopingana kwenye familia kuhusu wapi Mandela atakapozikwa.
Baada
ya kumchunguza wiki iliyopita, madaktari waliandika: "Yuko kwenye hali
ya kudumu ya kulala tu na anasaidiwa kupumua na mashine ya kuokoa
maisha."
Kitabibu, hii inamaanisha hajitambui na yuko kwenye hali katikati ya kuzimia kwa muda mrefu na kifo.
"Kwa kifupi ameshakufa," alisema Charlene Smith, mwandika wasifu wa Mandele aliyethibitishwa.
Taarifa
hizo zimekuja huku mabaki ya watoto watatu wa mzee huyo mwenye miaka 94
yakiwa yamezikwa upya kwenye makaburi yao ya awali kufuatia amri ya
mahamaka kuirejesha miili hiyo baada ya mjukuu wake, Mandla kuwa
ameihamisha.
No comments:
Post a Comment