
Howard alijiunga na Lakers akitokea Orlando Magic msimu uliopita
ambapo alicheza Lakers kwa mkataba mfupi huku akiwa na uchaguzi wa
kusajiliwa na timu nyingine kwa muda mrefu .
Los Angeles Lakers walimtumia nyota wake Kobe Bryant kumshawishi
Howard kubakia na Lakers lakini mchezaji huyo alivutiwa na Houston
Rockets ambayo ilimuahidi kusajili wachezaji wengine nyota ambao wataipa
timu hiyo nafasi ya kuwania ubingwa.
Timu nyingine zilizokuwa zinamsaka Dwight Howard ni Dallas Mavericks,Golden State Warriors na Brooklyn Nets .
Howard amesaini mkataba wa miaka mitano na timu hiyo ambapo ataungana
na nyota wengine kama Jeremy Lin na James Harden huku Wakitarajia
kumuongeza Josh Smith toka Atlanta Hawks kuongeza nguvu.
No comments:
Post a Comment